MALALAMIKO JUU YA MENEJIMENTI YA CHUO CHA KUMBUKUMBUKU YA MWALIMU NYERERE
1. SHERIA YA UANZISHWAJI CHUO
Mh.
Waziri Mkuu, sheria iliyopo ya uanzishwaji wa chuo inamapungufu kadha,
ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho. Mapungufu hayo ni:
i. Sheria haitaji sifa za mkuu wa chuo aweje
ii. Sheria haitaji sifa za Makamu Mkuu wa Chuo
iii. Sheria haitaji sifa za Msajili wa Chuo
iv. Pia
sheria inapigana na taratibu za NACTE ambazo zinataja uwepo wa Rector,
Deputy Rector Academic, Deputy Rector Adminstration.
v. Sheria Haitaji ukomo wa Msajili (registrar) imeiachia Bodi na Mkuu wa chuo suala la kuamua muda wa Msajili.
vi. Sheria inamtaja msajili kama Katibu wa kamati ya taaluma wakati yeye hahusiki na mambo ya taaluma.
vii. Kazi
za kamati zifuatazo Human Resource Development and Disciplinary
Committee, Finance and Planning Committee and Students' na Disciplinary
Appeals Committee hazitajwi na sheria, tofauti na kazi za kamati ya
taaluma ambapo kazi zake zimetajwa.
Mh.
Raistunakuomba sheria hii ya uanzishwaji wa chuo ipitiwe upya ili
kukidhi matakwa ya sasa na kuleta ufanisi wa kazi kwa ujumla.(P.T)
2. UWAKILISHI WA WAFANYAKAZI KATIKA BODI YA CHUO.
Pamoja na
sheria kusema kuwa kutakuwa na uwakilishi wa Wafanyakazi (The Mwalimu
Nyerere Memorial Academy Act, 2005 Ibara 6:1 (D Na G) katika bodi ya
chuo, Mkuu wa chuo amekuwa akimdanganya Waziri kwa kumpatia mapendekezo
ya majina ya wanataaluma na wafanyakazi kwa ujumla, ambao sio
wawakilishi halali. Suala
Mhe. Rais
tokea mwaka 2006 Bodi ya Chuo hakina wawakilishi wa wafanyakazi bali
wawakilishi hao huteuliwa kutokana na matakwa ya Menejimenti, hivyo
kufanya mawazo ya wafanyakazi kutowasilishwa kwenye bodi.
3. VIKAO VYA WAFANYAKAZI
Mh.
RaisTokea Mwenyekiti wa Bodi ateuliwe kwa muda wa miaka 8 sasa hajawahi
kufanya kikao na wafanyakazi. Suala hili limesababishwa na Menejimenti
ambayo kwa hakika imekuwa ikimficha Mh. Balozi ili kwa kumdanganya kuwa
mambo yanaenda. Hii imesababisha Mkuu wa Chuo kufanya vikao vichache
vyenye kututisha wafanyakazi na hivyo kushindwa kutoa mawazo yetu.
4. MALENGO YA CHUO
Mhe. Waziri Mkuu Kutokana na sheria ya chuo, Chuo kina malengo kumi na moja (11) kama ifuatavyo:
a) To provide facilities for study and training in social sciences, leadership and continuing education;
b) To conduct training programmes in the disciplines specified in paragraph (a);
c) to
engage in research and development in the disciplines specified in
paragraph (a) and to evaluate the results achieved by the Academy
training programmes;
d) To provide consultancy services to the public and private sectors in specified fields as prescribed in this Act;
e) To
sponsor, arrange, facilitate and provide facilities for conferences,
symposia, meetings, seminars and workshop, for discussion of matters
relating to social sciences, leadership and continuing education;
f) To conduct examinations and grant awards of the Academy as approved by the National Council for Technical Education;
g) To
arrange for publication and general dissemination of materials produced
in connection with the work and activities of the Academy;
h) To engage in income generating activities for effective financing and promotion of entrepreneurship;
i) To
establish and foster close association with the Universities and other
institutions of higher education and promote international cooperation
with similar institutions;
j) To do
all such acts and transactions as are in the opinion of the Governing
Board expedient or necessary for the proper and efficient discharge of
the functions of the Academy;
k) To
perform such other functions as the Minister or the Governing Board may
assign to the Academy, or as are incidental or conducive to the exercise
by the Academy of all or any of the preceding functions.
