Saturday, January 28, 2017


Andreas Weimann2-0 Wolverhampton Wanderers wanaongoza dhidi LiverpoolRichard Stearman Liverpool bado wako nyuma ya bao 1-0. Wolverhampton Wanderers tayari wanaongoza bao dhidi ya Liverpool kwa bao la dakika ya 1 la Richard Stearman.


MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amefungiwa Mechi 4 na kutwangwa Faini ya Pauni 25,000 na FA, Chama cha Soka England, kwa Kosa la Utovu wa Nidhamu alipopatikana na hatia ya kumkashifu Refa na pia kumsukuma Refa Msaidizi.

Wenger, mwenye Miaka 67, alimsukuma Refa Msaidizi Anthony Taylor baada ya Refa wa Mechi yao na Burnley Jon Moss kumuamuru kutoka Uwanjani kwa kutoa Lugha chafu.

Kifungo cha Wenger kinaanza kwa Mechi ya Leo Ugenini na Southampton huko Saint Mary ikiwa ni Mechi ya Raundi ya 4 ya FA CUP.
Mechi nyingine atakazozikosa ni zile za EPL, Ligi Kuu England dhidi ya Watford, Chelsea na Hull City.

Ikiwa Mechi ya Leo itaisha Sare basi Arsenal watarudiana na Southampton huko Emirates na hiyo itahesabika kwenye Kifungo na hivyo Kifungo chake kitaisha Mechi na Chelsea.

Kifungo cha Wenger ni cha kumkataza kukaa Benchi la Ufundi tu na hivyo ni ruhusa kuwepo kwake Uwanjani.
Klopp afanya mabadiliko 9 kwenye kikosi chake leo wakikaribia muda mchache ujao kuumana na Wolverhampton Wanderers


RAUNDI ya 4 ya Kombe Kongwe Duniani, FA CUP, imeanza kwa Sare ya 2-2 wakati Timu ya Daraja la chini Derby County ikiwa Nyumbani kwao ilipowavaa Mabingwa wa England Leicester City.
Wakiwa nyuma kwa Bao 2-1, Leicester walinusurika kichapo baada ya Kepteni wao Wes Morgan kusawazisha Dakika ya 86 na sasa Mechi hii itarudiwa huko King Power Stadium Nyumbani kwa Mabingwa hao wa England ili kupata Mshindi.

Leicester walitangulia kufunga Dakika ya 8 baada Darren Bent kujifunga mwenyewe lakini Bent ndie alieisawazishia Bao Derby Dakika ya 21 na kwenda mbele 2-1 katika Dakika ya 40 kwa Bao la Craig Bryson.
Leo, Jumamosi zipo Mecho 10 na Jumapili zipo 5 ikiwemo ile ya kule Old Trafford kati ya Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Manchester United na Wigan Athletic.

Baadhi ya Mechi za Jumamosi ni ile ya kule Stamford Bridge wakati Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea wakicheza na Timu ya Daraja la chini Brentford.

Siku hiyo hiyo, Vigogo wa England Liverpool, ambao Raundi iliyopita walilazimika kucheza Mechi mbili na Timu ya Daraja la chini Plymouth, wapo kwao Anfield kucheza na Timu nyingine ya Daraja la chini Wolverhampton Wanderers.
Nyingine ni huko White Hart Lane kati ya Tottenham Hotspur na Wycombe Wanderers.
Mechi ya mwisho Siku hiyo ni ile inayohusisha Timu za EPL pekee huko Saint Mary kati ya Wenyeji Southampton, ambao Juzi waliibwaga Liverpool na kutinga Fainali ya EFL CUP, dhidi ya Arsenal.

Jumapili, mbali ya Mechi ya Mabingwa Man United na Wigan, nyingine kali ni ile ya huko Selhurst Park wakati Crystal Palace wakicheza na wenzao wa EPL Man City.

