Friday, March 31, 2017


TANGU wafungwe 4-0 na Chelsea huko Stamford Bridge hapo Oktoba 23, Manchester United imekuwa Timu pekee ‘Isiyofungika’ kwenye EPL, Ligi Kuu England, ikimaliza zaidi ya Miezi 5 bila kufungwa zikiwa ni mbio za Mechi 18.

Licha kusakamwa na Mechi kedekede wakiwa Timu pekee wenye Mechi nyingi kupita yeyote huko England, Jose Mourinho ameongoza Kikosi hicho kwa ufanisi mkubwa na kuwawezesha Mwezi Februari kutwa Taji kubwa walipobeba Kombe la Ligi, EFL CUP.
Mwezi Aprili wanakabiliwa na Mechi 9 na ingawa Mourinho amelalamikia ugumu wa Ratiba yao lakini hilo ni dalili tosha ya mafanikio yao Msimu huu wao wa kwanza chini ya Jose Mourinho ambao walikuwemo kwenye mbio za Mashindano Manne na kutolewa tu Wiki 2 zilizopita kwenye FA CUP.

Hilo limempa Mourinho nafasi ya kubadili Kikosi chake katika kila Mashindano na kumwezesha kupata Kikosi imara cha kucheza EPL bila kufungwa.

Related imageMtizame Mchezaji wa Kimataifa wa Armenia, Henrikh Mkhitaryan, ambae kwenye Mechi yake ya kwanza tu Klabuni hapo, walipofungwa na Man City Mwezi Septemba, alitolewa nje lakini hilo halikumkatisha tamaa kwani aliibukia kwenye UEFA EUROPA LIGI na kung’ara na kurudi tena Kikosi cha Kwanza.

Kushiriki Mashindano mengi kumemfanya Mourinho azungushe Wachezaji kwenye kila Mechi ya EUROPA LIGI, EFL CUP na FA CUP lakini kwenye Ligi panga pangua wapo David de Gea; Antonio Valencia, Phil Jones, Marcos Rojo, Matteo Damian; Ander Herrera, Michael Carrick; Henrikh Mkhitaryan/Juan Mata, Paul Pogba, Marcus Rashford; Zlatan Ibrahimovic.

Wafutiliaji wa hizo Mechi zao 18 ambazo hawakufungwa kwenye Ligi wamebaini Man United hufungwa Goli chache, 11 tu, lakini pia kufunga chache, Bao 29 tu.

Hiyo ndiyo sababu kubwa Man United wako Nafasi ya 5 kwenye Ligi wakiwa Pointi 17 nyuma ya Vinara Chelsea.

Kwa ujumla Man United wamefunga Bao 42 katika Mechi 27 za Ligi tofauti na wenzao kama Liverpool waliofunga 62, Chelsea 59, Tottenham Hotspur 55, City 54, Arsenal 56 na Everton 51.

Kitu muhimu kwa Kikosi cha Mourinho kutofungwa Mechi 18 za Ligi ni Difensi yake hasa ule upacha wa Sentahafu ya Marcos Rojo na Phil Jones huku Ander Herrera akiwa nguzo kubwa kwenye Kiungo.

Walipofungwa Mechi yao ya mwisho ya Ligi na Chelsea, upacha wa Sentahafu ulikuwa ni wa Eric Bailly na Chris Smalling na kuumia kwao kukatoa mwanya kwa Rojo-Jones kucheza pamoja na wao ni kati ya Wachezaji 6 waliocheza Mechi nyingi kwenye hizo 18 ambazo hawakufungwa wakifuatia Herrera, Ibrahimovic, Pogba na Kipa De Gea anaeongoza.

Lakini tatizo kubwa ni ufungaji ambao umebaki kwa Zlatan Ibrahimovic pekee aliefunga Jumla ya Mabao 26 Msimu huu na 11 kati ya Mechi 16 za Ligi zilizopita.

Sasa Mwezi Aprili Man United wanakabiliwa na Mechi 9 wakianzia Jumamosi Old Trafford kucheza na West Brom na kisha Jumanne Everton watatua Uwanja huo huo wakati Jumamosi inayofuatia watakuwa safarini Stadium of Light kuivaa Timu ya Mkiani Sunderland inayoongozwa na Meneja wa zamani wa Man United David Moyes.

Mbio hizi za kutofungwa za Mechi 18 za Ligi ndio bora kabisa kwenye Ligi Kuu England tangu Machi 2013 pale Kikosi chini ya Sir Alex Ferguson kilivyofanya hivyo.


VPL, LIGI KUU VODACOM, inarejea tena kwa kishindo Jumamosi hii Aprili Mosi kwa Mechi 3 na kubwa kabisa ni ile itayopigwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kati ya Mabingwa Watetezi Yanga na Timu ngumu Azam FC.
Hakika Mechi hii ni Bigi Mechi na itatoa mwanga mkubwa kama kweli Yanga wanaweza kutetea Ubingwa wao hasa kwa vile wapo Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Simba huku wote wakiwa wamecheza Mechi 24 kila mmoja na kubakiza Mechi 6 tu kila mmoja.

Azam FC wao wapo Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 9 nyuma ya Yanga wakiwa bado wana matumaini finyu ya Ubingwa.

Mechi nyingine za hiyo Jumamosi, ambazo hasa nyingi ni vita za kutoshuka Daraja, ni huko Songea kati ya Maji Maji FC na Toto Africans wakati nyingine ni Mjini Mbeya kati Mbeya City na Ruvu Shooting.

Jumapili zipo Mechi 4 na Macho Kodo ni huko Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba kati ya Kagera Sugar, walio Nafasi ya 4, wakiwavaa Vinara Simba.

Nyingine za Jumapili ni Jijini Dar es Salaam kati ya African Lyon na Stand United, Mjini Mbeya ni Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar na huko Mwadui Complex, Shinyanga ni Mwadui FC na JKT Ruvu.

VPL – LIGI KUU VODACOM
Jumamosi Aprili 1

Yanga v Azam FC
Maji Maji FC v Toto Africans
Mbeya City v Ruvu Shooting

Jumapili Aprili 2

Kagera Sugar v Simba
African Lyon v Stand United
Tanzania Prisons v Mtibwa Sugar
Mwadui FC v JKT Ruvu

Jumamosi Aprili 8
Stand United v Tanzania Prisons
Kagera Sugar v JKT Ruvu
Yanga v Toto Africans
Mtibwa Sugar v Azam FC

Jumapili Aprili 9
Mbeya City v Ndanda FC
Maji Maji FC v African Lyon

Jumatatu Aprili 10
Mbao FC v Simba

Kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea Man United ya England Juan Mata jina lake limerudi kwenye headlines baada ya kufanyiwa upasuaji wa groin, Mata ambaye mwanzoni mwa wiki hii alikuwa akilalamika mazoezini kuwa anasumbuliwa na groin amefanyiwa upasuaji.
Taarifa zilizotoka usiku wa March 31 2017 kuhusu kiungo huyo ni kuwa upasuaji wake umeenda salama lakini kutokana na tatizo lake, kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mechi zote za kumalizika za Man United tofauti na awali alivyotazamiwa kuwa anaweza kukosa mechi tatu tu.

Juan Mata ambaye alijiunga na Man United akitokea Chelsea mwaka 2014 , hajawahi kukosa mechi za Man United katika kipindi cha miaka yote mitatu aliyokuwepo klabuni hapo pasipokuwa na majeruhi, mara zote amekuwa akikosekana kwa sababu za msingi ikiwemo majeruhi.

waliotembelea blog