Mh.
Raiskati ya malengo hayo juu ni lengo malengo a, f na J kidogo yameweza
kufanyiwa kazi. Lakini malengo mengine yote hajawahi kufanyiwa kazi
tokea chuo kianzishwe mwaka 2005. Mh. Raisnaomba ufanyie uhakiki haya
tuandikayo juu ya malengo. Chuo kimebaki kuwa kama sekondari, hakuna
tafiti zinazofanyika wala ushauri wa kitaalamu unaoendelea.
5. MISHAHARA YA WAFANYAKAZI
Mh.
Raistunapenda kutoa masikitiko yetu juu ya mishahara ya wafanyakazi.
Kumekuwa na tatizo kubwa la ongezeko la mishahara ya wafanyazi wa kada
zote, wafanyakazi wamekuwa hawapandishwi madaraja kulingana na stahili
yao. Mshahara unapandishwa ni ule wa ongezeko la litolewalo na serikali,
lakini annual increment kwa wafanyakazi haipo kabisa. Hili limepelekea
wafanyakazi wanaoajiriwa siku za karibuni kulingana mishahara na
wafanyakazi wa zamani.
Mhe.
Makamo wa Rais suala hili linafanyika makusudi kabisa ili kuwakomoa
wafanyakazi, hatuwezi amini kuwa utawala hawajui juu ya suala hili.
Hivyo tunaomba ulifanyie kazi pia.
6. AJIRA ZENYE UTATA
Mh.
RaisKumekuwa na ajira zenye utata kwa wahadhiri watatu (3), utata huu
umefanywa na msajili sio kwa bahati mbaya, bali kwa maslahi binasfi.
a. Ajira
ya Ndugu Ernest Luambano: Mh Waziri Mkuu Ndugu Luambano aliajiriwa na
chuo mwaka 2004 akiwa na miaka hamsini (50) akiwa kama afisa tawala.
Ajira yake ilikuwa ni ya mkataba wa miaka 4, hivyo muda wa mkataba wake
ulikuwa uishe mwaka 2008. Lakini mwaka 2006 kwa kushirikiana na mkuu wa
chuo walirudisha umri wa Luambano nyuma yaani akaonekana amezaliwa mwaka
1959, basi kuandika tarehe. Baada ya kurudisha umri nyuma wameficha
mafaili ya ajira yake ya mwanzo ya mkataba na kufanya au kuingiza mwaka
1959 kama mwaka wake wa kuzaliwa, hivyo kuonekana kwamba aliajiriwa
akiwa na miaka 44 au 45.
Suala hili ni kinyume na taratibu za ajira katika ofisi za umma kama inavyoelekezwa na standing order ya mwa 2009;
D.33 Appointment on Contracts:
(1) A
candidate appointed to a pensionable post in the public service on
non-pensionable terms, or to a non-pensionable post, shall be required
to enter into a contract (on gratuity terms) specifying the terms of his
employment as provided for in Appendix D/V. Contracts on gratuity
terms, which shall be the normal form of engagement in such cases,
provide for the payment by Government of a gratuity at a prescribed rate
on satisfactory completion of the contract.
(2) Under
special circumstances, certain persons may be engaged in the public
service to serve on contract terms. These shall include:
(a) a non-citizen who is engaged for some projects or on expatriate requirements;
(b) a citizen from outside the public service who is engaged to the Service under expatriate or consultancy requirements;
(c) a retired public servant who has been re-engaged in the Service; and
(d) a citizen who is first appointed to the Public Service after he has attained the age of 45 years.
(3) Where
it is in the opinion of the appointing authority that a public servant
be re-engaged on further terms of contract, the appointing authority
shall notify the Permanent Secretary (Establishments) who shall forward
to the Chief Secretary with recommendations.
