Sunday, July 7, 2013
4:10 AM
Unknown
July 7, 2013
Beyonce na Solange wamepatiwa mama mpya na baba yao ambaye pia ni mkuu
wa Music Entertainment world na pia alikuwa manager wa kundi la Destiny
Child.Matthew Knowles ambaye ndiyo baba yake Beyonce na Solange kwa mama
Tina Knowles, ambao wote waliachana na kumalizana mambo ya talaka mwaka 2009.
Gena Charmaine ns Matthew Knowles
Hivi karibuni, Matthew Knowles alifunga ndoa na model wa zamani Gena
Charmaine ambaye alikuwa mchumba wake kwa muda wa mwaka mmoja na nusu,
hii inamaanisha kwamba Beyonce na Solange wana haki zote za kumuita Gena
mama kwa sababu ameolewa na baba yao ambae ni Matthew mwenye umri wa
miaka 61, Gena ana 48 ambapo harusi hiyo inasemekana haikuhudhuriwa na
mabinti hao wa mzee Matthew.
3:51 AM
Unknown
DK SHEIN ATEMBELEA MAONYESHO YA SABA SABA LEO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Leila Issa Ali,katika mabanda ya washiriki wa maonesho ya sabasaba alipotembelea leo jijini Dar es Salaam, (katikati) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui {Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}
3:40 AM
Unknown
ULEVI KWA WATU WENYE WANAOUGUA MARADHI YA UGONJWA WA UKIMWI NI HATARI.
ULEVI miongoni mwa watu wenye Virusi Vya Ukimwi (VVU) umeelezwa kuwa ni hatari kwani pombe inaharibu mfumo wa kinga mwilini na kupunguza chembe hai za kinga -CD4 na kusababisha virusi kuzalishwa kwa wingi.
Chembe za CD4 ni jeshi la
kingamaradhi linalohusika na kukabiliana na magonjwa wakati mwili unapogundua
kuna virusi au vimelea vya magonjwa.
Kwa mujibu wa
kipeperushi cha madhara ya Pombe kwa Wenye VVU kilichoandaliwa na Mpango wa
Taifa wa Kudh
ibiti Ukimwi (NACP), aidha kuchanganya dawa za ARV na pombe
kunasababisha usugu na kuzalisha virusi hatari zaidi.
Pia, NACP
ilisema pombe inasababisha madhara kwenye ini na kwamba baadhi ya dawa za
Ukimwi ili zifanye kazi kikamilifu ni lazima zipitie kwenye ini na kwa mlevi
linaweza kuwa na matatizo.
NIPASHE Jumapili ilifuatilia athari za ulevi kwa wenye VVU baada ya
kupokea taarifa za baadhi ya watoa huduma wanaofuatilia mwenendo wa wagonjwa wa
Dar es Salaam na mikoa ya jirani zikieleza kuwa wapo watu hunywa pombe licha ya
kutumia dawa.
Walieleza kuwa
baadhi ya watumiaji dawa wanabadili ratiba kwa kunywa vidonge asubuhi, wakati
mwingine wanachanganya na kumeza dawa za mchana na usiku ili waende vilabuni
kunywa pombe jioni.
Watoa huduma
walisema wagonjwa huacha kunywa dawa kwa mujibu wa maelekezo jambo walilosema
linakwamisha mikakati ya tiba.
”Utawakuta
wanakimbilia kunywa komoni, kimpumu hata gongo” alisema mtoa huduma wa kituo
cha afya kilichoko mkoani Pwani.
Wahudumu
wengine waliozungumzia ukiukwaji wa masharti ya kumeza ARV walishauri kutoa
dawa hizo chini ya usimamizi wa mtaalamu wa afya kama inavyofanyika kwa
watumiaji wa dawa za kifua kikuu (TB) na kuandaa muongozo wa Wizara ya Afya
unaoelekeza matumizi ya dawa na kukataza ulevi.
Walisema
baadhi ya wagonjwa hupendelea pombe kwa madai kuwa hawaogopi kifo kwani wao ni
“marehemu japo wanaishi” na wakidai ARV zina madhara mengine mwilini.
3:06 AM
Unknown
Dagaa mchelee, Changuuu, Kibuaaaa, Satoo, Dagaa kambaa, Sangaraaa, Peregeee.
Samakiiii. Kweli wote hao ni samaki, tena ni samaki wanaopendwa sana na wala samaki sio Tanzania tu, bali duniani kote. Upenzi wa samaki hautokani na utamu wake tu, bali pia unatokana na obora na virutubisho alivyonavyo samaki kwa afya ya binadamu.
Samaki
ana madini ya Chuma, Chokaa na Ayodini kwa wingi yanayosaidia ukuaji wa
mifupa kwa watu wa rika zote. Na mafuta yake yake yajulikanayo kama
OMEGA 3 yanayosaidia ukuaji wa ubongo.
Wapo
samaki wa kukaanga, samaki wa kuchemsha, samaki wa kupaka, samaki wa
kukausha, samaki wa kubanika, mapishi yote hayo kuburudisha roho ya
mlaji.
Nchini THAILAND samaki wanaliwa kweli kweli. Katika mji wa BANGKOK kuna mgahawa maarufu unaouza aina zote za samaki wa baharini.
Mgawaha huo ulifunguliwa mwaka 1986, na walaji kutoka sehemu mbalimbali duniani hufika mgawaha huo kufaidi samaki.