EMIRATES FA CUP:
RAUNDI YA 4
Ratiba/Matokeo:
Ijumaa Januari 27

Derby County 2 Leicester City 2

Jumamosi Januari 28
1530 Liverpool v Wolverhampton Wanderers
1800 Blackburn Rovers v Blackpool
1800 Chelsea v Brentford
1800 Middlesbrough v Accrington Stanley
1800 Oxford United v Newcastle
1800 Rochdale v Huddersfield Town
1800 Lincoln City v Brighton & Hove Albion
1800 Burnley v Bristol City
1800 Tottenham Hotspur v Wycombe Wanderers
2030 Southampton v Arsenal

Jumapili Januari 29

1500 Millwall v Watford
1530 Fulham v Hull City
1700 Sutton United v Leeds United
1900 Manchester United v Wigan Athletic
1900 Crystal Palace v Manchester City


MECHI za Robo Fainakli za AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, zitaanza Jumamosi Januari 29 kwa Mechi 2 kati ya Burkina Faso na Tunisia na kufuatia ile ya Senegal na Cameroon.
Kati ya hizo Mechi mbili ile ya Senegal na Cameroon ndio yenye mvuto na mashamsham hasa baada ya Senegal kucheza vizuri mno kwenye Mechi zao za Kundi B kwa kuzifunga Zimbabwe na Tunisia, zote 2-0 kila moja, na kutoka 2-2 na Algeria wakati wakiwa tayari wamefuzu na pia kuchezesha Rizevu 10 wa Mechi zao 2 za awali.
Tofauti na Senegal, Cameroon, wakiwa Kundi A, walitoka Sare 1-1 na Burkina Faso, kuifunga Guinea-Bissau 2-1 na Sare na Wenyeji Gabon ya 0-0.

Lakini Kocha wa Senegal, Aliou Cisse, Mchezaji wao zamani wa Senegal, Nchi ambayo ni maarufu Kisoka kama Simba wa Teranga, amesisitiza Cameroon ni Vigogo Afrika ambao wametwaa Ubingwa wa Afrika mara 4 wakati wao hawajatwaa hata mara 1.

Ili kuondoa presha kwa Timu yake, Cisse, ambae alikuwa Nahodha wa Simba wa Teranga, amesisitiza: “Hatuwezi kuwa sisi ndio tunaotegemewa kutwaa Ubingwa wakati pia wapo Ghana, Morocco na Congo DR ambao wameonyesha ni wazuri mno!”

Robo Fainali nyingine mbili za AFCON 2017 zitachezwa Jumapili.

AFCON 2017
RATIBA
Robo Fainali

Jumamosi Januari 28
1900 Burkina Faso v Tunisia [RF 1]
2200 Senegal v Cameroon [RF 2]

Jumapili Januari 29
1900 Congo DR v Ghana [RF 3]
2200 Egypt v Morocco [RF 4]

Nusu Fainali
Jumatano Februari 1

2200 Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4

Alhamisi Februari 2
2200 Mshindi RF 2 v Mshindi RF 3

Mshindi wa 3
Jumamosi Februari 4

2200 Aliefungwa NF 1 v Aliefungwa NF 2

Fainali
Jumapili Februari 5

2200 Mshindi NF 1 v Mshindi NF 2

NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1


Beki wa Sunderland Papy Djilobodji amefungiwa Mechi 4 baada ya kukutwa na hatia ya kucheza kwa fujo.
Beki huyo mwenye Miaka 28 alipinga Kosa lake ilipodaiwa alimpiga Usoni kwa Mkono Mchezaji wa West Bromwich Albion Darren Fletcher wakati Timu yake ikichapwa 2-0 Jumamosi iliyopita kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

Tukio hilo halikuonwa na Waamuzi wa Mechi hiyo na kupitiwa na Jopo Huru ambalo sasa limeridhika ni Kosa lililostahili Kadi Nyekundu.

Papy Djilobodji, Mchezaji kutoka Senegal, atafungiwa Mechi 4 badala ya 3 kwa vile Novemba 19 pia alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Sunderland na Hull City.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea sasa atazikosa Mechi za Sunderland dhidi ya Tottenham hapo Januari 31 ikichezwa Nyumbani, na nyingine ni na Crystal Palace, Ugenini, Southampton, Nyumbani, na Everton, Ugenini.

Kukosekana huku kwa Papy Djilobodji ni pigo kwa Sunderland ambao wako mkiani mwa EPL.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli kwa kuridhia kufunguliwa tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kadhalika, TFF inamshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa juhudi zake na kwamba namna aliyoonesha ushirikiano kufanikisha suala la kufunguliwa uwanja huo uliofungiwa matumizi yake na Serikali, Oktoba mwaka uliopita.
TFF inachukua nafasi hii kuahidi kuwa itasimamia matumizi mazuri ya uwanja huo kwa kutoa elimu kwa wadau ili kuutumia uwanja huo vema ikitambua kuwa ni hazina ambayo imetokana na nguvu na gharama kubwa za Serikali kuujenga uwanja huo.

