Tuesday, June 10, 2014



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzani, Mark Childres, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 9, 2014 kwa mazungumzo na utambulisho wa balozi huyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childres, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 9, 2014 kwa mazungumzo na utambulisho wa balozi huyo.
*************************************** 
BALOZI MPYA WA MAREKANI AJITAMBULISHA KWA MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS
Ikulu, Dar es Salaam: 2014-06-09 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amekutana na Balozi mpya wa Marekani, Mheshimiwa Balozi Mark Childress ambaye amefika ofisini kwa mheshimiwa Makamu wa Rais kwa ajili ya kujitambulisha.
Balozi Childress alimueleza Mheshimiwa Mkamu wa Rais kuwa, Tanzania ni nchi yenye uhusiano maridhawa na Marekani na kwamba katika kipindi chake kama Balozi atahakikisha uhusiano huu mzuri uliojengwa unadumishwa na kwamba, nchi hizi mbili zinazidi kuwa na maeneo ya kushirikiana hasa yanayolenga kuboresha maisha ya watu na kuwapatia maendeleo.
Balozi Childress pia alisema kuwa Tanzania imekuwa ikitumia kama mfano kufuatia kuonesha mabadiliko ya haraka katika miradi mbalimbali inayoendeshwa hapa nchini kwa ushirikiano na watu wa Marekani na akafafanua kuwa, kazi iliyoko mbele ni kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua zaidi na sio kurudi nyuma.
“Mheshimiwa Makamu wa Rais, kila nikipata fursa ya kukutana na wenzangu tumekuwa tukizungumzia suala la Tanzania kupiga hatua kwa haraka. Mna mambo mengi yaliyofanyika na kazi iliyopo ni kuendelea kupiga hatua pasipo kurudi nyuma,” alisema.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Balozi Childress kuwa, Tanzania ipo katika kipindi ambacho kinaonesha mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kwamba kazi ya serikali ya Tanzania ni kuhakikisha kuwa uchumi unakuwa na unasaidia vizazi vya sasa na vijavyo.
“Mtazamo wetu katika serikali ni kuwa Tanzania itapiga hatua kubwa katika miaka michache ijayo. Lengo letu ni kutazama kuwa ukuaji wa uchumi hauwi wa muda mfupi, tunatazama pia maendeleo kwa vizazi vijavyo.
Kuhusu suala la utunzaji mazingira, Balozi Childress alisifu hatua za Mheshimiwa Makamu wa Rais hasa katika kazi ya uhamasishaji upandaji miti na akasema, utunzaji wa mazingira ni jambo la muhimu ili kuifanya nchi yetu iweze kuendelea na isikabiliane na matatizo yanayotokana na mazingira kuharibiwa.
“Nakupongeza Mheshimiwa Makamu kwa kazi yako ya uhamasishaji utunzaji wa Mazingira. Usichoke kufanya hivyo maana unasaidia dunia,” Balozi Childress alisema.
Imetolewa na : Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam

Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki(EALA) Mh. Adam Kimbisa akitoa tamko la wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu sakata la kumvua madaraka spika wa bunge hilo wakati wa Mkutano uliofanyika katikamukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene.
 Mbunge wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki(EALA) Mh. Twaha Taslima akieleza jambo kwa waandishi wa Habari(Hawapo pichani)wakati wa Mkutano uliofanyika katikamukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO). Kushoto ni Katibu wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo Mh. Shy-rose Bhanji.
*************************************
BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KANDA YA TANZANIA (EALA-TZ)
TAMKO LA PAMOJA LA WABUNGE WA TANZANIA WANAOWAKILISHA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) JUU YA SAKATA LA KUTAKA KUMVUA MADARAKA SPIKA WA BUNGE HILO 0/06/2014

