Saturday, January 25, 2014



Hati ya Usajili wa Emmanuel Okwi kama inavyoeneka kwenye system ya CAF

Uongozi wa klabu ya Young Africans umeamua kuweka hadharani ukweli kuhusiana na usajili wa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi ambaye kamati ya maadili na hadhi za wachezaji imemzuia kuichezea Young Africans mpaka watakapopata uthibitisho kutoka FIFA.

Young Africans ilikamlisha usajili wa mshambuliaji huyo tangu Disemba 15 mwaka 2013, na kupata hati ya uhamisho wake wa kimataifa (ITC) ambayo iliwasilishwa TFF pamoja na fomu mama za usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Baada ya kukamilisha zoezi hilo TFF ilipitisha jina lake kwa kutupatia leseni no: 921225001 ambayo inamruhusu mchezaji kuichezea Young Africans na kisha kulituma CAF Disemba 31, 2013 kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika ambapo CAF nao walimuidhinisha kuwa mchezaji halali wa Young Africans kwa mashindano hayo.
Cha kustaajabisha siku mbili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Kamati ya Maadili na hadhi za wachezaji wakamzuia mchezaji huyo kuichezea Young Africans ilihali akiwa ameshaidhinishwa na TFF na CAF kuwa mchezaji halali wa Young Africans.
Swali?? walikuwa wapi Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji kujiridhisha juu ya usajili ambao ulishakamilika tangu Disemba 15 2013?
Wanakuja kutoa maamuzi hayo mwezi mmoja na nusu baada ya dirisha la usajili kufungwa, ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom??

Emmanuel Okwi
JAMBO ambalo linaiumiza kichwa Yanga sasa ni kutaka kuhakiki kama kweli Etoile du Sahel imewasilisha jina la straika, Emmanuel Okwi kwenye usajili wake kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Lakini katika orodha ya Etoile du Sahel, ambayo Mwanaspoti imepata nakala yake jana Ijumaa ni kwamba klabu hiyo imepeleka CAF majina 24 tu, na hakuna jina la Emmanuel Okwi.
Iwapo ikitinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Etoile inaweza kuongeza majina sita kwani kila klabu inaruhusiwa kutuma majina 30.
Kwa kifupi ni kwamba, Etoile du Sahel haiwezi kumtumia Okwi katika Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa Yanga wanaweza kumtumia raia huyo wa Uganda kwani wametuma jina lake katika shirikisho hilo mjini Cairo, Misri.
Etoile kwenye usajili wake wa CAF imepeleka wachezaji 24 ambao pia hakuna jina la Okwi. 
Waliosajiliwa CAF ni  Aymen Mathlouthi, Saif Ghezal, Ghazi Abderrazzak, Radhouene Felhi, Marouene Tej, Hamza Lahmar, Alaya Brigui, Baghdad Bounedjah, Abdel Fadel Suanon, Issam Jebali, Franck Kom, Ahmed Mortadha na Ben Ouannes. 
Wengine ni Hamouda Chatti, Marouene Troudi, Hamdi Nagguez, Aymen Ben Ayoub, Drame  Michailou, Mohamed Slama, Zied Essoussi, Rami Bedoui, Aymen Trabelsi, Fehmi Kacem, Khaled Yahia na Youssef Mouihb
Ingawa, TFF imesimamisha kwa muda Yanga kumtumia Okwi, lakini jambo hilo inaelekea linakosa nguvu baada ya Etoile kuliondoa jina la mchezaji huyo CAF.
Yanga itacheza na Komorozine ya Comoro katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwezi ujao ikianza Dar es Salaam kabla ya kurudiana Comoro.
Okwi alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea SC Villa ya Uganda kwa mkataba wa miaka miwili huku ikidaiwa kuwa alipewa dola 100,000 (Sh 160 milioni).
SC Villa iliruhusiwa na Fifa kumtumia mchezaji huyo kwa mkataba wa miezi sita wakati sakata la madai ya mishahara na marupurupu yake Etoile yakifanyiwa kazi.
Mbali na madai ya Okwi kwa Etoile hata Simba ilikuwa ikidai dola 300,000 ambazo haijalipwa mpaka sasa na kesi  ipo Fifa.

waliotembelea blog