Saturday, October 19, 2013



STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu
Stori: Gladness Mallya
STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amekiri kuwa huwa anatumia sigara ‘fegi’ ili kuondoa mawazo.
Wema alifunguka hayo juzikati kupitia kipindi chake cha In My Shoes kinachorushwa na Runinga ya East Africa ambapo alikuwa akifungukia maisha yake likiwemo suala hilo la kuvuta sigara.

“Huwa navuta sigara pindi ninapokuwa na mawazo, nikivuta huwa inanisaidia kupunguza na kunifanya niwe vizuri,” alisema Wema.
-GPL

TATIZO la ujangili ambalo limekuwa sugu nchini kwa muda mrefu sasa linaanza kupata dawa, baada ya Serikali kutangaza ‘Operesheni Tokomeza’ itakayotumia mbinu za kijeshi.
SOMA ZAIDI..........
Katika operesheni hiyo inayotekelezwa kwa awamu, ndege za kivita zisizokuwa na marubani (Drones), zitatumika katika kufanikisha vita hiyo, iliyolenga kunusuru wimbi la wanyama kuuawa.

 

Akizungumza na RAI katika mahojiano maalumu jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alisema operesheni hiyo itatokomeza ujangili hususan wa tembo ambao umekuwa ukishika kasi kutokana na ukubwa wa soko.

Balozi Kagasheki alisema operesheni hiyo imepata nguvu, baada ya silaha za kupambana na ujangili zilizokuwa zimezuiliwa bandarini kutolewa kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete.

Kagasheki aliendelea kueleza mbali ya askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), operesheni hiyo pia itahusisha askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika kukabiliana na mtandao huo.

“Ninachotaka kusema katika hii vita, Serikali haitashindwa na kazi ambayo tumekuwa tukiifanya, kila mmoja wetu anajua nini kinachoendelea, nawaomba wananchi waendelee kutupa ushirikiano,” alisema.

Kwa mujibu wa Kagasheki awali oparesheni hiyo ilikuwa ni kukusanya taarifa mbalimbali, ambapo wizara yake imebaini kuwa baadhi ya vigogo wa Serikali wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo.

“Ninawaambia katika hili yeyote atakayekutwa hatasalimika, kwani siwezi kukaa kimya huku wanyama ambao ndiyo urithi wa Taifa wakiendelea kumalizwa na majangili ambao wana nia ovu na Tanzania yetu,” alisema Balozi Kagasheki.

Kuhusu ndege za kivita, Balozi Kagasheki alisema hiyo ni mbinu nyingine katika operesheni hiyo ambapo ndege maalumu ambazo hazina rubani zitakuwa zikizunguka katika maeneo yote ya hifadhi za Taifa na mapori ya akiba.

“Hizi ndege tutazitumia kwa lengo la kuzidisha mapambano na maharamia hawa ambao hivi sasa tunawaambia popote walipo wajue sasa Serikali ipo kazini hasa katika kulinda rasilimali za nchi,” alisema.

Akizungumzia hatua ya Rais Kikwete kuagiza kutolewa kwa silaha zilizokuwa zimekwama bandarini, Balozi Kagasheki alimpongeza rais kwa hatua hiyo ambayo alisema inalenga kujali maslahi ya taifa zaidi.

Hatua hiyo imekuja miezi kadhaa baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kudai kodi ya uingizaji wa silaha hizo zilizonunuliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kuimarisha vita hiyo.

Kagasheki, alisema hatua ya TRA hapo awali haikuwa sahihi kwani silaha hizo hazikuingizwa kwa ajili ya kumlinda yeye na familia yake, isipokuwa ni kwa ajili ya kulinda rasilimali za nchi.

“Uamuzi wa TRA ulimshangaza Rais Kikwete, baada ya kupata maelezo ya kina kuhusu hali hii alitoa agizo ili sihala hizo zitolewe bandarini mara moja.

“Ni vema jamii ikatambua kuwa tunachofanya ni kuimarisha ulinzi dhidi ya rasilimali za nchi yetu ambayo si mali ya mtu mmoja wala mali ya Kagasheki.

“Katika hili ni lazima kila mmoja atambue kuwa ana jukumu la kutoa taarifa juu ya ujangili huu unaofanywa dhidi ya tembo wetu waliopo katika hifadhi za Taifa pamoja na mapori yote ya akiba.

Waziri Kagasheki pia alilaumu hatua ya Ofisa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO), Duwan Nyanda, kwa kuruhusu kuachiwa kinyume cha sheria majangili wawili kutoka nchini Saud Arabia.

“RCO huyo wa Arusha akaona haitoshi akaamuru watu hawa ambao walikuwa wamefanya vitendo vya ujangili watolewe na wakabidhiwe na hati zao za kusafiria, kwa hili hapana na wala siwezi kukubaliana nalo hata kidogo.

“Nitafanya mawasiliano na waziri mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili kumweleza kwa kina jambo hili kuhusu kitendo hiki ambacho si cha kuungwa mkono hata kidogo kutokana na vita hii ya ujangili,” alisema.

Kwa mujibu wa takwimu kumekuwa na ongezeko la biashara ya meno ya tembo, ambapo kati ya mwaka 2008 hadi 2009 bei ya Kilo moja ya meno ya tembo ilikuwa ikiuzwa dola 10 na sasa imepanda hadi kufikia Dola za Marekani 1500 hadi 2000.

Kwa mujibu wa Kagasheki, soko kubwa la biashara hiyo hivi sasa lipo katika nchi za China, Vetnam na Thailand.

Aprili 29, mwaka huu katika Mkutano wa Bunge la Bajeti Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli alitaka TRA iachie silaha hizo ili kurahisisha vita dhidi ya ujangili.

“Kamati inaona kwamba japokuwa Wizara ya Maliasili na Utalii, imeonesha nia ya wazi ya kukabiliana na ujangili, na kununua silaha za kufanikisha azma hiyo, Serikali hiyo kupitia TRA imezuia silaha hizo bandarini ikidai kodi,” alisema.

Alisema kuzuiwa kwa silaha hizo za kisasa ni jambo la kushangaza kwani pamoja na wanyamapori ambao ni mali ya Serikali inayoiingizia mapato, bado taasisi kama TRA haioni jitihada za mkono mwingine wa Serikali wa kuokoa rasilimali ya taifa.

Kwa mujibu wa Lembeli tembo wasiopungua 30 huuawa kila siku, huku takwimu za Taasisi ya Utafiti wa Wanyama (TAWIRI ), zikibainisha wazi tishio kubwa na tembo kumalizika.


-Mtanzania

PINDA_8414e.jpg Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama vifaru na silaha nyingine za kivita wakati alipotembelea banda la kunadi silaha mbalimbali za kivita zinazotengenezwa na kampuni ya NORINCO nje kidogo ya Beijing akiwa katika ziara ya kikazi nchini China Oktoba 18, 2013.
SOMA ZAIDI........