D.34 Completion and Renewal of Contracts:
(1) The
Chief Executive Officer shall inform the public servant three months
before the expiry of the contract, whether or not he wishes to re-engage
him for further period of service. Similarly the public servant serving
on contract shall notify his Chief Executive at least three months
before the engagement is due to expire whether or not he wishes to be re
– engaged, for a further period of service.
(2)
Approval of the Appropriate Appointing Authority to be sought: On
receipt of the notification referred to in paragraph (1), the Chief
Executive Officer shall forward his recommendation regarding the
re-engagement of the public servant concerned to the appropriate
authority for approval.
(3) The
Chief Executive Officer shall not initiate or seek the approval of the
re-engagement of a public servant in contract unless:-
(a) There are special resources and arrangements of training of counter parts and successors in such post; and
(b) There
is a special provision in the contract obliging the employee in
contract to impart his knowledge to the counterparts and successors.
(4)
Re-engagement of a contract employee without consideration of the
requirements under paragraph (3) shall only be made by an approval of
the Chief Secretary.
D.39 Age of admission to a Pensionable Establishment:
Appointments
to the pensionable establishment shall be restricted to persons of and
below the age of 45 years who would be in a position to complete the
fifteen years' service required to qualify for the grant of a pension on
reaching the compulsory age of retirement. There shall be special
circumstances which may justify variations in the application of the
general principle, and such cases shall be submitted for consideration
of the Permanent Secretary (Establishments).
Katika
suala hili, bodi ya chuo ilidanganywa na Mkuu wa chuo kwa makusudi ili
bwana Luambano apate ajira ya kudumu. Hivyo Mh. Dr. Salim hajui lolote
juu ya hili kwani alidanganywa.
Tunakumba
Mh, ufanyie kazi hili suala kwa haraka, kwani Msajili amekuwa tatizo
katika taasisi, ajira zote zinazofuata hapa nchini yeye ndiye mhusika
mkuu wa kuzitengeneza. Kwasababu na yeye amegushi. Wafanyakazi
hatutakubali kuendelea kufanya kazi na mtu ambaye amegushi umri, lakini
pia akikabiliwa na tuhuma lukuki za ufisadi.
Hivi sasa
Mkuu wa chuo na Msajili wanahaha kuficha ukweli wa mambo kwa
kutengeneza na taarifa mbalimbali na kupoteza ushahidi juu ya hili,
lakini ni tumaini letu kuwa serikali ina mkono mrefu itaufikia ukweli
pasipo kumuonea mtu.
b. Ajira
ya Mhagama: Huyu alikuwa mwajiriwa wa chuo kabla ya kujiuzuru mwaka
2012. Ilikuwa ikifahamika tokea alipoajiriwa kuwa ana vyeti visivyo
halali. Lakini chuo kiliendelea kumulinda pasipo kufanyia kazi. Baadae
chuo kilimpeleka kusoma shahda ya uzamili chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Baada ya
kumaliza, chuo kikuu cha Dar es Salaam kilimnyima cheti, japo Msajili
alimpandisha mshahara pasipokuwa na vyeti na kumlipa mshahara wa kiwango
cha Uzamili. Suala hili liliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari
na mitandao ya jamii. Walipoona kuwa Mhagama anasakamwa Msajili
alimshauri ajiuzulu, wakati wa kujiuzulu alilipwa hela ya likizo. Pamoja
na sheria kuwa wazi, juu ya mfanyakazi anayeacha kazi ndani ya masaa
24, kutakiwa kulipa mshahara wa mwezi mmoja kwa mwajiri bw Mhagama
hakufanya hivyo.
Suala
hili lilichunguzwa na Ofisi ya Rais Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma, jambo la kushanga taasisi hii ilikisafisha chuo kwamba hakukuwa
na shida. Mambo la kujiuliza hapa:
i. Mhagama aliajiriwa lini Mwalimu Nyerere?
ii. Menejimenti ya Mwalimu Nyerere alijua lini suala hili la Mhagama kufoji vyeti?
iii. Baada ya kugundua Menejimenti ya Mwalimu Nyerere ilifanya nini?
