Thursday, July 24, 2014


KOCHA wa Yanga, Marcio Maximo amesema pamoja na kumpa mkataba wa miaka miwili mshambuliaji Geilson Santana Santos ‘Jaja’, bado anahitaji kuona uwezo wa washambuliaji wawili raia wa Uganda, Hamisi Kiiza na Emmanuel Okwi.
Yanga inalazimika kuachana na mchezaji mmoja wa kigeni kama kanuni za usajili zinavyoagiza, baada ya sasa kuwa na wachezaji sita wa kimataifa ambao ni Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite, Andrey Coutinho, Jaja, Kiiza na Okwi. Kanuni za usajili zinaruhusu timu kusajili wachezaji watano wa kigeni.
“Nalazimika kuwaona mazoezini Okwi na Kiiza ndiyo nitakuwa na jibu la kusema, lakini kwa sasa bado ni mapema mno kusema nitampunguza nani, kwa sababu hata katika rekodi za klabu naona wachezaji hawa wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu ukitoa usumbufu ambao inasemekana wanao,” alisema Maximo.
Maximo alisema anaufahamu fika uwezo wa kiungo wa Rwanda, Niyonzima hana shaka naye, lakini naye pia alazimika kumuangalia kwa mara nyingine uwezo wake ili ajiridhishe kwa sababu ni muda mrefu tangu amuone akicheza.
“Ninachokitaka ni kuwa na kikosi imara ambacho hakitakuwa kikitegemea baadhi ya wachezaji na ndiyo sababu ya kutaka kuwaona wachezaji hao ili nijue uwezo wao na baada ya hapo nitaweka hadharani nani ambaye hatutakuwa naye,” alisema Maximo.
Baada ya Maximo kumsajili Jaja wanachama na mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakiumiza kichwa kutaka kujua mchezaji gani kati ya Kiiza na Okwi atakatwa kwenye usajili wa msimu ujao huku kila mtu akiwa na mapendekezo yake.



KOCHA Mkuu wa Simba, Mcroatia Zdravko Logarusic, 


KWA muda mrefu tumekuwa tukizungumzia suala la klabu kuwa na viwanja vyake vya soka kwa ajili ya mazoezi huku mkazo wetu ukiwa katika klabu za Ligi Kuu.
Hoja yetu hii kwa wakati wote imekuwa ikizinyooshea kidole klabu kongwe za Simba na Yanga ambazo hazijalipa umuhimu wa kipekee suala hili.
Klabu hizi ambazo zimeanzishwa miaka zaidi ya 70 iliyopita hadi sasa havina viwanja vyenye hadhi japo kwa ajili ya  kufanyia mazoezi.
Hili ni jambo la aibu ambalo tumekuwa tukilikemea mara zote hasa inapotokea timu kama Azam ambayo imeanza kutamba katika Ligi Kuu katika kipindi kisichozidi miaka mitano iliyopita kumiliki uwanja wenye hadhi ya kucheza hata mechi za kimataifa.
Hivyo hivyo na Mtibwa Sugar ambayo haina miaka 20 katika ligi ya juu nchini lakini inamiliki uwanja wake unaofaa kwa mazoezi na hata mechi za ligi.
Kilio chetu hicho walau kimesaidia kuiamsha Simba ambayo imeanza harakati za ujenzi wa uwanja wake maeneo ya Bunju B nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Hali ni hivyo hivyo kwa Yanga ambao tofauti yao na Simba ni kwamba wao wana eneo lakini hawalijali na hawaonyeshi nia ya dhati ya kulifanya liwe uwanja wenye hadhi japo ya mazoezi.
Wakati Yanga na Simba wakionekana kupuuza hoja hiyo, juzi Jumanne Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alinukuliwa akisema kwamba kuanzia mwaka ujao hakuna klabu ya Ligi Kuu itakayoruhusiwa kushiriki mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) bila ya kuwa na leseni ya shirikisho hilo pamoja na uwanja.
Ni dhahiri kwamba Agizo hilo la CAF ambalo limo kwenye katiba ya TFF linaziumbua klabu hizi na nyinginezo zilizodhamiria kushiriki michuano inayoandaliwa na CAF.
Kwa kuwa Yanga na Simba ndizo ambazo zimekuwa zikichuana mara kwa mara kuwania tiketi ya kushiriki mashindano ya CAF, agizo hilo ni mtihani mwingine kwao.
Ni vyema viongozi wa klabu hizo wakaweka mikakati thabiti ya kuepukana na fedheha ambayo itajitokeza siku za mbele kwa kujikuta wakihaha kutafuta uwanja wa kuazima wakati wana uwezo wa kuwa na viwanja vyao.
Tunaamini kwamba iwapo CAF watawabana, watatafuta viwanja vya kuwalinda ambavyo vina hadhi lakini jambo hilo kwetu tunaliona kuwa ni la aibu.



Akizungumza na Mwanaspoti, Coutinho raia wa Brazil alisema kwa sasa bado hawezi kusema moja kwa moja kuwa ana uhakika wa kuingia katika kikosi cha kwanza cha Yanga kwa vile hajajua uwezo wa wenzake wanaocheza nafasi kama yake ambao wapo katika vikosi vya mataifa yao. 

KIUNGO wa Yanga, Mbrazil Andrey Coutinho (pichani )amesema anafurahia zaidi staili ya uchezaji ya kiungo Nizar Khalfan na kwamba ndiye kiungo anayejua zaidi wapi kwa kumwekea mpira anapokuwa akikimbia.

Coutinho aliliambia Mwanaspoti kuwa, “ Yanga ina viungo wengi na wote wazuri lakini nimependa jinsi Nizar anavyocheza kwani anaonekana kujua jinsi mimi ninavyotaka kupewa pasi nikiwa nakimbia.

“Kwanza naona ana nguvu lakini pili anapiga pasi kwa kukuwekea pale ulipo, napenda hata kwenye mazoezi niwe napangwa naye kwani ananifanya nicheze kwa ufasaha zaidi na kufanya malengo yangu kutimia vizuri.

“ Pia ana uwezo mzuri wa kupiga pasi pia kupiga mashuti ya nguvu ambayo yanaweza kuwa na faida pale kipa anapotema na straika wetu akanasa mpira,” alisema.

Katika hatua nyingine kiungo huyo amesema  kuwa bado hajawa mpenzi wa vyakula vya Kitanzania kwa kuwa hapendezwi sana na ulaji wa vyakula vingi vya Kitanzania vya asili.
“Vyakula vya asili sijavizoea, nimevizoea vya kwetu kule Brazil, huku Tanzania napenda zaidi kula kuku, nyama ya kusaga ‘Beef’ na tambi pamoja na wali kwani ndiyo vyakula ambavyo utakavyoweza kuvikuta kwetu Brazil,” alisema



Wayne Rooney  


WAYNE Rooney amempagawisha Kocha Louis van Gaal mazoezini. Wakati kikosi cha Manchester United kikiwa kwenye maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu England huko Marekani, straika Rooney alionyesha maajabu mazoezini na kumfanya kocha kupagawa.
Kocha Van Gaal alimkimbilia Rooney na kumkumbatia baada ya straika huyo kufunga moja kwa moja kwa mpira wa kona aliopiga mazoezini juzi Alhamisi.
Baada ya kuonyesha kiwango hicho kwa kupiga kona na kutinga moja kwa moja wavuni, Van Gaal hakuna njia nyingine iliyobora kumpongeza mchezaji huyo zaidi ya kumfuata na kumkumbatia.
Akiwa hana siku nyingi kwenye kikosi hicho cha Man United, tayari Van Gaal amejikusanyia mashabiki wengi kutokana na kufurahishwa na mbinu zake mazoezini.
Kwenye mazoezi ya juzi Van Gaal alikuwa akiwanoa wachezaji wake namna ya kupiga mipira iliyokufa ndipo Rooney alipopiga kona na kwenda moja kwa moja wavuni. Kocha Van Gaal anaonekana kuwa na bahati ya mastaa wake kufanya maajabu ndani ya uwanja baada ya straika wake mwingine, Robin van Persie kufunga kwa kichwa kwa staili ya ajabu kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu wakati Uholanzi ilipoichapa Hispania mabao 5-1 mwezi uliopita.
Mwanzoni ilidhaniwa kwamba Rooney angekuwa kwenye wakati mgumu chini ya Van Gaal, lakini kwa sasa mambo yamekuwa tofauti na staa huyo anaonekana kuelewana na kocha wake mpya tangu alipotua kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.
Man United inafanya mazoezi California na Alfajiri ya leo Alhamisi ilitarajiwa kumenyana na LA Galaxy kwenye mchezo wao wa kwanza wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya.
Man United ambayo ilidai kwamba mwaka huu itafanya usajili utakaovunja rekodi ya uhamisho Uingereza ni miongoni mwa timu zitakazocheza Kombe la Chevrolet linalozishirikisha pia Washington DC, Detroit, AS Roma, Inter Milan na Real Madrid.


