Friday, October 30, 2015

PAMBANO LA AZAM FC NA JKT RUVU KATIKA PICHA


Kikosi cha JKT Ruvu kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika katika uwanja wa Karume Dar es Salaa dhidi ya Azam FC. Katika mchezo huo Azam iliibuka na ushindi wa bao 4-2.

Kikosi cha Azam FC.

Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco akiwania mpira na mchezaji wa JKT Ruvu, Michael Aidan.

Bocco akimtoka Michael Aidan.

Wacheza wa Azam wakishangilia baada ya kufunga.

Hekaheka katika lango la JKT Ruvu.

Erasto Nyoni (kushoto) akiwania mpira na Mussa Juma.



Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu ya taifa Taifa Stars kwenda nchini, Algeria kwa mchezo utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu.

Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu hiyo kwenda nchini Algeria kushiriki mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu. Kampuni ya Ndege ya Fastjet imedhamini safari hiyo kwa kutoa ndege yake kwa kwenda na kurudi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati na Kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie.

Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (katikati),akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kudhamini timu ya Taifa Stars kwenda na kurudi nchini Algeria kwa ndege yake kushiriki mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu. Kulia ni Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda na Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie.

Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Ndege ya Fastjet imetoa ndege kwa ajili ya kuisafirisha timu ya Taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wake na timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati alisema hatua ya kuisaidia timu hiyo ni mwanzotu wa ushirikiano baina ya kampuni hiyo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

"Kampuni yetu imeanza ushirikiano na TFF katika kukuza michezo nchini na ndio maana tumeanza kuwasafirisha wachezaji hao kwenda nchini humo kwa ajili ya mchezo huo" alisema Kibati
Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda alisema safari ya kwenda nchini humo itakuwa Novemba 16 na kuwa mchezo huo utafanyika Novemba 17.
Alisema gharama za kusafiri na timu hiyo kwa mtu atakayependa kusafiri ni dola 800 kati ya hizo dola 640 ni kwa ajili ya safari na 60 ni malipo ya kodi ya uwanja wa ndege hapa nchini na Algeria.

Alisema safari hiyo itaanza asubuhi na kuwa ndege hiyo watakayosafiri nayo inabeba abiria zaidi ya 150.



Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) leo hii limeamuru Kamati ya muda inayoongoza Chama cha Mpira Zanzibar (ZFA) iondoe mahakamani mashatka yote dhidi ya uongozi halali wa ZFA.
Katika barua yake kwenda kwa Katibu Mkuu wa ZFA na nakala yake kuletwa TFF, CAF imesisitiza kuwa kwa mujibu wa katiba za CAF na FIFA ni marufuku masuala ya mpira kupelekwa mahakamani, ZFA ni mwanachama mshiriki wa CAF (Associate Member).
CAF inaigiza kamati ya muda ya ZFA hadi tarehe 07 Novemba, 2015 iwe imetekeleza maagizo na kuhakikisha uongozi halali uliochaguliwa na ZFA unarejea katika shughuli zake uongozi ZFA.
Jambo hili lisipotekelezwa CAF imesema itaifungia Zanzibar uanachama wake. Kikanuni na kikatiba kufungiwa uanachama maana yake ni Mwanachama husika kusitishwa ushiriki katika shughuli zote zinazosimamiwa na FIFA, CAF na wanachama wake wote.
Shughuli hizo ni pamoja na kushiriki mashindano ya kimataifa, kozi mbalimbali na misaada ya kifedha, vifaa, ufundi nk. 


TFF inatoa wito kwa mara nyingine kwa pande zinazokinzana kukaa meza moja na kumaliza tofauti zao kwa faida ya mpira wa Zanzibar, Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).



Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limetuma salamu za pongezi kwa viongozi wa mpira wa miguu nchini waliochaguliwa kuwa wabunge na madiwani katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Viongozi waliochaguliwa katika nafasi ya Ubunge ni John Kadutu – mbunge wa Ulyankulu – Tabora, (mjumbe wa mkutano mkuu kutoka Mwanza) na Alex Gashaza – mbunge wa Ngara (Makamu mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kagera)

Aidha waliochaguliwa Udiwani katika maeneo yao ni Khalid Abdallah (Mjumbe wa kamati ya Utendaji – TFF), Yusuph Kitumbo- (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tabora), Omari Gindi- (Mwnyekiti wa Chama cha mpira wa Miguu mkoa wa Kigoma), Bathromeo Kimaro - (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Singida) na Omar Kinyeto (Mjumbe wa mkutano mkuu mkoa wa Singida), Golden Sanga (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Ruvuma), Pachal Kihanga (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa mkoa Morogoro), Yusuf Manji (Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC) ambao wote ni wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF.

TFF inawaomba kutumikia halmashauri zao kwa mafanikio na kutilia mkazo kuhifadhi maeneo ya wazi kwa ajili ya michezo mbalimbali hususani mpira wa miguu mashuleni.



Professor Jay ni mmoja wa rappers waliojitahidi kuwekeza nguvu nyingi kwenye Bongo Fleva, lakini 2015 aliamua kubadili nguvu hizo kwa kuwekeza zaidi kwenye Siasa… Kagombea Ubunge wa Jimbo la Mikumi Morogoro na kafanikiwa kupita kw
enye nafasi hiyo.
Prof Jay
Prof. Jay, mshindi wa kiti cha Ubunge Jimbo la Mikumi.
Prof. Jay amesema amefurahi kwa ushindi huo, anachoangalia zaidi kwa sasa ni kujitahidi kuleta maendeleo Jimbo lake kwa kushirikiana na kila mtu kwa sababu maendeleo yanatakiwa na kila mtu bila kujali itikadi ya chama.
Nikki wa Pili kaingia kwenye story za +255 leo ambapo amesema ilikuwa aachie kazi nyingine inayokwenda kwa jina la ‘Baba Swalehe‘ lakini mipango imesogezwa mbele ili kupisha masuala ya Uchaguzi mkuu uliofanyika Tanzania.
nikki1
Member wa Kundi la Weusi, Nikki wa Pili.
Nikki amesema wanategemea promo kubwa toka kwa vyombo vya habari kwa ajili ya kutangaza kazi zao, lakini vyombo vingi vilibebwa na story za Siasa kwa kipindi hiki ndio maana kazi hiyo ikasogezwa.
Diamond
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz ameshinda Tuzo ya Best Worldwide Act siku chache zilizopita nchini Italy, rapper Joh Makini kaupokea kwa furaha ushindi huo kwa sababu ushindi wake ni heshima kwa Africa pia…
Joh Makini
Joh Makini

waliotembelea blog