TFF inatahadharisha mashabiki wa mpira wa miguu kwamba uwanja huo umejengwa kwa gharama kubwa hivyo ni jukumu letu kuutuza na kuutumia vema kwa sababu ni hazina kubwa tuliyonayo na ni miongoni mwa urithi bora kwa vizazi vijavyo.

Kwa sasa tumetuma maombi yetu Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuomba kuutumia uwanja huo kwenye mchezo wa kesho Jumamosi Januari 28, mwaka huu kati Simba na Azam utapigwa kwenye uwanja huo wa Taifa, Dar es Salaam kadhalika keshokutwa katika mchezo kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na Mwadui ya Shinyanga.

Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inaonesha kuwa ligi hiyo huko Mbeya kutakuwa na ‘derby’ kwa maana ya mchezo wa upinzani baina ya timu zinazotoka mkoa mmoja wa Mbeya ambazo ni Tanzania Prisons na Mbeya City utakaochezwa na Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Jumapili Januari 29, mwaka huu kutakuwa na mchezo mwingine ambao Young Africans itacheza na Mwadui jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Majimaji ya Songea itasafiri hadi Mtwara kucheza na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Jumatatu Januari 30, 2017 kutakuwa na mchezo mwingine kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


BEKI wa Sunderland Patrick van Aanholt anafanyiwa upimwaji Afya yake huko Crystal Palace baada Klabu hizo mbili kuafikiana Dili inayotegemewa kufikia Pauni Milioni 14.
Beki huyo wa Kimataifa wa Netherlands mwenye Miaka 26 ataungana tena na Bosi wa Palace Sam Allardyce ambae walikuwa nae wote Sunderland.
Van Aanholt alianza kuchezea Chelsea lakini akapelekwa kucheza nje kwa Mkopo kewenye Klabu 5 na hatimae kusaini Mkataba wa kudumu na Sunderland Mwaka 2014 na kuichezea Mechi 95.

Big Sam, kama anavyojulikana Meneja wa Palace, amedokeza kuwa wapo kwenye mipango ya kusaini Wachezaji wengine wapya kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa Januari 31 huku akidokeza hawajapokea Ofa yeyote ya Mchezaji yao yeyote kutakiwa na Klabu nyingine.

Ameeleza: “Zipo dili kadhaa lakini hazijakamilika.”
Van Aanholt amekuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Allardyce tangu atue Palace Mwezi uliopita kuchukua nafasi ya Alan Pardew.

Mwingine aliesainiwa na Big Sam ni Jeffrey Schlupp kutoka kwa Mabingwa wa England Leicester City kwa Dau la Pauni Milioni 13.


Kwa mara nyingine tena Refa Jon Moss amemkwaruza Meneja wa Manchester United Jose Mourinho baada ya maamuzi yake kwenye Mechi ya Pili ya Nusu Fainali ya EFL CUP hapo Jana kumkera Mreno huyo wakati Hull City ikiifunga Man United 2-1.