Manchester City wamevunja Mechi yao ya Vijana wa chini ya Miaka 21, U-21, dhidi ya HNK Rijeka huko Novigrad, Croatia hapo Jana kwa madai ya kukashifiwa Kibaguzi kwa mmoja wa Wachezaji wao.
Wakati Mechi ikivunjika, City walikuwa mbele kwa Bao 1-0 na walitoka nje mara tu baada ya Kiungo wao, Seko Fofana, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada kumtandika Teke mpinzani lakini inaaminika hiyo ni sababu ya kukashifiwa.
Lakini kila upande umetoa taarifa tofauti kwa Man City kudai kuwa katika Kipindi cha Kwanza Uongozi wao ulilazimika kuitoa nje Timu yao kufuatia kukashifiwa Kibaguzi kwa Mchezaji wao anaeaminika kuwa ni Seko Fofana, Raia wa France.

Timu ya HNK Rijeka imedai kuwa Kocha wa Man City, Patrick Vieira, aliingia Uwanjani na kuongea na Refa na, kwa mshangao wa wengi, kuamua kuitoa nje Timu yake bila wao kujua ni kwa sababu gani.

Fofana, ambae huchezea France U-19, alijiunga na City Januari 2013 akitokea Klabu ya Ligue 1 huko France, FC Lorient.

Januari 2013, AC Milan walivunja Mechi yao ya Kirafiki dhidi ya Timu ya Daraja la chini huko Italy, Pro Patria, baada ya Mashabiki kumpigia kelele za Kibaguzi Mchezaji wao Kevin-Prince Boateng ambae aliukamata Mpira na kuubutua kwa Mashabiki hao na kisha kuongoza Timu yake kutoka nje na Mechi kuvunjika.


Barcelona wamemsaini Beki wa Valencia Jeremy Mathieu kwa Mkataba wa Miaka Minne kwa Ada ya Euro Milioni 20.
Mathieu, mwenye Miaka 30, ameichezea France mara mbili na anaweza kucheza kama Fulbeki wa Kushoto au Sentahafu.
Beki huyo anarithi nafasi ya Nahodha wa zamani wa Barcelona Carlos Puyol ambae amestaafu baada ya kuitumikia Klabu kwa Miaka 15. 

Taarifa kutoka Barcelona imesema gharama ya Uhamisho wa Mathieu ni Euro Milioni 20 lakini itabidi pia walipe gharama inayotajwa kwenye Kipingele cha Mkataba wa Mchezaji huyo na Valencia kwamba akiuzwa kabla Mkataba kwisha inabidi ilipwe Euro Milioni 50.
Dau hilo limemfanya Mathieu awe Beki wa umri mkubwa ghali kununuliwa kupita yeyote.
Mathieu aliichezea Valencia Mechi 126 katika Misimu mitano na kufunga Bao 6.
Manchester United imetoa Ofa ya mwisho kwa Juventus ya Pauni Milioni 39 kumnunua Kiungo wao, Juventus, kwa mujibu wa Jarida la Michezo la Italy, Tuttosport.
Ofa hiyo, ya staili ya: 'Chukua Hutaki Basi', inaaminika inaweza kufungua milango kwa Juventus kukubali kumuuza Kiungo wao mahiri kutoka Chile alieng’ara sana huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia. 

Barcelona, ambao walimaliza Msimu uliopita wakiwa Nafasi ya Pili kwenye La Liga, Msimu ujao watakuwa chini ya Kocha mpya Luis Enrique ambae tayari ameshavunja Rekodi kwa kumsaini Straika wa Liverpool, Luis Suarez, kwa Pauni Milioni 75.
Wapya wengine ni Kiungo Ivan Rakitic kutoka Sevill, Kipa Marc-Andre Ter Stegen na Claudio Bravo.
Wachezaji waliohama Nou Camp ni Cesc Fabregas, Puyol, Victor Valdes, Bojan Krkic na Alexis Sanchez.