222_99aad.jpg
Waziri Mkuu, Mizengo pinda akizungumza baada ya kutembelea kampuni ya Aluminium Corporation of China , Beijing akiwa katika ziara ya kikazi nchini China Oktoba 18, 2013. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). (P.T)

*Ataka viongozi wabadili mitazamo yao kuhusu sekta binafsi WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kuna haja ya taasisi za mafunzo ya uongozi za China na Tanzania kuandaa kozi zenye kuwafaa makundi fulani ya viongozi ambazo zitasaidia kubadili mwelekeo wao na utendaji wao wa kazi hasa katika masuala yanayohusu sekta binafsi. Amesema taasisi hizo zinapaswa kuwa na uelewa mkubwa kuhusu ushirikiano wa pamoja baina ya sekta binafsi na za umma (PPP), zinapaswa kujua faida za ushirikiano huo na zinapaswa kubainisha ni sekta zipi zinapaswa kutekeleza mpango huo wa ushirikiano. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Oktoba 18, 2013) wakati akifungua mafunzo ya siku 14 kwa maafisa 20 kutoka idara na taasisi za serikali ya Tanzania yanayoendeshwa kwa pamoja baina ya Chuo cha Uongozi cha China na Taasisi ya Uongozi ya Tanzania. Mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa Serikali kuboresha utendaji wa Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZ) yameanza leo kwenye Chuo cha Uongozi cha China (China Governance Academy), jijini Beijing, China. Alisema Tanzania imefanya maamuzi ya kutumia ushirikiano wa pamoja baina ya sekta binafsi na za umma (PPP) kama njia ya kukuza na kuendeleza miundombinu, kuhamisha ujuzi na teknolojia pamoja na ujenzi wa viwanda. "Ni muhimu taasisi zetu hizi mbili zikatambua jambo hili na kuchangia kwa juhudi zote ili kuhakikisha kuwa linafanikiwa," alisema. Alisema kozi kama hizo zinapaswa kuwalenga watumishi kutoka taasisi za serikali pamoja na sekta binafsi na akazitaka taasisi hizo kuhakikisha zinaisaidia kuwepo kwa ufanisi wa hali ya juu kwenye ushirikiano wa pamoja baina ya sekta binafsi na za umma. "Muwasaidie watu hawa waweze kutambua ni wakati gani ushirikiano wa aina hii unakuwa wa manufaa zaidi kwa wahusika, ni wakati gani wahusika wanafaidika na PPP, je wanakabiliwa na changamoto zipi, na wanafanyaje ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza," aliongeza. Alisema jambo lililo wazi kuwa ushirkiano baina ya wajasiriamali wa Kichina na wa Kitanzania utasaidia kuongeza fursa za kuhamisha ujuzi na teknolojia pamoja na kuendeleza miundombinu. "Natambua kwamba kuna wafanyabiashara zaidi ya 500 wa kutoka China ambao wako nchini Tanzania, hawa wanachangia maendeleo ya kiuchumi Tanzania kwa kuingiza teknolojia mpya na kutoa fursa za ajira," aliongeza. Waziri Mkuu ambaye yuko katika siku ya tatu ya ziara ya kikazi yake ya siku tisa kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo, alitembelea kiwanda cha aluminium cha China CHINALCO) na kiwanda cha kutengeneza zana za kijeshi ambako alionyeshwa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda hivyo.Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Nchi, (OWM) Uwezeshaji na Uwekezaji, Dk. Mary Nagu; Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Waziri wa Uvuvi na Mifugo wa Zanzibar, Bw. Abdallah Jihad Hassan; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Waziri wa Fedha, Bibi Saada Salum Mkuya. Pia amefuatana na Balozi wa China, Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahaman Shimbo, Wakuu wa mikoa ya Mtwara, Shinyanga na Simiyu; wabunge wawili, Bw. Godfrey Zambi (Mbozi) na Dk. Titus Kamani (Busega) na viongozi wakuu wa Tanzania Private Sector Foundation, Bw. Reginald Mengi, Bw. Salum Shamte na Bw. Godfery Simbeye.


Msanii wa HipHop mwenye mashahiri yenye maneno yanayolenga mastaa tofauti tofauti nchini ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Salamu Zao’ Nay wa Mitego, ameingizwa kwenye vipengele viwili kwenye tuzo zitakazofanyika nchini Kenya November 23 mwaka huu.
SOMA ZAIDI...... 
“Thnx kwa mashabiki na media zote zina nazo sapoti muziki wangu #966. Nimeingia katika tunzo nchini kenya katika category mbili wimbo bora wa mwaka East Africa ambao ni Muziki Gani category ya pili Msanii bora wa kiume Tanzania. #966 tuombe Mungu izi zote mbili tuchukue.. Siku ya tuzo ni tarehe 23 mwezi 11..!!.”- Naywa Mitego.


Mechi kali ikibwa kati ya Manchester United VS Arsenal katika viwanja vya Leaders Club ikiwa ni Serengeti Fiesta Soccer Bonanza 2013 katika kuelekea Serengeti Fiesta 2013 siku ya Jumamosi 26 October 2013 --> Noma Saana!! TWENZETU


Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Daniel Sturridge amefichua hisia zake kwa nyota wa muziki wa Pop Rihanna . Katika Interview moja aliyoifanya kwenye jarida la rapa wa marekani Jay Z, Sturridge alizungumzia usajili wake toka Chelsea kwenda Liverpool na pia maisha yake ya Mapenzi na zaidi alizungumza kumhusu Rihanna . Soma maneno yake hapa.....

MNENGUAJI wa kiume wa Mashujaa Band, Juma Nyamwela (Nyamwela Jr) amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume wa umri wa miaka sita.

Kwa sasa mnenguaji huyo yupo kituo cha polisi cha Mabatini Kijitonyama jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya tatu tangu akamatwe kwa tuhuma hizo.

Habari za uhakika kutoka kituoni hapo zinasema katika maelezo ya awali, mnenguaji huyo amekiri kosa.

  
Chanzo cha salute5  kimeeleza kuwa huenda mnenguaji huyo akafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.


Nyamwela ambaye ni mdogo wake na Super Nyamwela wa Extra Bongo, aliwahi kuitumikia TOT Plus kabla ya kujiunga na Mashujaa Band. 


Mwaka 2007 aliibuka bingwa wa mashindano ya dansa bora wa kiume yaliyoandaliwa na Usher Family na kujinyakulia zawadi ya gari.


Duniani kuna maajabu mengi,kati ya maajabu hayo ni huu mgahawa uitwao Rock uliopo visiwani Zanzibar uliojengwa juu ya mwamba mkubwa katika bahari ya Hindi.
ANGALIA PICHA ZAIDI.........


Mgahawa huo ulifunguliwa rasmi mwaka jana na kuna viti 45 ambapo wateja huchukuliwa na boti maalum kutoka pwani hadi kupata huduma katika mgahawa huo ili wasikanyage maji wakati wakiingia kwenye mgahawa huo.

Chakula kinachopatikana muda wote katika mgahawa huo ni samaki pekee kutoka baharini na vinywaji.

