Tuesday, February 24, 2015

LEO JUMANNE, Februari 24, Uwanja wa Etihad Jijini Manchester utalipuka kwa mpambano mkali wa Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI kati ya Manchester City na FC Barcelona.
Mechi hii ni Marudio ya Mechi ya Msimu uliopita ya Raundi hii hii ya Mashindano haya wakati Man City ilipotolewa na Barcelona kwa Jumla ya Mabao 4-1 katika Mechi mbili ambazo kila Mechi City ilimaliza Mtu 10 baada ya Mchezaji wao mmoja kupewa Kadi Nyekundu.

Katika Mechi hizo, Barcelona walishinda Mechi ya Kwanza iliyochezwa Etihad Bao 2-0 na kwenye Marudiano huko Nou Camp, Barca ilishinda Bao 2-1.Katika Mechi hizo, Barcelona walishinda Mechi ya Kwanza iliyochezwa Etihad Bao 2-0 na kwenye Marudiano huko Nou Camp, Barca ilishinda Bao 2-1.

NAHODHA wa Manchester United ametamka kuwa baada ya kufungwa na Swansea City basi hawana budi kuifunga Sunderland Jumamosi la sivyo wataikosa UEFA CHAMPIONS LIGI.
Jumamosi, wakicheza huko Liberty Stadium, Man United waliongoza Bao 1-0 lakini wakairuhusu Swansea kuwachapa Bao 2-1 kikiwa ni kipigo chao cha pili katika Mechi 20 zilizopita chini ya Meneja Louis van Gaal.

Ingawa bado zipo Mechi 12 hadi Msimu wa Ligi Kuu England kunamalizika, lakini Mechi zao 7 baada ya Sunderland Jumamosi hii ni dhidi ya Tottenham na Liverpool, zinazowania 4 Bora kama wao, pia dhidi ya Manchester City na Chelsea ambazo ndizo ziko kwenye mbio za Ubingwa Msimu huu na pia dhidi ya Everton inayozidi kuimarika baada ya kuyumba.
Hali hiyo imemfanya Kepteni Wayne Rooney kupiga Mbiu ya Mgambo kwamba ushindi Jumamosi hii inayokuja dhidi ya Sunderland Uwanjani Old Trafford ni kitu cha lazima.
Kepteni Rooney ametamka: “Tunahitaji kulipa Mechi ijayo. Ni Gemu ambayo ushindi ni lazima. Tunatakiwa kushinda ili turudi kwenye reli na kuanza mbio nyingine za ushindi tumalize 4 Bora!”
Luis Van Gaal akitoka Uwanjani baada ya kubamizwa bao 2-1 na Swansea City Wachezaji wa Swansea City wakishangilia baada ya kuibamiza United  hivi karibuni.

waliotembelea blog