Tukijibu
maswali haya unagundua kuwa hata Ofisi ya Rais Sekreatieti ya Maadili ya
Viongozi wa haikufanya kazi yake ipasavyo. Haiwezekani suala hili
ligundulike miaka miwili nyuma, pasipo kuchukuliwa hatua (ushahidi upo).
Hata baada ya kulitambua hili hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
c. Ajira
ya Bi Sara Mwakyusa: Muhadhiri huyu alipewa mkataba wa mwaka mmoja
ilikufundisha Tawi la Zanzibar. Menejimenti ilitambua kuwa huyu mhadhiri
ni muajiriwa wa manispaa ya Ilala shule ya Sekondari Azania, iliamua
kuumpa mkataba wa ajira ya mwaka mmoja, huku menejimenti ikijua ni kosa
kisheria.
d. Ajira
ya Bwana Rodgiers Kiowi, mwaka 2010 chuo kilimuajiri ndugu Kiowi kama
mhadhiri Msaidizi, wakati kikijua kuwa ni muajiriwa wa Taasisi ya
Teknolojia ya Dar es Salaam. Tunasema chuo kilijua kuwa ni mwajiriwa wa
DIT kwa ushahidi wa kimazingira.
i. Tokea
aingie hajawahi kuingizwa kwenye payroll ya hazina na sasa ni muda wa
miaka mitatu. Kwanini ichukue muda mrefu kiasi hicho wakati Hazina na
MNMA ni viko karibu kama ni suala la ufuatiliaji.
ii. Pili,
suala hili menejimenti ilifahamishwa na afisa mitihani aliyejiuzulu,
lakini haikuchukua hatua badala yake alihudhuria kikao cha kamati ya
taaluma.
iii. Mpaka sasa hajafunguliwa mashtaka ya kuiibia serikali.
Kwa
ushahidi huu hakika Menejimenti ya chuo inajua suala hili, ndio maana
msajili amekuwa akitoa ushauri wa kiupotoshaji kwa mkuu wa chuo, ili bw
Kiowi asichukuliwe hatua.
Mh.
Raistunaomba uchunguze ajira hizi tata ambazo kwa hakika zimetafuna pesa
za walipa kodi. Mfano Kiowi amekuwa analipwa mshahara na marupurupu
yote kwa mapato ya ndani na sio hazina kwa muda wote.
7. UJENZI WA CHUO ZANZIBAR
Mh.
Waziri Mkuu, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Mkuu wa Chuo amefanikiwa
kufanikisha kujenga Chuo Zanzibar, hili ni takwa la kisheria. Lakini
ujenzi huu kwa mujibu wa kamati ya huduma za jamii za Bunge hakukudhi
baadhi ya mambo. Licha ya Naibu Waziri wa Elimu kutoa agizo juu ya
kutofunguliwa kwa jingo hilo, menejimenti ya chuo ilimdanganya Mh. Salim
(Mkiti), likafunguliwa. Ufunguzi huo haukuhudhuriwa na kiongozi yeyote
wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi. Hii ni kutokana msigano
uliokuwepe kati ya menejimenti, Naibu Waziri wa Elimu na Kamati ya
kudumu ya huduma za jamii ya bunge.
Mh.
Raiskwa kuwa suala la ujenzi ni linaonekana, tunaomba utume watu wako
wakaangalie ujenzi ule kama umekidhi matakwa ya ujenzi.
8. UKARABATI WA NYUMBA YA MTU KUWA HOSTEL YA WANAFUNZI ZANZIBAR
Mh.
Waziri Mkuu, kuna suala ambalo linatia shaka, ambalo ni ukarabati wa
nyumba ya mtu kuwa hostel ya wanafunzi Zanzibar. Hii ilikuwa ni njia ya
kufanya ufisadi kwani haukufuata taratibu za kimanunuzi. Bahati mbaya,
kamati ya huduma za jamii yz bunge ilifichwa juu ya ukweli huu.
Yafuatayo hayakufanyika:
i. Menejimenti haikutanganza tenda ya kutafuta hosteli.
ii. Haikutangaza tenda ya zaidi ya shilingi 700 kwa ajili ya kukarabati jengo hilo.
iii. Pesa
zaidi ya shilingi 700 zingeliweza kuanzisha ujenzi wa hosteli ya chuo,
kuliko kinachofanyika sasa hivi kwa kulipa dola 20,000 kwa mwaka kwenye
jingo hilo.
Mh. Raishuu ni ufisadi mkubwa unaoendelea hapa, kwani hata bodi ya tenda haijui jambo lolote juu ya ujenzi huu
9. UJENZI WA HOSTELI YA KIGAMBONI
Mh.
Raissasa hivi chuo kinaendeleza ujenzi wa hosteli hapa Kigamboni, Ujenzi
huo uko kwenye awamu ya pili. Jambo la kushangaza katika awamu hii ya
pili hakuna tenda iliyotangazwa hii ni kinyume na taratibu. Mkandarasi
anayefanya kazi hii ni Yule Yule aliyejenga Zanzibar, aliyekarabati
hosteli ya wanafunzi Zanzibar.
Ujenzi wa
awamu ya pili haujulikani sehemu yoyote zaidi ya Mkuu wa chuo na
Msajili, bodi ya Tenda haikushirikishwa kwa jambo lolote.
10. MADENI YA NDANI
Mh.
RaisMadeni ya ndani ya yamezidi kuwa makubwa, wafanyakazi sasa wanadai
posho mbalimbali kama posho za nyumba na posho za nauli. Tokea mwezi wa
Saba posho hizi zimesitishwa pasipokuwa taarifa yoyote. Hakuna taarifa
yoyote iliyotolewa sababu ya kustisha posho hizi, japo tunasikia
tutalipwa mwezi wa kumi kwasababu sasa chuo hakina pesa.
Mh.
RaisWahadhiri hupata posho kwa ajiri ya kusimamia mitihani, kusahishisha
mitihani, Kusimamia tafiti za wanafunzi na vikao mbalimbali, mpaka sasa
wahadhiri nao hawajalipwa. Japo la kushangaza hakuna sababu yoyote
iliyotolewa. Sasa wahadhiri wanapanga kugoma kwa sababu ya posho zao.
Mh.
Waziri Mkuu, wafanyakazi hawawezi kuzungumza jambo lolote, kwasababu
mkuu wa chuo amekuwa akitumia vitisho kwa wafanyakazi kwamba yeye yuko
karibu na Rais, hivyo hakuna mtu anayeweza kumfanya lolote.
11. VITISHO DHIDI YA WAFANYAKAZI (KUACHA KAZI) UBABE
Mh.
Waziri Mkuu, kumekuwa na vitisho vya mara kwa mara kwa wafanyakati ambao
huonekana wanakwenda kinyume na matakwa maovu ya menejimenti. Tokea
mwaka 2005 wafanyakazi wengi sana wameacha kazi kwasababu ya kunyanyaswa
na menejimenti ya chuo.
Mh.
Raishili suala limekuwa likifichwa kwa mwenyekiti wa Bodi, akidanganywa
kuwa wafanyakazi hao wameacha kazi kwasababu zao binafsi, wakati sio
kweli. Mh. Raishili limesababisha mara kwa mara upungufu wa wafanyakazi
hapa chuoni.
12. MANUNUZI
Mh.
RaisSuala la manunuzi limekuwa tatizo kubwa hapa kwetu, msajili wa chuo
amekuwa ndiye muhusika mkuu katika manunuzi ya chuo, suala hili
limekubikwa misingi ya rushwa. Msajili ndiye afisa manunuzi ya chuo,
watu waliopo katika kaitengo cha manunuzi wao ni alama tu, hawafanyi
kazi zao. Japo wamekuwa wakishiriki kumfanikishia msajili mambo yake ili
yaonekane yamefata taratibu.
