Sunday, August 2, 2015
2:15 AM
Unknown
Mesut Ozil
Ligi kuu ya Uingereza inaanza tena siku ya jumapili wakati ambapo mabingwa wa ligi hiyo Chelsea wanakutana na washindi wa kombe la FA Arsenal katika kombe la Charity Shield itakayogaragazwa katika uwanja wa Wembley.
Mechi hiyo inajiri siku 64 baada ya kumaliza ligi hiyo na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa katika fainali ya FA.
Pande zote mbili hazijafanya usajili mkubwa katika msimu huu ijapokuwa kipa Petr Cech ataanzishwa dhidi ya timu yake ya zamani Chelsea.Makipa - Emiliano, David Ospina na Petr Cech
Chelsea vilevile inaweza kumuanzisha mchezaji wao mpya Radamel Falcao.
Falcao mwenye umri wa miaka 29 alihudumu katika kilabu ya Manchester United msimu uliopita lakini hakuweza kutamba kwani aliweza kufunga mabao 4 katika mechi 29 alizocheza pekee.
Siku ya jumapili itazikutanisha timu hizo mbili huku mkufunzi wa Arsenal akitarajia kuishinda timu inayofunzwa na Mourinho kwa mara ya kwanza kati ya mechi 13 walizocheza huku wakufunzi hao wawili tayari wakitofautiana. Mourinho alisema kwamba Arsenal imetumia fedha nyingi msimu huu ikilinganishwa na Chelsea katika kipindi cha miaka kadhaa iliopita ,huku Wenger akijibu kwamba hasikizi kile watu wanachosema ama kufikiri.Aaron Ramsey Ramsey kwa furaha wakati wa mazoeziMesut Ozil Kocha Arsene Wenger akiwacheki Vijana wake wakati wa mazoeziAaron Ramsey akiwa kona akiwapigia wenzake konaGabrielHector akivutwa shati na IwobiOzilJeff nae kafanya mazoezi na kulia ni Aaron RamseyFlaminiGibbsChambers
Per Mertesacker na LaurentJeff na Iwobi nao wakijifuaChambers akibadilishana mawazo na wenzake

2:11 AM
Unknown
Dirisha
la Usajili kwa Vilabu vya Ligi Kuu (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
na Ligi Daraja la Pili (RCL) linatarajiwa kufungwa tarehe 06 Agosti,
2015.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linavikumbusha vilabu vyote kufanya usajili wa wachezaji wao mapema kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo, ili kuondokana na usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho.
Pindi dirisha hilo litakapofungwa Agosti 06, hakuna klabu au timu yoyote itakayoweza kufanya tena usajili wake, hivyo ni vyema vilabu vitahakikisha vinamaliza mausala ya usajili mapema kabla ya siku ya mwisho.

1:59 AM
Unknown
Mtangaza
nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa
akiwapungia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa Chama hicho, wakati
alipowasili kwenye Ofisi ya Makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni Jijini
Dar es Salaam jioni ya leo. Mh. Lowassa alifika ofisini hapo kurudisha
fomu za kuomba ridhaa ya Chama hicho, kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.Kulia kwake ni Mbunge wa
Jimbo la Arumeru Magharibi, Mh. Godluck Ole Medeye alieambatana nae.
1:56 AM
Unknown
Kuelekea kuanza kwa Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga August 1 imepigwa mechi ya Fainali ya Super Cup, mchezo huo ulizikutanisha timu za FC Bayern Munchen dhidi ya klabu ya Wolfsburg katika uwanja wa Volkswagen Arena.
Mchezo umemalizika kwa Wolfsburg kuibuka
washindi baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1,
hadi dakika ya 88 FC Bayern Munchen walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0 goli lililofungwa na Arjen Robben dakika ya 47 ya mchezo kabla ya Nicklas Bendtner kufunga goli la kusawazisha dakika 89 kwa upande wa Wolfsburg.
Hivyo ikalazimika kupigwa mikwaju ya penati ambapo Wolfsburg wakaibuka na ushindi kwa jumla ya penati 5-4 kwa upande wa FC Bayern Munchen kiungo wa Kihispania Xabi Alonso alikosa penati. Sambamba na hayo kiungo wa kimataifa wa Ubeligiji Kevin De Bruyne alipata tuzo ya mchezaji bora wa mwaka inayotolewa na waandishi wa habari za michezo Ujerumani.
Pichaz na Video nimekusogezea mtu wangu
1:52 AM
Unknown
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ameingia tena kwenye headlines kwa kauli zake anazozitoa kuelekea mchezo wa Ngao ya Hisani, Chelsea itakutana na Arsenal August 2 saa 11 jioni kwenye uwanja wa Wembley wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 90,000. Mourinho ambae anajulikana kwa kuwa na uwezo wa kucheza na akili ya kocha wa timu pinzani amerudi na kauli nyingine dhidi ya Wenger.
“Sifikirii
kuhusu nini kilitokea nyuma, nafikiria kuhusu mechi mimi kushinda mechi
sita, saba, nane au tisa bila kupoteza mechi hata moja haiweki utofauti
wowote na sifikiri kama itasaidia chochote kwenye huu mchezo, mechi
inayofuata kwangu haina mahusiano yoyote na mechi iliyopita
“>>>Mourinho
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger hajawahi kuifunga klabu ya Chelsea hata mara moja ikiwa chini ya Jose Mourinho, wachambuzi wa masuala ya soka wanatafsiri kauli za Mourinho kama ni njia ya kumdanganya kocha wa Arsenal Arsene Wenger ili ajiamini zaidi.
Mourinho amekuwa na rekodi nzuri dhidi ya kocha wa Arsenal kwani akiwa na kikosi cha Chelsea amewahi kucheza na Arsenal mechi 12 na kushinda mechi saba na kutoka suluhu mechi tano hivyo hiyo ni sababu inayoendelea kumtia jeuri.
Subscribe to:
Posts (Atom)