Thursday, August 14, 2014

KWENYE Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo, Mabingwa wa Dunia Germnay bado wako Nambari Wani na Tanzania imeporomoka Nafasi 4 na sasa iko Nafasi ya 110.
Timu ya juu kabia kwa Afrika ni Algeria ambayo iko Nafasi ya 24 ikifuatiwa na Ivory Coast ambayo iko Nafasi ya 25.
Listi nyingine ya Ubora itatolewa Septemba 18.



FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI: Agosti 14, 2014
NAFASI
NCHI
PTS
KUPANDA/KUSHUKA
1
Germany
1736
-
2
Argentina
1604
-
3
Netherlands
1507
-
4
Colombia
1495
-
5
Belgium
1407
-
6
Uruguay
1316
-
7
Spain
1241
+1
7
Brazil
1241
-
9
Switzerland
1218
-
10
France
1212
-
11
Portugal
1152
-
12
Chile
1100
-
13
Greece
1092
-
14
Italy
1069
-
15
Costa Rica
1023
+1
16
Croatia
964
+1
17
Mexico
942
+1
18
USA
937
-3
19
Bosnia
925
-
20
England
915
-


Cheer up,  Antonio! Conte will be appointed the manager of the Italian national team after the 2014 World CupItaly imemteua aliekuwa Kocha Mkuu wa Juventus Antonio Conte kuwa Kocha wa Timu ya Taifa yao hadi Mwaka 2016.
Conte anarithi wadhifa huo kutoka kwa Cesare Prandelli ambae alijiuzulu mara baada ya Italy kutupwa nje ya Fainali za Kombe la Dunia Mwezi Juni huko Brazil waliposhindwa kuvuka hata hatua za Makundi.
Conte, mwenye Miaka 45 na Kiungo wa zamani wa Italy, alijiuzulu ghafla Juventus, ambako kwa Misimu Mitatu iliyopita aliipa Ubingwa, mara tu baada ya kujiuzulu kwa Prandelli lakini wakati huo haikusemwa chochote kwanini alifanya hivyo.
In charge: Conte will become the second-highest paid manager in international football after leaving Juventus
Mbali ya kuwa Kocha Mkuu wa Juve, Conte pia aliwahi kuziongoza Klabu za Bari na Siena na kuzipandisha kutoka Ligi Serie B kwenda Serie A na pia alifanya kazi na Klabu za Arezzo na Atalanta.

Wakitangaza uteuzi wa Conte, Shirikisho la Soka la Italy limesema Kocha huyo, mbali ya Mshahara wake, atapata Bonasi ikiwa Italy itafuzu kucheza Fainali za EURO 2016 na pia Bonasi nyingine wakipanda Nafasi 5 kwenye Listi ya Ubora ya FIFA ambayo sasa wako Nafasi ya 5 na Bonasi ya Tatu ikiwa watatinga Fainali halisi ya EURO 2016.


KIFUNGO cha Miezi Minne cha Luis Suarez kinabaki pale pale lakini sasa anaruhusiwa kufanya Mazoezi na Timu yake Barcelona kwa mujibu wa CAS, Mahakama ya Usuluhisho Michezoni.
CAS, [Court for Arbitration in Sports], ambayo ilikuwa ikitoa uamuzi wao kuhusu Rufaa ya Suarez kwao hii Leo huko Lausanne, Uswisi, imesema itatoa maelezo ya kina kuhusu uamuzi wao huu hapo baadae.
Suarez aliadhibiwa na FIFA huko Brazil Mwezi Juni baada ya kumng’ata Meno Beki wa Italy, Giorgio Chiellini, wakati wa Mechi ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy.

Pamoja na Kifungo hicho cha Miezi Minne kilichamzuia kushiriki kwenye shughuli yeyote ya Soka, Suarez pia alifungiwa kutocheza Mechi 9 za Uruguay na kupigwa Faini Pauni 66,000.
Kifungo cha Miezi Minne kitamalizika Oktoba 26.
Wakati akiadhibiwa Suarez alikuwa ni Mchezaji wa Liverpool na kuhamia Barcelona Mwezi uliopita na uamuzi huu unamaanisha yupo ruksa kufanya Mazoezi na Barca na Mechi yake ya kwanza inaweza kuwa hapo Oktoba 29 wakati Barcelona itacheza Mechi ya La Liga na Real Madrid.
Msimu wa La Liga unaanza Agosti 24 na Barca inaanza na Elche.

SUAREZ – Matukio yake ya utata:
-Juni 2014 – Afungiwa Miezi 4 kwa kumng’ata Beki wa Italy Giorgio Chiellini
-Aprili 2013 – Afungiwa Mechi 10 kwa kumng’ata Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic
-Des 2011 – Afungiwa Mechi 8 kwa kumkashifu Kibaguzi Patrice Evra wa Man United
-Nov 2010 – Afungiwa Mechi 7 kwa kumuuma Otman Bakkal wa PSV Eindhoven


Kikosi cha Timu Ya Survey wakiwa katika picha ya pamoja.Wachezaji wa Survey Veterani wakiwa katika picha yapamoja Wachezaji wa Coastal U 20 kabla ya mechi.Mchezaji wa Timu ya Survey Veterani Hamad Shawejiakimtoka mchezaji wa Coastal Union U 20 katika mashindano ya kilele cha nane nanae yaiyofanyika viwanja vya mkwakwani Jijini Tanga.

