Friday, October 31, 2014



Wachezaji wa timu za Boom FC na Vijana ya Ilala wakisalimiana kabla ya mchezo wao wa hatua ya 16 Bora ya michuano ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.

Kikosi cha timu ya Vijana ya Ilala kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na Boom FC katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha timu ya Boom FC kikiwa katika picha ya pamoja.

Mashabiki wa timu ya Boom FC, wakipiga ngoma wakati timu yao ikicheza na Vijana ya Ilala.

Nahodha wa timu ya Vijana Ilala (kushoto) akisalimiana na mwenzake wa Boom FC, kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.

Mshambuliaji wa timu ya Vijana Ilala, Matola Selemani, kushoto akiwania mpira na winga wa timu ya Boom FC, Nambongo Hussein katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.

Mshambuliaji wa timu ya Boom FC,Issac Tesha (katikati) akijaribu kufunga bao katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup

Winga wa timu ya Boom FC, akiwatoka mabeki wa timu ya Vijana ya Ilala katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.

Beki wa timu ya Vijana Ilala Ramadhani Yasini, (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa timu ya Boom Ally Kondo, katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.

Baadhi ya wadau wa Soka wakifuatilia mechi kati ya Tabata FC na Sifa Politan kwenye Uwanja wa Bandari.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Sifa Politan, Mathayo Edward (kulia) akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa timu ya Tabata FC, katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Bandari Dar es Salaam. Tabata ilishinda kwa Penati 4-3.

Mashabiki wa timu ya Sifa Politan wakishangilia timu yao.

waliotembelea blog