Thursday, October 1, 2015


Mchezaji soka mmoja nchini Uingereza amefungwa jela mwaka mmoja kwa kosa la kumvunja mguu mchezaji wa klabu pinzani kwa kumkanyaga mara kadha wakati wa mechi.
Nathaniel Kerr, 24, alikiri mashtaka mbele ya hakimu katika mahakama mjini Manchester, Uingereza.
Mchezaji aliyeumizwa Stuart Parsons, 30, alikuwa akijibizana na mmoja wa mchezaji mwenzake Kerr kwenye mechi ya ligi ya Sunday muda mfupi kabla ya kisa hicho uwanjani katika eneo la Stockport.
Kerr alimkanyaga Parsons mara kadha hadi mguu wake ukavunjika na ilimbidi kufanyiwa upasuaji na kukaa wiki kadha hospitalini.
Parsons alipokuwa amelala uwanjani akiwa na maumivu tele, Kerr alimwambia mwenzake kwa sauti: “Nimefanya haya kwa ajili yako”
Konstebo wa polisi Louise Spencer, wa kikosi cha polisi cha eneo kubwa la Mancheste, alisema: "Jeraha hili lilimwathiri sana mwathiriwa, na hakuweza kufanya kazi wala kusaidia familia yake change.
"Alilazimika kutegemea hisani ya wachezaji wenzake waliolazimika kufanya michango kukidhi mahitaji yake ya kifedha.
"Wakati huo wote, Kerr hajaonyesha majuto yoyote.”
Alisema kukamatwa na kuadhibiwa kwa Kerr ni ishara kwamba “uhuni na ujambazi” katika mechi za kandanda hautavumiliwa tena.



Msanii vichekesho, Tausi akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini humo.

Msanii Kupa akiwa amembeba msanii wa vichekesho, Tausi huku Msanii Ndede akipunga mkono kuwasilimia wana Igunga mara baada ya kuwasili mjini hapo kwa shuguli za Kampeni.

Msanii Kajala akitoa ishara ya Gole Gumba kama alama ya CCM kwa wakazi wa mji wa Igunga alipoitwa jukwaani kuwasalimia wana Igunga.

Msanii Ray Kigosi akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.

Sehemu ya baadhi ya wakazi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo.

Msanii Aunt Ezekiel akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.

Msanii wa vichekesho, Mr Kupa akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Mcheza tennes maarufu duniani kwa ubora Serena Williams atapumzika kucheza mchezo huo kwa mwaka mzima kutoka na kuwa na majeraha.
Mshindi huyo wa Grand Slam 21 alitolewa kwenye michuano ya wazi ya Wuhan baada ya kuumia na tayari alikuwa ni majeruhi.
Nyota huyo wa tenesi tayari ametoa taarifa ya kupumzika kwake kwa chama cha mchezo wa tenesi kwa wanawake (WTA)
Msimu huu wa 2015 Serena ameshinda mataji ya wazi Australian French Open, French Open na Wimbledon na hakuweza kucheza tena tangu afungwe na Muitaliano Roberta Vinci.



Hii imekuwa kawaida kwa wanasoka wengi barani Ulaya kupenda kununua magari ya kifahari kutokana na mahitaji yao lakini hii huchangiwa na mishahara yao mikubwa wanayolipwa na vilabu vyao. Mapema mwaka 2015 tuliona nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry alionesha gari lake jipya.
October 1 mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na klabu ya FC Barcelona ya Hispania Neymar ameonesha gari lake jipya aina ya  Ferrari 458 Spider, gari ambalo thamani yake inafikia pound 200000/= ambazo ni zaidi ya milioni 600 za kitanzania. Neymar kapiga picha na gari lake hilo la kifahari na kuweka katika account yake ya instagram.
2CF8F40300000578-3256270-image-a-32_1443706780157
Neymar akiwa na gari lake jipya Ferrari 458 Spider
Neymar ambaye ni moja kati ya wachezaji walioisaidia FC Barcelona kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Bayer Leverkusen bila kuwa na staa tegemeo wa timu hiyo Lionel Messi, picha ya Neymar iliambatana na ujumbe huu >>>”asante mungu kwa kunipa afya na matunda ya kazi yangu kwa kutimiza ndoto yangu”



September 10 mwaka huu alinukuliwa Rais wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Florentino Perez kuhusiana na stori za klabu ya PSG ya Ufaransa kuhitaji kumsajili Cristiano Ronaldo akitokea Real Madrid. Rais wa Real Madrid alidaiwa kukataa kabla ya siku hiyo kukubali kuwa Ronaldo anaweza kuuzwa ila kwa dau la pound milioni 728.
Stori kutoka klabu ya Orlando City ya Marekani inahitaji kumsajili Cristiano Ronaldo kutokea Real Madrid, lakini haijulikani wanahitaji kumsajili kwa kiasi gani. Mmiliki wa klabu ya Orlando City Flavio Augusto Da Silva amethibitisha kumuhitaji Cristiano Ronaldo katika timu yao. Flavio Augusto Da Silva amekiri kuwa Ronaldo ni bora kuliko Lionel Messi na wanafikiria kumsajili nyota huyo.
2CF1B5DB00000578-3256336-image-a-83_1443707764566
“Kiukweli tunampenda Ronaldo sana tusingeweza kutaka kumsajili bila ya kufikiria, Ronaldo amekamilika kuliko Lionel Messi anaweza kufanya vizuri MLS kuliko Messi, tunamatumaini tutamsajili msimu huu unaofuata tulisikia kuwa alikuwa anapenda kuja kucheza Ligi Kuu Marekani”>>> Flavio Augusto Da Silva
Orlando City ni moja kati ya klabu inayoshiriki Ligi Kuu Marekani yenye makao makuu yake Florida, kwa sasa timu ya Orlando City  ina mchezaji bora wa Dunia wa mwaka 2007 Ricardo Kaka. Orlando City inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani ambayo inachezwa kwa kikanda ipo nafasi ya saba katika timu 10 zinazoshiriki Ligi hiyo ukanda wa mashariki.
2CF98C1C00000578-3256336-image-a-94_1443708630628
Flavio Augusto Da Silva wa upande wa kushoto


Kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo, Argentina wamebakia Namba 1 huku Mabingwa wa Dunia Germany wakipanda na kukamata Nafasi ya Pili wakati Tanzania imebaki pale pale Nafasi ya 140.
Kwenye 10 Bora, Belgium imeshuka na kushika Nafasi ya Tatu, Portugal wamepanda hadi Nafasi ya 4 na Spain kurudi 10 Bora baada ya Miezi Mitatu na sasa wapo Nafasi ya 6 baada kupanda Nafasi 5.
Kwa Afrika, Timu ya juu bado ni Ivory Coast na imebakia nafasi yake ile ile ya 21 ikifuatiwa na Ghana walio Nafasi ya 25.
Listi nyingine ya Ubora Duniani itatolewa Tarehe 5 Novemba 2015.

10 BORA:
1 Argentina
2 Germany
3 Belgium
4 Portugal
5 Colombia
6 Spain
7 Brazil
8 Wales
9 Chile
10 England



Meneja biashara wa kitengo cha  Airtel Money,  Bwn Asupya Naligingwa
(kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza Airtel
kugawa gawio la faida la zaidi ya  shilingi billion 5 kwa wateja na
mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima.  Pichani
ni Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Bi Jane Matinde

KAMPUNI ya simu za mkononi
ya Airtel leo imetangaza kugawa zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa wateja
na mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima

Uamuzi huo wa kutoa gawio la faida lililopo katika akaunti  ya
udhamini ya wateja wa Airtel Money (Trust account)  litawawezesha
wateja wa Airtel kulipwa kiwango kizuri cha gawio la faida.  Kiwango
hiki cha pesa kitalipwa kutokana na  kiasi cha pesa mteja alichokuwa
nacho kw



Stori nyingi na matukio mengi tumewahi kuyasikia na kuyaona yakitokea uwanjani kama wachezaji kuvunjana miguu, kuanguka na kupoteza fahamu wakati mwingine hata kupoteza maisha uwanjani. Matukio yote hayo tumekuwa tukiyaona yakimalizika uwanjani au adhabu hutolewa na Shirikisho au kamati husika, basi hii ni tofauti kidogo kwa Uingereza mchezaji amefungwa jela kwa kosa la kumvunja mguu mchezaji wa timu pinzani wakati wa mchezo.
Mchezaji wa Sunday Ligi nchini Uingereza Nathaniel James Kerr amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumvunja mguu mchezaji wa timu pinzani. Nathaniel James Kerr ambaye ana umri wa miaka 27 amehukumiwa September 30 jijini Manchester katika mahakama ya Minshull.
Inaripotiwa kuwa Nathaniel James Kerr aliwahi kuingia katika malumbano na mchezaji aliyemvunja mguu August 31 2014 katika mechi za mwanzo za Sunday Ligi. Nathaniel James Kerr alipelekwa mahakamani baada ya kuonekana akijivunia kumvunja mguu mchezaji wa timu pinzani kwa makusudi. Hivyo kosa lake lilikuwa linahusishwa na chuki wala sio kosa la bahati mbaya.

Licha ya kuwa ugenini, Benfica imefanikiwa kuitwanga Atletico Madrid kwa mabao 2-1 ikiwa nyumbani kwao Madrid, Hispania.

Kikosi hicho cha Ureno kilionyesha soka safi na kushinda mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hali iliyoonyesha kuwaudhi sana mashabiki wa A. Madrid.
Siku moja kabla, wapinzani wakubwa wa Benfica, FC Porto walifanikiwa pia kupata ushindi kama huo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea.
Atletico Madrid: Oblak; Juanfran, Godin, Giminez, Luis; Gabi, Tiago, Oliver (Saul 63), Correa (Torres 77); Griezmann (Vietto 71), Martinez. 
Subs unused: Moya, Savic, Siqueira, Carrasco.
Goals: Correa 23
Booked: Martinez, Oliver
Benfica: Julio Cesar; N. Semedo, Luisao, Jardel, Eliseu; A. Almeida, Samaris (Fejsa 73), Goncalo Guedes, Nico Gaitan; Jimenez (Mitroglou 73), Jonas (Pizzi 80). 
Subs unused: Ederson, Silvio, Talisca, Carcela-Gonzalez.
Goals: Gaitan 36, Goncalo Guedes 51
Booked: Luisao, Eliseu, Samaris, Jardel
Referee: Gianluca Rocchi















waliotembelea blog