Pia Hiddink amemwambia nahodha wa timu hiyo Robin van Persie kupatana na Pierre van Hooijdonk ambaye waligombana wakati wa fainali za kombe la dunia, wakati Pierre van Hooijdonk aliposema Van Persie hafai kucheza kwenye mchezo wa mshindi wa 3 kutokana na kutokuwa na kiwango kinachostahili.
Monday, August 4, 2014
8:04 AM
Unknown
Pia Hiddink amemwambia nahodha wa timu hiyo Robin van Persie kupatana na Pierre van Hooijdonk ambaye waligombana wakati wa fainali za kombe la dunia, wakati Pierre van Hooijdonk aliposema Van Persie hafai kucheza kwenye mchezo wa mshindi wa 3 kutokana na kutokuwa na kiwango kinachostahili.
7:56 AM
Unknown
Mheshimiwa Zitto Kabwe - "#TaifaStars imecheza mechi
nyingi ambazo nimehudhuria, ndani na nje ya nchi. Sijaona wachezaji wakitokwa
machozi kama Jana. Ndani ya chumba cha kubadilisha nguo niliona uchungu na
machozi ya vijana wetu. Kwa pamoja walikuwa wanasema 'nyumbani kama ugenini,
ugenini ugenini'. Somo kubwa sana hilo."
7:42 AM
Unknown
MABINGWA wa Ulaya, Real Madrid wamemsajili mlinda
mlango na shujaa wa Costa Rica katika fainali za kombe la dunia majira ya
kiangazi mwaka huu nchini Brazil, Keylor Navas.
Navas amekubali
kusaini mkataba wa miaka sita na sasa anaingia katika ushindani na kipa Iker
Casillas kwasababu kuna dalili kuwa kipa mwingine Diego Lopez anasepa zake.
Taarifa
iliyochapishwa kwenye mtandao rasmi wa klabu ya Real Madrid jana jioni inasomeka:
"Real Madrid CF na Levante UD zimefikia makubaliano juu ya uhamisho wa
Keylor Navas, ambaye atajifunga klabuni kwa misimu sita ijayo""Mchezaji
atatambulishwa jumanne, Agosti 5, saa 7:00 mchana (saa za Hispania) kwenye
uwanja wa Bernabeu, baada ya kuchukuliwa vipimo vya afya".
7:41 AM
Unknown
Tabasamu 'bab kubwa': Ashley Young
akiungana na wachezaji wenzake Wayne Rooney na Danny Welbeck kwenye
mazoezi ya Manchester United.
LOUIS van Gaal atawachana macho kwa
macho wachezaji wake ambao wataachwa na Manchester United baada ya
kumaliza ziara ya Marekani ambapo amewapa nafasi ya kumuonesha viwango
vyao.
Anderson, Nani, Javier Hernandez, Shinji
Kagawa na Marouane Fellaini ni miongoni mwa majina makubwa yaliyopo
katika mstari mwekundu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Lakini inafahamika kuwa Van Gaal hatakuwa na huruma kabisa ingawa hajafanya maamuzi ya hadharani.
'Nitafikia maamuzi baada ya ziara hii,' alisema. Nimewapa nafasi ya kucheza wachezaji wote na najua zaidi hata kabla ya ziara.
Louis van Gaal atawaambia wachezaji asiowahitaji kuwa wapo tayari kutafuta timu nyingine.
'Kwa sasa nimefikia maamuzi kidogo,
lakini kwenye mpira wa miguu lazima uamue. Unatakiwa kuwapa nafasi
wachezaji kufanya usajili pale unapoona hawana nafasi ya kucheza kwenye
kikosi chako.
'Unatakiwa kusema mapema kwasababu ni
mbali sana baada ya Agosti 31. Nitawaambia wachezaji baada ya ziara hii,
lakini nitawaambia wao na sio ninyi.'
Van Gaal aliyasema hayo wakati akiongea
na waandishi wa habari mjini Miami jana kuelekea mechi ya fainali ya leo
usiku ya kombe la kimataifa nchini Marekani dhidi ya mahasimu wao
wakubwa England, klabu ya Liverpool.
Subscribe to:
Posts (Atom)