Tuesday, December 10, 2013


Baana da Diamond kumkubari huyu jamaa Pia alifunguka 
maneno haya: ilikuwa ni juzi kwenye show yangu 
TCC chang'ombe.ambapo sikuwa na mwanangu,Nay true boy so
 ilinibidi niombe mtu mmoja kati ya mamia ya 
mashabiki waliokuwepo amwakilishe True boy kwenye
 music gani ndipo dogo akajitokeza na siku hiyo ndiyo...
  nimekubali kweli vipaji vya kweli vinatoka huku kwetu
 uswahilini, the kid is so talented saana,mbali na kuimba
 mule mule kama nay,lakin pia alijua kucheza na 
 mashabiki,kucheza na jukwaa, ni kama mzoefu wa majukwaa siku nyingi.

 

 
 
 
 
 
 







 

 
 mpaka wimbo unaisha kila mtu alikipenda
alichokishuhudia na kusuuzika na
 roho yake..i sarute you dogo
 










MECHI ya Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya
 Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kati ya 
Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ na Kenya ‘Harambee Stars’
 iliyopangwa kuanza Saa 7:00 mchana huu Uwanja wa Kenyatta, 
Machakos, imeahirishwa na sasa itachezwa Saa 12:00 jioni
 Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
1
Hii ndiyo hali halisi ya Uwanja wa Kenyatta, Machakos
6
Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na
 Kati (CECAFA), Nicholas
 Musonye amesema kwamba sababu ya kufikia hatua hiyo 
ni hali mbaya ya Uwanja wa Kenyatta
 kufuatia mvua kubwa iliyonyesha leo.
Makocha wa timu zote, Kim Poulsen wa Tanzania Bara
 na Adel Amrouche wa Kenya wamekagua
 Uwanja na kujiridhisha haufai kuchezewa, ingawa 
Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) 
alikuwa anashinikiza mechi hiyo ichezwe hapo hapo.
Lakini pamoja na Musonye kutoa uamuzi huo, 
 Nyamweya amewaamuru wafanyakazi wa Uwanja
 wachote maji uwanjani aking’ang’aniza mechi ichezwe hapo.
2
Amrouche kushoto akimbishia Nyamweya mbele ya Musonye

3
Kim Poulsen ameweka msimamo hachezi Kenyatta
 
4
 
5







Melfu waliokusanyika kuhudhuria misa ya wafu ya Mandela

Maelfu wamekaidi hali mbaya ya hewa na kufurika uwanja wa FNB kuhudhuria misa ya wafu ya rais mstaafu wa Afrika Nelson Mandela. Je una ujumbe wowote kwa watu wa Afrika Kusini?
Unaweza kuutuma kwenye ukurasa wetu wa  na kisha nitauweka hapa kwenye mtandao wetu wa Je uko Afrika Kusini? nini kinajiri huko mbali na misa hii kufanyika?

12:48 Stanley Kisaka aakiwa nchini Tanzania kupitia ukurasa wa  anasema kuwa ni kweli kabisa hatutakuwa na viongozi wazalendo kama MANDELA zaidi ya kupata viongoz wanaojipenda wenyewe MUNGU IBARIKI AFRIKA!!!!!
12:00 Obama: ''Hatutawahi kuwa na kiongozi kama Mandela duniani tena. Lakini nataka kuwashauri vijana kote Afrika na duniani kote kuhakikisha kuwa wanafuata nyayo zake Mandela.''


11:51 Obama :'Kumbukumbu za Mandela hunifanya kila siku kutaka kuwa mtu mwema na nataka kuwashauri vijana kuhakikisha kuwa wanafuata nyayo za Mandela'
1135 Obama: ''Asanteni sana kwa kuturuhusu kumuenzi Nelson Mandela, alikuwa mkombozi aliyetetea demokrasia na anaweza tu kufananishwa na marehemu Mahatma Ghandi. Ni vyema kumkumbuka Mandela kama mtu aliyejitolea sana na hakuogopa kushauriana nasi kuhusu maoni yake na hisia zake na kwa sababu Mandela aliweza kukubali kuwa mtu wa kawaida mtu ambaye aliweza kufanya makosa kama mwanadamu mwengine yeyote ule.''