Manchester United imetoa Ofa ya mwisho kwa Juventus ya Pauni Milioni 39 kumnunua Kiungo wao, Juventus, kwa mujibu wa Jarida la Michezo la Italy, Tuttosport.
Ofa hiyo, ya staili ya: 'Chukua Hutaki Basi', inaaminika inaweza kufungua milango kwa Juventus kukubali kumuuza Kiungo wao mahiri kutoka Chile alieng’ara sana huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia.

Vidal alijiunga na Juve Mwaka 2011 na kila Mwaka ameisaidia sana Klsbu hiyo kuibuka Mabingwa wa Italy.
Hadi sasa Juve wamekuwa wagumu kumuachia Vidal lakini ofa hii pamoja na imani kwamba Mchezahi huyo anataka kuondoka vinaweza kuwanufaisha Man United.
Hivi sasa Vaidal amebakisha Miaka Mitatu kwenye Mkataba wake na Juve. 

Wiki iliyopita Gazeti moja huko Nchini kwao Chile liliripoti kuwa Mchezaji huyo anawindwa na Man United.
Akiongea na Gazeti la El Mercurio Vidal alisema: “Nimesikia uvumi huu lakini sitaki kuongelea. Kwa sasa nipo vakesheni na nikirudi Italy tutaona.”
Aliongeza: “Manchester United? Nimepoa lakini ukweli nani hatapendezewa ikiwa moja ya Klabu kubwa Duniani inamtaka?”
Vidal aliichezea Nchi yake Chile huko Brazil na wakatolewa Raundi ya Pili na Brazil kwa Mikwaju ya Penati.

Kabla ya kutua Juve, Vidal alikuwa huko Germany akiichezea Bayer Leverkusen na kuhamia Juve Mwaka 2011 na kutwaa Ubingwa wa Italy mara 3.
Tayari Man United, chini ya Meneja wao mpya Louis van Gaal, imeshanunua Wachezaji wawili wapya, Fulbeki Luke Shaw na Kiungo Ander Herrera. 

Wakati huo huo, Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, Ed Woodward, amesisitiza kuwa wao wako tayari kuvunja Rekodi ya kununua Mchezaji kwa bei yeyote ile ikiwa tu Mchezaji huyo atatakiwa na Meneja Van Gaal.
Woodward amesema uwezo wa kifedha upo na Klabu haiogopi kutumia kiasi chochote cha Fedha kununua Wachezaji watakaowafaa.


Rooney na Welbeck wakipongezanaWelbeck ndie aliyeanza kuifungia bao la mapema dakika ya 13 United
Asubuhi hii Manchester United waliifunga LA Galaxy Bao 7-0 Uwanjani Rose Bowl, Pasadena, California mbele ya Mashabiki 86,432 katika Mechi ya kwanza chini ya Meneja wao mpya Louis van Gaal na kutwaa Kombe la  Chevrolet.
Dakika ya 13 Danny Welbeck ameifungulia mlango wa mabao Man United baada ya kupata pasi kuoka kwa Juan Mata na bao hilo likiwa la Mbali kama yadi 25.
Wayne Rooney aliwapatia bao la pili kupitia kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 41 baada ya Valencia kufanyiwa ndivyo sivyo eneo la penati.
Dakika za mwishoni dakika ya 45 Wayney Rooney aliwafungia United bao la tatu na kufanya mtanange kwenda mapumziko zikiwa 3-0 dhidi ya Wenyeji La Galaxy.Rooney akikatiza mbele kipa wa LA Galaxy na kufunga bao!Wayney Rooney akichonga penati katika kipindi cha kwanzaRooney aki[pongezwa.
Kipindi cha pili dakika ya 63 Reece James aliwafungia bao la 4 United na kufanya 4-0 baada ya kupata mpira kutoka kwa Ashley
Young.
Reece James aliwafungia bao la tano na kufanya 5-0 dhidi ya LA Galaxy katika dakika ya 84 ya Mchezo kipindi cha pili dakika zikiyoyoma.

Dakika ya 88 Ashley Young anaifungia bao la sita na kufanya 6-0 dhidi ya LA Galaxy baada ya kupata mpira kutoka kwa Ander Herrera.Herrera aliongoza sana kwa kutoa mapande kwa wenzakeNani akibanwa James akipongezwa kwa kufunga bao la pili
Dakika ya 90 Ashley Young anaifungia bao tena United katika dakika za lala salama baada ya kupewa pasi na Ander Herrera.
Nyota wa mchezo huo alikuwa ni Mchezaji mpya wa Man United Ander Herrera alietanda katikati ya Uwanja na kutoa pasi murua. Mechi inayofuata kwa Man United ni hapo Jumamosi Julai 26 dhidi ya AS Roma Sports Authority Field, Denver ikiwa ni Mechi ya Kundi A kugombea International Champions Cup
Wafungaji: Welbeck, 13', Rooney (pen) 41, 45, James, 62, 84, Young 88, 90.


