FRANCE,
wakiwa njiani kwenda Brazil kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia
zinazoanza Alhamisi, Jana waliifumua Jamaica Bao 8-0 kwenye Mechi
iliyochezwa Grand Stade Lille Métropole huko Mjini Lille, France.Hadi Mapumziko, Franza walikuwa mbele kwa Bao 3-0 kwa Bao za Yohan Cabaye, Blaise Matuidi na Karim Benzema.
Kipindi cha Pili, Matuidi na Benzema waliongeza Bao zao huku Olivier Giroud na Antoine Griezmann wakipiga Bao zilizobaki.
Huko Brazil, France wako KUNDI E pamoja na Honduras, Switzerland na Ecuador.
Kwenye
Mechi hii, Straika wa Real Madrid Benzema aling’ara mno na kuficha
kabisa pengo la Franck Ribery ambae ataikosa Brazil baada ya kuumia.
ILIVYOKUWA UPANDE WAO FRANCE
May 27 - France 4 Norway 0
Stade de France, Paris
Paul Pogba 15; Olivier Giroud 51, 69; Loic Remy 67
June 1 - France 1 Paraguay 1
Allianz Riviera, Nice
Antoine Griezmann 82
June 8 - France 8 Jamaica 0
Stade Pierre-Mauroy, Lille
Yohan Cabaye 17, Blaise Matuidi 20, 66; Karim Benzema 38, 63; Olivier Giroud 53; Antoine Griezmann 77, 89