Barack Obama kwenye misa ya wafu ya Mandela
11:31...Rais wa Marekani Barack Obama aanza kuhutubia wanachi wa Afrika Kusini wanaohudhuria misa ya wafu ya Mandela
11:15.....Dlamini Zuma, 'Tunamuenzi Madiba, alikuwa shujaa aliyekuwa tayari kusikiliza maoni ya watu wengine licha ya kukinzana na yake. Ni shujaa wa Afrika ambaye alijitolea kuikiomboa Afrika na juhudi hizo hazikuwahi kumuondoka daima hadi kifo chake.''
11:12 am Mwenyekiti wa tume ya Muungano wa Afrika Dr Nkosazana Dlamini Zuma anahudhuria umati wa watri kwenye misa hiyo


11:09 am: Denis bazira kutoka kahama Tanzania ameandika kwenye ukurasa wa facebook amesesma Mungu aiweke pahala pema roho ya shujaa na mkombozi wa Afrika. R.I.P MADIBA
11:05 Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemaliza kuhutubia umati wa watu waliokusanyika kwenye misa ya wafu ya Mandela

Ban Ki moon akihutubia watu uwanjan FNB
11:03 am Ban Ki Moon: ''Ni Muhimu sote kuendeleza sera za shujaa wetu Mandela''
11:00 Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anahutubia umati wa watu waliokusanyika katika uwanja wa FNB


Maelfu ya watu wanaendelea kuwasili katika uwanja mkubwa wa FNB mjini Johanessburg kwa ajili ya misa ya wafu ya hayati Nelson Mandela,
Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video
Misa ya kitaifa ya wafu kumuaga Hayati Nelson Mandela, inaendelea mjini Johannesburg Afrika Kusini.
Rais wa Marekani Barack Obama na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon watakuwa miongoni mwa viongozi wa dunia watakaohutubia muhadhara huo.
Viongozi hao pia watahutubia wananchi sawa na wajukuu wanne wa Mandela .
Maelfu ya watu wamehudhuria misa hiyo katika uwanja wa FNB.
Afrika Kusini imeandaa shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya siku ya kuzikwa kwake nchini Afrika Kusini siku ya Jumapili.
Misa ya leo ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya viongozi wa kimataifa iliyoshuhudiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.
Viongozi wengine Watakaohudhuria misa ya wafu ya Mandela:

Viongozi wanaohudhuria misa ya wafu ya Mandela

  • Rais wa Marekani Barack Obama
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
  • Rais wa Cuba Raul Castro
  • Rais wa Ufaransa Francois Hollande
  • Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
  • Rais wa Brazil Dilma Rousseff
  • Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Watu wengi wamekaidi hali mbaya ya hewa ambapo mvua kubwa imenyesha huku wakikusanyika uwanjani humo wakisubiri kwa muda mrefu kabla ya misa hiyo kuanza muda mfupi uliopita.
Waliohudhuria misa hiyo wamesemekana kuwa wenye furaha wakiimba nyimbo na kutaja jina la Mandela kwa shangwe unaweza kudhani ni mkutano wa kisiasa.
Misa hiyo itafanyika katika uwanja ambako Nelson Mandela alionekana kwa mara ya mwisho hadharani.
Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya uwanja ili kuzuia msongamano wa watu.
Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini.
Nelson Mandela
MARAIS 91 akiwemo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa viongozi wengine kutoka pembe zote ulimwenguni wanaotarajiwa kuhudhuria ibada ya wafu ya aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Jumanne mjini Johannesburg.

Huo unatarajiwa kuwa mkusanyiko mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika karne hii, ambapo marais wanne wa Amerika watahudhuria. Itakuwa pia mara ya kwanza kwa  marais wanne wa Amerika katika kipindi cha miaka 15 kuhudhuria hafla ya
aina hiyo kwa pamoja.

