Thursday, April 16, 2015


VfL Wolfsburg 0 vs 2 Napoli Bao zimefungwa Gonzalo Higuaín dakika ya  15 na  Marek Hamsik dakika  23. 
Kipindi cha kwanza kilimalizika Napoli wakiongoza kwa bao 2-0 dhidi ya VfL Wolfsburg. Kipindi cha pili Napoli walifanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa Marek Hamsik dakika ya 64 na kufanya 3-0 Wolfsburg ambao walikuwa kwao kwenye mchezo huu. Bao la nne lilifungwa kwa kichwa na Manolo Gabbiadini dakika ya 76 kwa kuunganisha Krosi ya Lorenzo. Bao la Wolfsburg lilifungwa na Nicklas Bendtner dakika ya 80 na kufanya matokeo kuwa 4-1.Marek Hamsik dakika 23 akishangilia bao lake na kupongezwa na wenzie wa Napoli.
Mitanange ya leo Rafael Benitez

MATOKEO  YA MECHI ZA LEO


Sevilla                                                   2   vs. 1Zenit St Petersburg
Dnipro Dnipropetrovsk0    vs.0Club Brugge
Dynamo Kiev1    vs.1Fiorentina
Vfl Wolfsburg                                         1vs. 4Napoli



Diego Costa na Eden Hazard wameiongoza Chelsea kufikia ilipo mpaka sasa Kileleni kwenye Ligi Kuu England BPL Na sasa wapo kwenye Listi ya Wachezaji 6 wanaowania Tuzo hiyo.Straika wa England Harry Kane mwenye goli 19 mpaka sasa, Listi hiyo inahusishwa pia kuwemo Philippe Coutinho, Kipa wa Manchester United David de Gea na Mchezaji wa Arsenal fowadi Alexis Sanchez.
Luis Suarez ndie aliyekuwa mshindi wa Tuzo hiyo msimu uliopita na sasa akikipiga kwenye Klabu la Barcelona na jana amefunga bao mbili kwenye Klabu Bingwa Ulaya.
Tuzo hiyo itatolewa mwezi huu April 26.
Harry Kane - SpursEden Hazard - ChelseaAlexis Sanchez - ArsenalDiego Costa - ChelseaDavid De Gea - Man United.
PFA, Professional Footballers' Association, Chama cha Wachezaji wa Kulipwa wa England, kila Mwaka hutoa Tuzo hizi za Madaraja mawili, zile za Wakubwa na Vijana, na hao Wanne wanagombea Tuzo zote mbili kwa mpigo kwa vile Umri unawaruhusu na pia sababu ya ustadi wao.
Pamoja na Kane, Coutinho, Hazard na De Gea, kugombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka, pia wapo Winga wa Arsenal, Alexis Sanchez, na Straika wa Chelsea, Diego Costa.
Kwenye Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana, hao Wanne watajumuika na Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois, na Fowadi wa Liverpool, Raheem Sterling, kuiwania.
Kwa Eden Hazard, hii ni mara ya 3 kugombea Tuzo hii baada ya kubwagwa na Gareth Bale na Luis Suarez.
Ikiwa David De Gea atatwaa Tuzo hii, basi itakuwa mara ya kwanza kwa Golikipa tangu Kipa wa England, Peter Shilton, kuitwaa Mwaka 1977.

(PFA) WACHEZAJI BORA WANAOWANIA TUZO HIYO YA MWAKA NI:-
1. Eden Hazard

2. Harry Kane
3. Alexis Sanchez
4. David De Gea

5. Philippe Coutinho
6. Diego Costa

MCHEZAJI BORA KIJANA WA MWAKA

Thibaut Courtois (Chelsea)
Philippe Coutinho (Liverpool)
David De Gea (Manchester United)
Eden Hazard (Chelsea)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)
Raheem Sterling (Liverpool)


LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Ijumaa Aprili 17

Stand United vs JKT Ruvu
Jumamosi Aprili 18
Polisi Moro v Ndanda FC
Mbeya City v Simba
Azam FC v Kagera Sugar
Jumapili Aprili 19
Ruvu Shooting v Mgambo JKT
 

MSIMAMO ULIVYO KWA SASA:


Yanga, Wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia kwenye michuano ya Klabu Barani Afrika, Jumamosi wapo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Etoile du Sahel ya Tunisia katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.Yanga imetua hatua hii baada ya kuzibwaga BDF XI ya Botswana na FC Platinum ya Zimbabwe katika Raundi za awali.
Akizungumzia Mechi hii, Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema ni muhimu kushinda Mechi hii ya Nyumbani na pia kuwa makini na staili ya kupoteza muda ambayo Etoile du Sahel wanategemewa kuitumia.Yanga inatarajiwa kuwatumia tena Wachezaji wao muhimu ambao walikuwa Majeruhi ambao ni Salum Telela na Coutinho.
Etoile du Sahel inatarajiwa kutua Dar es Salaam leo hii kwa Ndege ya kukodi.