NA ELIZABETH KILINDI, TANGA
TIMU ya Survey Veteran ya jijini Dar es Salaamu, Jumapili iliyopita ilivuna sare ya bao 1-1 dhidi ya kikosi cha vijana wa chini ya miaka 20 wa timu ya Coastal Union katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.


Edinson Cavani had a fine debut season with Paris Saint-Germain.
Here he is at the Ligue 1 celebration party with the silver wares.







BAADA ya Msimu uliopitwa kutupwa Nafasi ya Tatu nyuma ya Mabingwa Manchester City na Liverpool kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England, safari hii José Mourinho ametabiri Timu yake Chelsea itatawala Soka la England.
Imani ya Mreno imekuja hasa baada ya kufanya mabadiliko kwenye Kikosi chake kufuatia kuondoka kwa Wakongwe Frank Lampard na Ashley Cole, Demba Ba, Samuel Eto’o na Beki wa Brazil David Luiz na kutumia zaidi ya Pauni Milioni 75 kuwanunua Wachezaji wapya Cesc Fábregas, Diego Costa na Filipe Luís, na pia kurudi tena Stamford Bridge kwa Didier Drogba.

Mabadiliko hayo yamemfanya Mourinho awe na kiburi cha kutamka watapigania Mataji katika kila Mashindano kwenye Msimu huu mpya WA 2014/15.
Admirer: Chelsea boss Jose Mourinho has publicly praised Fabregas' impact at Chelsea in pre-season
“Tuna Kikosi ambacho tulitaka kuwa nacho.” Mourinho ametamba. “Ni Kikosi cha kesho, cha Msimu ujao na Kikosi chenye nafasi kubwa kwa Miaka ijayo Mitano au Kumi kikiwa na Wachezaji Vijana. Nakipenda sana Kikosi changu!”
Summer spending: Chelsea have signed Diego Costa, Cesc Fabregas and Filipe Luis during this window
Aliongeza: “Naipenda Klabu hii kwa sababu imenipa Wachezaji Watatu niliowataka. Beki wa Kushoto, Kiungo na Straika. Ukweli wamenipa Mastraika wawili kwa sababu Didier amerudi tena!”
Former Gunner: Fabregas spent eight years at Arsenal and used to captain Chelsea's north London rivals
Hata hivyo, Mourinho ameonya: “Lakini ukweli hii ni Ligi Kuu na kila Timu inajaribu kuwa bora hasa kwa Timu za juu. Je tuko tayari kwa hilo? Ndio lakini hii ni England. Nchi nyingine mbio za Ubingwa ni kati ya Timu mbili na nyingine moja tu. Hapa ni kati ya Timu 5 au 6!”



Msanii OMMY DIMPOZ na wenzake wakishuka kwenye Ndege aina ya Precision leo asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege Mjini Bukoba tayari kwa kukamua vilivyo katika mwendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta, Tamasha linalotarajiwa kufanyika kesho Ijumaa kwenye uwanja wa Kaitaba hapa Bukoba.
Wasanii hao pamoja na watangazaji na wafanyakazi wengine wameingiatayari Bukoba wakitokea jijini Mwanza.

Wasanii wakishuka kwenye Ndege tayari kwa Fiesta kesho Ijumaa.

Chistian Bella huyoo langoni mwa pipa.
Salaam za Bella kwa ardhi ya Bk.

Christian Bella akikaribishwa na Mwenyekiti wa kamati ya jukwaa la wasanii Hamza.

Dj Ziro langoni mwa ndege akiwa na mwanadada mtangazaji wa Clouds Tv Shadee mbele.

Karibu bhana.

Msanii wa Bongoflava Jux.

Ney wa Mitego.

Barnaba.

Barnaba mbele akifuatiwa na Madee na Fiesta Crew.
Willy Kiroyera (kushoto, akiteta jambo na Ruge Mutahaba kwenye Uwanja wa Ndege leo Asubuhi

Katika Picha ya Pamoja
wakiteta jambo na kuoneshana kitu kwenye Simu
Jux na Stamina
Tupo tayari kwa Fiesta 2014 Bukoba
Tayarikwa Makamuzi ya Fiesta 2014 hapo Kesho Ijumaa

Fiesta 2014 Mjini Bukoba itakuwa balaa!! Wasanii wakitokelezea huku wakishoo lavu tayari kwa  Fiesta kesho.
Linah akiwa kwenye picha ya pamoja na wenzake

Muziki ni sehemu yetu ya Maisha

Ommy Dimpoz kwenye tabasamu la nguvu baada ya kutua Bukoba

32 yote papp!!! Ommy
Barnaba akipeana Hi na Dj Fetty
Mr. Blue nae ndani!
Wakipeana habari za hapa na pale
Willy O. Ruta akiwa na Bw. Ruge Mutahaba

waliotembelea blog