|
Waziri
mkuu Mizengo Pinda akitua na ndege katika uwanja wa ndege wa Buzwagi
mjini Kahama mkoani Shinyanga kujionea hali hali ya maafa ya mvua kubwa
ya mawe na upepo iliyonyesh juzi katika kata ya
Mwakata-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kahama
|
Ndege aliyokuja nayo waziri mkuu Mizengo Pinda-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kahama
Waziri mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama baada ya kuwasili-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kahama
|
Waziri
mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa
Shinyanga akiongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kahama |
|
Waziri mkuu Mizengo Pinda baada ya kufika katika kata ya Mwakata-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kahama |
|
Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwa katika moja ya familia ya Masemba Mabuli iyofiwa na watoto watano katika maafa ya mvua-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kahama |
Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenister
Muhagama, akielekeza kuwa misaada yote inayotolewa na wadau mbalimbali
isipelekwe makao makuu ya wilaya, badala yake ipelekwe katika eneo la
maafa-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kahama
Moja ya nyumba zilizoharibika-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kahama
Wakazi
wa Mwakata wakiwa na ndugu jamaa na marafiki wakifarijiana katika moja
ya familia iliyopatwa maafa wakiishi kwa pamoja baada ya kukosa makazi-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kahama
|
Waziri mkuu akishuhudia makaburi katika kata ya Mwakata-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kahama |
Makaburi 5 ya familia moja-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kahama
+++++++++++++++
Wakati idadi ya watu waliopoteza maisha katika maafa yaliyosababishwa
na mvua iliyonyesha ikiambatana mawe, upepo mkali na kubomoa nyumba za
wananchi Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, ikiongezeka kutoka 42 na
kufikia 46, baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamelihusisha janga hilo na
ushirikina.
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Mwakata wilayani Kahama, Salum
Mohamed, alimweleza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa baadhi ya wananchi
wamejenga dhana kuwa tukio hilo limetokana na ushirikina.
Hata hivyo, Pinda aliyewasili eneo hilo jana, aliwataka wananchi hao
kuachana na dhana hiyo potofu kuwa mvua zilizonyesha na kusababisha
maafa hayo, zimetokana na ushirikina.
Mvua hiyo ilinyesha juzi usiku na kuleta maafa katika vijiji vya
Mwakata, Nhumbi na Magung’hwa vilivyopo kata ya Isaka wilayani Kahama.
Idadi hiyo imeongezeka kufuatia majeruhi wanne waliokuwa wamelazwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kufariki dunia usiku wa kuamkia
jana kuongeza idadi ya waliokufa katika janga hilo kufikia 46.
Waziri Mkuu, alitembelea vijiji vilivyoathirika na kuwapa pole
waathirika na kusema serikali itahakikisha waathirika wote wanapewa
msaada unaotakiwa na kwamba tayari chakula kimeanza kugawiwa kwa
wananchi na mahema ya kutosha yametolewa.
Pinda aliagiza waatalam kutoka
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuweka kambi katika kijiji cha
Mwakata kilichoathirika kwa ajili ya kufanya tathmini.
Waziri Mkuu alisema kutokana na janga hilo, kuna uwezekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko.
Aidha, aliiagiza timu ndogo ya uratibu wa maafa iliyoundwa na Mkoa
wa Shinyanga, isimamie vizuri misaada inayotolewa na wasamaria wema ili
iwafikie waathirika wote.
MBUNGE WA MSALALA
Mbunge wa Msalala (CCM), Ezekiel Maige, ambaye alitembelea katika
hospitali hiyo jana, alithibitisha kuwa kati ya walioongezeka ni watoto
watatu, wakazi wa kijiji cha Mwakata na mazishi yalifanyika jana katika
kijiji hicho.
PINDA AWASILI, ATOA TAMKO
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, jana aliwasili Kahama na kutembelea
vijiji vilivyoathirika na kuwapa pole waathirika na kuwataka wananchi
waondokane na fikra potofu kuwa tukio limetokana na masuala ya
kishirikina.
Alisema serikali itahakikisha waathirika wote wanapewa msaada
unaotakiwa na kwamba tayari chakula kimeanza kugawiwa kwa wananchi na
mahema ya kutosha yametolewa.
Pinda aliagiza waatalam kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
kuweka kambi katika kijiji cha Mwakata kilichoathirika kwa ajili ya
kufanya tathmini.
Waziri Mkuu alisema kutokana na janga hilo, kuna uwezekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko.
Aidha, aliiagiza timu ndogo ya uratibu wa maafa iliyoundwa na Mkoa
wa Shinyanga, isimamie vizuri misaada inayotolewa na wasamaria wema ili
iwafikie waathirika wote.
