Thursday, August 13, 2015

LIGI KUU ENGLAND

RATIBA:
Ijumaa Agosti 14

21:45 Aston Villa vs Man United

Jumamosi Agosti 15
14:45 Southampton vs Everton
17:00 Sunderland vs Norwich
17:00 Swansea vs Newcastle
17:00 Tottenham vs Stoke
17:00 Watford vs West Brom
17:00 West Ham vs Leicester
Jumapili Agosti 16
15:30 Crystal Palace vs Arsenal
18:00 Man City vs Chelsea

Jumatatu Agosti 17
22:00 Liverpool vs Bournemouth


MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema Jack Wilshere atarejea Uwanjani baada ya Wiki 2 baada ya kujiuguza Enka yake lakini Kiungo wao mwingine Tomas Rosicky atakuwa nje kwa Miezi Miwili baada ya kupasuliwa Goti lake.
Wilshere, mwenye Umri wa Miaka 23, aliumia Enka ambayo ilipata ufa kwenye mfupa wake Mazoezini hapo Agosti 1 na ilidhaniwa atakuwa nje kwa kipindi cha hadi Miezi Miwili.
Lakini Wenger amesisitiza wao walitegemea atapona ndani ya Wiki 4 na kwa sasa mambo yako sawa.
Akiongea na Wanahabari kabla Arsenal kucheza Ugenini na Crystal Palace hapo Jumapili kwenye Mechi yao ya pili Ligi Kuu England baada ya kuchapwa 2-0 katika Mechi yao ya kwanza na West Ham, Wenger amesema: “Tulisema Jack atakuwa nje kwa Wiki 4 na sasa ni Wiki ya pili.”

Lakini habari si njema kwa Kiungo wao Rosicky mwenye Miaka 34 ambae aliumia wakati akiichezea Nchi yake Czech Republic dhidi ya Iceland kwenye Mechi ya Makundi ya EURO 2016 Mwezi Juni ambae sasa amefanyiwa operesheni ya Goti na Wenger kuthibitisha atakuwa nje kwa muda mrefu unaodhaniwa kuwa Zaidi ya Miezi Miwili.


FIFA Leo imetoa tamko la kumzodoa Meneja wa Chelsea Jose Mourinho baada kumtupa nje kusimamia Timu ya Kwanza Dokta wao Mwanama Eva Carneiro kwa kuingia Uwanjani kumtibu Mchezaji alieumia.
Profesa Jiri Dvorak, Daktari Mkuu wa FIFA, ametamka kuwa Mameneja hawana haki yeyote kuwaambia Matabibu wao waingie Uwanjani au la kumtibu Mchezaji alieumia kwani jukumu hilo ni la Dokta aliepo Uwanjani.

Jumamosi iliyopita Uwanjani Stamford Bridge Dokta Carneiro na Tabibu wa Viungo Jon Fearn waliingia Uwanjani kumtibu Eden Hazard kwenye Dakika za Majeruhi wakati Chelsea ipo 2-2 na Swansea City huku wakiwa Mtu 10 baada ya mapema Kipa wao Thibaut Courtois kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Kitendo hicho kilimkera Mourinho kwani Mchezaji akihudumiwa na Madokta basi huwajibika kutoka nje ya Uwanja na husubiri amri ya Refa kuingia tena huku Gemu ikiendelea na hilo liliiacha Chelsea iwe Mtu 9 kwa Dakika kadhaa.

Ingawa Dokta Carneiro na Msaidizi wake waliingia Uwanjani baada ya ishara ya Refa na pia kuitwa na Hazard mwenyewe, baada ya Mechi, akiongea kwenye TV, Mourinho alimponda Dokta huyo bila simile na kumsema hajui mchezo unakwendaje.
Kisha zikaibuka ripoti kuwa Mourinho ameamua kumzuia Dokta Carneiro kuhudhuria Mechi na Mazoezi ya Timu ya Kwanza ya Chelsea.
Jambo hilo limezua mjadala mkubwa huko England na wengi kumponda Mourinho.
Leo, Profesa Dvorak amesema Meneja hana wajibu wowote Mchezaji akiumia: “Kitaaluma, kitabibu, Meneja hana sauti. Hiyo ndio Sheria yetu Kitaaluma, na wajibu wetu kimaadili, kumwangalia Mchezaji tu.”
Profesa Dvorak pia ametamka Daktari ni lazima awe Benchi na anaruhusiwa kuingia Uwanjani hata bila ya ridhaa ya Refa kama akiona Mchezaji amekumbwa na tatizo la moyo au ameumia kichwani au amepoteza fahamu.
Profesa Dvorak amenena: “Hapo ni uamuzi wake Dokta na FIFA Siku zote itamuunga mkono.”


Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva wa tatu kutoka kushoto akiwa na Washindi wa bahati nasibu Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup ImanKajula kushoto na Msemaji wa Timu hiyo Manara Rais wa Simba Evans Aveva Akikabidhi Zawadi kwa Mmoja wa Washindi. Uongozi wa klabu ya Simba leo umetoa zawadi kwa washindi wa bahati na sibu iliyochezeshwa siku ya Simba Day Aosti 8 mwaka huu wakati wa kilele cha sherehe za siku ya Simba Day zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Zawadi zilizo kabidhiwa kwa washindi ni jezi pamoja simu


David De Gea hatarudi kwenye Kikosi cha Manchester United dhidi ya Aston Villa hapo Ijumaa huko Villa Park kwa mujibu wa Meneja Louis Van Gaal.
Kipa wa Kimataifa wa Argentina Sergio Romero ataendelea kuwa Golini kama alivyofanya Jumamosi iliyopita huko Old Trafford Man United ilipoifunga Tottenham 1-0 katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Msimu mpya wa 2015/16.
Hivi sasa Kipa David De Gea yupo kwenye sakata kubwa la kutaka kuhamia Real Madrid huku Man United ikitia ngumu na kutaka kitita kikubwa.
Kwenye Mahojiano hayo ya Leo yaliyofanyika huko Carrington kwenye Kituo cha Mazoezi cha Man United kuzungumzia Mechi yao ya pili ya Ligi hapo Kesho, Van Gaal alisema msisitizo wao mkubwa ni kushinda Mechi za Ugenini tofauti na Msimu uliopita ambao ulikuwa Msimu wake wa kwanza tu ambapo walishinda Mechi 6 tu.
Van Gaal ameeleza kuwa Msimu uliopita wao walikuwa bora Nyumbani Old Trafford na rekodi hiyo iliwafanya wawe wa 3 katika Timu zilizofanya vizuri Nyumbani kwenye Ligi.
Meneja huyo pia alihojiwa kuhusu matamshi ya Straika wa zamani wa Barcelona Hristo Stoichkov ambae amemtaka Pedro kutohamia Man United kwa sababu yake yeye Van Gaal.
Stoichkov, aliecheza chini ya Van Gaal katika Miaka ya 1990 huko Barca, amedai Van Gaal huzibomoa Klabu kwa sababu ya uduni wake.

Van Gaal alijibu: “Siku zote humtazama nani kasema maneno na kisha najua kwa nini. Hainisumbia. Yeye ndie alikuwa Mchezaji wa kwanza kumtosa [kumuuza] na ndio maana anasema hivyo.”
Huku Manchester City na Chelsea wakipambana huko Etihad hapo Jumapili, Waandishi walidokeza kuwa ushindi kwa Man United Ijumaa huko Villa Park utawafanya wachepuke haraka mbele ya Vigogo hao lakini Van Gaal alisema: “Ushindi utatupa mwanzo mzuri kupita Msimu uliopita. Lakini ni mapema na Msimu ni mrefu.”
Kuhusu Javier Hernandez ‘Chicharito’, Van Gaal alieleza: “Straika ni Rooney na Chicharito ni Straika wa Pili na yeye anajua hilo.”
Alipoulizwa kuhusu habari kuwa Adnan Januzaj anauzwa, Van Gaal: “Hauzwi.”


Kukiwa na kila dalili kuwa Fowadi wa Barcelona Pedro yuko njiani kwenda Manchester United, Kocha wa Mabingwa hao wa Spain Luis Enrique amesisitiza ni juu ya Mchezaji huyo mwenyewe kuamua nini hatima yake.
Pedro, mwenye Miaka 28, aliijulisha rasmi Barcelona Juzi Jumanne nia yake kuhama ikiwa ni Masaa kadha kabla hajaifungia Klabu hiyo Bao la ushindi walipotwaa UEFA Super Cup kwa kuibwaga Sevilla 5-4.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Luis Enrique alisema: “Tumesikia maoni yake, ni uamuzi mgumu anaotakiwa kufanya lakini tutasubiri tujue ataamua nini. Yeye anataka kuhama kwa vile hapati namba lakini tunataka acheze na ni uamuzi mgumu.”
Hata hivyo, Enrique amesema Pedro ataanza Mechi ya Kwanza ya Supercopa de Espana hapo Ijumaa huko Estadio San Mames, Bilbao watakapocheza na Athletic Bilbao.