Wafanyakazi wa The Rock

The Rock umetajwa kuwa ni mgahawa wa ajabu katika Afrika Mashariki na watu wengi wakiwemo watalii hupenda kwenda kutokana na habari zake kuenenea kwa kasi na wengi hupendelea kupata hewa safi ya baharini na kuona jinsi kilivyokuwa ndani.

Rock, ambayo ilifunguliwa mwaka jana, inaweza kufikiwa kwa miguu, lakini pia kuna usafiri wa mashua wa kuwasafirisha wateja kutoka pwani hadi kwenye mgahawa huo.


Titica
Mwanamke huyu  kwa jina akijulikana kama  Titica, amekuwa ni gumzo kubwa nchini Angola.
 Siku chache zilizopita UNAIDS ilimpa heshima  mwanamke huyu aliyejibadili jinsia kuwa  Balozi wake.

Alizaliwa Luanda kama Teca Miguel Garcia,  akiwa muimbaji na mchezaji, Titica alibadili  maumbile yake miaka minne iliyopita mara
 baaada kufanya upasuaji wa maziwa  nchini Brazil.

Sasa, akiwa na miaka 26, Titica amekuwa 
kioo cha Angola kwa aina ya muziki anaoufanya
 wenye mchanganyiko wa miondoko ya rap na
 techno unaojulikana kama “kuduro”.

Akiongea na BBC mwaka jana, akiwa kwenye 
kwenye utengenezwaji wa video ya wimbo wake unaotamba sasa uitwao Olha o Boneco, wimbo
 ambao amemshirikisha muimbaji mashuhuri wa  muziki aina ya kizomba aitwaye Ary, Titica  alisema amefanikiwa kukabiliana na  vikwazo vyake.

“Shukrani kwa Mungu, nina furaha sana, 
imechukua muda kufika hapa na imehusisha  mambo mengi ya kujitolea ila asante Mungu,
 kila kitu kinakwenda sawa kwangu.
 
Nilikuwa nikipigwa mawe, nimekuwa nikipigwa  na kumekuwa na vikwazo vingi vya kisheria dhidi
 yangu, watu wengi walionyesha hilo. Kuna miiko  mingi sana,”.

Licha ya miiko hiyo, bado Titica anaonekana 
kuwa hana upungufu wa mashabiki huku wengi  wakiwa wanavutiwa zaidi na muziki wake kuliko
 jinsia yake.

Kukamatwa kwa washukiwa 11 wa al-Shabaab waliokuwa wakifanya mafunzo ya kijeshi katika mkoa wa Mtwara mapema mwezi huu kumeibua wasiwasi miongoni mwa wachambuzi wa usalama na maofisa kwamba kikundi hicho cha wanamgambo kinajaribu kudanganya walalamikaji wa Tanzania katika jitihada za kupanua eneo lake la ushawishi.
  • Picha ya skirini ya video ya lugha ya Kiswahili iliyotolewa na Al-Kataib, kitengo cha habari cha Shabaab.  Katika video hiyo, mwanamgambo ambaye anajulikana kwa jina la Abu Tarub al-Kenyi alieleza kwa watazamaji namna ya kutumia AK-47. [File] Picha ya skirini ya video ya lugha ya Kiswahili iliyotolewa na Al-Kataib, kitengo cha habari cha Shabaab. Katika video hiyo, mwanamgambo ambaye anajulikana kwa jina la Abu Tarub al-Kenyi alieleza kwa watazamaji namna ya kutumia AK-47. [File]
Washukiwa hao walikamatwa katika mlima wa Makolionga katika wilaya ya Nanyumbu tarehe 7 Oktoba na walikutwa wanamiliki silaha za moto, mapanga na DVD 25 zenye miongozo ya mafunzo ya al-Shabaab, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara Zelothe Stephen.
"Moja ya DVD waliyokutwa nayo ilikuwa na programu yenye jina Zinduka Zanzibar," aliiambia Sabahi, maana yake "Amka Zanzibar". "Ilifundisha namna ya kuua kwa haraka na kutoa mafunzo kwa wanamgambo. DVD nyingine zilikuwa na mafunzo yanayohusu ugaidi yanayohusiana na al-Shabaab."
Mamlaka za ndani zinachambua ushahidi huo na kuwatafuta washukiwa wengine katika eneo hilo pamoja na msaada wa vyombo vya upelelezi kutoka makao makuu ya polisi huko Dar es Salaam, Stephen alisema.
Jina lake ni Mohammed Makande mwenye umri wa miaka 39 kama kiongozi kinara wa washukiwa waliokamatwa. Washukiwa wengine walibainishwa kama: Said Mawazo (miaka 20), Ismail Chande (miaka 18), Abdallah Hamisi (miaka 32), Ramadhani Rajabu (miaka 26), Salum Wadi (miaka 38), Hassan Omary (miaka 39), Fadhili Rajabu (miaka 20), Abbas Muhidini (miaka 32), Issa Abeid (miaka 21) na Rashid Ismail (miaka 27).

Kuenea kwa wasiwasi

Wachambuzi wa usalama wasema serikali lazima iboreshe jitihada za kushuhulikia malalamiko ya ndani kuondoa msimamo mkali na kuanza kwa vurugu katika maeneo ambayo tayari yameshakosa utulivu.
Gideon Shoo, mwandishi wa habari mkongwe na mmiliki wa G&S Media Consultants, alisema al-Shabaab walikuwa hasa wakilenga Mtwara na Zanzibar ili kutumia hali iliyopo ya malalamiko ambayo wakaazi wanaweza kuwa nayo dhidi ya serikali.
"Kila mmoja anajua udhaifu huko Mtwara kuhusiana na uchimbaji wa gesi, na kuangalia kile kinachotokea huko Zanzibar pamoja na mashambulio ya asidi," Shoo aliiambia Sabahi. "Siyo siri kwamba al-Shabaab wanapanga kutumia hali ya kutoridhika katika maeneo hayo kama njia ya kuingilia Tanzania."
Shoo alisema serikali ya Tanzania inapaswa kuzungumza na Wazanzibari kufikia suluhisho ya kirafiki na la hakika kutatua malalamiko yanayohusiana na sehemu yao katika serikali ya umoja.
Kinyume chake, alisema, serikali lazima ihusishe wakaazi wa Mtwara na kutoa taarifa zaidi kuhusu faida muhimu zitakazotokana na kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, ambayo ilikuwa sababu kuu ya vurugu na ukosefu wa utulivu katika mkoa mapema mwaka huu.
Oswald Kasaizi, mkurugenzi mtendaji wa Msaada kwa Chama cha Maendeleo, asasi isiyo ya kiserikali ambayo inatoa msaada kwa jamii katika maeneo yenye mizozo, alisema habari za mafunzo ya washukiwa wa al-Shabaab nchini Tanzania ni mwanzo wa wasiwasi.
"Ukweli kwamba watu hawa wamefanikiwa kukutana pamoja na kuanza mafunzo katika ardhi yetu ni ishara mbaya sana," alisema.
Kasaizi alisema majeshi ya usalama yanapaswa kuwa makini na taarifa kuhusu vitabu vya mafunzo ya al-Shabaab yaliyokusudiwa kuishawishi Wazanzibari kwa sababu kikundi cha wanamgambo kinatumia maeneo ambayo tayari yana mgogoro kama eneo zuri kwa ajili ya operesheni zao.
"Al-Shabaab na al-Qaeda sasa wanatumia Zanzibar kama njia ya kuingilia," aliiambia Sabahi. "Lengo lao ni nchi nzima ya Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla. Hili ni tishio kubwa lililowahi kutokea. Mafunzo nchini kwetu yanahakikisha kwamba wapo hapa."
Kasaizi alilaumu mfumo wa usalama nchini kwa kuruhusu hali ya al-Shabaab kuanzisha kambi ya mafunzo katika ardhi ya Tanzania kwa mara ya kwanza.
"Jeshi letu la usalama limeonyesha kiwango kisichokubalika cha uzembe ambacho kinaweza kuigharimu nchi yetu kwa kiasi kikubwa," alisema.