Suala
hili lilipelekwa PCCB, PCCB nao wamepewa rushwa na msajili, masjili
amekuwa na mawasiliano makubwa na afisa mmoja wa PCCB makao makuu. Afisa
huyo amekuwa akitoa siri za wapeleka taarifa, pia amekuwa akisaidia
kuficha maovu ya MNMA. Kwa uhakika zaidi juu ya suala hili naomba
uchunguze mawasiliano (simu) ya Msajili wa Chuo na maafisa wa PCCB
waliokuwa wanashughulikia masuala ya MNMA.
Pia
Taasisi ya PPRA baadhi ya maafisa wake wanatumika kuficha ukweli juu ya
tuhuma zinazopelekwa huko. Pia uchunguzi ufanyike juu ya mawasiliano
(simu) ya siri kati ya afisa mmoja wa PPRA na Msajili wa chuo.
13. MCHAKATO WA KUMPATA MWENYEKITI WA BODI NA MKUU WA CHUO
Mh.
RaisMkuu wa chuo amemuandikia Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi barua za tarehe 19 na 24 Julai aweze kumuomba Waziri wa Elimu,
akuombe umuungezee muda Dr. Salim Ahmed Salim. Hili tunakubaliana nalo
kabisa, sio kwamba Dr. Salim katenda makubwa, hapana ni kwasababu
tunaimani menejimenti haikumtumia ipasavyo. Tunaimani menejimenti mpya
ikiwekwa na Dr. Salim akaendelea kuwa Mwenyekiti, chuo chetu
kitabadilika sana, kuliko kilivyosasa.
Mh.
Raisitakumbukwa kwamba Mkuu wa chuo wa muda wake wa miaka miwili
uliyomuongezea unakwisha mwezi wa 12 2013. Jambo la kushanganza mpaka
sasa hakuna mchakato wowote ambao umeanzishwa kwa ajili ya kumpata mkuu
wa chuo mpya. Jambo hili linafanyika makusudi ili Kaimu Naibu Mkuu wa
Chuo aje akaimu ukuu wa Chuo. Kukaimu kwake kutakuwa kunatoa nafasi kwa
msajili wa chuo kuwa Mkuu wa Chuo kwa "remote".
Katika
suala hili, ni muendelezo wa Mkuu wa chuo kutotaka kufanya kazi na watu
wenye sifa na uwezo. Mfano Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo amekaimu nafasi hiyo
kwa muda wa mwaka mmoja na miezi miwili sasa. Mkuu wa chuo na amekataa
kuomba utumishi ili chuo kiajiri mtu mwenye sifa yaani mwenye Shahada ya
Uzamivu. Kwa kuwa Mkuu wa chuo na Msajili wanapenda watu wasiokuwa na
uwezo na ambao wanawasikiliza wao basi mchakato wa Naibu mkuu wa chuo
haukufanyiwa kazi.
Mh.
Raistunakuomba kwa dhati, uingilie mchakato huu, ili malendo yao ya
kukaa na kaimu mkuu wa chuo asiye na sifa yasiweze kufikiwa.
14. WANATAALUMA KUTOKUWA NA SIFA
Chuo
chetu kinakabiliwa na tatizo kuwa katika taaluma, wanataaluma waliowengi
hawana sifa ya kufundisha. Ajira zao zina utata mkubwa sana, hii
imesababisha wahadhiri wengi kutojiamini kwa kuwa hawana sifa za
kufundisha elimu ya juu. Taratibu za walimu wa elimu ya juu wanatakiwa
wawe na ufaulu angalau wa GPA ya 3.5 lakini wahadhiri wengi wako chini
ya hapo.