Mteja
huchagua samaki ambaye bado anapumua, ndipo wapishi humtoa ndani ya
maji, wakakatisha maisha yake na kumuweka mekoni, akitayarishwa kwenda
kwenye minywa cha mlaji ambako, ndiko yatakuwa maziko yake.
Hata
hapa kwetu, samaki hawatoshi, wakati mwingine wavuvi wanatumia mbinu
haramu kuwavua. Wavuvi, samaki watamu jamani, kuna mbinu mpya ya
kuwaongeza? Tupeni mbinu hiyo tufaidi. Samakiii, Dagaa mchelee,
Changuuu, Kibuaaaa, Satoo, Dagaa kambaa, Sangaraaa, Peregeee.
2:12 AM
Unknown
Safari ya Rais KIkwete Sunderland huenda ikawa mwisho wa kiu ya mpira Tanzania
Jumapili iliyopita nilibahatika kuwa ndani ya msafara mahususi uliozunguka na mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete.
Ingawa msafara huo ulihusu michezo na mpira,
uliwakutanisha pia baadhi ya Watanzania wakazi wa Jiji la Sunderland na
wale wasomao Chuo Kikuu cha New Castle, Kaskazini Mashariki ya Uingereza
Rais Kikwete alipotua jijini Sunderland jua
lilikuwa liking’ara, saa za adhuhuri...Mwezi wa sita huwa kiangazi ndiyo
kinaanza anza Ulaya hivyo siyo lazima kuvaa makoti mazito. Mkuu wa nchi
alikuwa nadhifu na wasaizidi wake kama kawaida, akiwemo Waziri wa
Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk Fenella Mukangara, Balozi wetu
hapa Peter Kallaghe na maofisa wengine husika walichangamkia shughuli
hii muhimu na ya kihistoria, kama tutakavyoona.
Upande wa wenyeji je?
Mmiliki klabu ya Sunderland ni tajiri wa
Kimarekani, Ellis Short kipato chake kinakisiwa kuwa Dola za Marekani
3.5 bbilioni, ndiye alimwalika Rais Jakaya Kikwete na Paul Hinks,
Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi Umeme ya Symbion Power, yenye
makao Marekani. Pande hizi mbili ndizo zitashirikiana, moja kujenga
Symbion chuo cha kufundishia watoto mpira, mwingine kutoa mafunzo hayo
Sunderland AFC.
Kwa vipi klabu iliyochukua nafasi ya 17 mwaka huu
ndani ya Ligi ya Uingereza kati ya timu 20, ichaguliwe kutufariji,
aliulizwa Rais Kikwete baadaye na wanahabari? Kwa nini wasiwe Arsenal,
Chelsea, Liverpool au watemi wa Manchester United?
Rais Kikwete akajibu ilitokana na Ellis Short
mwenyewe kuitembelea Tanzania kwa shughuli zake nyingine; Hapo msosi
ukatayarishwa. Sunderland inasifika kwa kituo chake bora kufunzia watoto
kiitwacho “Academy of Light.” Ukichunguza sana maendeleo ya wachezaji
wote wakubwa duniani, huanzia vilabu vidogo ndiyo wakanunuliwa na
hatimaye kutamba na timu zenye fedha na uwezo zaidi. Mfano mzuri ni
wanasoka maarufu wa ligi ya Uingereza Theo Walcott (Arsenal) Oxlade
Chamberlain( Arsenal ) na Gareth Bale wa Tottenham walioanzia mpira
utotoni Southampton Football Academy.
Sidhani ni wengi tunaoijua au kuisikia,
Southampton, barani Afrika. Lakini huu ni ushahidi wa namna klabu ndogo
zisizojulikana zinavyoivisha na kumeng’enya wachezaji chipukizi. Gareth
Bale sasa hivi anapiganiwa na kila klabu na inasemekana Real Madrid
wanamtamani kwa mate na udenda. Hata kwetu Bongo wachezaji wengi huanzia
klabu ndogo za mikoani kabla ya kununuliwa Simba na Yanga.
Hivyo Sunderland inaweza isiwe kubwa, lakini uwezo
wake wa kiufundi utaikidhi sana Tanzania. Msafara wa Rais ulionyeshwa
eneo hili kubwa lililokamilika miaka kumi iliyopita. Humo mna sehemu za
kuogelea, viwanja vyenye majani safi ndani na nje, Gym za mazoezi,
madarasa na vyombo mbalimbali vya mafunzo. Mbali na chuo, Rais Kikwete
alitembezwa uwanja wa “Stadium of Light” ambao hujaza watazamaji 49,000.
Huu ni uwanja wa tano kwa ukubwa Uingereza nzima. Hapa huwepo vilevile
maonyesho siyo madogo ya muziki, kama lile la mwimbaji nguli Rihanna
toka Barbados aliyetumbuiza juzi Alhamisi.
Kuna hilo la kiufundi, halafu historia.
Si wengi wanaofahamu historia za vilabu vyetu.
Rais alipowaeleza wanahabari wa Kizungu kuwa
zamani Simba ilipoanzishwa mwaka 1936 iliitwa Dar Sunderland, alikuwa
akikumbusha tulikotoka.
2:02 AM
Unknown
PILIKA PILIKA ZA SABA SABA YA 37.
Wakazi wa Jiji la Dar Wakiwa kwenye foleni tayari kwa kuingia kwenye
viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika barabara ya kilwa Jijini Dar Es
Salaam Mapema leo Asubuhi.
Baadhi ya Wafanyabiashara wakiendelea kuingia vifaa vyao tayari kwa maonyesho na kuuza bidhaa na huduma zao
Subscribe to:
Posts (Atom)