Thursday, August 13, 2015


Kukiwa na kila dalili kuwa Fowadi wa Barcelona Pedro yuko njiani kwenda Manchester United, Kocha wa Mabingwa hao wa Spain Luis Enrique amesisitiza ni juu ya Mchezaji huyo mwenyewe kuamua nini hatima yake.
Pedro, mwenye Miaka 28, aliijulisha rasmi Barcelona Juzi Jumanne nia yake kuhama ikiwa ni Masaa kadha kabla hajaifungia Klabu hiyo Bao la ushindi walipotwaa UEFA Super Cup kwa kuibwaga Sevilla 5-4.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Luis Enrique alisema: “Tumesikia maoni yake, ni uamuzi mgumu anaotakiwa kufanya lakini tutasubiri tujue ataamua nini. Yeye anataka kuhama kwa vile hapati namba lakini tunataka acheze na ni uamuzi mgumu.”
Hata hivyo, Enrique amesema Pedro ataanza Mechi ya Kwanza ya Supercopa de Espana hapo Ijumaa huko Estadio San Mames, Bilbao watakapocheza na Athletic Bilbao.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog