Tuesday, December 24, 2013


1016243_622850427736775_2127148511_n
1. Diamond Platnumz
Hakuna ubishi kuwa, mwaka 2013 Diamond Platnumz ndiye msanii aliyeingiza fedha nyingi zaidi. Pesa nyingi ya Diamond imetokana na malipo ya show zake za ndani na nje ya nchi. Kwa uhakika, mwaka huu pekee, Diamond amefanikiwa kuingiza takriban shilingi bilioni 1.
Kwa show za ndani peke yake, Diamond hutoza si chini ya shilingi milioni 10 ama 15 na kila wiki hufanya show zaidi ya 2. Hivyo tangu mwaka uanze, Diamond amekuwa akiingiza shilingi milioni 40 kila wiki. Tour za nje alizofanya mwaka huu ni pamoja na zile za Uingereza ambako alifanya show kwenye miji mitatu, show ya Burundi na Congo, show mbili za Kenya (Nairobi na Mombasa), show ya nchini Comoro ambako alilipwa si chini ya dola 30,000 na show ya Malaysia wiki iliyopita.
Kwa upande wa show za hapa nyumbani ambazo ni nyingi mno zisizo na idadi, ukiachana na zile za kawaida, Diamond aliingiza shilingi milioni 40 kwenye show 4 za Kili Music Tour ambapo kila show alilipwa shilingi milioni 10. Ndiye msanii aliyelipwa fedha nyingi zaidi kwenye ziara hiyo.
Pia amefanya show kadhaa za Fiesta 2013, show za promotion za Tigo na makampuni mengine, Tamasha la Matumaini, show ya Tulizana Tuko Wangapi ya Leaders Club, show yake na Nay wa Mitego (Dar Live na Maisha Club). Mwezi February 16 mwaka huu, Diamond alifanya show jijini Arusha ambayo kiingilio chake kilikuwa ni shilingi 150,000 ndani ya Club Safari na ukumbi kufurika.
Miezi kadhaa iliyopita pia hitmaker huyo wa ‘Number 1’ ameshaalikiwa kwenye show corporate kuburudisha wafanyakazi wa benki na taasisi zingine pamoja na watu binafsi na zote hizo zimemuingizia fedha nyingi. Pamoja na show, Diamond amekuwa akiingiza fedha nyingi zaidi kwenye malipo ya ringtones ambapo kila baada ya miezi mitatu amekuwa akiingiza si chini ya shilingi milioni 20. Kwa mujibu wa Push Mobile, akaunti ya Diamond kwenye kampuni hiyo ndio inayoingiza fedha nyingi kuliko msanii mwingine yeyote wa Bongo Flava.
Mkataba exclusive alioingia na kampuni ya simu ya Vodacom kuuza wimbo wake mpya My Number One kama muito wa simu, umezidi kumpandisha juu na ikidaiwa kuwa mkataba huo ni wa mamilioni ya shilingi.
1239507_650218681669184_1372786191_n
Ikumbukwe pia, Diamond ni balozi wa Cocacola. Mkataba huo ambao haijajulikana umemuingizia shilingi ngapi, lakini ni fedha inayoweza kuwa si chini ya shilingi milioni 100.
584fe16a273711e3b8f522000a1fbce9_7
Diamond ni miongoni mwa wasanii wengine 23 wa Afrika akiwemo Lady Jaydee kwenye mradi mkubwa wa Cocacola wa Coke Studio Africa.