Licha ya kipigo hicho, Man United imetinga Fainali ya EFL CUP baada ya kuifunga Hull City 2-0 katika Mechi ya kwanza na hivyo kusonga kwa Jumla ya Mabao 3-2 na Fainali itakumbana na Southampton hapo Februari 26 huko Wembley Jijini London.
Wakiwa kwenye wimbi la kutofungwa Mechi 17, Man United Jana huko KCOM Stadium walijikuta wako nyuma kwa Bao 1-0 baada ya Refa Jon Moss kutoa Penati kwa Hull City na Tom Huddlestone kufunga.
Penati hiyo ilizua utata na hata kuleta Mjadala mkali kwa Wachambuzi wa Soka huko England.
Man United walisawazisha Bao hilo la Dakika ya 35 kwa Bao la Dakika ya 66 la Paul Pogba lakini Hull wakafunga Bao la Pili Dakika ya 85 kupitia Oumar Niasse.
Kwenye Mechi hiyo, mara 3 Man united walilia kupewa Penati na Refa Jon Moss kupeta tu na ya wazi kati ya zote ni pale Chris Smalling aliposukumwa ndani ya Boksi na Tom Huddlestone.
Akihojiwa baada ya Mechi hiyo, Mourinho alionyesha kukerwa na Refa Jon Moss alieamua Marcos Rojo alimsukuma Harry Maguire na kutoa Penati.
Mourinho alieleza: “Sikuona Penati. Ujumbe ni Wachezaji wetu kusherehekea tumetinga Fainali! Sitaki kuzungumzia Penati!”
Mourinho na Historia yake na Refa Jon Moss:
-Mwezi Novemba Mwaka Jana Refa Jon Moss alimtoa Uwanjani Jose Mourinho kwenye Mechi ya Man United na West Ham kwa kuipiga Teke Chupa ya Maji na akapigwa Faini na Kufungiwa kutokaa Benchi.
-Akiwa Meneja wa Chelsea, Mourinho alifungiwa kutokanyaga Uwanjani baada ya kumtukana Refa Jon Moss kwenye Mechi na West Ham na juu yake kupigwa Faini ya Pauni 40,000.

Nae Mchezaji wa zamani wa Manchester United Phil Neville alimponda Refa Jon Moss kwa kutoa hiyo Penati.

Alisema: “Kwanza nilidhani Phil Jones kamchezea Faulo Oumar Niasse nilipoangalia tena nikaona na Rojo. Ilikuwa ni Rojo kwa Harry Maguire lakini haikustahili Penati. Refa Jon Moss alikuwa kwenye nafasi nzuri kuona. Haikuwa Penati na ni uamuzi mbovu kabisa!”


LIGI DARAJA LA KWANZA
Mechi namba 34 (Pamba vs Friends Rangers). Kamishna wa mechi hiyo Mnenge Suluja amepewa Onyo Kali kwa kutoripoti kitendo cha timu ya Pamba kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) ikiwa na wawakilishi watatu badala ya wanne. Kitendo hicho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 35 (Kiluvya United vs Lipuli). Timu ya Lipuli imepewa Onyo Kali kwa kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) ikiwa na wawakilishi watatu badala ya wanne. Kitendo hicho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Pia mshabiki wa Kiluvya United, Bw. Athuman Mzongela anapelekwa Kamati ya Nidhamu kwa kuwavamia waamuzi na kutaka kuwapiga wakati wa mapumziko. Hata baada ya mchezo aliendelea kuwatolea lugha chafu waamuzi na Msimamizi wa Kituo.
Mechi namba 36 (African Sports vs Ashanti United). Daktari wa Ashanti United, Andrea Mbuguni amefungiwa miezi sita na kupigwa faini ya sh. 200,000 kwa kuondolewa kwenye benchi baada ya kumtolea lugha chafu Mwamuzi Msaidizi namba moja.
Mechi namba 38 (Lipuli vs Mshikamano FC). Kocha wa Mshikamano FC, Hamisi Kinonda amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 baada ya kuondolewa kwenye benchi kwa kupinga muda wa nyongeza wa dakika tano, na kumtolea lugha ya matusi Mwamuzi wa Akiba. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Wachezaji wa Mshikamano FC, John Mbise jezi namba 9, Abdallah Makuburi (5), Ally Mangosongo (12) na kipa Steven Peter (1) wanapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kumshambulia Mwamuzi Bryson A. Msuya.
Lakini pia Mwamuzi Bryson A. Msuya amefungiwa mwaka mmoja kwa kutozingatia sheria ipasavyo wakati akitoa penalti dhidi ya timu ya Mshikamano FC, na ripoti yake kufanana na ile ya Kamishna.
Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Makongo Katuma amefutwa katika orodha ya waamuzi wanaotambuliwa na TFF kwa kuwapiga vichwa wachezaji wawili wa Mshikamano FC wakati Mwamuzi wa Kati alipokuwa akishambuliwa na wachezaji wa timu hiyo wakati wakipinga adhabu ya penalti dhidi yao.
Adhabu hizo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1) na 38(1c) na (1e) za Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi. Mwamuzi Katuma pia alipata alama za chini ambazo zisingemruhusu kuendelea kuchezesha Ligi Daraja la Kwanza.
Naye Mwamuzi wa Akiba, Hashim Mgimba ameondolewa kwenye ratiba kwa kuonyesha muda wa nyongeza (added time) tofauti na ule alioelekezwa na Mwamuzi. Adhabu dhidi ya Mgimba imezingatia Kanuni ya 38(1d) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Kamishna wa mechi hiyo Fidelis Ndenga wa Njombe ameondolewa kwenye ratiba ya makamishna kwa taarifa yake kufanana na ile ya Mwamuzi. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Makamishna.
Pia Kamati imetoa mwito kwa vyombo vya usalama (askari polisi) kutumia nguvu za wastani katika kutuliza ghasia viwanjani, hasa pale wanapotaka kushughulikia eneo linalohusu wachezaji.
Uwanja wa Kichangani umeondolewa kutumika kwa mechi za Ligi, hivyo klabu za Iringa sasa timu zao zitatumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini humo kwa mechi zao la Ligi. Uwanja huo ulikuwa kwenye matengenezo ambayo tayari yamekamilika.
Mechi namba 39 (Polisi Dar vs Pamba FC). Klabu ya Pamba imepewa Onyo Kali kwa kutofika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting). Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 33 (KMC vs JKT Mlale). Kocha wa JKT Mlale, Edgar Msabila amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 baada ya kuondolewa kwenye benchi la ufundi (orderd off) kwa kutoa lugha chafu. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 38 (Kimondo FC vs Njombe Mji). Kocha wa Njombe Mji, Abdul Banyai amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 kwa kumtolea Mwamuzi lugha ya matusi, na kulazimisha wachezaji wake wajiangushe ili kupoteza muda.
Mechi namba 40 (Coastal Union vs Kurugenzi). Wachezaji wawili wa Kurugenzi; Kipa Hamza Mpatula na Optatus Lupekenya wamefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 kila mmoja kwa kosa la kupigana wakiwa uwanjani baada ya mechi kumalizika. Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 37(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Mechi namba 36 (Rhino Rangers vs Polisi Mara). Klabu ya Rhino Rangers imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 20. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(9) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 38 (Mgambo Shooting vs Rhino Rangers FC). Kocha wa Mgambo, Moka Shabani amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 kwa kutoa lugha ya matusi kwa Mwamuzi wakati timu zikielekea vyumbani baada ya kumalizika kipindi cha kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 40(1) ya Ligi Daraja la Kwanza.


LIGI DARAJA LA PILI

Mechi namba 17 (Abajalo vs Burkina Faso). Klabu ya Burkina Faso imepigwa faini ya sh. 100,000 kwa kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting). Adhabu imezingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 18 (Cosmopolitan vs Changanyikeni). Klabu ya Changanyikeni FC imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani kushangilia ushindi baada ya filimbi ya mwisho. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 19 (Kariakoo vs Cosmopolitan). Klabu ya Kariakoo imepewa Onyo Kali kwa timu yake kutokuwa na daktari katika mechi hiyo. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(3).
Mechi namba 16 (Sabasaba vs Namungo). Klabu ya Sabasaba imepewa Onyo Kali kutokana na washabiki wake kuwazonga waamuzi wakati wakielekea vyumbani baada ya mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kumalizika. Uamuzi huo umezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Pili.
Mechi namba 17 (Mawezi Market vs Mkamba Rangers). Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 100,000 kwa kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting), na pia kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 35. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
Mechi namba 19 (Namungo vs Mighty Elephant). Mighty Elephant imepigwa faini ya sh. 100,000 kutokana na wachezaji wa akiba na viongozi wake kuingia uwanjani kushangilia bao la timu yao. Kitendo hicho ni kinyume na Kanuni ya 14(7), na adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(47) ya Ligi Daraja la Pili.

Friday, January 27, 2017

Ongeza kichwa






Saturday, January 21, 2017



Ni taarifa rasmi kutoka IKULU Dar es salaam juu ya maamuzi mapya ya Rais John Pombe Magufuli ambaye leo January 21 2017 amemteua Anne Kilango Malecela kuwa Mbunge kwenye bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Cheo cha mwisho alichopewa Anne Kilango kilikua ni ukuu wa mkoa wa Shinyanga lakini April 11 2016 Rais Magufuli alitengua uteuzi wake na katibu tawala wa mkoa Abdul Rashid Dachi baada ya mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa hauna Watumishi hewa.
Taarifa ya IKULU leo imesema baada ya Anne Kilango kuteuliwa, ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za bunge.