Sio tukio pekee

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai Robert Manumba alisema mamlaka hazichukulii kirahisi tatizo la vitisho vya ugaidi na linajitahidi kusambaratisha makundi ya magaidi na mitandao yao.
"Tuna maelekezo kuhusu kuwepo kwa al-Shabaab na tunawafuatilia kwa karibu," aliiambia Sabahi.
"Kilichotokea huko Mtwara sio tukio pekee," alisema. "Inatokea hivyohivyo nchini Kenya, Uganda, Sudan, Somalia, Ethiopia na nchi nyingine nyingi, lakini kila inapotokea tunapeana taarifa katika njia ya kufuatilia mwenendo na kutafuta suluhisho."
"Mara kwa mara tunabadilishana taarifa za usalama kikanda na kimataifa," alisema Manumba.
Hii ni nyongeza ya Operesheni Kimbunga ya Serikali, ambayo inakusudia kuwarejesha kwao wahamiaji haramu nchini Tanzania.
"Kati ya tarehe 10 Septemba na Oktoba 10 tulifanikiwa kuwarejesha kwao zaidi ya wahamiaji haramu 22,000," alisema, akiongeza kwamba kutokana na upelelezi wa polisi, wahamiaji wengi walikuwa wakijihusisha na shughuli haramu.
Manumba aliwashukuru wananchi wa Mtwara kwa kuwatonya mapolisi kuhusu washukiwa wa ugaidi na kuwaagiza Watanzania kuendelea kuripoti kwa mamlaka zinazohusika kuhusu jambo lolote linalotiliwa wasiwasi ili kuhakikisha usalama.

Kurejesha mfumo wa nyumba kumi

Mjumbe wa Baraza la Kata ya Kitunda Israel Kimune aliiomba serikali kurejesha mfumo wa nyumba kumikumi ambao ulikuwa na mamlaka kitaifa wakati wa utawala wa Rais Julius Nyerere.
Chini ya mfumo huo, kila nyumba kumi zilizo karibu zilibainishwa kuwa chini ya kiongozi aliyewajibika kubainisha na kumwandikisha kila mmoja katika eneo lake, hata wageni na muda wao wa kuishi katika eneo hilo.
"Ninaelewa wazo la [mfumo] nyumba kumi lilitokana na [chama tawala] Chama Cha Mapinduzi, kisha wapinzani hawakujisikia vizuri kuufuata na ulifutwa kisheria, lakini tulifanya kosa kubwa," Kimune aliiambia Sabahi. "Unapaswa kurejeshwa kwa ajili ya usalama."
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Ame Silima alisema serikali ilikuwa ikizingatia kurejesha mfumo huo.
"Ulifanya kazi vizuri wakati wa mfumo wa chama kimoja lakini ulifutwa baada ya kuja kwa siasa za vyama vingi," Alisema Silima tarehe 11 Oktoba katika mahojiano na gazeti la serikali la Daily News.
Silima alisema maofisa polisi 8,000 wamekuwa wakisambazwa nchi nzima kuhakikisha kwamba ulinzi wa jamii unaimarishwa. "Mipango pia inafanyika kuangalia kwamba kila tarafa inakuwa na inspekta wa polisi anayeisimamia, sio kama sasa ambapo inspekta anawajibika kwa ngazi ya wilaya," alisema.
dscf0012_3d544.jpg
MALALAMIKO JUU YA MENEJIMENTI YA CHUO CHA KUMBUKUMBUKU YA MWALIMU NYERERE
1. SHERIA YA UANZISHWAJI CHUO
Mh. Waziri Mkuu, sheria iliyopo ya uanzishwaji wa chuo inamapungufu kadha, ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho. Mapungufu hayo ni:
i. Sheria haitaji sifa za mkuu wa chuo aweje
ii. Sheria haitaji sifa za Makamu Mkuu wa Chuo
iii. Sheria haitaji sifa za Msajili wa Chuo
iv. Pia sheria inapigana na taratibu za NACTE ambazo zinataja uwepo wa Rector, Deputy Rector Academic, Deputy Rector Adminstration.
v. Sheria Haitaji ukomo wa Msajili (registrar) imeiachia Bodi na Mkuu wa chuo suala la kuamua muda wa Msajili.
vi. Sheria inamtaja msajili kama Katibu wa kamati ya taaluma wakati yeye hahusiki na mambo ya taaluma.