WAKATI himaya mpya ya Meneja mpya Louis van Gaal imeanza Jumatano huko Pasadena Rose Bowl kwa Washabiki 70,000 kufurika kuiona Manchester United, Mchezaji wa zamani wa Timu hizo mbili David Beckham alitembelea Hoteli ya Beverly Hills kuwasabahi Marafiki zake wa Man United.
Beckham, Lejendari wa Man United, yuko huko Los Angeles kwa matembezi na alifika Hotelini na kuongea na Wachezaji wa Man United na Mameneja wao, Louis van Gaal na Ryan Giggs, ambae waliwahi kucheza pamoja huko Man United tangu wakiwa wadogo.
Ingawa Mechi hii ni ya Kirafiki, Mshindi hutunzwa Chevrolet Cup, Mashabiki wa Man United walifuatilia kwa hamu kuona Van Gaal anaanza vipi wadhifa wake.

Wiki nzima kwenye Mazoezi Man United wamekuwa wakitumia Mfumo wa 4-3-3 na  wameutumia kwenye Mechi na LA Galaxy.
Lakini pia mvuto ni kuwaona Wachezaji wapya, Ander Herrera na Luke Shaw, wakivaa jezi ya Man United kwa mara ya kwanza.
Mmoja wa Wachezaji wa LA Galaxy ambae Man United watamjua vizuri ni Mchezaji wa zamani wa Tottenham na Liverpool ambae sasa ni Nahodha wa Republic of Ireland, Robbie Keane.
Baada ya Mechi hii, Man United watasafiri kwenda Miji ya Denver, Washington na Detroit kucheza na AS Roma, Inter Milan na Real Madrid kwenye Mashindano ya International Champions Cup.

10514673_338168816341103_5043683657096333091_n
Bendi Mahiri na Machachari Jijini Dar Skylight Band wametoa wimbo wao wa Tano ikiwa ni muendelezo wa kutoa nyimbo tofauti tofauti kupitia Studio yao ya kisasa ya Skylight Production.
Akiongea na Mtandao huu Meneja wa Band hiyo Aneth Kushaba AK47 amesema wimbo huo unaitwa “Pasua Twende” ambo umetungwa na Mkurugenzi Mkuu wa bendi hiyo Dk. Sebastian Ndege akishirikiana na wanamuziki wa Bendi hiyo.
Aneth akaongezea kwamba wimbo huo ni wa tano kutolewa katika mtiririko wa nyimbo zao zilizokwisha kutoka na imetengenezwa ndani ya studio yao ya Skylight Production chini ya Produzya Joobanjo.

Bondia Ibrahimu Maokola akipiga beg zito wakati akijifua katika GYM ya okaido iliyopo Mbagala Charambe  kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Mkalakala pambano litakalofanyika Agosti 9 ,2014 katika ukumbi wa Amenya Pub uliopo Mbagala picha na 
Bondia Ibrahimu Maokola akijifua Okaido GYM iliyopo Mbagala Charambe kwa ajili ya kujitaharisha na mpambano wake wa ubingwa wa taifa na Selemani Mkalakala mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub uliopo Mbagala Agosti 9.
Bondia Ibrahimu Maokola akijifua Okaido GYM iliyopo Mbagala Charambe kwa ajili ya kujitaharisha na mpambano wake wa ubingwa wa taifa na Selemani Mkalakala mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub uliopo mbagala Agosti 9,2014.
Bondia Ibrahimu Maokola akifanya mazoezi ya kuimalisha misuli ya tumbo kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Mkalakala litakalofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub uliopo Mbagala siku ya ya Agosti 9.2014.
Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akielekezwa kupiga ngumi na Ayubu Tezikoma wakati wa mazoezi yake kwa ajili ya kujiandaa kupambana na Selemani Mkalakali mpambano wa ubingwa raundi kumi utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub Agosti 9 ,2014.
Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akielekezwa kupiga ngumi na Ayubu Tezikoma wakati wa mazoezi yake kwa ajili ya kujiandaa kupambana na Selemani Mkalakali mpambano wa ubingwa raundi kumi utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub Agosti 9 ,2014.
Bondia Ibrahimu Maokola
Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akipiga beg kubwa kwa kusimamiwa na Athumani Magambo wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Mkalakali litakalofanyika Agosti 9 ,2014 katika ukumbi wa Amenya Pub Mbagala.

