KIFUNGO
cha Miezi Minne cha Luis Suarez kinabaki pale pale lakini sasa
anaruhusiwa kufanya Mazoezi na Timu yake Barcelona kwa mujibu wa CAS,
Mahakama ya Usuluhisho Michezoni.
CAS, [Court for Arbitration in Sports], ambayo ilikuwa ikitoa uamuzi wao kuhusu Rufaa ya Suarez kwao hii Leo huko Lausanne, Uswisi, imesema itatoa maelezo ya kina kuhusu uamuzi wao huu hapo baadae.
Suarez aliadhibiwa na FIFA huko Brazil Mwezi Juni baada ya kumng’ata Meno Beki wa Italy, Giorgio Chiellini, wakati wa Mechi ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy.
Pamoja na Kifungo hicho cha Miezi Minne kilichamzuia kushiriki kwenye shughuli yeyote ya Soka, Suarez pia alifungiwa kutocheza Mechi 9 za Uruguay na kupigwa Faini Pauni 66,000.
Kifungo cha Miezi Minne kitamalizika Oktoba 26.
Wakati akiadhibiwa Suarez alikuwa ni Mchezaji wa Liverpool na kuhamia Barcelona Mwezi uliopita na uamuzi huu unamaanisha yupo ruksa kufanya Mazoezi na Barca na Mechi yake ya kwanza inaweza kuwa hapo Oktoba 29 wakati Barcelona itacheza Mechi ya La Liga na Real Madrid.
Msimu wa La Liga unaanza Agosti 24 na Barca inaanza na Elche.
SUAREZ – Matukio yake ya utata:
-Juni 2014 – Afungiwa Miezi 4 kwa kumng’ata Beki wa Italy Giorgio Chiellini
-Aprili 2013 – Afungiwa Mechi 10 kwa kumng’ata Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic
-Des 2011 – Afungiwa Mechi 8 kwa kumkashifu Kibaguzi Patrice Evra wa Man United
-Nov 2010 – Afungiwa Mechi 7 kwa kumuuma Otman Bakkal wa PSV Eindhoven

0 maoni:
Post a Comment