vii. Kazi za kamati zifuatazo Human Resource Development and Disciplinary Committee, Finance and Planning Committee and Students' na Disciplinary Appeals Committee hazitajwi na sheria, tofauti na kazi za kamati ya taaluma ambapo kazi zake zimetajwa.
Mh. Raistunakuomba sheria hii ya uanzishwaji wa chuo ipitiwe upya ili kukidhi matakwa ya sasa na kuleta ufanisi wa kazi kwa ujumla.(P.T)
2. UWAKILISHI WA WAFANYAKAZI KATIKA BODI YA CHUO.
Pamoja na sheria kusema kuwa kutakuwa na uwakilishi wa Wafanyakazi (The Mwalimu Nyerere Memorial Academy Act, 2005 Ibara 6:1 (D Na G) katika bodi ya chuo, Mkuu wa chuo amekuwa akimdanganya Waziri kwa kumpatia mapendekezo ya majina ya wanataaluma na wafanyakazi kwa ujumla, ambao sio wawakilishi halali. Suala
Mhe. Rais tokea mwaka 2006 Bodi ya Chuo hakina wawakilishi wa wafanyakazi bali wawakilishi hao huteuliwa kutokana na matakwa ya Menejimenti, hivyo kufanya mawazo ya wafanyakazi kutowasilishwa kwenye bodi.
3. VIKAO VYA WAFANYAKAZI
Mh. RaisTokea Mwenyekiti wa Bodi ateuliwe kwa muda wa miaka 8 sasa hajawahi kufanya kikao na wafanyakazi. Suala hili limesababishwa na Menejimenti ambayo kwa hakika imekuwa ikimficha Mh. Balozi ili kwa kumdanganya kuwa mambo yanaenda. Hii imesababisha Mkuu wa Chuo kufanya vikao vichache vyenye kututisha wafanyakazi na hivyo kushindwa kutoa mawazo yetu.
4. MALENGO YA CHUO
Mhe. Waziri Mkuu Kutokana na sheria ya chuo, Chuo kina malengo kumi na moja (11) kama ifuatavyo:
a) To provide facilities for study and training in social sciences, leadership and continuing education;
b) To conduct training programmes in the disciplines specified in paragraph (a);
c) to engage in research and development in the disciplines specified in paragraph (a) and to evaluate the results achieved by the Academy training programmes;
d) To provide consultancy services to the public and private sectors in specified fields as prescribed in this Act;
e) To sponsor, arrange, facilitate and provide facilities for conferences, symposia, meetings, seminars and workshop, for discussion of matters relating to social sciences, leadership and continuing education;
f) To conduct examinations and grant awards of the Academy as approved by the National Council for Technical Education;
g) To arrange for publication and general dissemination of materials produced in connection with the work and activities of the Academy;
h) To engage in income generating activities for effective financing and promotion of entrepreneurship;
i) To establish and foster close association with the Universities and other institutions of higher education and promote international cooperation with similar institutions;
j) To do all such acts and transactions as are in the opinion of the Governing Board expedient or necessary for the proper and efficient discharge of the functions of the Academy;
k) To perform such other functions as the Minister or the Governing Board may assign to the Academy, or as are incidental or conducive to the exercise by the Academy of all or any of the preceding functions.
Mh. Raiskati ya malengo hayo juu ni lengo malengo a, f na J kidogo yameweza kufanyiwa kazi. Lakini malengo mengine yote hajawahi kufanyiwa kazi tokea chuo kianzishwe mwaka 2005. Mh. Raisnaomba ufanyie uhakiki haya tuandikayo juu ya malengo. Chuo kimebaki kuwa kama sekondari, hakuna tafiti zinazofanyika wala ushauri wa kitaalamu unaoendelea.
5. MISHAHARA YA WAFANYAKAZI
Mh. Raistunapenda kutoa masikitiko yetu juu ya mishahara ya wafanyakazi. Kumekuwa na tatizo kubwa la ongezeko la mishahara ya wafanyazi wa kada zote, wafanyakazi wamekuwa hawapandishwi madaraja kulingana na stahili yao. Mshahara unapandishwa ni ule wa ongezeko la litolewalo na serikali, lakini annual increment kwa wafanyakazi haipo kabisa. Hili limepelekea wafanyakazi wanaoajiriwa siku za karibuni kulingana mishahara na wafanyakazi wa zamani.
Mhe. Makamo wa Rais suala hili linafanyika makusudi kabisa ili kuwakomoa wafanyakazi, hatuwezi amini kuwa utawala hawajui juu ya suala hili. Hivyo tunaomba ulifanyie kazi pia.
6. AJIRA ZENYE UTATA
Mh. RaisKumekuwa na ajira zenye utata kwa wahadhiri watatu (3), utata huu umefanywa na msajili sio kwa bahati mbaya, bali kwa maslahi binasfi.
a. Ajira ya Ndugu Ernest Luambano: Mh Waziri Mkuu Ndugu Luambano aliajiriwa na chuo mwaka 2004 akiwa na miaka hamsini (50) akiwa kama afisa tawala. Ajira yake ilikuwa ni ya mkataba wa miaka 4, hivyo muda wa mkataba wake ulikuwa uishe mwaka 2008. Lakini mwaka 2006 kwa kushirikiana na mkuu wa chuo walirudisha umri wa Luambano nyuma yaani akaonekana amezaliwa mwaka 1959, basi kuandika tarehe. Baada ya kurudisha umri nyuma wameficha mafaili ya ajira yake ya mwanzo ya mkataba na kufanya au kuingiza mwaka 1959 kama mwaka wake wa kuzaliwa, hivyo kuonekana kwamba aliajiriwa akiwa na miaka 44 au 45.
Suala hili ni kinyume na taratibu za ajira katika ofisi za umma kama inavyoelekezwa na standing order ya mwa 2009;
D.33 Appointment on Contracts:
(1) A candidate appointed to a pensionable post in the public service on non-pensionable terms, or to a non-pensionable post, shall be required to enter into a contract (on gratuity terms) specifying the terms of his employment as provided for in Appendix D/V. Contracts on gratuity terms, which shall be the normal form of engagement in such cases, provide for the payment by Government of a gratuity at a prescribed rate on satisfactory completion of the contract.
(2) Under special circumstances, certain persons may be engaged in the public service to serve on contract terms. These shall include:
(a) a non-citizen who is engaged for some projects or on expatriate requirements;
(b) a citizen from outside the public service who is engaged to the Service under expatriate or consultancy requirements;
(c) a retired public servant who has been re-engaged in the Service; and
(d) a citizen who is first appointed to the Public Service after he has attained the age of 45 years.