1238789_10151593260760025_1742196233_n
2. Lady Jaydee
Huwezi amini, vuguvugu la Anaconda limemsaidia Jaydee si tu kukusanya mashabiki wengi zaidi, bali pia limempa fedha nyingi mno. Zaidi ya tiketi 3,500 zilinunuliwa kwenye show yake ya mwezi June ya Miaka 13 ya Muziki na kuingiza takribani shilingi milioni 100. Haikuishia hapo, albam yake Nothing But The Truth ilinunuliwa kwa kiasi kikubwa na kumfanya kuwa msanii pekee wa Bongo Flava anayeendelea kufurahia mauzo ya albam zake.
Hits zake mbili, Joto Hasira na Yahaya kutoka kwenye albam yake hiyo, zimebadilisha maisha yake na kumfanya kuwa mwanamuziki mwenye show nyingi zaidi pia. Lady Jaydee ametumbuiza kwenye karibu show zote za Kili Music Tour ambako ameingiza shilingi milioni 25.
Mwaka huu pia Lady Jaydee amefanya show nyingi kubwa ikiwemo ile ya uzinduzi wa filamu ya Lulu, Foolish Age, show yake kwenye Miss Tanzania 2013, Family Day Show ya Arusha iliyofanyika Eid Pili, Anaconda Show iliyofanyika Triple A na nyingine iliyofanyika Snow View Hotel. Akiwa Arusha pia, Lady Jaydee aliuza kopi za albam yake kama njugu pamoja na tiketi za Anaconda zilizouzwa kwa shilingi 15,000 kila moja.
June mwaka huu pia, Lady Jaydee alitumbuiza kwenye semina ya kuwezesha wanawake kuondokana na njaa na umaskini, iliyofanyika chini ya mfuko wa fursa sawa kwa wote chini ya mama Anna Mkapa. Biashara yake ya Nyumbani Lounge, imeendelea kufanya vizuri pia kwa kupata wateja wengi wanaoenda kupata chakula, vinywaji na burudani kutoka kwa bendi yake ya Machozi.
Bado anaingiza fedha kupitia udhamini wa Airtel kwenye show yake ya TV ya Diary of Lady Jaydee. Msanii huyo ambaye jina lake ni Judith Wambura pia miongoni mwa wasanii 24 wa bara la Afrika waliochukuliwa kwenye mradi wa Coke Studio Africa wa kampuni ya Cocacola unaoendelea jijini Nairobi Kenya.
Coke Studio Africa – the new, exciting music show featuring incredible live performances by the very best in Africa

421451_10150581514944221_264981067_n
3. AY
Humsikii sana rapper huyu kwenye show za Tanzania. Tofauti na wasanii wengine, fedha anazoingiza AY zinatokana zaidi na endorsements na biashara zake anazofanya. Pesa nyingi alizoingiza zimetokana na mkataba wa mwaka mmoja na Airtel wa ubalozi uliokamilika mwezi May mwaka huu.
Katika ubalozi huo wa Airtel Africa, AY aliungana na wasanii wengine watatu wa Afrika ambao ni pamoja na Papa Wemba, Tuface na Daddy Owen wa Kenya. Katika mkataba huo AY alilipwa dola za Kimarekani 80,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 129.
Rapper huyo wa ‘Machoni Kama Watu’ ni balozi pia wa bia ya Peroni ya Italia na kupitia mkataba huo, AY ameingiza mkwanja mwingi. AY pia ni mwanzilishi mwenza wa kipindi cha Mkasi kinachoendeshwa na Salama Jabir. Kipindi hicho kina wadhamini wawili, Cocacola na Airtel na hivyo kupitia mgawanyo wa mapato, AY amekuwa akiingiza pia fedha ya kutosha.
AY ni CEO wa kampuni ya Unity Entertainment inayojihusisha na kuandaa show, matangazo, kuleta wasanii wa nje na mambo mengine. Mwaka huu pekee, ikishirikiana na kampuni ya SK Entertainment, kampuni yake imeandaa show kibao zikiwemo zile zilizofanyika Elements Lounge ambapo Avril, Prezzo, Huddah Monroe na J-Martins wamewahi kuhudhuria.
Maisha ya kawaida ya rapper huyu ndio yanayowafanya watu wengi wasijue ukubwa wa kile anachokiingiza. Macho yake ameyaelekeza zaidi kwenye uwekezaji na anawekeza haswaa. Kuna tetesi kuwa, AY anajenga ghorofa lake maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. Anasemekana kuwekeza pia mkoani Mtwara alikonunua ardhi ya kutosha. Mungu ndio anajua ni wapi alikowekeza tena.

