Thursday, July 11, 2013
8:50 AM
Unknown
CHECK HAPA TID ALIVYOJIACHIA UK, WAZUNGU WAMSHANGAA WAMGEUZA KIVUTIO
T.I.D msanii wa long time kwenye game ya bongoflava tangu enzi za Zeze,Siamini hadi leo hii na Kiuno na bado anafanya vizuri. Wiki kadhaa zilizopita baada ya kumaliza msiba wa mshikaji wake Mangwea, T.I.D alisafiri kwenda England kufanya show ambako huko pia ndiyo alifanya interview inayozungumziwa sana hivi sasa kwenye mitandao. Chukua time kidogo kumcheki T.I.D akiwa kwenye mitaa ya huko UK.
8:44 AM
Unknown
China imekubali kutoa mkopo wa dola bilioni 1.1 kwa
Nigeria ili kufadhili ukarabati wa miundo msingi.Mkataba huu umeafaikiwa
wakati wa ziara ya Rais Goodluck Jonathan mjini Beijing,ambapo
alikutana na mwenyeji wake Xi Jinping.
Fedha hizi zitasaidia ujenzi wa barabara,
viwanja vya ndege na kujenga miji minne na njia mpya ya reli.China
inawekeza kwa kiwango kikubwa Barani Afrika ambapo pia imekua ikipata
raslimali za mafuta na madini.Nigeria inaongoza kwa kuzalisha mafuta Afrika lakini kwa miaka imekua na miundo msingi mibovu, huku mamilioni ya raia wake wakiishi kwa umasikini. Bw. Xi amesema nchi mbili zinashirikiana kwa minajili ya kuboresha maisha ya watu wake.
Rais Jonathan anaongoza ujumbe wa wawekezaji wa Nigeria huko China na ziara ya siku nne itasaidia kuleta mshikamano wa karibu wa kibiashara.
Kampuni za ujenzi za Ki-China zimeanza kujenga barabara nchini Nigeria, kwa kandarasi ya dola bilioni 1.7.China kwa upande wake inatarajia kupata mapipa laki mbili ya matufa ghafi kutoka Nigeria ifikapo mwaka 2015.
8:40 AM
Unknown
Marekani inaendelea na mpango wake wa kutoa ndege za
kivita kwa jeshi la Misri licha ya msukosuko wa kisiasa unaokumba nchi
hiyo. Hatua hii inajiri wakati Marekani ikiendelea kutathmini matukio ya
wiki jana ambapo jeshi lilimuondoa madarakani Rais Mohammed Morsi.
Msaada wa kijeshi kwa Misri ungesitishwa endapo
Marekani ingelitaja matukio ya wiki jana kama mapinduzi ya kijeshi.
Kundi la Muslim Brotherhood linalomuunga mkono Morsi linasisitiza
arejeshwe madarakani.Wafuasi wake wamekua wakiandamana karibu na kambi kuu ya jeshi ambapo anaaminika kuuzuiliwa. Hapo Jumatatu,wafuasi wa Brotherhood 51 waliuawa kwa kupigwa risasi na jeshi wakati wanakabiliano.
Utawala wa mpito umesema kwamba Bw. Morsi anazuiliwa eneo salama na kwamba haki zake zinazingatiwa.Maafisa wa Marekani wamesema ndege mpya za kivita aina ya F-16 zitawasilishwa katika wiki chache zijazo.
Mpango wa kufadhili jeshi ulianza kutekelezwa mapema mwaka huu na jeshi inatarajia kupokea ndege 20 za kivita. Msemaji wa ikulu ya Rais amesema Marekani haitabadilisha mpango wa kufadhili jeshi la Misri, japo inaendelea kutathmini kuhusu matukio ya kisiasa. Msaada wa kijeshi nchini Misri ambao hutolewa na Marekani hufikia dola bilioni 1.3 kila mwaka.
Hapo Jumanne, kibali cha kumkamata kiongozi wa Muslim Brotherhood Mohamed Badie kilitolewa pamoja na wakuu wengine tisa wa kundi hilo. Viongiozi hao wamelaumiwa kwa kuchochea ghasia mjini Cairo ambapo zaidi ya watu 50 waliuawa na mamia kujeruhiwa.
5:57 AM
Unknown
HII NDIO KAULI YA JOKETI BAADA YA DIAMOND KUJUTIA KUMUACHA
Hivi karibuni, katika kipindi cha “Take One” cha Clouds TV na Zamaradi
Mketema, msanii Diamond Platnumz aliongelea jinsi anavyojutia kumuingiza
mrembo Jokate Mwegelo kwenye mapenzi halafu, halafu akachanganya mambo
na Wema Sepetu.
kama uliikosa interview hiyo, click link ifuatayo kuiangalia video: VIDEO: Diamond – Najuta kumuingiza Jokate kwenye mapenzi, kisha nikamrudia Wema
Jokate amesema
amefurahi kuona Diamond amefunguka na kusema ukweli.
Na hii ndio kauli yake:
“Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was innocent in that whole matter,” amenukuliwa Jokate na mtandao huu.
Na hii ndio kauli yake:
“Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was innocent in that whole matter,” amenukuliwa Jokate na mtandao huu.
Subscribe to:
Posts (Atom)