Pia
tatizo hili linatokea katika masomo ya ufundishaji, (specialization)
mfano Mhadhiri aliyesoma shahaha ya "Political Science and Public
Administration" (PSPA) na ufaulu wake ukawa ni 3.2 GPA, shahada ya
Uzamili akasoma "Development Studies". Kwa MNMA Mwalimu huyu anaweza
kufundisha "Public Policy" kwa wanafunzi wa shahada. Mwalimu huyu ufaulu
wake katika somo hili ulikuwa alama "C" wakati akisoma shahada ya
kwanza, na shahada ya pili hakusoma somo hili. Hivyo unakuta Mwalimu wa
huyo hajui anachokifundisha licha ya wanafunzi kulalamika.
Mfano
hapo juu ni baadhi tu, ya wahadhiri waliopo hapa, wengi hawana sifa kama
vyuo vingine. Ndio maana hata chuo chetu hakisikiki kutokana na aina ya
walimu tulionao.
15. SERA YA MAENDELEO YA WAFANYAKAZI (STAFF DEVELOPMENT POLICY)
Maendeleo
ya wafanyakazi ni motisha kwa wafanyakazi wenyewe, tokea mwaka 2005
chuo kianzishwe hakuna sera ya maendeleo ya wafanyakazi. Sera hii ni
muhimu sana kwa maendeleo ya taasisi. Kutokuwepo kwa sera hii
wafanyakazi wamekuwa hawapelekwi shule, hivyo kufanya wafanyakazi wengi
kuanza kusoma kwa kuibia.
Pia wapo wafanyakazi waliokataliwa kwenda kusoma kwa madai kuwa utendaji kazi wao hauridhishi.
Tokea
mwaka 2005 mpaka leo, mfanyakazi mmoja tu ndiye aliyeweza kuhitimu
shahada ya Uzamivu, tena kwa juhudi binafsi, kwani chuo kilikuwa
kinamlipia ada tu.
Miaka
nane wa uwepo wa Mkuu wa chuo huyu ni mfanyakazi mmoja tu ambaye amepata
PHD, japo hata yeye upandishwaji wake daraja umekuwa na shida kubwa.
16. MSAJILI WA KUWA MHADHIRI MWANDAMIZI (LECTURE)
Upandaji
wa madaraja katika elimu ya juu upo wazi, Msajili wa chuo ameajiriwa na
chuo kama afisa Tawala, baadae akapewa nafasi ya msajili. Msajili hana
uzoefu wowote katika kufundisha na hajawahi andiko lolote kabla na hata
akiwa mwajiriwa wa MNMA. Jambo la ajabu msajili sasa ametunikiwa cheo
cha mhadhiri mwandamizi (Lecturer), pasi kuwa na sifa. Menejimenti
imeidanganya bodi ya chuo, kwa kuumpa mshahara ambao sio stahili yake.
17. KAMATI YA UBORA YA CHUO
Ofisi hii
imekuwa ni picha tu, wakuu wa idara hii wamekuwa wakilipwa posho za
ukuu wa idara pasipokuwa na kazi yoyote. Tokea 2005 chuo kianzishwe
kamati hii haijawahi kukaa kikao hata kimoja wakati ubora ndio suala
muhimu katika mustakabali wa taasisi yetu.
18. MITIHANI KUTOSAHIHISHWA
Mwaka wa
masomo 2011/2012 katika tawi la Zanzibar, ilibainika kuwa mitihani na
majaribio ya somo la "Bookkeeping" haikusahihishwa, hivyo matokeo
yalipikwa. Hii ilisababisha matatizo makubwa kwa wanafunzi kwani wengi
walifeli somo hilo. Matokeo yaliyowekwa yalikuwa yamepikwa hivyo kuondoa
uhalisia. Mwalimu wa somo husika hakuchukuliwa zozote.
Menejimenti
ya chuo kwa kushirikiana, mkuu wa tawi Zanzibar na afisa mitihani, wa
chuo walificha ukweli huku wakiwaacha wanafunzi wakipoteza haki zao.
Suala hili lichunguzwe kwani limewasababishia wanafunzi kuapta alama
zisizo kuwa zao.
19. UDAHILI WA WANAFUNZI
Udahili
wa wanafunzi umekuwa ukishuka mwaka hadi mwaka, udahili huu umesababisha
kushuka kwa mapato ya chuo. Kutoka wanafunzi 2235 mwaka 2010/2011 hadi
wanafunzi 1742 mwaka 2012/2013.
Pia ofisi
ya udahili imekuwa ikijihusisha na rushwa kwa kushirikiana na ofisi ya
mitihani. Katika mwaka wa masomo 2012/2013 wanafunzi wa ngazi ya shahada
24 walikuwa hawana sifa. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya
ofisi hiyo. Ili kuficha uovu kwenye ofisi ya udahili, mpaka sasa mafaili
ya wanafunzi wote hayana kumbukumbu zao, hili linafanyika ili ionekane
kuwa wanafunzi wote hawana kumbukumbu kama walioingia pasipokuwa na
sifa.
Mh.
Raiskuna maswala mbalimbali ya ukiukaji wa taratibu za mitihani,
ukiukwaji huo umefanywa na Naibu Mkuu wa chuo, jambo la kushanga hakuna
hatua zozote zilizochukuliwa. Afisa mitihani huyu naye achunguzwe kwani
amekuwa akishirikiana na afisa udahili kufanya ufisadi. Pia ana tuhumiwa
kutengeneza vyeti feki na kuwapa wanafunzi waliofeli.
20. OFISI YA UHASIBU
Ofisi ya
uhasibu inakiuka taratibu nyingi za kifedha kwa kisingizio cha raslimali
watu. Mh. Tunaomba ufanyie uchunguzi ofisi hii kwa kina utaona uozo
uliopo. Kwasasa chuo kimemuongezea muda mhasibu mkuu aliyemaliza muda
wake, hili lilifanyika ili muhasibu huyo aweze kuwafichia maovu. Pia
kampuni inayofanya ukaguzi wa ndani imetiwa ndani ya mifuko ya wakubwa
hawa. Suala la pre auditing halifanyiki kwa makusudi kabisa
21. PESA ZA PENSHENI
Mh, Pesa
za Pensheni za michango ya wafanyakazi za mwezi wa Agosti (8) 2013
zimeliwa. Pesa hizi ni pesa halali za wafanyakazi, kutokana na ukata
mkubwa uliokikumba chuo kwasababu ya ufisadi pesa hizo zimetumika kwa
ajili ya vikao vya wakubwa. Serikali ilileta michango hiyo ya
wafanyakazi.
22. AJIRA MPYA
Tunaishukuru
Tume ya ajira kwa kuingilia kati mchakato wa ajira ambao chuo tayari
kilikuwa kimefanya bulanda tayari, kwa kutaka kuajiri watu wasio na
sifa. Baadhi ya wakuu wa idara ambao walipewa uwezo wa kushort list
walikuwa wamekwisha pokea rushwa ya pesa wengine waliomba rushwa ya
ngono, ushahidi upo. Ukitaka kupata ushahidi huo chukueni namba za simu
za wakuu wa idara angalieni pesa zilizoingia kwa Tigo na M-pesa. Japo
wapo waliopewa cash.
Mh.
Raistunakuomba upitie madai yetu haya, jambo haya ni baadhi tu ya
malalamiko ya wafanyakazi wa MNMA. Tuma watu wako waje wajionee uozo
uliokidhiri na kupindukia. Kuna malalamiko ya mfanyakazi mmoja mmoja,
pia ya vyama vya wafanyakazi.
Pia
utakumbukua ulipokuja kututembelea chuo chetu, ulituambia kuwa tuko
kimya sana, ukimya wetu ni matatizo yaliyokidhiri hapa kwetu. Pia
viongozi wetu hawafanyi jitihada zozote za kusikikia kwa kuogopa
tutaonekana, na viongozi wataweza kujua matatizo yaliyopo. Njia hii Mkuu
wa chuo ameitumia sana ili kufanikisha adhima zake mbaya za kifisadi.
Natumaini ombi letu litafanyiwa kazi.
Sisi wafanyakazi
MNMA
Nakala kwa:
Ofisi ya Rais Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi
source-matukio na michapo
0 maoni:
Post a Comment