Benfica wamekamilisha Usajili wa Kipa Brazil Julio Cesar ambaye alikuwa anaidakia timu ya QPR
Julio Cesar mwenye miaka 34 alisainiwa na Klabu ya Uingereza QPR mwaka 2012.
Julio Cesar akiokoa mkwaju wa penati kwenye Kombe la Dunia
LUIS SUAREZ: ‘SITAUMA MTU MENO TENA NIMEPATA USHAURI NA ONYO KALI...SASA NITUPIENI MACHO MUONE MAKALI YANGU UWANJANI!!
Hivi sasa Suarez yupo kwenye Kifungo cha Miezi Minne alichopewa na FIFA baada ya kumuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini wakati wa Mechi ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil hapo Juni 25 wakati Uruguay inacheza na Italy na hilo lilikuwa tukio lake la 3 la kung’ata Meno Uwanjani.
Lakini Suarez, mwenye Miaka 27, amesema: “Nawaambia Mashabiki, msiwe na wasiwasi kwa sababu sitarudia tena!”
“Nimeongea na Madaktari wa Magonjwa ya Akili na wameniambia nilikabili tatizo hili na kuomba msamaha. Nimefanya hivyo. Sasa naangali baadae kuhusu Barcelona.”
Mara baada ya Kifungo hicho alichopewa Brazil ambacho kilimkataza kushughulika na lolote kuhusu Soka, Suarez alikata Rufaa huko CAS, Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, na kupunguziwa Adhabu kwa kuruhusiwa kufanya Mazoezi na pia kucheza Mechi za Kirafiki.
Jana Usiku Suarez aliweza kuichezea Barcelona kwa mara ya kwanza kwenye Mechi ya Kirafiki Uwanjani Nou Camp alipoingizwa Dakika 13 za mwishoni wakati Barcelona ilipoichapa Club Leon ya Mexico Bao 6-0 na kutwaa Joan Gamper Trophy.
Wakati huo huo, Barcelona imekanusha kuwa ilimnunua Suarez kwa Pauni Milioni 75 kutoka Liverpool na kusema Fedha sahihi ni Pauni Milioni 65.
SUAREZ: Matukio yake ya utata:
Juni 2014: - Afungiwa Miezi 4 kwa kumng’ata Beki wa Italy Giorgio Chiellini
Aprili 2013: – Afungiwa Mechi 10 kwa kumng’ata Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic
Des 2011: – Afungiwa Mechi 8 kwa kumkashifu Kibaguzi Patrice Evra wa Man United