Wednesday, August 19, 2015

Mshambuliaji  wa kimataifa wa Italia mwenye asili ya Ghana anayeichezea klabu ya Liverpool ya Uingereza Mario Balotelli ambaye amezoeleka kuingia katika headlines mbalimbali kuhusiana na tabia yake ya ukorofi na vituko vyake safari kaingia tena katika headlines ila sio kwa ukorofi au utukukutu.

Hii ni good news kwa mashabiki watoto wa mshambuliaji huyo kwani amekuja na Brand ya viatu vya mpira wa miguu na mipira, vifaa hivyo vitakuwa vinapatikana kwa ajili ya watoto, huku vikiwa vinastahili ya kipekee tofauti na tulivyozoea.
balo_ball_3411075b
Brand hiyo ya vifaa vya michezo ya Balotelli imetengenezwa na kampuni maarufu ya Kijerumani kwa utengenezaji wa vifaa vya michezo PUMA, vifaa hivyo vinastahili kama ya manyoya au nywele kama ambavyo Balotelli amekuwa akinyoa stahili ya kiduku katika kichwani kwake.


balo_boots_3411072b

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog