TIMU ya Coastal Union imewasili
jijini Tanga ikiwa na mikakati mizito ya kuhakikisha inawanyamazisha
wapinzani wao Azam FC ikiwa ni muendelezo wa Michuano ya Ligi kuu soka
Tanzania bara mchezo unaotarajiwa kucheza kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani
wikiendi ijayo.
Akizungumza leo na waandishi wa
habari, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa sasa
nguvu zao watazielekeza kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye mjini
hapa.
Amesema kuwa dhamira yake
aliyoipanga ni kuchukua pointi tatu muhimu dhidi ya Ruvu Shooting
haikuweza kutimia na kujikuta wakilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1
hivyo atahakikisha inatimia kwenye mechi hiyo.
Amesema timu hiyo imerudi salama
mkoani hapa na tayari wameshaanza kujipanga imara kuhakikisha mechi hiyo
timu inapata ushindi n kutokana na uimara wa kikosi chao
Aidha amesema kuwa wachezaji wa
kikosi hicho wameimarika zaidi na wapo imara kuweza kupambana kufa na
kupona ili kuchukua pointi tatu muhimuzo zitawasogeza kwenye nafasi za
juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Hata hiyo amewataka wapenzi na
mashabiki wa soka mkoani hapa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika
mchezo huo ili kuipa hamasa timu hiyo kuweza kutimiza ndoto zake.
Mwisho.