MABINGWA wa Ulaya, Real Madrid wamemsajili mlinda
mlango na shujaa wa Costa Rica katika fainali za kombe la dunia majira ya
kiangazi mwaka huu nchini Brazil, Keylor Navas.
Navas amekubali
kusaini mkataba wa miaka sita na sasa anaingia katika ushindani na kipa Iker
Casillas kwasababu kuna dalili kuwa kipa mwingine Diego Lopez anasepa zake.
Taarifa
iliyochapishwa kwenye mtandao rasmi wa klabu ya Real Madrid jana jioni inasomeka:
"Real Madrid CF na Levante UD zimefikia makubaliano juu ya uhamisho wa
Keylor Navas, ambaye atajifunga klabuni kwa misimu sita ijayo""Mchezaji
atatambulishwa jumanne, Agosti 5, saa 7:00 mchana (saa za Hispania) kwenye
uwanja wa Bernabeu, baada ya kuchukuliwa vipimo vya afya".
0 maoni:
Post a Comment