Thursday, August 20, 2015


Fowadi wa Barcelona Pedro sasa atahamia Chelsea baada ya Klabu hiyo kukubali kulipa Pauni Milioni 22 kwa mkupuo kitu ambacho Manchester United waligomea kulipa.
Kwa muda mrefu iliaminika kuwa Pedro atatua Old Trafford huku kukiripotiwa kuwa tayari ameshaafikiana maslahi yake binafsi lakini kusita kwa Man United kulipa kwa mkupuo mmoja Dau ambalo Barca walikuwa wakitaka kumetoa mwanya kwa Chelsea kutumbukia na kukubali kulipa Dau hilo lote na kumnasa Staa huyo.

Man United walikuwa tayari kulipa Dau la Pauni Milioni 17.7 mbele na kisha kulipa pole pole Pauni Milioni 3.6 zikiwa nyongeza ambazo zitaendana na mafanikio atakayopata Mchezaji huyo akiwa na Man United.
Kitu hicho Barca waligomea na kutaka Fedha zote kwa mkupuo na hapo ndipo Chelsea wakawapiku Man United.
Inatarajiwa wakati wowote kuanzia sasa Pedro, mwenye Miaka 28, atapimwa Afya yake huko Stamford Bridge na kisha kusaini Mkataba.


Kiungo wa kimataifa wa Cameroon ambaye amewahi kuichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza kwa muda mrefu kabla ya kutimkia FC Barcelona ya Hispania Alex Song na msimu uliopita kuitumikia klabu ya West Ham United ya London kwa mkopo akitokea FC Barcelona amepoteza matumaini ya kuendelea na West Ham United.
Song alikuwa na matumaini ya kubakia katika kikosi hicho baada ya kuwa hana namba katika kikosi cha kwanza cha FC Barcelona ya Hispania hivyo matumaini ya kujiunga jumla na klabu hiyo yalikuwa makubwa baada ya kufanya vipimo vya Afya na kufuzu, taarifa zilizotoka August 19 ni kuwa West Ham wamesitisha mpango huo.
Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu golikipa mkongwe na mahiri Juma Kaseja kuwa bila timu na kuhusishwa kujiunga na vilabu mbalimbali hatimaye uvumi huo umemalizika August 19 baada ya kusaini mkataba wa miezi sita wa kuitumikia klabu ya Mbeya City kutoka Jijini Mbeya.
IMG-20150819-WA0008 (1)
Mkataba wa Juma Kaseja wa kujiunga na klabu ya Mbeya City umesainiwa August 19 mbele ya meneja wake mpya Athumani Tippo hivyo huo ni mwisho wa uvumi wa habari za Juma Kaseja atacheza wapi msimu ujao, taarifa hizo zinakuwa pigo kwa kocha wa Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu ambaye alikiri katika vyombo vya habari kuwa ana hitaji huduma ya Kaseja kikosini mwake.
kaseja atua mbeya city 4
Kabla ya kusaini mkataba na Mbeya City Juma Kaseja alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya miezi nane baada ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na iliyokuwa klabu yake ya zamani ya Yanga nakufanya kesi hiyo kutinga mahakamani.

waliotembelea blog