Rais Kenyatta aliondoka Kenya mwendo wa saa kumi na mbili jioni Jumatatu kuelekea Afrika Kusini. Kwa mujibu wa Chumba cha Habari cha Rais (PSCU), Rais Kenyatta aliyeandamana na mkewe Margaret aliagwa uwanja wa ndege na Naibu Rais William Ruto.

Mandela ameombolezwa ulimwenguni kote katika makanisa, misikiti na masinagogi na kupelekea maombolezo yake kuwa ya kipekee kuwahi kuunganisha makabila na dini zote ulimwenguni.

Maombolezo yake yanaweza kulinganishwa na ya aliyekuwa Rais wa Amerika J F Kennedy, aliyeuawa mnamo 1963, na yale ya Binti Mfalme Diana aliyefariki kwenye ajali ya barabarani mnamo Agosti 31, 1997. Mengine ni ya Papa John Paul wa Pili aliyefariki mnamo 2004 na kuombolezwa ulimwenguni kote.

Mazishi ya Mandela yatahudhuriwa na Rais Barack Obama na mkewe Michelle, waliokuwa marais George Bush, Bill Clinton na Jimmy Carter. Rais Obama, mkewe Michelle na aliyekuwa Rais George Bush na mkewe Laura waliondoka Jumanne Amerika kuelekea Afrika Kusini.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki-Moon pia atahudhuria.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu hatahudhuria mazishi ya Hayati Nelson Mandela kwa sababu ni ghali mno kusafiri hadi nchini Afrika Kusini, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari.

Awali, Bw Netanyahu alikuwa amefahamisha serikali ya Afrika Kusini kuwa angehudhuria mazishi hayo lakini akafutilia mbali safari hiyo katika dakika ya mwisho.

Kulingana na redio ya taifa la Israeli, waziri  huyo itatumia kiasi cha 7.0 milioni shekels ambazo ni sawa na Sh170 milioni kusafiri nchini Afrika Kusini pamoja na walinzi  wake:  “Uamuzi huo umeafikiwa kutokana na gharama kubwa ya usafiri kwani safari hiyo ilipangwa katika kipindi cha muda mfupi,” ikasema radio ya taifa, Haaretz.

Kiongozi huyo wa Israeli amekuwa akishutumia na raia wa nchi hiyo kuwa amekuwa akitumia zaidi ya dola $1 milioni kuendesha shughuli za kasri zake tatu. Vyombo vya habari vilidokeza kuwa kiongozi huyo hutumia fedha za walipa ushuru dola $23,000 kulipia maji  ya kujaza mabwawa ya maji.

Zaidi ya viongozi 70 kutoka kote duniani tayari wamethibitisha kuwa watasafiri kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mazishi ya hayati  Nelson Mandela.

Kwa upande wake, mbali na kuwa shujaa ulimwenguni, Mandela pia anaashiria mwanzo mpya Afrika kwa kuleta pamoja kwa mara ya kwanza kongamano kubwa la viongozi ulimwenguni kando na Umoja wa Mataifa au Umoja wa Afrika.

Maishani mwake hadi kufariki kwake, Mandela ameweza kuendeleza ulimwengu. Maisha yake, kuanzia kufungwa kwake gerezani, kuchukua hatamu ya urais, kustaafu, hadi kufariki kwake, kumefanyika wakati ambapo kuna maendeleo makubwa ya kiteknolojia.

Mbali na televisheni na redio, magazeti na mitandao ya kijamii imeeneza habari kumhusu kwa kiwango kikubwa. Teknolojia imewezesha ulimwengu kuweza kuomboleza kwa pamoja, huku kila mmoja akiweza kuamua kuhusu watu wanaostahili kuombolezwa kwa taadhima kuu.

Hadhi kubwa inayoonekana katika maombolezo ya Mandela, ikiwemo idadi kubwa ya viongozi wa kitaifa wanaotarajiwa kuhudhuria, huenda isifikiwe na viongozi wengine katika karne hii.

Mandela, ambaye amecha watoto sita, wajukuu 17 na vitukuu 14, atazikwa nyumbani kwao Qunu, Cape Mashariki, Jumapili, Desemba 15.

waliotembelea blog