Tuesday, October 13, 2015


Robin Van Persie akiifich uso!
Dakika ya 83 Robin van Persie Alifunga bao na kuifanikishia bao la pili na matokeo kuwa 3-2.Bao za Czech Republic zimefungwa na Pavel Kaderabek dakika ya 24 na  Josef Sural dakika ya 35 bao la tatu likiwa la kujifunga kupitia kwa Robin van Persie dakika ya 66, Bao la Netherlands limefungwa na Klaas-Jan Huntelaar dakika ya 70 na kufanya bao kuwa 3-1.
Van Persie akipagawa baada ya kukosa nafasi ya wazi
Netherlands 0 v 2 Czech Republic

Siku 11 zimebaki kuifikia October 25 2015, ambapo Tanzania itakuwa kwenye tukio jingine kubwa na la kihistoria, Watanzania Milioni 22.7 waliothibitishwa na Tume ya Uchaguzi NEC, watapiga Kura kuchagua Viongozi katika ngazi ya Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Kwa sasa bado mchakamchaka wa Kampeni kwenye Majukwaa ya Siasa bado unaendelea, jana October 12 2015 Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA ambaye anawakilisha umoja wa wa Vyama vya UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa alitua kwa mara nyingine kwenye Viwanja vya Furahisha, ndani ya Mwanza kwa ajili ya kuendelea na Kampeni zake.
CRIdqzEWgAAnrjB
6
.
OTH_0562
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru
OTH_0667
OTH_0892
OTH_0900
OTH_0764
OTH_9729
Kutokana na wingi wa watu, wengine walizidiwa wakawa wanapoteza fahamu.
OTH_9751
OTH_9823
 CRIeJ-qWoAAJVAq CRIfHSWWsAA0F2B CRIOWX0WoAAVkyd


Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Crsistiano Ronaldo ameingia tena katika headlines baada ya kutwaa tuzo nyingine ya ufungaji bora. Cristiano Ronaldo ambaye September 30 aliweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid kwa kufunga jumla ya goli 324 na kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Raul Gonzalez.
2D5E96FB00000578-0-image-a-40_1444741292286
October 13 Cristiano Ronaldo alipokea kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka mfungaji bora wa Ulaya kwa kufunga magoli mengi katika mechi zinazohushisha mechi za ndani ya nchi husika kwa kufunga jumla ya goli 48 katika mechi 35. Ronaldo amechukua kiatu cha dhahabu cha tatu akiwa na Real Madrid baada ya mara ya kwanza kutwaa tuzo hiyo akiwa Man United msimu wa 2007/2008.
2D5F31A500000578-3270764-image-a-87_1444745041945
Kwa ujumla Ronaldo anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mara nne, huenda ukawa unajiuliaza namna au mfumo unaotumika kutoa tuzo hiyo, tuzo hii uhusisha wachezaji wanaotokea katika Ligi kubwa kama Ligi Kuu Uingereza au Hispania hata kama watafunga magoli machache kuliko wachezaji wanaotoka Ligi dhaifu wanaweza kutwaa tuzo hiyo.
2D5EAEB500000578-0-image-a-35_1444741243390
2D5F432100000578-3270764-image-a-68_1444744302882
2
Waliowahi kutwaa tuzo hiyo
1
Waliokuwa wanawania kwa msimu wa 2014/2015



Klabu ya Manchester United ya Uingereza ni moja kati ya vilabu vilivyotumia fedha nyingi katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August 2015. Toka kocha Louis van Gaal ajiunge na klabu ya  Man United, uongozi wa klabu hiyo umetumia zaidi ya pound milioni 250 kwa ajili ya kusajili wachezaji.
1D9FF5C700000578-0-image-a-43_1444732250406
Ed Woodward
Man United inaonekana kufanya usajili kwa malengo ya baadae zaidi kwani imekuwa ikisajili wachezaji wenye umri mdogo kama Memphis DepayAnthony Martial na Morgan Schneiderlin. Stori kutoka kwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward kuhusu matumizi hayo ya fedha yaliyotumika katika usajili. 2CF1C2B400000578-0-image-a-44_1444732290529
Ed Woodward amekiri kuwa bado Manchester United itaendelea na matumizi ya fedha nyingi kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake, Ed Woodward amesema Man United katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August walikuwa wakihusishwa kutaka kusajili wachezaji wengi zaidi lakini walifanikiwa kusajili sita. Hivyo Man United bado itaendelea kutumia fedha nyingi katika usajili ili kuimarisha kikosi.


RAIS JAKAYA KIKWETE (KUSHOTO) AKIPOKEA TUZO KUTOKA KWA MWENYEKITI WA TASWA, JUMA PINTO.

Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo za Michezo Tanzania (Taswa) kimetoa tuzo maalum kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na mchango wake mkubwa katika michezo katika kipindi cha miaka yake 10 ya uongozi.


Kikwete alipewa tuzo hiyo jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Lakini pamoja na tuzo hiyo, Kikwete naye aliwakabidhi tuzo wanamichezo mbalimbali waliofanya vizuri wakati wa kipindi chake.

