Monday, November 16, 2015


Mchezaji wa timu ya mpira wa Kikapu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ephraim Mlawa (kushoto) akichuana na Juvenary Shichose wakati Bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo hicho lililofanyika, mwishoni mwa wiki katika Kituo cha Michezo cha JMK Youth Park na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kutoa vifaa vya michezo kwa timu zilizoshiriki mchezo wa soka. (Picha na Francis Dande)
Timu za mpira wa kikapu kutoka Chuo cha IFM zikichuana katika Bonanza la michezo la wanafunzi wa chuo hicho.
Kikosi cha timu ya Soka ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), BBF kikiwa katika picha ya pamoja.



KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimewasili salama nchini Algeria leo jioni majira yaa 10 jioni, kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika mji wa Bilda.
Msafara wa Taifa Stars unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Athumani Kambi, ambapo jumla ya watu 40 wapo katika mji wa Bilda wakiwemo wachezaji 21 wanaojiandaa kwa mchezo wa marudiano.
Mara baada ya kufika katika uwanja wa ndege Algiers, Stars ilipokelewa na watanzania na wanafunzi wanaoshi nchini Algeria, na kuongozana na timu mpaka katika mji wa Bilda ilipofiki timu.
Mchezaji tegemeo, Mrisho Ngassa akiwaongoza wenzake baada ya kuwasili
Stars inatarajiwa kufanya mazoezi kesho saa 1 jioni katika uwanja wa Mustapha Tchaker utakaotumika kwa mchezo wa marudiano siku ya Jumanne.
Katika mchezo wa awali uliochezwa jana jioni jijini Dar es salaam, Tanzania ilitoka sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya Algeria, hivyo kuifanya Stars kusaka ushindi katika mchezo wa marudiano ili kuweza kusonga mbele.
Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vjana wake wote wapo katik ahali, hakuna majeruhi na wapo tayari kwa ajili ya kusaka ushindi siku ya Jumanne, na kusema makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana wanayafanyia kazi yasijitokeze tena katika mchezo unaofuata.
Taifa Stars imefikia katika hoteli ya Ville Des Roses imetumia takriabn muda wa saa 1 kutoka katika uwanja wa Ndege wa Algiers mpaka katika hoteli hiyo iliyopo eneo la Bilda.



Ikiwa timu ya Taifa ya Tanzania ipo Algeria tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi dhidi ya timu ya taifa ya Algeria katika mji wa Blida uwanja wa Mustapha Tchaker Jumanne ya November 17, majirani zao wa Kenya bado wanaripotiwa kukwama uwanja wa ndege kwa muda sasa.
Timu hiyo ya taifa ya Kenya Harambee Stars imeshindwa kusafiri kuelekea Cape Verde na kukwama katika uwanaj wa ndege wa Wilson  baada ya kampuni ya ndege iliyokuwa inatajwa kuingia makubaliano ya kuisafirisha kugoma kuruhusu ndege hiyo iondoke hadi wakamilishiwe malipo yao yote kwani hawana imani na shirikisho la soka la Kenya KFF kama litalipa deni.
harambee-stars-have-been-drawn-to-face-rivals-uganda-in-cecafa-tournament_ss0apl92zbfu1o5xvggnmdzak
Harambee Stars ambao wanapaswa kwenda Cape Verde kucheza mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 Urusi dhidi ya Cape Verde baada ya mchezo wa awali uliochezwa Kenya na Harambee Stars kuibuka na ushindi wa goli 1-0, wanakabiliwa na ukata kwa muda sasa hata awali waliripotiwa wachezaji kudai malimbikizo ya posho zao.



Staa wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi November 16 ameingia katika headlines baada ya stori zake za kutaka kujiunga na Arsenal kuandikwa katika headlines za magazeti ya Ulaya, awali Lionel Messi ambaye ameichezea FC Barcelona toka akiwa mdogo aliwahi kukiri kuvutiwa kujiunga na klabu ya Arsenal ya Uingereza.
Messi-490728
Messi ambaye wengi wamewahi kumkejeli na kudhani kuwa hana uwezo wa kutamba nje ya FC Barcelona anatajwa kuwa radhi kujiunga na Arsenal ila sharti lake la mshahara ndio tatizo linalotajwa kuwa huenda hana lengo la kwenda Arsenal, Messi anatajwa kuiomba Arsenal iwe inamlipa mshahara wa pound 600000/= kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1 za Tanzania mshahara ambao ni mgumu kwa Arsenal kumlipa hususani kwa hulka za kocha wa timu hiyo.
hi-res-2b2f4449796e8b2e48790d5220f12f0d_crop_north
Stori za Lionel Messi kuvutiwa kujiunga na Arsenal aliwahi kukiri kupenda kuichezea klabu hiyo ila November 16 habari zinazotajwa kuwa za kichunguzi kutoka katika gazeti la Star Sport zinasema Messi ameombwa kulipwa mshahara kiasi ambacho ni kigumu kwa Arsenal kukubali au kumudu kulipa, Lionel Messi kwa sasa anatajwa kulipwa mshahara usiofikia pound 300000/= kwa wiki na FC Barcelona na kwa upande wa Arsenal mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa ni Mesut Ozil pound 140000/= kwa wiki.
CT4my_cWwAESlOf

waliotembelea blog