Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa pole wanafamilia wa MzeeZakaria Limbe ambao
wamepoteza wototo wane katika mafa ya mvua kubwa yenye upepo na mawe
iliyonyesha katika eneo la Mwakata Machi 3 usiku. Alikwenda katika
maeneo yaliyoathirika leo kuwapa pole wananchi.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipa pole Shoma Petro ambaye ni mmoja wa majeruhi
wa maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa yenye upepo na mawe iliyonyesha
kwenye eneo la Mwakata wilayani Kahama Machi 3, 2015 usiku.
Mheshimiwa Pinda alikwenda kwenye hospitali a wilaya ya Kahama kuwapa
pole majeruhi waliolazwa hospitalini hapo.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Mzee Donald Lubunda ambaye amepoteza
watoto wane katika maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha
katika eneo la Mwakata wilayani Kahama Machi 3 usiku. Mheshimiwa Pinda
alikwenda kuwapa pole waathirka leo
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu,
Jenista Mhagama (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa ShinyangaDr Rufunga kukagua
maeneo yalyoathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na mawe
katika eneo Mwakata wilayani Kahama usiku Machi 3, 2015. Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametembelea baadhi ya familia zilizopoteza
wapendwa wao pamoja na majeruhi waliolazwa kwenye hospitali ya wilaya
ya Kahama kutokana na maafa ya mvua ya mawe iliyonyesha usiku wa
kuamkia jana.
Akizungumza na wafiwa katika vijiji vya Mwakata na Magugung’hwa katika
kata ya Mwakata wilayani Kahama leo mchana (Alhamisi, Machi 5, 2015)
Waziri Mkuu alisema Serikali haitawaacha katika kipindi hiki kigumu
walichonacho.
Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuwafikishia wafiwa na waathirika
wa maaafa hayo salamu kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye aliwaomba
wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
Akiwa katika shule ya msingi Mwakata ambako watu 250 wanahifadhiwa
hapo kwa muda, Waziri Mkuu aliwaambia wakazi hao pamoja na wananchi
waliofika kumsikiliza kwamba Serikali imepanga kuleta vyakula, mahema,
mablanketi na madawa ya hospitali ili kuwasaidia waathirika hao.
“Serikali haitaacha mtu afe kwa njaa,” alisema.
0 maoni:
Post a Comment