(3) Where it is in the opinion of the appointing authority that a public servant be re-engaged on further terms of contract, the appointing authority shall notify the Permanent Secretary (Establishments) who shall forward to the Chief Secretary with recommendations.
D.34 Completion and Renewal of Contracts:
(1) The Chief Executive Officer shall inform the public servant three months before the expiry of the contract, whether or not he wishes to re-engage him for further period of service. Similarly the public servant serving on contract shall notify his Chief Executive at least three months before the engagement is due to expire whether or not he wishes to be re – engaged, for a further period of service.
(2) Approval of the Appropriate Appointing Authority to be sought: On receipt of the notification referred to in paragraph (1), the Chief Executive Officer shall forward his recommendation regarding the re-engagement of the public servant concerned to the appropriate authority for approval.
(3) The Chief Executive Officer shall not initiate or seek the approval of the re-engagement of a public servant in contract unless:-
(a) There are special resources and arrangements of training of counter parts and successors in such post; and
(b) There is a special provision in the contract obliging the employee in contract to impart his knowledge to the counterparts and successors.
(4) Re-engagement of a contract employee without consideration of the requirements under paragraph (3) shall only be made by an approval of the Chief Secretary.
D.39 Age of admission to a Pensionable Establishment:
Appointments to the pensionable establishment shall be restricted to persons of and below the age of 45 years who would be in a position to complete the fifteen years' service required to qualify for the grant of a pension on reaching the compulsory age of retirement. There shall be special circumstances which may justify variations in the application of the general principle, and such cases shall be submitted for consideration of the Permanent Secretary (Establishments).
Katika suala hili, bodi ya chuo ilidanganywa na Mkuu wa chuo kwa makusudi ili bwana Luambano apate ajira ya kudumu. Hivyo Mh. Dr. Salim hajui lolote juu ya hili kwani alidanganywa.
Tunakumba Mh, ufanyie kazi hili suala kwa haraka, kwani Msajili amekuwa tatizo katika taasisi, ajira zote zinazofuata hapa nchini yeye ndiye mhusika mkuu wa kuzitengeneza. Kwasababu na yeye amegushi. Wafanyakazi hatutakubali kuendelea kufanya kazi na mtu ambaye amegushi umri, lakini pia akikabiliwa na tuhuma lukuki za ufisadi.
Hivi sasa Mkuu wa chuo na Msajili wanahaha kuficha ukweli wa mambo kwa kutengeneza na taarifa mbalimbali na kupoteza ushahidi juu ya hili, lakini ni tumaini letu kuwa serikali ina mkono mrefu itaufikia ukweli pasipo kumuonea mtu.
b. Ajira ya Mhagama: Huyu alikuwa mwajiriwa wa chuo kabla ya kujiuzuru mwaka 2012. Ilikuwa ikifahamika tokea alipoajiriwa kuwa ana vyeti visivyo halali. Lakini chuo kiliendelea kumulinda pasipo kufanyia kazi. Baadae chuo kilimpeleka kusoma shahda ya uzamili chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Baada ya kumaliza, chuo kikuu cha Dar es Salaam kilimnyima cheti, japo Msajili alimpandisha mshahara pasipokuwa na vyeti na kumlipa mshahara wa kiwango cha Uzamili. Suala hili liliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya jamii. Walipoona kuwa Mhagama anasakamwa Msajili alimshauri ajiuzulu, wakati wa kujiuzulu alilipwa hela ya likizo. Pamoja na sheria kuwa wazi, juu ya mfanyakazi anayeacha kazi ndani ya masaa 24, kutakiwa kulipa mshahara wa mwezi mmoja kwa mwajiri bw Mhagama hakufanya hivyo.
Suala hili lilichunguzwa na Ofisi ya Rais Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, jambo la kushanga taasisi hii ilikisafisha chuo kwamba hakukuwa na shida. Mambo la kujiuliza hapa:
i. Mhagama aliajiriwa lini Mwalimu Nyerere?
ii. Menejimenti ya Mwalimu Nyerere alijua lini suala hili la Mhagama kufoji vyeti?
iii. Baada ya kugundua Menejimenti ya Mwalimu Nyerere ilifanya nini?
Tukijibu maswali haya unagundua kuwa hata Ofisi ya Rais Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa haikufanya kazi yake ipasavyo. Haiwezekani suala hili ligundulike miaka miwili nyuma, pasipo kuchukuliwa hatua (ushahidi upo). Hata baada ya kulitambua hili hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
c. Ajira ya Bi Sara Mwakyusa: Muhadhiri huyu alipewa mkataba wa mwaka mmoja ilikufundisha Tawi la Zanzibar. Menejimenti ilitambua kuwa huyu mhadhiri ni muajiriwa wa manispaa ya Ilala shule ya Sekondari Azania, iliamua kuumpa mkataba wa ajira ya mwaka mmoja, huku menejimenti ikijua ni kosa kisheria.
d. Ajira ya Bwana Rodgiers Kiowi, mwaka 2010 chuo kilimuajiri ndugu Kiowi kama mhadhiri Msaidizi, wakati kikijua kuwa ni muajiriwa wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam. Tunasema chuo kilijua kuwa ni mwajiriwa wa DIT kwa ushahidi wa kimazingira.
i. Tokea aingie hajawahi kuingizwa kwenye payroll ya hazina na sasa ni muda wa miaka mitatu. Kwanini ichukue muda mrefu kiasi hicho wakati Hazina na MNMA ni viko karibu kama ni suala la ufuatiliaji.
ii. Pili, suala hili menejimenti ilifahamishwa na afisa mitihani aliyejiuzulu, lakini haikuchukua hatua badala yake alihudhuria kikao cha kamati ya taaluma.
iii. Mpaka sasa hajafunguliwa mashtaka ya kuiibia serikali.
Kwa ushahidi huu hakika Menejimenti ya chuo inajua suala hili, ndio maana msajili amekuwa akitoa ushauri wa kiupotoshaji kwa mkuu wa chuo, ili bw Kiowi asichukuliwe hatua.
Mh. Raistunaomba uchunguze ajira hizi tata ambazo kwa hakika zimetafuna pesa za walipa kodi. Mfano Kiowi amekuwa analipwa mshahara na marupurupu yote kwa mapato ya ndani na sio hazina kwa muda wote.
7. UJENZI WA CHUO ZANZIBAR