Sisi, Wabunge saba wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania (EALA-TZ), tunapenda kusisitiza msimamo wetu wa kutounga mkono jaribio la kutaka kumuondoa madarakani Spika wa EALA, Mh. Margaret Nantongo Zziwa.
Baada ya kutafakari kwa uangalifu na kwa umakini mkubwa kuhusu chanzo halisi cha hoja yenyewe ya kutaka kumuondoa Spika wa EALA madarakani, tuligundua mambo yafuatavyo:
1. Hoja hii haina maslahi ya Tanzania na iko kinyume na malengo ya ushirikiano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Tumebaini kuwa hoja yenyewe ni sehemu ya "mchezo mchafu" wa ajenda ya siri ya kujaribu kuweka mbele maslahi ya baadhi ya wanachama wachache wa jumuiya badala ya kuzingatia maslahi mapana ya EAC.
2. Tuhuma mbalimbali zilizotajwa dhidi ya Spika wa EALA kuhusu yeye kuonesha upendeleaji, ujeuri na mapungufu mengine ya uongozi zimegundulika kuwa hazina mashiko na wala mantiki .
3. Kitendo ambacho kimetushtua ni kuwa kumekuwa na majaribio kadhaa ya baadhi ya Wabunge wa EALA kutoka nje ya Tanzania na viongozi wa Sekretarieti ya EAC kutaka kulazimisha sahihi za baadhi ya Wabunge wa Tanzania zitumike kinyume na utaratibu kuunga mkongo Azimio tajwa (kitu ambacho tunakipinga kwa nguvu zote). Hii inadhihirisha kuwepo kwa ajenda ya siri katika sakata hilo dhidi ya maslahi ya Tanzania na jumuiya kwa ujumla.
4.            Kufuatia malumbano yaliyoibuka katika kikao cha Bunge cha mwezi Machi huko Arusha, sisi Wabunge wa Tanzania tulipokea maoni na masikitiko mengi kutoka kwa wana Afrika Mashariki na viongozi kwa ujumla wakitusihi kumaliza tatizo hili kwa njia ya amani na utulivu, lakini jitihada zetu ziligonga ukuta. Hatua hii ilizidi kutudhihirisha kuwepo kwa ajenda ya siri.
Ikumbukwe kuwa azimio la kutaka kumuondoa Spika madarakani awali lilipangiwa kuwasilishwa katika kikao cha Bunge la EALA cha mwezi Machi 2014 huko Arusha lakini liligonga mwamba baada ya kuibuka mabishano ya kisheria, hali iliyopelekea kuahirishwa kwa kikao hicho.
Hoja hii ililetwa tena kwenye vikao vingine vya EALA, lakini baada ya kutafakari kwa makini kuhusu chanzo halisi cha mzozo huu, idadi kubwa ya Wabunge kutoka Tanzania (7 kati ya 9) waliamua kwa pamoja kuipinga hoja hii kwani imekosa mashiko na haizingatii maslahi ya Tanzania na maslahi mapana ya jumuiya kwa ujumla.
Aidha, wabunge watatu wa EALA kutoka Tanzania ambao awali waliunga mkono hoja hii waliamua baadae kuipinga kwa kutoa sahihi zao kwa hiari yao wenyewe na walimwandikia barua Katibu wa Bunge wa EALA kumueleza maamuzi yao kwa mujibu wa utaratibu mnamo tarehe 29 Mei 2014. Barua hizo za Wabunge wa Tanzania wa EALA kutoa sahihi zao kwenye hoja hiyo zilipokelewa rasmi na Katibu wa Bunge.
Wabunge hao wa EALA kutoka Tanzania walitumia haki zao za kikanuni kuondoa sahihi zao kama inavyoeleza katika kanuni ya 9 (2) ya Kanuni na Utaratibu wa Uendeshaji wa Bunge (Rules of Procedure of the Assembly) inayosema: "Azimio la kumuondoa Spika madarakani halina budi kuambatana na sahihi zisizopungua nne kutoka kila nchi mwanachama."

