Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WEKUNDU wa Msimbazi Simba
wamedhamiria kurejesha heshima yao iliyopotea kwa miaka mitatu mfululizo
katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Simba ambayo imemuongezea mkataba
wa mwaka mmoja kocha wake mkuu, Mcroatia, Zdravko Logarusic ipo katika
maandalizi ya msimu mpya na malengo yao kwasasa ni kuelekea katika
mchezo maalumu wa kirafki utakaopigwa siku ya Agosti 9 mwaka huu dhidi
ya Ismailia ya Misri kwenye tamasha la klabu hiyo la ‘Simba Day’ ndani
ya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Tamasha la ‘Simba Day’ ni maalumu
kwa mashabiki, viongozi na wanachama wa klabu hiyo kukutana kwa lengo la
kubadilishana mawazo. Pia linatumika kama sehemu ya kutambulisha
wachezaji wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya.
0 maoni:
Post a Comment