AKIMPA TUZO MWANARIADHA, SAMSON RAMADHANI

KWA NIABA YA MWANAYE AKIMPA TUZO MAMA YAKE MZAZI MWANAKIKAPU, HASHEEM THABEET...

AKIMPA TUZO BONDIA FRANCIS CHEKA

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI AKITOA NGAO KUONYESHA KUTAMBUA MCHANGO WA JAKAYA KIKWETE KATIKA MCHEZO WA SOKA

SALEH ZONGA, MMOJA WANAKIKAPU WAKONGWE NA KIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA (TBF) AKIMPA RAIS KIKWETE TUZO YA MPIRA


Mchezaji wa Manchester United Memphis Depay amekwaruzana na Mchezaji wa zamani wa Klabu hiyo Robin van Persie wakati wa mazoezi wa Timu ya Taifa ya Netherlands. Tukio hilo limethibitishwa na Kocha wa Netherlands Danny Blind lakini amepuuza umuhimu wake na imefahamika kuwa lilitokea kabla ya Mechi ya Jumamosi ya EURO 2016 ambayo Netherlands iliifunga Kazakhstan 2-1.
Kocha Blind, ambae mwanawe, Daley, ni Mchezaji mwenzake Depay huko Man United ambae pia yumo Timu ya Taifa ya Netherlands, alieleza: “Yapo matukio mazoezini ambapo Wachezaji hutofautiana. Mnayazungumza. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa na yamekwisha.”
Blind pia alisisitiza kuwa tukio hilo halikumfanya ampige Benchi Van Persie kwenye Mechi na Kazakhstan ambayo aliingizwa Kipindi cha Pili na kufikisha Mechi 100 kwa Nchi yake.
Pia Van Persie, ambae aliihama Man United Mwezi Julai kwenda Fenerbahce ya Uturuki ukiwa ni Mwezi mmoja tu baada ya Depay kuhamia Man United, ndie Mfungaji Bora wa Holland katika Historia ya Nchi hiyo akiwa na Bao 49.


Mshambuliaji matata Mbwana Aly Samatta anayeichezea klabu ya TP Mazembe ametajwa miongoni mwa wachezaji 24 watakaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika anayecheza ligi ya barani Afrika.

Uteuzi wake umetokea siku chache tu baada yake kuisaidia Taifa Stars kufika raundi ya pili ya mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Magoli yake matano katika awamu za robo fainali na nusu fainali yaliiwezesha TP Mazembe kufika fainali ya kombe la kilabu bingwa barani Afrika kwa mara yake ya kwanza tangu mwaka wa 2010.

Mwaka jana, tuzo hiyo ilitwaliwa na raia wa Congo Firmin Ndombe Mubele.
Katika hatua ya robo fainali, Samata alifunga magoli matatu walipoicharaza Moghreb Tetouan kwa magoli 5-0 na kufuzu kwa nusu fainali.
Licha ya kupoteza mechi ya mkondo wa kwanza wa nusu fainali kwa magoli 2-1 dhidi Al Merreikh ya Sudan, Mazembe iliibuka na ushindi wa 3-0 baada ya Samatta kufunga magoli mawili katika dakika za 53 na 70.
Raia wa Ivory Coast, Roger Assale alifunga kazi dakika ya 72 na kuiwezesha Mazembe kuondoka na ushindi wa 4-2 na kuingia fainali ambapo itachuana na USM Alger Oktoba 30.
Mwaka jana, Samatta alitambulika na klabu yake ya TP Mazembe kwa kutunukiwa mchezaji bora wa klabu mwaka wa 2013.

Uteuzi huo huenda ukampiga jeki mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Simba kwani tayari amefichua hamu yake ya kucheza soka barani Ulaya.


UONGOZI wa Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park umetoa mwaliko kwa Vijana wote na Watanzania kwa ujumla kwenda kutumia Eneo hilo jipya na la kisasa kabisa.
Uwanja huo upo Kidongo Chekundu katikati ya Jiji la Dar es Salaam na umejengwa kutokana na kuhudi kubwa za Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, na kwa ushirikiano wa Klabu ya Ligi Kuu England, Sunderland, na Kampuni ya Marekani ya Nishati, Symbion.
Ndani ya Eneo hilo upo Uwanja mkubwa wa kisasa wenye Kapeti la 3G pamoja na Kiwanja cha kucheza Mechi za Timu za Wachezaji Watano dhidi ya Watano, upo Uwanja wa Mpira wa Vikapu, Mpira wa Mikono na wa Magongo.
Viwanja vyote vina Taa za kutumika Usiku na yapo ya Majengo ya Menejimenti pamoja na Vyumba vya Kubadilishia Jezi.

Akitangaza mwaliko huu kwa Vijana, Afisa Mwandamizi wa Utawala, Ismail A. Shah, amesema Timu ambazo zitahitaji kufanya mazoezi au kucheza Mechi kwa Kipindi cha kuanzia Saa 1 Usiku hadi Saa 4 Usiku, zipeleke maombi na majina kamili ya Wachezaji/Washiriki.
Kwa maelezo zaidi Waombaji wametakiwa kuwasiliana na Namba ya Simu 0714436347.

waliotembelea blog