Mh. Waziri Mkuu, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Mkuu wa Chuo amefanikiwa kufanikisha kujenga Chuo Zanzibar, hili ni takwa la kisheria. Lakini ujenzi huu kwa mujibu wa kamati ya huduma za jamii za Bunge hakukudhi baadhi ya mambo. Licha ya Naibu Waziri wa Elimu kutoa agizo juu ya kutofunguliwa kwa jingo hilo, menejimenti ya chuo ilimdanganya Mh. Salim (Mkiti), likafunguliwa. Ufunguzi huo haukuhudhuriwa na kiongozi yeyote wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi. Hii ni kutokana msigano uliokuwepe kati ya menejimenti, Naibu Waziri wa Elimu na Kamati ya kudumu ya huduma za jamii ya bunge.
Mh. Raiskwa kuwa suala la ujenzi ni linaonekana, tunaomba utume watu wako wakaangalie ujenzi ule kama umekidhi matakwa ya ujenzi.
8. UKARABATI WA NYUMBA YA MTU KUWA HOSTEL YA WANAFUNZI ZANZIBAR
Mh. Waziri Mkuu, kuna suala ambalo linatia shaka, ambalo ni ukarabati wa nyumba ya mtu kuwa hostel ya wanafunzi Zanzibar. Hii ilikuwa ni njia ya kufanya ufisadi kwani haukufuata taratibu za kimanunuzi. Bahati mbaya, kamati ya huduma za jamii yz bunge ilifichwa juu ya ukweli huu. Yafuatayo hayakufanyika:
i. Menejimenti haikutanganza tenda ya kutafuta hosteli.
ii. Haikutangaza tenda ya zaidi ya shilingi 700 kwa ajili ya kukarabati jengo hilo.
iii. Pesa zaidi ya shilingi 700 zingeliweza kuanzisha ujenzi wa hosteli ya chuo, kuliko kinachofanyika sasa hivi kwa kulipa dola 20,000 kwa mwaka kwenye jingo hilo.
Mh. Raishuu ni ufisadi mkubwa unaoendelea hapa, kwani hata bodi ya tenda haijui jambo lolote juu ya ujenzi huu
9. UJENZI WA HOSTELI YA KIGAMBONI
Mh. Raissasa hivi chuo kinaendeleza ujenzi wa hosteli hapa Kigamboni, Ujenzi huo uko kwenye awamu ya pili. Jambo la kushangaza katika awamu hii ya pili hakuna tenda iliyotangazwa hii ni kinyume na taratibu. Mkandarasi anayefanya kazi hii ni Yule Yule aliyejenga Zanzibar, aliyekarabati hosteli ya wanafunzi Zanzibar.
Ujenzi wa awamu ya pili haujulikani sehemu yoyote zaidi ya Mkuu wa chuo na Msajili, bodi ya Tenda haikushirikishwa kwa jambo lolote.
10. MADENI YA NDANI
Mh. RaisMadeni ya ndani ya yamezidi kuwa makubwa, wafanyakazi sasa wanadai posho mbalimbali kama posho za nyumba na posho za nauli. Tokea mwezi wa Saba posho hizi zimesitishwa pasipokuwa taarifa yoyote. Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa sababu ya kustisha posho hizi, japo tunasikia tutalipwa mwezi wa kumi kwasababu sasa chuo hakina pesa.
Mh. RaisWahadhiri hupata posho kwa ajiri ya kusimamia mitihani, kusahishisha mitihani, Kusimamia tafiti za wanafunzi na vikao mbalimbali, mpaka sasa wahadhiri nao hawajalipwa. Japo la kushangaza hakuna sababu yoyote iliyotolewa. Sasa wahadhiri wanapanga kugoma kwa sababu ya posho zao.
Mh. Waziri Mkuu, wafanyakazi hawawezi kuzungumza jambo lolote, kwasababu mkuu wa chuo amekuwa akitumia vitisho kwa wafanyakazi kwamba yeye yuko karibu na Rais, hivyo hakuna mtu anayeweza kumfanya lolote.
11. VITISHO DHIDI YA WAFANYAKAZI (KUACHA KAZI) UBABE
Mh. Waziri Mkuu, kumekuwa na vitisho vya mara kwa mara kwa wafanyakati ambao huonekana wanakwenda kinyume na matakwa maovu ya menejimenti. Tokea mwaka 2005 wafanyakazi wengi sana wameacha kazi kwasababu ya kunyanyaswa na menejimenti ya chuo.
Mh. Raishili suala limekuwa likifichwa kwa mwenyekiti wa Bodi, akidanganywa kuwa wafanyakazi hao wameacha kazi kwasababu zao binafsi, wakati sio kweli. Mh. Raishili limesababisha mara kwa mara upungufu wa wafanyakazi hapa chuoni.
12. MANUNUZI
Mh. RaisSuala la manunuzi limekuwa tatizo kubwa hapa kwetu, msajili wa chuo amekuwa ndiye muhusika mkuu katika manunuzi ya chuo, suala hili limekubikwa misingi ya rushwa. Msajili ndiye afisa manunuzi ya chuo, watu waliopo katika kaitengo cha manunuzi wao ni alama tu, hawafanyi kazi zao. Japo wamekuwa wakishiriki kumfanikishia msajili mambo yake ili yaonekane yamefata taratibu.
Suala hili lilipelekwa PCCB, PCCB nao wamepewa rushwa na msajili, masjili amekuwa na mawasiliano makubwa na afisa mmoja wa PCCB makao makuu. Afisa huyo amekuwa akitoa siri za wapeleka taarifa, pia amekuwa akisaidia kuficha maovu ya MNMA. Kwa uhakika zaidi juu ya suala hili naomba uchunguze mawasiliano (simu) ya Msajili wa Chuo na maafisa wa PCCB waliokuwa wanashughulikia masuala ya MNMA.
Pia Taasisi ya PPRA baadhi ya maafisa wake wanatumika kuficha ukweli juu ya tuhuma zinazopelekwa huko. Pia uchunguzi ufanyike juu ya mawasiliano (simu) ya siri kati ya afisa mmoja wa PPRA na Msajili wa chuo.
13. MCHAKATO WA KUMPATA MWENYEKITI WA BODI NA MKUU WA CHUO
Mh. RaisMkuu wa chuo amemuandikia Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi barua za tarehe 19 na 24 Julai aweze kumuomba Waziri wa Elimu, akuombe umuungezee muda Dr. Salim Ahmed Salim. Hili tunakubaliana nalo kabisa, sio kwamba Dr. Salim katenda makubwa, hapana ni kwasababu tunaimani menejimenti haikumtumia ipasavyo. Tunaimani menejimenti mpya ikiwekwa na Dr. Salim akaendelea kuwa Mwenyekiti, chuo chetu kitabadilika sana, kuliko kilivyosasa.
Mh. Raisitakumbukwa kwamba Mkuu wa chuo wa muda wake wa miaka miwili uliyomuongezea unakwisha mwezi wa 12 2013. Jambo la kushanganza mpaka sasa hakuna mchakato wowote ambao umeanzishwa kwa ajili ya kumpata mkuu wa chuo mpya. Jambo hili linafanyika makusudi ili Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo aje akaimu ukuu wa Chuo. Kukaimu kwake kutakuwa kunatoa nafasi kwa msajili wa chuo kuwa Mkuu wa Chuo kwa "remote".
Katika suala hili, ni muendelezo wa Mkuu wa chuo kutotaka kufanya kazi na watu wenye sifa na uwezo. Mfano Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo amekaimu nafasi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja na miezi miwili sasa. Mkuu wa chuo na amekataa kuomba utumishi ili chuo kiajiri mtu mwenye sifa yaani mwenye Shahada ya Uzamivu. Kwa kuwa Mkuu wa chuo na Msajili wanapenda watu wasiokuwa na uwezo na ambao wanawasikiliza wao basi mchakato wa Naibu mkuu wa chuo haukufanyiwa kazi.
Mh. Raistunakuomba kwa dhati, uingilie mchakato huu, ili malendo yao ya kukaa na kaimu mkuu wa chuo asiye na sifa yasiweze kufikiwa.
14. WANATAALUMA KUTOKUWA NA SIFA
Chuo chetu kinakabiliwa na tatizo kuwa katika taaluma, wanataaluma waliowengi hawana sifa ya kufundisha. Ajira zao zina utata mkubwa sana, hii imesababisha wahadhiri wengi kutojiamini kwa kuwa hawana sifa za kufundisha elimu ya juu. Taratibu za walimu wa elimu ya juu wanatakiwa wawe na ufaulu angalau wa GPA ya 3.5 lakini wahadhiri wengi wako chini ya hapo.
