Thursday, August 14, 2014

BAADA ya Msimu uliopitwa kutupwa Nafasi ya Tatu nyuma ya Mabingwa Manchester City na Liverpool kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England, safari hii José Mourinho ametabiri Timu yake Chelsea itatawala Soka la England.
Imani ya Mreno imekuja hasa baada ya kufanya mabadiliko kwenye Kikosi chake kufuatia kuondoka kwa Wakongwe Frank Lampard na Ashley Cole, Demba Ba, Samuel Eto’o na Beki wa Brazil David Luiz na kutumia zaidi ya Pauni Milioni 75 kuwanunua Wachezaji wapya Cesc Fábregas, Diego Costa na Filipe Luís, na pia kurudi tena Stamford Bridge kwa Didier Drogba.

Mabadiliko hayo yamemfanya Mourinho awe na kiburi cha kutamka watapigania Mataji katika kila Mashindano kwenye Msimu huu mpya WA 2014/15.
Admirer: Chelsea boss Jose Mourinho has publicly praised Fabregas' impact at Chelsea in pre-season
“Tuna Kikosi ambacho tulitaka kuwa nacho.” Mourinho ametamba. “Ni Kikosi cha kesho, cha Msimu ujao na Kikosi chenye nafasi kubwa kwa Miaka ijayo Mitano au Kumi kikiwa na Wachezaji Vijana. Nakipenda sana Kikosi changu!”
Summer spending: Chelsea have signed Diego Costa, Cesc Fabregas and Filipe Luis during this window
Aliongeza: “Naipenda Klabu hii kwa sababu imenipa Wachezaji Watatu niliowataka. Beki wa Kushoto, Kiungo na Straika. Ukweli wamenipa Mastraika wawili kwa sababu Didier amerudi tena!”
Former Gunner: Fabregas spent eight years at Arsenal and used to captain Chelsea's north London rivals
Hata hivyo, Mourinho ameonya: “Lakini ukweli hii ni Ligi Kuu na kila Timu inajaribu kuwa bora hasa kwa Timu za juu. Je tuko tayari kwa hilo? Ndio lakini hii ni England. Nchi nyingine mbio za Ubingwa ni kati ya Timu mbili na nyingine moja tu. Hapa ni kati ya Timu 5 au 6!”

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog