Najua kuna
watu wangu wanaopenda kufanya matembezi sehemu mbalimbali duniani iwe
kwa issue zao binafsi au hata kwa issue za kibiashara. Lakini ulishawahi
kujiuliza ni viwanja gani vya ndege vyenye mvuto zaidi duniani? na Africa viko vingapi?
Nimekutana na
stori kwenye mitandao ambao wenyewe wamefanya utafiti na kuja na orodha
ya viwanja 10 vya ndege vyenye mvuto wa kipekee kwa mwaka huu wa 2015 haswa ukiwa bado uko angani unakaribia kutua.
Kwenye list upo uwanja wa Queenstown Airport uliyopo New Zealand, uwanja wa McCarran Airport uliopo Las Vegas na uwanja wa Nice Cote D’Azur Airport uliopo Ufaransa. Na kwa Africa upo uwanja wa…!?
Hapa chini
nimekusogezea picha 10 za viwanja vya ndege vyenye mvuto zaidi duniani,
unaweza kuvitazama kujua uwanja gani wa ndege kutoka Africa umeingia.
1. Queenstown Airport, New Zealand.
2. Las Vegas McCarran Airport, United States.
3. Nice Cote D’Azur Airport, France.
4. Barra Airport, Scotland, UK.
5. St. Maarten Airport (Princess Juliana International), Caribbean.
6. Saba Airport (Juancho E Yrausquin), Caribbean Netherlands.
7. Billy Bishop Toronto City Airport, Canada.
8. Gibraltar Airport, UK.
9. London City Airport, UK.
10. Cape Town Airport, South Africa.
Unaambiwa uwanja namba 3 uliingia kwenye hii orodha mwaka 2014, uwanja namba 4 ulikuepo pia kwenye hii orodha mwaka 2013 na uwanja namba 5 ulikuwepo pia kwenye orodha ya viwanja vizuri zaidi duniani mwaka 2012 na hii ni mara ya pili kwa wao kuingia kwenye orodha hii.