Hoja yenyewe ya kumuengua Spika wa EALA ni batili kisheria kwa kuwa haikuwasilishwa Bungeni ndani ya siku 7 tangu ilipopelekwa kwa Katibu wa Bunge na pia imekosa sahihi za kuungwa mkono na wabunge wanne kutoka kila nchi mwanachama wa EAC kama kanuni zinavyotamka.
Uamuzi wa Wabunge wa EALA kutoka Tanzania kuondoa sahihi zao kwenye hoja hiyo ni lazima uheshimiwe na kila mtu kwa kuwa wanatekeleza haki yao ya kidemokrasia.
Tunaomba uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ngazi zote ikiwemo Sekretarieti ya jumuiya kuheshimu maamuzi ya Wabunge wa EALA kutoka Tanzania. Ikumbukwe kuwa hapo awali, wabunge wa 5 wa EALA kutoka Tanzania kati ya jumla ya wabunge wote 9 wa Tanzania walionesha kuunga mkono hoja hii. Baada ya kubaini kuwepo kwa “mchezo mchafu” na ajenda ya siri, Wabunge watatu wa EALA kutoka Tanzania waliondoa sahihi zao na hivyo basi kufanya idadi kubwa ya Wabunge kutoka Tanzania (7 kati ya 9) kuipinga hoja hii batili.
Wabunge wa EALA wameshapoteza muda mwingi, fedha na rasilimali nyingine mpaka sasa kwenye hoja hii isiyo na tija ya kujaribu kumng'oa madarakani Spika wa EALA. Sasa hatuna budi kuweka jitihada zetu kwenye kazi muhimu ya kutetea maslahi ya raia wapatao milioni 140 wa Afrika Mashariki.
Hatuwezi kuwahudumia raia wa Afrika Mashariki kwa kuweka mbele ajenda za siri na kujishughulisha kwenye siasa za malumbano. Wananchi wa Afrika Mashariki wanataka kuona faida halisi kutoka kwenye jumuiya yao. Tuna imani na Spika wa sasa wa Bunge la EALA kuwa ni kiongozi sahihi wa kuongoza Bunge hilo.
Tunaamini kuwa hakuna tija yoyote kwa Wabunge wa EALA kuendelea kupoteza fedha za walipa kodi wa Afrika Mashariki kwa kujadili hoja hii batili. Badala yake, Wabunge wa EALA wana kazi ngumu ya kusimamia maslahi ya wananchi wa jumuiya wanaotaka kupata elimu bora, maji safi na salama ya kunywa, uhakika wa chakula, afya bora, miundombinu ya kisasa na maendeleo ya kiuchumi -- siyo siasa za ulaghai.
Tunatoa wito pia kwa Wabunge wenzetu wa EALA kutoka nchi nyingine wanachama na kwa viongozi wa Sekreterieti ya EAC kutojihusisha na ajenda zozote za siri za kujaribu kumng'oa Spika wa sasa wa EALA aliyepo madarakani kisheria. Wananchi wa Afrika Mashariki wanastahili zaidi ya hayo.
Njia pekee ya kufikia maslahi yetu ya pamoja ni kwa kutumia ushirikiano, badala ya kuendekeza malumbano na siasa za chuki na kututenganisha.  Sisi Wabunge saba bado tunasisitizia AMANI NA UTULIVU kwani bila ya hivyo hakuna maendeleo na ustawi wa jamii.

Tamko hili limetolewa Dar es Salaam tarehe 9 Juni 2014 na Wabunge wafuatao:
Mhe. Adam Kimbisa, Mwenyekiti wa Wabunge wa EALA wa Tanzania
Mhe. Shy-rose Bhanji, Katibu wa Wabunge wa EALA wa Tanzania
Mhe. Charles Makongoro Nyerere, Mbunge wa EALA
Mhe. Maryam Ussi, Mbunge wa EALA
Mhe. Bernard Murunya, Mbunge wa EALA
Mhe. Twaha Taslima, Mbunge wa EALA
Mhe. Angellah Kizigha, Mbunge wa EALA                        
Mwenyekiti, Wabunge wa EALA wa Tanzania                  
Katibu, Wabunge wa EALA wa Tanzania                    
Mwanasheria, Wabunge wa EALA wa Tanzania     

Cameroon_2fb4e.jpg
Timu ya taifa ya Cameroon 'Indomitable Lions'
Cameroon sasa wameenda Brazil baada ya mzozo kuhusu marupurupu yao kutatuliwa.
Wachezaji hao , almaarufu 'Indomitable Lions' walikuwa wamesusia kuingia ndegeni hadi marupurupu yao yaongezwe.
Akiwemo nyota wao mshambuliaji wa Chelsea,
Samuel Eto'o, walikuwa wamegoma kuingia ndegeni hapo Jumapili asubuhi hivyo safari ikachelewa kwa zaidi ya saa 12.
Wachezaji hao walikuwa wakilalamikia kiwango cha fedha £61,000 ambazo walikuwa wamepangiwa kupewa wakisema hazingetosha.
Haijabainika vyema ni idadi gani walichoongezewa ndio wakakubali safari.
Hata hivyo rais wa shirikisho la soka la Cameroon Bw.Joseph Owona amesema 'baada ya kuweka kila kitu wazi ,mzozo huo umetatuliwa na sasa hamna tatizo'.
Tatizo lililopo sasa kwa masimba hao ni kupata mkakati madhubuti wa kukabiliana vilivyo na timu za kundi lao A ambamo wamo miamba ya soka wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.