e23fe27c081911e3a88722000a1f90d0_7
4. Ommy Dimpoz
Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yupo kwenye ziara ya muziki nchini Marekani ameingiza fedha zake nyingi kupitia show alizofanya. Ziara zake za Ulaya na Marekani pekee zimemuingizia dola 50,000 ambazo ni sawa shilingi milioni 81.
Tangu aachie wimbo wake mpya Tupogo, tayari Ommy ameshaingiza shilingi milioni 50. Kwenye show yake ya hivi karibuni ya Tupogo Night iliyofanyika Club Billicanas, Ommy alipeleka nyumbani shilingi milioni 10 baada ya kukata gharama zote. Watu 1,770 walihudhuria show hiyo.
Show yake ya Burundi ya mwanzoni mwa mwezi uliopita ilimuingizia staa huyo shilingi milioni 30. Ommy hutoza si chini ya shilingi milioni 7 kwa show na kwa mwezi, amekuwa na uhakika wa kufanya show tatu ama nne za ndani bila kusahau show za Kili Music Tour.
Hivi karibuni kwenye segment ya Tell it All ya Bongo5, Ommy alifunguka kuwa makampuni mengi yamekuwa yakimfuata kumpa endorsements lakini msimamo wake wa kutaka kulipwa fedha ya uhakika imemfanya azikatae nyingi lakini yupo mbioni kupata deal kubwa. Mpaka sasa Ommy anajenga nyumba mbili kwa mpigo zenye thamani ya shilingi milioni 250 hadi zilipofikia. Tayari ana viwanja vingine viwili anavyotaka kuangusha mijengo mingine. Hivi karibuni pia atakuja na clothing line yake ya PKP.

7203_294710874001268_1825630445_n
  5. Madee
Hii inaweza kuwa surprise kwa wengi lakini Madee ni mfano tosha wa jinsi single moja inavyoweza kubadilisha maisha ya msanii. Tangu atoe single yake, Sio Mimi, Madee ameshaingiza si chini ya shilingi milioni 200.
Mwaka huu ameshafanya show 10 za kampeni ya Tigo ambapo kila moja alilipwa shilingi milioni 3, show 15 za Airtel kwa kiwango hicho hicho. Alifanya show mbili za kampeni za Coca Cola, ile ya uzinduzi wa Coke Zero na Cocacola Bonanza Mlimani City. Bado ameendelea kufanya show za Fiesta 2013. Madee pia alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye show ya Fuse ODG iliyofanyika September 7 kwenye viwanya vya ustawi wa jamii jijini Dar es Salaam.

IMG_1010 (800x534)
6. Mwana FA
Mwanzoni mwa mwaka huu, Hamis Mwinjuma aka Mwana FA alikuwa msanii wa tatu miongoni mwa wasanii waliongiza fedha nyingi kupitia malipo ya miito ya simu, RBT ambapo aliingiza shilingi milioni 18. Alifanya show mbili kwenye Kili Music Tour ambapo aliingiza si chini ya shilingi milioni 7 pamoja na show kadhaa za Fiesta 2013.
Show yake ya The Finest ilimuingizia shilingi milioni 19. Hivi karibuni alichukuliwa na kampuni ya Vodacom kuzunguka baadhi ya mikoa kwenye kampeni yao na CCBRT kuhusiana na kukuza uelewa wa tatizo la Fistula na kulipwa mkwanja kama balozi wa kampeni hiyo.
Mwaka huu FA amefanya matangazo kadhaa ya Vodacom. Hivi karibuni pia aliingia kile kilichoonekana mkataba kama balozi wa simu za Samsung Galaxy Tanzania japo haijulikani kama ulikuwa mkataba wa ubalozi kama ilivyo mingine.
Mwana FA pia amefanya show za nje zikiwemo za Kenya na Afrika Kusini aliyofanya siku ya Eid mwezi uliopita. Kama wasanii wengine pia, FA ameingiza fedha nyingi kwa show za kawaida za hapa nyumbani na zile za promotion.
3ec62770206d11e382b622000ae912ed_7
CHEGE
Mwaka huu Chege peke yake alifanya show sita nje ya nchi ambazo kila show alilipwa shilingi milioni 4. Akiwa na Temba ambao kwa pamoja hutoza shilingi milioni 6, Chege amefanya show zaidi ya 30 zikiwemo zile za Fiesta, za promotion mbalimbali na zile za kawaida.
 Pamoja na hivyo, Chege ana biashara ya salon.

1010701_10151711560347558_1761716231_n
8.PROFESA J
Profesa Jay aliingiza shilingi milioni 20 za Kili Music Tour, alifanya show kubwa ya Jose Chameleone April mwaka huu, show kibao za promotion za makampuni, show ya kampuni ya IPP kwaajili ya Walemavu, Diamond Jubilee mwezi January, na show zingine za kawaida za Dar na mikoani. Pia nguli huyo wa rap ya Tanzania ameingiza fedha nyingi kupitia show nyingi za Lady Jaydee.
Prof J amewekeza kwenye biashara ya salon ambayo tayari inafanya vizuri na ameshafungua studio ya kurekodi muziki iliyopo kwenye hatua za mwisho kuanza kazi. Jize aliingiza pia fedha kupitia kampeni ya magazeti ya Mwananchi kwa kufanya matangazo na show za mikoani.
9. Nay wa Mitego
53c24b9c156c11e3959e22000aeb1b4e_7
NAY WA MITEGO
Tangu mwaka uanze, Nay wa Mitego ameshafanya show zaidi 20 zilizomuingizia si chini ya shilingi milioni 60. Show hizo ni pamoja na zile za promotion za makampuni ya simu, show mbili za Muziki Gani, show ya Kili Music Tour, show za Fiesta na zile za kawaida. Pia ana biashara zake ambazo kwa pamoja humuingizia si chini ya shilingi milioni 4 kwa mwezi. 10.Temba
 2648cdb8274f11e3a2f822000a1f985f_7
MH TEMBA
 
 


Mchungaji Gwajima.
Stori:  Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
SIRI nzito imefichuka! Baadhi ya maaskofu na wachungaji (baadhi lakini) wa makanisa ya kilokole nchini wanadaiwa kutumia hirizi ili kujaza waumini, Uwazi limenyetishiwa.
SEHEMU ZINAZOKAA HIZIRI
Kwa mujibu wa mfichua siri huyo, watumishi hao wa Mungu wanaojihusisha na ushirikina wamekuwa wakizifunga hiziri hizo sehemu ya juu ya mkono wa kulia na kufichwa na shati la mikono mirefu ambalo nalo huwa ndani ya koti la suti.
Ikadaiwa kuwa, wengine huficha sehemu ya siri ya nguo ya ndani kulingana na maelekezo ya waganga wanaowatengenezea hirizi hizo.
Mchungaji Rwakatare.
WAUMINI NAO WANENA
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mapaparazi wetu jijini Dar juzi, baadhi ya waumini wa makanisa hayo ya kiroho walisema wamegundua kuwa, wapo viongozi wa makanisa hayo ambao hutumia nguvu za giza ili kuvuta waumini wengi.
LENGO LA KUTUMIA HIRIZI
Waumini hao ambao walidai wana uhakika kuna watumishi wa Mungu feki wengi siku hizi, walisema maaskofu na wachungaji wanaotumia hiziri wana lengo la kujipatia ‘kondoo’ wengi hivyo kuwa na uhakika wa kukusanya sadaka nyingi.
Kaldinali Polycarp Pengo.
NI WALE WENYE NIA YA UTAJIRI TU
Habari zaidi zinadai kuwa, watumishi wa Mungu waliotumbukia kwenye ushirikina huo ni wale wanaosaka utajiri tu na neno la Mungu kwao si kitu cha lazima.
Watumishi hao wanadaiwa kusema kwenye madhabahu ya makanisa yao kwamba wameokoka, wanatembea na Bwana Yesu, lakini ndani ya mioyo yao hakuna ulokole wala uinjilisti zaidi ya blaablaa tu.
ROMANI, KKKT, ANGLIKANA WALIA
Ikazidi kudaiwa kuwa, pigo kubwa la kuwepo na kutanuka kwa makanisa ya kiroho nchini ni kwa Romani Katoliki (chini ya Kaldinali Polycarp Pengo) Walutheri, KKKT (chini ya uongozi wa Alex Malasusa) na Anglikana (lililokuwa likiongozwa na Valentine Mokiwa) ambao miaka ya karibuni makanisa yao yamemegwa, baadhi ya waumini wamekimbilia katika makanisa ya kiroho.
Askofu Alex Malasusa.
Hata hivyo, si waumini wote waliokimbilia kwenye makanisa hayo wapo kwa watumishi wanaodaiwa kutumia hiziri, wengine wapo kwenye makanisa salama.
WATUMISHI WA MUNGU WASAKWA
Kufuatia kufichuka kwa siri hiyo, Uwazi liliwatafuta viongozi mbalimbali wa makanisa nchini ili kuzungumzia madai hayo.
Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania  ambaye sasa ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Dk. Valentine Mokiwa alipoulizwa juzi na Uwazi kuhusu kuwepo kwa matumizi ya hirizi kwa baadhi ya watumishi wa Mungu, alisema:
Askofu Kakobe.
“Watu wanasema kuwa nguvu za giza hutumika katika baadhi ya makanisa ya kiroho, lakini kwa upande wangu sijaujua ukweli wala sijathibitisha kwa sababu ni mambo ya kishetani.
“Siku hizi dini imekuwa kama soko  kwani wengi hutumia uongo kanisani  kwa lengo la kuwajaza watu.”
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima kwa upande wake alisema wingi wa waumini katika makanisa mbalimbali ya kilokole hutokana na huduma nzuri na mafundisho mema yanayotolewa na wasimamizi wa makanisa hayo.
Kwa upande wake Kiongozi wa Kanisa la Huduma ya Maombezi,  Mbezi Salasala jijini Dar es Salaam, Nabii Flora Peter alisema mtumishi wa Mungu  kutumia hirizi katika kuendesha Neno la Mungu ni dhambi kubwa katika utumishi.
“Mungu hapendi, kama kuna  mtu wa namna hiyo  basi huyo hafai kuongoza kanisa  kwa sababu dini ni imani ya mtu, sasa haiwezekani utumikie  mabwana wawili,” alisema Nabii Flora.
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Magnus Muhiche  yeye alisema hajawahi kuona ila anachokijua wingi wa watu katika makanisa ni sawa  na biashara.
Askofu John Said  wa Kanisa la Victoria lililopo Mabibo External jijini Dar es Salaam alipoulizwa kuhusu hilo  hakupenda kuchangia kitu chochote.
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi la Ubungo Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’  alipigiwa simu, hakupokea, akatumiwa ujumbe wa simu wa meneno (SMS) hakujibu licha ya ujumbe huo kurudiwa mara mbili kwa saa tofauti.
Mwaka 1993, Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel & Bible Fellowship, Zakaria Kakobe alifanya mkutano wa Injili kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi, Gangilonga, Iringa ambapo baadhi ya wachungaji wa makanisa wa mkoa huo walifika kumshuhudia.
Baada ya mkutano kumaliza, wachungaji hao walisikika wakisema kuwa, walifika kwa lengo la kuthibitisha kwa macho yao uvumi ulionea kwamba, Kakobe anatumia hirizi kuhubiri, hasa wakati wa kuponya wagonjwa akiwa ameishika mkononi.
Wachungaji hao walishangaa mpaka mwisho wa mahubiri, Kakobe hakuwa ameshika hirizi na kumpongeza kwamba, kumbe maneno ya watu juu ya mtumishi huyo wa Mungu hayakuwa na ukweli hasa kwa jinsi alivyoliitia jina la Yesu kuponya watu.

waliotembelea blog