Kwa sababu za kiusalama Gemu ya Ligi Kuu England kati ya Aston Villa na Manchester United imewekwa Ijumaa Usiku kutokana na Mji wa Birmingham kuwa na Maandamano badala ya kuchezwa Wikiendi.
Mechi hii, ambayo itachezwa Villa Park, inazikutanisha Timu ambazo zilishinda Mechi zao za kwanza za Msimu mpya Wikiendi iliyopita kwa zote kushinda kwa Bao 1-0.
Man United walishinda kwao Old Trafford kwa kuiangusha Tottenham kwa Bao la kujifunga mwenyewe Beki wa Tottenham Kyle Walker wakati Villa wakishinda Ugenini walipocheza na Timu mpya kabisa kwenye Ligi Kuu England Bournemouth huku Bao lao moja likifungwa na Rudy Gestede.
Kila Timu itatinga kwenye Mechi hii ikiwakosa baadhi ya Wachezaji wake kwa Man United kuwakosa Marouane Fellaini, ambae yuko Kifungoni na hii ni Mechi yake ya pili akibakiza moja, na pia watamkosa Majeruhi Phil Jones.
Villa wao wana Majeruhi Gary Gardner, Jores Okore na Jack Grealish na wote wana hati hati kucheza Mechi hii.

Mchezo huo utapigwa kesho ijumaa 14th Aug, 2015 kwenye Uwanja wa nyumbani wa Villa Park, Birmingham.

USO KWA USO
22.04.13 PRE Manchester United Aston Villa 3 : 0
04.04.15 PRE Manchester United Aston Villa 3 : 1
20.12.14 PRE Aston Villa Manchester United 1 : 1
29.03.14 PRE Manchester United Aston Villa 4 : 1
15.12.13 PRE Aston Villa Manchester United 0 : 3


VIKOSI VINATEGEMEA KUWA HIVI:
Man United (4-3-3): Romero, Darmian, Smalling, Blind, Shaw, Schneiderlin, Carrick, Mata, Depay, Young, Rooney.

Aston Villa (4-2-3-1): Guzan, Bacuna, Richards, Clark, Amavi, Gueye, Westwood, Sanchez, Ayew, Sinclair, Gestede.



www.bukobasports.com
Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Edin Dzeko amejiunga na kilabu ya ligi ya Seria A Roma kwa mkopo.
Kilabu hiyo imetoa kitita cha pauni milioni 2.9, na nyengine pauni 7.9 zikitarajiwa kulipwa iwapo uhamisho huo utabadilika na kuwa wa kudumu.
''Nimekuja hapa kushinda mataji'',alisema Dzeko.
''Ninaweza kuahidi kitu kimoja kwamba nitajitahidi vilivyo katika kilabu hii''.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na kilabu ya Etihad kutoka Wolfsburg mnamo mwaka 2011 kwa pauni milioni 27.
Alikuwa ameweka sahihi ya kandarasi ya miaka minne katika uwanja wa Etihad msimu uliopita.
Hatahivyo,meneja manuel Pelegrini hivi majuzi alikiri kwamba Dzeko alikuwa na uwezo mkubwa kuondoka katika Etihad kufutia usajili wa Raheem Sterling kutoka Liverpool kwa kitita cha pauni milioni 49.
Kutoka makao makuu ya shirikisho la soka ulimwenguni FIFA, Rais wa FIFA Sepp Blatter ametoa ushauri kwa nia njema kwa nchi za Ulaya Magharibi kuiga na kujifunza kitu kutoka katika nchi ya Urusi ambayo sheria ya soka ya nchi hiyo ina ruhusu idadi maalumu ya wachezaji wa kigeni kucheza katika mechi moja.
Kupitia katika Magazine ya FIFA Blatter alishauri kujali vipaji vya nchi husika kwa kuwapa nafasi ya kucheza zaidi kiasi hata cha kuwa shauri waige mfano kutoka katika nchi ya Urusi ambayo ina namba maalum ya kuanza kwa wachezaji wa kigeni.
blatter_3031222b
Wazo hilo la Blatter lilizua ugomvi kati yake na Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platin kabla ya mpango huo kufutwa mwaka 2010, kwani Umoja wa nchi za Ulaya (EU) unaunga mkono mpango uhuru wa kufanya kazi, hata hivyo Urusi haipo ndani ya Umoja wa nchi za Ulaya (EU).
“Kuwaiga Urusi kwa kudhibiti idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoanza katika mechi moja, kuweka idadi ya wachezaji sita au watano ili kulinda vipaji vya wachezaji wa nchi husika, asilimia 77 ni wachezaji wa kigeni waliopata muda wa kucheza zaidi katika Ligi Kuu Uingereza msimu uliopita”
sepp_blatter_rtr_img
Hata hivyo Blatter anaunga mkono Urusi kuweka kiwango hicho cha idadi ya wachezaji wazawa kupewa nafasi kubwa ya kuanza katika mechi za Ligi kuu ya Urusi na anaamini mpango wao huo utawapa nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 litakalofanyika Urusi.

waliotembelea blog