Na Mwandishi Wetu

Bondia Mtanzania anaeshika boxrec namba moja nchini Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amerudi na ubingwa wa WPBF  nchini akitokeza Zambia ambapo alifanikiwa kumpiga kwa K,O mbaya sana bondia Mwansa Kabinga wa Zambia mchezo uliochezwa
Arthur Davis Stadium, Kitwe, Zambia
 
akizungumzia safari yake ya kuelekea kunyakuwa ubingwa huo alisema amepata tabu sana wakiwa njiani ambapo wame ondoka alhamisi usiku sana na kufika jumamosi asubui nchini Kenya ambapo alizuiwa kutokana na kuwa na passiport ndogo hivyo akufanikiwa kwenda Zambia walivyofika kenya waka ongea na Balozi wa Tanzania wa Kenya akawasaidia ata hivyo ndege waliyokuwa wapande ilikuwa imesha ondoka zamani

baada ya hapo kuna pesa flani walitakiwa waongeze wakaongeza kiasi kwa kudunduliza wakasafili mpaka Zambia

hata hivyo bondia huyo ni mchezo wake wa kwanza kucheza nje ya nchi tangia ajiunge na ngumi za kulipwa na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa huo ambao umemuweka katika ramani nyingine kabisa ya kimataifa zaidi


akitoa ahadi hiyo Mkuu huyo alisema watu wengi wanapenda mchezo wa ngumi hivyo kwa niaba ya serekali nitafanya jitiada nikupatie mchezo mmoja kwa ajili ya kutetea mkanda wako hata burundi ili uzidi kufahamika na kukuza kipaji chako

bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ajawa nyuma kuwashukuru makocha wake ambao wamemwezesha kufika hapo ambapo ni Habibu Kinyogoli 'Masta' Kondo Nassoro, Sako  Mtulya na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anamtafutia mapambano mbalimbali na humpa ushauli awapo ulingoni

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kocha ya makocha wa mpira wa miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Uzinduzi wa kozi hiyo ya wiki mbili utafanywa leo (Juni 10 mwaka huu) saa 6 mchana kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Makocha zaidi ya 20 wenye Leseni C kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki katika kozi hiyo inayoendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday Kayuni. Mkufunzi mwingine wa kozi hiyo anayetambuliwa na CAF ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi.



KANALI MWANAKATWE KUZIKWA LEO BABATI
Maziko ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati huo likiitwa FAT, Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe yanafanyika leo (Juni 10 mwaka huu) Magugu, Babati mkoani Manyara.
Kanali Mwanakatwe alifariki dunia Juni 7 mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu baada ya kuanguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach.
TFF imetoa ubani wa sh. laki tano kwa familia ya marehemu Kanali Mwanakatwe, na katika maziko hayo inawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Kanda ya Arusha na Manyara, Omari Walii.


AMBUNDO, SHIZA WATESA UHOLANZI
Wachezaji wa Tanzania walioko Uholanzi, Dickson Ambundo na Shiza Yahya wameanza kuonekana muda na waandaaji ya mashindano ya AEGON Copa Amsterdam.
Kwa mujibu wa wakala wa wachezaji wa Uholanzi, Denis Kadito, AEGON Copa Amsterdam ni mashindano ya kimataifa yanayoshirikisha timu kubwa kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni kwa wachezaji wa miaka chini ya 19.
Kwa Uholanzi, Ajax Amsterdam huwa lazima washiriki, na pia huwa kuna timu ya ridhaa inayotengenezwa kwa kuchagua “best talent” kutoka Uholanzi. Mchujo wa wachezaji hao kutengeneza timu ya kombaini, ulianza na wachezaji wasiopungua 1,000.

Kombaini hiyo inaitwa Men United na inafundishwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Ronald de Boer. Ronald e Boer ni pacha wa kocha wa Ajax (First team).
Ronald de Boer pia ni kocha wa wachezaji washambuliaji wa Ajax. Shiza na Ambundo waliingizwa kwenye mchujo na wakafanya vizuri, mwishoni wakaitwa kwenye timu ya wachezaji 18 waliotengeneza timu ya Men United. Hii ni mara ya kwanza wachezaji wasio Waholanzi kuingizwa katika timu hiyo.
Mashindano ya Copa Amsterdam yameanza juzi (Juni 8 mwaka huu) na yanaisha kesho (Juni 11 mwaka huu. Katika mashindano hayo kuna makundi mawili. Kundi A ni AFC Ajax (Amsterdam), Ajax Cape Town ( Afrika Kusini), Fluminense (Brazil), Hamburg SV (Ujerumani) wakati B ni Men United, Panathinaikos (Ugiriki), FC Aerbin (China) na Cruizero (Brazil).
Shiza na Ambundo wamecheza mechi zote tatu. Shiza amekuwa akicheza namba tatu wakati Ambundo anapiga namba tisa, saba na kumi na moja.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza Alhamisi Juni 12, Afrika inawakilishwa na Nchi 5.
Zipo Ghana, Nigeria, Ivory Coast, Cameroon na Algeria na kila Mwafrika angependa kuona Timu hizi zikivunja ule mwiko wa kukwama Robo Fainali na kuziona zikitinga kwa mara ya kwanza Nusu Fainali za Kombe la Dunia.

Mwaka 2010, huko Afrika Kusini, Ghana nusura watinge Nusu Fainali kama si ‘ushenzi’ wa Straika wa Liverpool, Luis Suarez, ambae alidaka Mpira Golini na kuinyima Ghana Bao la ushindi la wazi la Dakika ya mwishoni.
Mara nyingine pekee ambapo Afrika nusura itinge Nusu Fainali ni wakati Cameroon ilipoikaba England kwenye Robo Fainali na Gemu kwenda Dakika za Nyongeza 30 huko Italy Mwaka 1990 na kisha Senegal kutolewa kiume kwenye Robo Fainali za Kombe la Dunia la Mwaka 2002. 
Je huko Brazil nani ana nafasi bora?
Ghana na Nigeria zinatinga huko Brazil zikiwa na Makocha wenye Asili za Nchi zao ambao wanataka kuweka historia ya kuwa Makocha wa kwanza Waafrika kuzivusha Nchi zao hatua ya Makundi.
Ghana wanae Kwesi Appiah na Nigeria ni Stephen Keshi.
Ivory Coast, Algeria na Cameroon zote zina Makocha wageni.


Nigeria
Nigeria wapo Kundi F na wataanza na Iran na wana Kikosi kilichosheheni wazoefu na vipajikuanzia Kipa Vincent Enyeama hadi Sentafowadi Emmanuel Emenike anaechezea Fenerbahce ya Turkey.
Kiungo yupo John Obi Mikel wa Chelsea ambae Kocha Keshi anamtaka ashambulie zaidi badala ya kuwa nyuma kama anavyocheza Chelsea.

Ghana
Ghana wapo Kundi G na wataanza na USA ambayo waliibwaga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010.

Baada ya USA, Ghana wana kimbembe dhidi ya Germany na Portugal ya Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo.
Lakini Ghana ni Timu pekee Afrika yenye Vipaji asilia na safari hii wapo kina Asamoah Gyan, Ayew, Mtoto wa Abedi Pele anaechezea Marseille, KwadwoAsamoah wa Juventus, Kevin-Prince Boateng wa Schalke 04 na Mkongwe Michael Essien.

Ivory Coast

Ivory Coast ndio Timu iliyojaza Majina makubwa kupita yeyote Afrika na wapo chini ya Mfaransa Sabri Lamouchi mwenye asili ya Tunisia.
Wapo Ndugu wawili, Yaya Toure na Kolo Toure, wapo Gervinho, Didier Zokora, Winga wa zamani wa Chelsea, Salomon Kalou, Wilfried Bony na pia yupo Didier Drogba.
Majina yote hayo na mengine mengi yanacheza Klabu kubwa Ulaya.
Huko Brazil, Kundi la Ivory Coast lina Japan, Colombia na Greece.

Cameroon
Cameroon wapo Kundi A pamoja na Wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.
Wakongwe hao wa Afrika wako chini ya Kocha wa Germany Volker Finke na wameelekea huko Brazil baada ya Mgomo wa Masaa 12 Wachezaji walipogoma wakipinga Bonasi ndogo.
Ingawa wana Kikosi cha wazoefu kina Samel Eto’o, Kipa Charles Itandje, Alex Song na wengineo, matayarisho yao yameleta shaka kubwa.

Algeria

Wako chini ya Kocha kutoka Bosnia, Vahid Halilhodzic, na Wachezaji wao karibu wote ni wale wenye makazi huko Ulaya hasa France.
Kwa sasa mwenye Jina kubwa linalovuma kwenye Kikosi chao ni Kiungo wa Valencia Sofiane Fegouhli.

Wachezaji-Nani Nyota mpya?

Mbali ya Yaya Toure, ambae ndie Mchezaji Bora Afrika kwa Miaka Mitatu iliyopita na Didier Drogba na Samuel Eto’o ambao nao wamezoa Tuzo hiyo mara 5 kati yao katika Miaka 7 iliyopita, nani mpya anaweza kuibuka Nyota Mpya wa Afrika huko Brazil?


England players attempt CapoeiraSturridge and Welbeck were joined by Jack Wilshere, Adam Lallana and Fraser ForsterThe Manchester United forward learns the Brazilian martial art capoeira Liverpool striker Sturridge shows off his dancing movesEngland players attempt CapoeiraEngland players attempt CapoeiraEngland players attempt CapoeiraLiverpool striker Sturridge shows off his dancing moves

waliotembelea blog