Friday, October 17, 2014


Ligi Kuu England wikiendi hii baada ya wiki mbili kupisha Mechi za Kimataifa na Mabingwa Watetezi Manchester City ndio watafungua dimba Jumamosi wakiwa kwao Etihad.
City wataanza mapema Jumamosi kucheza na Tottenham Hotspur na kisha kufuata Mechi 6 zitakazoanza Saa 11 Jioni ambapo Arsenal watakuwa Nyumbani kucheza na Hull City na Chelsea Ugenini kucheza na Crystal Palace.

Jumapili zipo Mechi mbili moja ikiwa ya Liverpool wakiwa Ugenini kucheza na QPR.
Mechi pekee ya Jumatatu Usiku ni ile ya The Hawthorns pale West Bromwich Albion watacheza na Manchester United.


RATIBA - LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi Oktoba 18

14:45 Man City v Tottenham
17:00 Arsenal v Hull
17:00 Burnley v West Ham
17:00 Crystal Palace v Chelsea
17:00 Everton v Aston Villa
17:00 Newcastle v Leicester
17:00 Southampton v Sunderland

Jumapili Oktoba 19
15:30 QPR v Liverpool
18:00 Stoke v Swansea

Jumatatu Oktoba 20
22:00 West Brom v Man United


Luis Suarez ametunukiwa Buti ya Dhahabu na Bosi wake wa zamani huko Liverpool Kenny Dalglish na hapo hapo kuthibitisha yuko tayari kwa El Clasico huko Spain kwenye mtanange kati ya Barcelona na Real Madrid.Luis Suarez looks delighted as he receives the Golden Shoe award from Liverpool legend Kenny Dalglish
Suarez alitwaa Tuzo hiyo kwa kufunga Bao nyingi za Ligi Barani Ulaya, alipofunga Bao 31 kwenye Ligi Kuu England alipokuwa na Liverpool Msimu uliopita zikiwa ni idadi sawa na zile alizofunga Cristiano Ronaldo akiwa na Real Madrid kwenye La Liga.
Msimu huu, Luis Suarez amehamia Barcelona na hivi sasa anaelekea ukingoni kumaliza Kifingo chake cha Miezi Minne alichopewa na FIFA kwa kumng’ata Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwezi Juni.
The pair laugh and shake hands as Suarez, now at Barcelona, accepts the award in front of an audience
Kifungo cha Suarez kinamalizika baada ya Siku 10 na anaweza kucheza Mechi yake ya kwanza kwa Barcelona kwenye La Liga watakapoivaa Real Madrid hapo Oktoba 26, Mechi inayobatizwa Jina la El Clasico.
Alipoulizwa kama yuko tayari kuivaa Real, Suarez alijibu: “Ungeniuliza Wiki moja nyuma ningekuwa na wasiwasi lakini baada ya kuichezea Uruguay Mechi mbili Wiki hii nipo fiti. Nipo tayari kucheza na Real!”

waliotembelea blog