Pia tatizo hili linatokea katika masomo ya ufundishaji, (specialization) mfano Mhadhiri aliyesoma shahaha ya "Political Science and Public Administration" (PSPA) na ufaulu wake ukawa ni 3.2 GPA, shahada ya Uzamili akasoma "Development Studies". Kwa MNMA Mwalimu huyu anaweza kufundisha "Public Policy" kwa wanafunzi wa shahada. Mwalimu huyu ufaulu wake katika somo hili ulikuwa alama "C" wakati akisoma shahada ya kwanza, na shahada ya pili hakusoma somo hili. Hivyo unakuta Mwalimu wa huyo hajui anachokifundisha licha ya wanafunzi kulalamika.
Mfano hapo juu ni baadhi tu, ya wahadhiri waliopo hapa, wengi hawana sifa kama vyuo vingine. Ndio maana hata chuo chetu hakisikiki kutokana na aina ya walimu tulionao.
15. SERA YA MAENDELEO YA WAFANYAKAZI (STAFF DEVELOPMENT POLICY)
Maendeleo ya wafanyakazi ni motisha kwa wafanyakazi wenyewe, tokea mwaka 2005 chuo kianzishwe hakuna sera ya maendeleo ya wafanyakazi. Sera hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya taasisi. Kutokuwepo kwa sera hii wafanyakazi wamekuwa hawapelekwi shule, hivyo kufanya wafanyakazi wengi kuanza kusoma kwa kuibia.
Pia wapo wafanyakazi waliokataliwa kwenda kusoma kwa madai kuwa utendaji kazi wao hauridhishi.
Tokea mwaka 2005 mpaka leo, mfanyakazi mmoja tu ndiye aliyeweza kuhitimu shahada ya Uzamivu, tena kwa juhudi binafsi, kwani chuo kilikuwa kinamlipia ada tu.
Miaka nane wa uwepo wa Mkuu wa chuo huyu ni mfanyakazi mmoja tu ambaye amepata PHD, japo hata yeye upandishwaji wake daraja umekuwa na shida kubwa.
16. MSAJILI WA KUWA MHADHIRI MWANDAMIZI (LECTURE)
Upandaji wa madaraja katika elimu ya juu upo wazi, Msajili wa chuo ameajiriwa na chuo kama afisa Tawala, baadae akapewa nafasi ya msajili. Msajili hana uzoefu wowote katika kufundisha na hajawahi andiko lolote kabla na hata akiwa mwajiriwa wa MNMA. Jambo la ajabu msajili sasa ametunikiwa cheo cha mhadhiri mwandamizi (Lecturer), pasi kuwa na sifa. Menejimenti imeidanganya bodi ya chuo, kwa kuumpa mshahara ambao sio stahili yake.
17. KAMATI YA UBORA YA CHUO
Ofisi hii imekuwa ni picha tu, wakuu wa idara hii wamekuwa wakilipwa posho za ukuu wa idara pasipokuwa na kazi yoyote. Tokea 2005 chuo kianzishwe kamati hii haijawahi kukaa kikao hata kimoja wakati ubora ndio suala muhimu katika mustakabali wa taasisi yetu.
18. MITIHANI KUTOSAHIHISHWA
Mwaka wa masomo 2011/2012 katika tawi la Zanzibar, ilibainika kuwa mitihani na majaribio ya somo la "Bookkeeping" haikusahihishwa, hivyo matokeo yalipikwa. Hii ilisababisha matatizo makubwa kwa wanafunzi kwani wengi walifeli somo hilo. Matokeo yaliyowekwa yalikuwa yamepikwa hivyo kuondoa uhalisia. Mwalimu wa somo husika hakuchukuliwa zozote.
Menejimenti ya chuo kwa kushirikiana, mkuu wa tawi Zanzibar na afisa mitihani, wa chuo walificha ukweli huku wakiwaacha wanafunzi wakipoteza haki zao. Suala hili lichunguzwe kwani limewasababishia wanafunzi kuapta alama zisizo kuwa zao.
19. UDAHILI WA WANAFUNZI
Udahili wa wanafunzi umekuwa ukishuka mwaka hadi mwaka, udahili huu umesababisha kushuka kwa mapato ya chuo. Kutoka wanafunzi 2235 mwaka 2010/2011 hadi wanafunzi 1742 mwaka 2012/2013.
Pia ofisi ya udahili imekuwa ikijihusisha na rushwa kwa kushirikiana na ofisi ya mitihani. Katika mwaka wa masomo 2012/2013 wanafunzi wa ngazi ya shahada 24 walikuwa hawana sifa. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya ofisi hiyo. Ili kuficha uovu kwenye ofisi ya udahili, mpaka sasa mafaili ya wanafunzi wote hayana kumbukumbu zao, hili linafanyika ili ionekane kuwa wanafunzi wote hawana kumbukumbu kama walioingia pasipokuwa na sifa.
Mh. Raiskuna maswala mbalimbali ya ukiukaji wa taratibu za mitihani, ukiukwaji huo umefanywa na Naibu Mkuu wa chuo, jambo la kushanga hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Afisa mitihani huyu naye achunguzwe kwani amekuwa akishirikiana na afisa udahili kufanya ufisadi. Pia ana tuhumiwa kutengeneza vyeti feki na kuwapa wanafunzi waliofeli.
20. OFISI YA UHASIBU
Ofisi ya uhasibu inakiuka taratibu nyingi za kifedha kwa kisingizio cha raslimali watu. Mh. Tunaomba ufanyie uchunguzi ofisi hii kwa kina utaona uozo uliopo. Kwasasa chuo kimemuongezea muda mhasibu mkuu aliyemaliza muda wake, hili lilifanyika ili muhasibu huyo aweze kuwafichia maovu. Pia kampuni inayofanya ukaguzi wa ndani imetiwa ndani ya mifuko ya wakubwa hawa. Suala la pre auditing halifanyiki kwa makusudi kabisa
21. PESA ZA PENSHENI
Mh, Pesa za Pensheni za michango ya wafanyakazi za mwezi wa Agosti (8) 2013 zimeliwa. Pesa hizi ni pesa halali za wafanyakazi, kutokana na ukata mkubwa uliokikumba chuo kwasababu ya ufisadi pesa hizo zimetumika kwa ajili ya vikao vya wakubwa. Serikali ilileta michango hiyo ya wafanyakazi.
22. AJIRA MPYA
Tunaishukuru Tume ya ajira kwa kuingilia kati mchakato wa ajira ambao chuo tayari kilikuwa kimefanya bulanda tayari, kwa kutaka kuajiri watu wasio na sifa. Baadhi ya wakuu wa idara ambao walipewa uwezo wa kushort list walikuwa wamekwisha pokea rushwa ya pesa wengine waliomba rushwa ya ngono, ushahidi upo. Ukitaka kupata ushahidi huo chukueni namba za simu za wakuu wa idara angalieni pesa zilizoingia kwa Tigo na M-pesa. Japo wapo waliopewa cash.
Mh. Raistunakuomba upitie madai yetu haya, jambo haya ni baadhi tu ya malalamiko ya wafanyakazi wa MNMA. Tuma watu wako waje wajionee uozo uliokidhiri na kupindukia. Kuna malalamiko ya mfanyakazi mmoja mmoja, pia ya vyama vya wafanyakazi.
Pia utakumbukua ulipokuja kututembelea chuo chetu, ulituambia kuwa tuko kimya sana, ukimya wetu ni matatizo yaliyokidhiri hapa kwetu. Pia viongozi wetu hawafanyi jitihada zozote za kusikikia kwa kuogopa tutaonekana, na viongozi wataweza kujua matatizo yaliyopo. Njia hii Mkuu wa chuo ameitumia sana ili kufanikisha adhima zake mbaya za kifisadi.
Natumaini ombi letu litafanyiwa kazi.
Sisi wafanyakazi
MNMA
Nakala kwa:
Ofisi ya Rais Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi source-matukio na michapo

waliotembelea blog