CAF KOMBE LA SHIRIKSHO
Mechi za Kwanza Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Mechi kuchezwa Wikiendi ya Aprili 18

Association Sportive Olympique de Chlef vs Club Africain
Djoliba AC vs Hearts of Oak
Young Africans vs E.S. Sahel
Royal Leopards vs AS Vita Club
Onze Createurs vs ASEC Mimosas Abidjan
Warri Wolves vs Etanchéité
CF Mounana vs Orlando Pirates
Al Zamalek vs Fath Union Sport de Rabat

Marudiano Wikiendi ya Mei 5

Washindi 8 wa Raundi hii watajumuika na Timu 8 zilizobwagwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na kuwekwa kwenye Droo maalum kupanga Mechi 8 za Mtoano na Washindi wake 8 kutinga hatua ya Makundi ambayo yatakuwa na Makundi mawili ya Timu 4 kila mmoja yatakayocheza Mtindo wa Ligi wa Nyumbani na Ugenini.


Balozi Henry Mdimu akiongea na vyombo vya habari
Taasisi isiyo ya ki serikali ya Imetosha Foundation inayopinga unyanyapaa, ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu, inatarajia kutuma ujumbe mzito kanda ya ziwa hapo kesho kwa maandalizi ya ujio wa timu nzima ya taasisi hiyo iliyojikita kwenye kubadilisha mtazamo (mind set) wa watu juu ya janga hili. Ujumbe huo utaongozwa na mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw Masoud Kipanya, Balozi Henry Mdimu Mgaya na katibu Salome Gregory,wajumbe watakaongozana na viongozi hao ni pamoja na Mkala Fundikira, Isaya Mwakilasa (wakuvwanga aka Baba Andunje) Zaytun Biboze, Kelvina John na msanii wa muziki wa reggae Jhikoman Manyika.

Mwenyekiti Masoud Kipanya akiongea katika kilele cha matembezi ya hamasa yaliyofanyika jijini Dar
Dhumuni la safari hiyo itakayoupeleka ujumbe huo mpaka mkoani Shinyanga ni kwenda kujitambulisha kwa viongozi wa serikali na usalama wa mikoa na za kanda hiyo iliyoathiriwa sana na janga la ukatili na mauaji ya watu wenye ualbino. Taasisi ya Imetosha imepanga kwenda kanda ya ziwa baadaye mwezi ujao ambapo timu itaenda maeneo yaliyoathiriwa na kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo hayo kuwa si kweli kwamba ukiwa na kiungo cha mtu mwenye ualbino utapata mafanikio, elimu hizo zitatolewa kwa njia ya filamu mbali mbali, michezo ya kuigiza na matamasha ya muziki.

Hoteli ya Green Palm utakapofikia ujumbe wa Imetosha Foundation jijini Mwanza aka the Rock City.
Ujumbe huu ukiwa mjini Mwanza utakuwa chini ya udhamini wa hoteli ya Green Palm iliypo maeneo ya Bwiru, vile vile kampuni ya Mwananchi communication ltd (MCL) inayozalisha gazeti bora la Mwananchi na mengineyo itachapisha habari zote kuhusiana na msafara huo wa Imetosha kanda ya ziwa. Meneja wa hotel .

Isaya Mwakilasa wa (Orijino komedi) Henry Mdimu na familia ya Isaya aka Wakuvwanga


EUROPA LIGI, Mashindano makubwa ya pili kwa Klabu Barani Ulaya, Alhamisi yanaingia hatua za Robo Fainali kwa Mechi zake za kwanza kuchezwa.
Kama ilivyo kwa UEFA CHAMPIONS LIGI, England haina hata Timu moja kwenye hatua hii baada ya Everton na Tottenham kutupwa nje hatua iliyopita.

Mabingwa Watetezi, Sevilla ya Spain, bado wamo kwenye Mashindano haya na wanaanza Nyumbani katika Mechi na Klabu ya Urusi, Zenit St Petersburg.
Italy inazo Klabu 2, Fiorentina na Napoli.

EUROPA LIGI
Robo Fainali
Alhamisi Aprili 16

22:05 Club Brugge vs Dnipro Dnipropetrovsk
22:05 Dynamo Kiev vs Fiorentina
22:05 Sevilla vs Zenit St Petersburg
22:05 VfL Wolfsburg vs Napoli 


Marudiano
22:05 Dnipro Dnipropetrovsk vs Club Brugge
22:05 Fiorentina vs Dynamo Kiev
22:05 Napoli vs VfL Wolfsburg
22:05 Zenit St Petersburg vs Sevilla

waliotembelea blog