MISAADA KWA WAATHIRIKA
Serikali kupitia Kitengo cha Maafa kilichopo Ofisi ya Waziri Mkuu,
imetoa tani 20 za chakula ambapo kati ya kiasi hicho, maharage tani
tano, sukari tani 1.3 na mafuta ya kupikia lita 1,126.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Florens Turuka, katika
taarifa yake jana kwa vyombo vya habari alisema misaada mingine
iliyotolewa kwa waathirika hao ni blanketi 650, ndoo 82 zenye ujazo wa
lita 20, ndoo 82 za lita 10 vifaa vya kupikia seti 82 na madumu 82.
Dk.Turuka alisema misaada zaidi inahitajika kwa waathirika kama
vile sare za shule, madaftari ya wanafunzi, mavazi ya kike na kiume na
chakula.
“Kwa kuzingatia kuwa waathirika hawa wamepoteza mali na fedha
katika maafa haya, misaada ya vifaa vya ujenzi inahitajika, utaratibu wa
kupokea misaada hiyo kwa walio Dar es Salaam wanaweza kuiwasilisha
Idara ya Kuratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu au kwa Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga,” alisema.
Dk.Turuka alisema serikali itaendelea kuwasaidia waathirika dhidi
ya changamoto zinazoweza kujitokeza hususani za kiafya zinazosababisha
na uchafuzi wa vyanzo vya maji na mazingira.
WAZIRI JENISTER MHAGAMA
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Bunge), Jenister Muhagama, alielekeza kuwa misaada yote
inayotolewa na wadau mbalimbali isipelekwe makao makuu ya wilaya, badala
yake ipelekwe katika eneo la maafa.
Kituo kikubwa cha waathirika kimewekwa katika Shule ya Msingi
Mwakata ambako waathirika wamehifadhiwa kwa muda katika majengo matatu.
Mbunge wa Msalala, Maige alimuomba Waziri Mkuu kuangalia uwezekano
wa kufuta kodi ya majengo ili vifaa vya ujenzi viuzwe kwa bei rahisi
kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora.
Nyumba nyingi zilizobomoka katika tukio hilo zimejengwa kwa
matofali ya tope, hivyo mvua kubwa zinaponyesha zinabomoka kirahisi.
Maige aliomba ahadi ya serikali ya kuwasaidia waathirika wa tukio hilo
ifanyiwe kazi haraka.
Wananchi kwa upande wao, waliiomba serikali kuwajengea vyoo zaidi
katika kambi waliyohifadhiwa kwa kuwa wanachokitumia sasa ni kimoja tu.
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Mwakata, Salum Mohamed, alisema
kutokana na idadi kubwa ya wananchi walioathirika kuendelea kutumia choo
kimoja ni hatari kiafya kwa kuwa kunaweza kutokea magonjwa ya mlipuko.
Mohamed aliomba huduma ya umeme irejeshwe kijijini hapo kufuatia nguzo za umeme zilizokuwapo kuharibiwa na mvua.
DC KAHAMA
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya, alisema katika tukio hilo
kaya zilizoathirika ni 400 zenye idadi ya watu zaidi ya 1,500.
Mpesya alisema majeruhi 52 ambao ni kati ya 98 waliokuwa wamelazwa
katika Hospitali ya wilaya hiyo, wameruhisiwa baada ya hali zao kuwa
nzuri.
CUF WATOA SALAMU
Wakati huo huo, Chama cha Wananchi (CUF), kimetoa salamu za
rambirambi kwa ndugu na jamaa za watu waliopoteza maisha katika tukio
hilo.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Shaweji Mketo, katika taarifa yake
kwa vyombo vya habari alisema chama hicho kimebaini kuwa madhara makubwa
ya mafuriko yanayotokea katika maeneo mbalimbali nchini yanasababishwa
na miundombinu ya mikondo ya maji kutozingatiwa kurekebishwa.
Alisema mfano katika Wilaya ya Kahama, imebainika kwamba wakazi
walio pembezoni mwa barabara, kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kupunguza
madhara endapo barabara zingejengwa mitaro yenye uwezo wa kupitisha maji
ili kuyaelekeza mahali stahiki na siyo kwenye nyumba za watu.
Mketo alisema CUF inaitaka serikali kupitia upya utaratibu wa
kukabiliana na majanga makubwa ili kuongeza uharaka wa kuyashughulikia.
Alisema serikali inapaswa kuhakikisha mazingira yote yanayoweza kuleta
madhara ya mafuriko yanaepushwa mapema na mikondo yote ya maji hasa
mito, ilindwe na kuangaliwa mara kwa mara kuhakikisha uwezo wake wa
kutiririsha maji unaongeza ufanisi wake.
“CUF kinatoa pole kwa wananchi wote wa Kahama, Moshi, Rufiji,
Morogoro na Katavi walioathiriwa na mafuriko haya. Pia CUF inatoa salamu
za rambirambi kwa wote waliofiwa na ndugu na jamaa zao katika mvua
hizi,” alisema Mketo.