Mchezo wa soka ni mchezo ambao unapendwa
na watu wengi duniani ila mtu pekee ambaye anatajwa kuwa na nafasi ya
kuweza kufanya maamuzi ndani ya uwanja ni refa ambaye mara nyingi
amekuwa akiambulia lawama kutoka kwa wachezaji na viongozi wa timu
wanaoamini kuwa wameonewa, najua umewahi kusikia refa akipigwa na
wachezaji au mashabiki wa timu fulani.
Hata kuna wakati wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Stephane Mwasika waliwahi kumpiga refa Israel Nkongo ambaye waliamini kuwa hakuchezesha mechi yao kwa haki bali alipendelea Azam FC, tukio ambalo liliwafanya wapate adhabu, achana na beki huyo wa Yanga wa zamani mtu wangu, nimekutana na video mtandaoni ya vioja vya refa mbabe.
Najua umezoea kusikia wachezaji
wakimpiga refa, ila refa huyu anakupiga na kadi anakuonesha kama
unapingana na uamuzi wake, cheki kipande cha video cha dakika 2 baada ya
refa kuamuru penati wachezaji walianza kumzonga na yeye akawa
anawakwepa ila baadae akampiga ngumi mchezaji hadi na kumuangusha chini
na mwingine alimpiga teke yaani hataki kukupa nafasi ya kumpiga.