ULIPITWA? TAZAMA WANAJESHI WA TANZANIA WAKIONYESHA UWEZO WAO MBELE YA RAIS MAGUFULI


Usiku wa January 21 2017 wawakilishi pekee wa ukanda wa Afrika Mashariki katika michuano ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON 2017, timu ya taifa ya Uganda ilitolewa rasmi katika michuano ya mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini nchini Gabon.
Uganda wameaga mashindano hayo baada ya kukubali kipigo cha goli 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Misri katika mchezo wao wa pili wa Kundi D, Uganda wanaaga mashindano hayo na kuwa wanasubiria mchezo wao wa kukamilisha ratiba dhidi ya Mali, hawana uwezo wa kufuzu hatua ya robo fainali hata wakipata ushindi wa aina yoyote ile.
Abdallah El Said wa Misri ndio alihitimisha safari ya Uganda katika michuano ya AFCON 2017, baada ya kufunga goli dakika ya 89 kwa kutumia vyema assist iliyotolewa na Mohamed Salah, kwa mujibu wa rekodi Uganda ni dhaifu kwa Misri, kwani leo wanakuwa wamefungwa kwa mara ya 16 na mara ya mwisho Uganda



Ay ambaye ni staa wa smash hit ya ‘zigo’ na kwasasa akiwa ana brand new single na Nyasinski amechukua time yake na kuwaandikia Wasanii wenzake yafuatayo >>>> ‘Ndugu zangu Wasanii wa kibongo, Wadau na Mashabiki wa muziki nimeona sio vibaya kuwashirikisha na nyie jambo hili
Ili Producers wa Kibongo waweze kubadilisha Tunes kwa beats zao na waendelee kutisha KULIKO JANA nawaomba wasanii wenzangu muweke utaratibu wa kusafiri nao mnavyotoka nje ya Afrika Mashariki wakienda, wakiona, wakijifunza na kujiongeza LAZIMA TUTATISHA SANA‘ – AY
Nimeona sana Afrika Magharibi wana hesabu hizo ndio maana wana Tunes za kila aina,Tuna Producers wazuri sana ila wanahitaji kusafiri zaidi,Mfano mzuri ni @majani187 @nahreel@hermyb na @marcochali wamepata exposure ndio maana wana Tunes Unique‬ all the time #ZEE – @AyTanzania kwenye Instagram
UMEPITWA? Kijana aliyemshtua Mama Kanumba, Dully Sykes kuhusu ushirikiano na Alikiba je? tazama kwenye hii video hapa chini kujionea kila kitu


January 21 2017 Mabingwa watetezi wa Kombe la ASFC klabu ya Dar es Salaam Young Africans ilishuka dimba kuanza kutetea taji lake hilo, kwa kucheza dhidi ya Ashanti United katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, katika mchezo huo Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 4-1.


1-1Juan Mata kawapa zawadi Stoke City dakika ya 19 ya kipindi cha kwanza.Mata kajifunga bao dakika ya 19 na kuwapa zawadi Stoke City kipindi cha kwanza. mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika United 0 Stoke City 1.Man United kwenye harakati za kupunguza pengo na kusonga mbele...




Bao za liverpool zilifungwa na Roberto Firmino dakika ya (55' na dakika ya 69') Huku bao za Swansea City zikifungwa na Fernando Llorente dakika ya (48' na dakika ya 52')
Kipindi cha pili Gylfi Sigurdsson akiwafungia bao la ushindi dakika ya (74') na mtanange kumalizika dakika 90 kwa Swansea kujikwamua mkiani na kupanda juu na kuwashangaza Mashabiki wa Majogoo na kwenye Uwanja wao.



Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya soka ya FIFA kwa miaka minne ijayo. Uteuzi huo unaanza mwaka huu 2017 hadi 2021.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Januari 18, 2017 iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samoura inasema: “Tuna faraja kukufahamisha kuwa umeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya FIFA. Tunachukua nafasi hii kukupongeza kwa uteuzi huu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Kamati hiyo inayoongozwa na Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Bara la Asia, ina majukumu ya kusimamia mipango ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani kote.
Wajumbe wengine wote watatangazwa kwenye tovuti ya FIFA ambayo ni www.FIFA.com.
Huu ni mfululizo wa Tanzania kupata nafasi katika vyombo vikubwa vinavyoendesha soka FIFA na CAF. Mwishoni mwa mwaka jana, CAF – Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika lilimteua Rais Malinzi kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati maalumu inayoongozwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou ya kuboresha mfumo wa uongozi wa CAF.
TFF inamshukuru Rais Gianni Infantino na kamati yake ya ushauri kwa kumteua Malinzi katika nafasi ya ujumbe katika kamati hiyo muhimu ya maendeleo ya soka ulimwenguni.


Ligi Kuu England
RATIBA
Jumamosi Januari 21

15:30 Liverpool v Swansea City
18:00 Bournemouth v Watford
18:00 Crystal Palace v Everton
18:00 Middlesbrough v West Ham United
18:00 Stoke City v Manchester United
18
:00 West Bromwich Albion v Sunderland
20:30 Manchester City v Tottenham Hotspur
Jumapili Januari 22
15:00 Southampton v Leicester City
17:15 Arsenal v Burnley
19
:30 Chelsea v Hull City

MANCHESTER City sasa wameruhusiwa kumtumia Staa Mbrazil wa Miaka 19 Gabriel Jesus kwenye Mechi yao ya EPL, Ligi Kuu England, ya kesho Jumamosi dhidi ya Tottenham Hotspur.
City walishafikia makubaliano na Klabu ya Brazil Palmeiras tangu Mwezi Julai Mwaka Jana kumnunua Kinda huyo wa Brazil mwenye Miaka 19 kwa Dau la Pauni Milioni 27 na pia kukubali Mchezaji huyo abakie Palmeiras hadi Msimu wa Brazil utakapoisha Mwezi Desemba.
Jesus amekuwa Kambini na City kwa Wiki 3 sasa lakini ukiritimba umekwamisha Uhamisho wake kukamilika rasmi na hivyo kusitisha kuichezea rasmi City.
Kinda huyo ndio kwanza amechomoza kwenye Soka la Dunia akiwa na Msimu wa Pili tu na Palmeiras lakini akaiongoza Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Taifa Mwezi Novemba baada ya kutwaa Medali ya Dhahabu akiichezea Brazil kwenye Michezo ya Olimpiki, RIO 2016, Mwezi Julai.
Jesus alianza kukichezea Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Taifa ya Brazil Mwezi Septemba Mwaka Jana na kufunga Bao 4 katika Mechi zake 6.
Hivi sasa Man City wapo Nafasi ya 5 kwenye EPL, wakiwa Pointi 10, nyuma ya Vinara Chelsea baada ya kufungwa Mechi 2 kati ya 3 walizocheza mwisho.


JE WAJUA?
-Jesus alijilukana kama Gabriel Fernando alipoanza kuichezea Palmeiras akiwa na Miaka 17.

-Akiwa huko alipewa Jezi Namba 33 [Umri wa Yesu Kristu] na mmoja wa Maafisa Habari wa Klabu hiyo akammwambia atumie Jina la Gabriel Jesus.

-Akiwa na Man City, Jesus pia atavaa Jezi Namba 33 ambayo awali ilivaliwa na Nahodha wa City Vincent Kompany.

Wednesday, January 18, 2017


 Wasichana wanne wa Tanzania wakiaga  kwa kupungia mikono huku wakiwa na , Bendera ya Taifa waliyokabidhiwa na Kamishna Mkuu wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), Symphorosa Hangi katika hafla ya kuwaaga kwenda Uganda ambako watakutana na wenzao 31 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati katika mafunzo ya uongozi na utamaduni katika nchi hizo. Hafla hiyo ilifanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi. Kutoka kulia ni Farida Mjoge,Elizabeth Betha, Edna Chembele na Ummy Mwabondo. (PICHA, HABARI NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Kamishna Mkuu wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), Symphorosa Hangi (kushoto) akiwakabidhi wasichana wanne, Bendera ya Taifa katika hafla ya kuwaaga kwenda Uganda ambako watakutana na wenzao 31 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati katika mafunzo ya uongozi na utamaduni katika nchi hizo. Hafla hiyo ilifanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi. Kutoka kulia niElizabeth Betha, Edna Chembele, Farida Mjoge na Ummy Mwabondo. 