IMG_0618 
Kikosi cha Mtibwa Sugar msimu uliopita. Mlinda mlango Hussein Sharrif `Casillas` amejiunga na Simba majira haya ya kiangazi na kusaini mkataba wa miaka miwili
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TIMU nyingi zinazoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara zipo katika maandalizi ya kujiwinda na msimu mpya utakaoanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu.
Wakata miwa wa mashamba wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar wapo jijini Dar es salaam kujifua katika fukwe za Koko ili kujiimarisha zaidi.
Mtibwa Sugar chini ya kocha mkuu, Mtanzania Mecky Mexime, msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya 7 kwa kujikusanyia pointi 31 kibindoni.
Mabingwa hao mara mbili mfululizo wa Tanzania kwa mwaka 1999 na 2000 walishinda mechi 7, sare 10 na kufungwa mechi 9. Walitikisa nyavu za wapinzani mara 30 na zao kuguswa mara 31.

DSC_0612-1 
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamedhamiria kurejesha heshima yao iliyopotea kwa miaka mitatu mfululizo katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Simba ambayo imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja kocha wake mkuu, Mcroatia, Zdravko Logarusic ipo katika maandalizi ya msimu mpya na malengo yao kwasasa ni kuelekea katika mchezo maalumu wa kirafki utakaopigwa siku ya Agosti 9 mwaka huu dhidi ya Ismailia ya Misri kwenye tamasha la klabu hiyo la ‘Simba Day’ ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Tamasha la ‘Simba Day’ ni maalumu kwa mashabiki, viongozi na wanachama wa klabu hiyo kukutana kwa lengo la kubadilishana mawazo. Pia linatumika kama sehemu ya kutambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya.

article-2703725-1FED6D4600000578-662_634x476Raha tupu: Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney  akimpongeza Danny Welbeck baada ya kufunga bao la kwanza.
LOUIS Van Gaal ni kiboko. Awaonya Jose Mourinho na Asernal Wenger kuwa amekuja kufanya kazi Old Trafford.
Jana usiku ameshusha majanga kwa LA Galaxy baada ya kuitandika mabao 7-0 katika mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya kabla ya Msimu nchini Marekani.
Hii imezidi sasa! Van Gaal atakuwa anawaomba viongozi wa Manchester United kuipeleka timu kwenye ziara ya maandalizi ya kabla ya msimu kila majira ya kiangazi.
Ikiwa ni siku moja tu imepita tangu alalamike kuhusu ziara ya Marekani kwa madai kuwa inawafanya wachezaji wake wachoke, kocha huyo mpya wa Man United aliitazama timu yake ikipata ushindi mkubwa na kuonesha kiwango kizuri. 
article-2703725-1FED699100000578-453_634x388 
Mwanzo mzuri: Welbeck akishangilia baada ya kuifungia Man United goli la kuongoza katika dakika ya

MECHI kati ya timu Israeli ya Maccabi dhidi ya Lille ya Ufaransa iliahirishwa baada ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina kuvamiwa uwanja.
Waandamanaji hao walioripotiwa kuwa na asili ya Uturuki waliingia katika uwanja wa Austrian ambapo mchezo ulikuwa unaendelea na kuwavamia wachezaji wa Maccabi na kuzua vurugu.
Mmoja wa wachezaji alionekana akizozana na shabiki kabla ya kuanza kurushiana makonde mazito.
Hata hivyo wachezaji wa Maccabi walifanikiwa kutoka uwanjani bila kujeruhiwa.
Tukio hili limekuja wakati huu ambao majeshi ya Israel yamevamia na kufanya uhalifu dhidi ya majeshi ya Hamas huko Gaza.
NEWS : Altercation Lille vs Maccabi Haifa - 07/23/2014Mashambulizi: Waandamanaji walivamia uwanja na kuanzisha dhoruba ya kuwashambulia wachezaji wa  Maccabi Haifa
NEWS : Altercation Lille vs Maccabi Haifa - 07/23/2014 
Hatari sana: Waandamanaji waliwavamiwa wachezaji wa Maccabi Haifa na kusababisha mechi kuahirishwa.

waliotembelea blog