Na Richard Mwaikenda

WASICHANA wanne wameondoka kwenda Uganda  kwenye programu maalumu ya kubadilishana uzoefu wa mafunzo ya uongozi na utamaduni.


Wakifika Uganda wataungana na wenzao 31 kutoka nchi nane za Afrika Mashariki na Kati, ambapo watapigwa msasa wa mafunzo hadi Januari 25, mwaka huu watakapotawanywa kwenda nchi mbalimbali.


Wasichana hao wanachama wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA),waliondoka Uwanja wa Ndege wa Kimaitafa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, juzi kwa Ndege  ya Kenya Airways, baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Kamishna Mkuu wa Tgga,  Symphorosa Hangi.


Wasichana hao 35 watagawanywa katika nchi hizo nane ambapo nchini wataletwa watatu kutoka katika baadhi ya nchi hizo, kuja kujifunza masuala ya uongozi na utamaduni.


Akizungumza wakati wa kuwaaga wasichana hao, Kamishna Mkuu wa Tgga, Hangi  alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wasichana ili wawe viongozi bora wa baadaye katika nchi zao ikiwemo pia kujiamini na kujithamini.


Alitaja nchi zitakashiriki kwenye programu hiyo ambayo kwa hapa nchini  ilianza mwaka jana, kuwa ni; Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi, Zimbabwe na Afrika Kusini.


Alisema kuwa watakapokuwa kwenye nchi hizo husika, kila mmoja ataishi maisha ya kujitegemea kwa kwenda vijijini kuishi na wananchi na kuzungumza nao kuhusu mambo mbalimbali ya maisha ikiwemo uongozi, utamaduni, kujiamini na kujithamini. Gharama za kwenda katika nchi hizo hufahiliwa na Taasisi ya FK Norway ambayo huwapatia nauli, fedha za malazi, posho na masuala ya afya.


Alisema kuwa watakaporejea nchini Julai mwaka huu, watapaswa kutoa mrejesho wa waliojifunza huko, ili usaidie kuwaelimisha wasichana wengine nchini.



 Kamishna akiwakabidhi nyaraka mbalimbali za kazi


 Ni furaha iliyoje

 Wakipiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa TGGA


 Wakipiga picha na dereva wa TGGA,Juma Rashid

Kamishna akiagana na mmoja wa wasichana hao

Tuesday, January 17, 2017



Meneja wa zamani wa Manchester United na Uholanzi Louis van Gaal amesema amestaafu kazi ya ukufunzi baada ya miaka 26 katika taaluma yake. Van Gaal, 65, hajafanya kazi uwanjani tangu alipopigwa kalamu na United saa chache baada ya kushinda kombe la FA mwezi Mei 2016.
Akiongea na jarida la Telegraaf la nchini Uholanzi Van Gaal amesema ”Mambo mengi yametokea kwa familia yangu, unakuwa binadamu kwa mara nyingine kwa kukiri ukweli, kwa fikra zangu nilidhani nitastaafu, nikafikiria pia itakuwa ni mapumziko ya muda, lakini kwa hivi sasa sidhani kama nitarudi kwenye kazi ya ukocha,” Van Gaal 
Van alitangaza uamuzi wake siku ya Jumatatu baada ya kupata tuzo ku katika taaluma yake kutoka kwa serikali ya Uholanzi kwa mchango wake katika soka. Alisema shida za kifamilia ndizo zilichangia uamuzi wake huo, huku gazeti la De Telegraaf likisema uamuzi wake ulichangiwa na kifo cha mkwe wake mwezi Disemba.
Van Gaal pia alikuwa kocha wa klabu ya Ajax, Barcelona, Bayern Munich, AZ na Manchester United ambayo ilikuwa club yake ya mwisho kuifundisha msimu uliopita. Mbali na kuwa kocha, Van Gaal pia amewahi kuzichezea club za Ajax, Royal Antwep, Telstar, Sparta Rotterdam na AZ.

Raia huyo muholanzi ameweka wazi kuwa alikataa nafasi nzuri za kuendeleza taaluma yake kwa kukataa kazi mataifa ya Mashariki ya Mbali.

waliotembelea blog