Friday, August 29, 2014

KUNDI A 

Atletico Madrid 
Juventus 
Olympiakos 
Malmo 

KUNDI B 

Real Madrid 
Basle 
LIVERPOOL
Ludogorets 

KUNDI C 

Benfica 
Zenit St Petersburg 
Bayer Leverkusen 
Monaco 

KUNDI D 

ARSENAL
Borussia Dortmund 
Galatasaray 
Anderlecht 

KUNDI E 

Bayern Munich
MANCHESTER CITY
CSKA Moscow 
Roma 

KUNDI F 

Barcelona 
Paris St-Germain 
Ajax 
Apoel Nicosia 

KUNDI G 

CHELSEA
Schalke 
Sporting Lisbon 
Maribor 

KUNDI H 

Porto 
Shakhtar Donetsk 
Athletic Bilbao 
Bate Borisov 



UEFA Leo imempa Tuzo yao ya Mchezaji Bora wa Mwaka Cristiano Ronaldo baada ya kuwabwaga kwenye Kura Kipa wa Mabingwa wa Dunia Germany, Manuel Neuer na Mchezaji mwenzake wa Klabu ya Bayern Munich anaechezea Holland, Arjen Robben.
Ronaldo, Miaka 29, alifunga Bao 17 katika Mechi 11 za Ulaya wakati Real Madrid inaelekea kutwaa Taji lao la 10 la Ulaya walipobeba Kombe la UEFA CHAMPIONS LIGI na pia kuisaidia Klabu yake kutwaa Copa del Rey Msimu uliopita huko Spain.
Baada ya kukabidhiwa Tuzo yake, Ronaldo alisema: “Nimefurahi kweli kweli. Lazima niwashukuru Wachezaji wenzangu, Familia yangu, Marafiki zangu. Sina Kombe hili kwenye Makumbusho yangu, nitaliweka!”


Awali Majina ya Wachezaji 35 yalipigiwa Kura na kubakia 10 na kutangazwa hapo Julai 18 na kisha kubakishwa Matatu ambayo hii Leo ndio Mshindi kapatikana.
Wapigaji Kura ya Tuzo hii ni Jopo la Wanahabari maalum toka Nchi zote Wanachama wa UEFA.
Tuzo hii ilianzisha na UEFA Mwaka 2011 ili kuziba pengo la Ballon d'Or ambayo iliunganishwa na Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani na pia kuibadili ile Tuzo ya zamani ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Klabu.

WASHINDI WALIOPITA:
2010–11 Lionel Messi [Barcelona]
2011–12 Andrés Iniesta [Barcelona]
2012–13 Franck Ribéry [Bayern Munich]


DROO ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI imefanyika leo hii usiku  huko Monaco na Timu 4 za England, Manchester City, Liverpool, Chelsea,na Arsenal zimepata timu za kucheza nazo.
Taswira huko MonacoRonaldo Mchezaji Bora 2014 Ulaya.Ronaldo akibusu tuzo yake yake baada ya kuchaguliwa mchezaji boraRonaldo amewabwaga chini wachezaji wa Bayern Munich kipa Manuel Neuer na Arjen Robben

Mchezaji wa zaani wa  Real madrid captain Fernando Hierro akionesha karatasi ya kuonesha City Kundi E kundi ambalo linaonekana gumu.

Kipa wa Spain Iker Casillas alionesha Chelsea kwenye kundi G

Droo ya UEFA Champions League ni kama ifuatavyo:-
DROO YA MAKUNDI - UEFA CHAMPIONS
Kundi A: Atletico Madrid, Juventus, Olympiakos, Malmo
Kundi B: Real Madrid, Basel, Liverpool, Ludogorets Razgrad
Kundi C: Benfica, Zenit St Petersburg, Bayer Leverkusen, Monaco
Kundi D: Arsenal, Borussia Dortmund, Galatasaray, Anderlecht
Kundi E: Bayern Munich, Manchester City, CSKA Moscow, Roma
Kundi F: Barcelona, Paris St-Germain, Ajax, APOEL Nicosia
Kundi G: Chelsea, Schalke, Sporting Lisbon, Maribor
Kundi H: Porto, Shakhtar Donetsk, Athletic Bilbao, BATE Borisov


KEPTENI wa Manchester United Wayne Rooney ndie ameteuliwa Nahodha mpya wa England na Meneja wa Timu Roy Hodgson.
Rooney, mwenye Miaka 28, anachukua wadhifa huo kutoka kwa Steven Gerrard wa Liverpool ambae amestaafu kuichezea England mara baada ya Nchi hiyo kutolewa hatua ya Makundi ya Fainali za Kombe la Dunia Mwezi Juni huko Brazil.

Rooney ameichezea England mara 95 na kufunga Bao 40 na Mwezi uliopita aliteuliwa kuwa Nahodha wa Manchester United na Meneja Louis van Gaal.
Mechi za kwanza kwa Rooney kama Nahodha wa England hapo Septemba 3 wakati England itacheza Mechi ya Kirafiki na Norway Uwanjani Wembley na kisha Septemba 8 kusafiri kwenda kucheza na Uswisi katika Mechi yao ya kwanza ya EURO 2016.
Mara baada ya kuteuliwa Rooney, Meneja Roy Hodgson alitangaza Kikosi chake cha England chenye Wachezaji wapya Wanne.
Wapya hao nI beki wa Arsenal mwenye Miaka 19, Calum Chambers, Mchezaji wa Newcastle Jack Colback, Danny Rose wa Tottenham na Fabian Delph wa Aston Villa, wote wakiwa na Umri wa Miaka 24.

KIKOSI CHA ENGLAND:
Makipa:
Fraser Forster (Southampton), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City)
Mabeki: Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Calum Chambers (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Danny Rose (Tottenham Hotspur), John Stones (Everton)
Viungo: Jack Colback (Newcastle United), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal) Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), Jack Wilshere (Arsenal)
Mafowadi: Rickie Lambert (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United)


Emanuel Okwi wa Uganda ambaye msimu uliopita alikuwa anaichezea Yanga, akiwa na jezi namba 25 aliyokabidhiwa mara baada ya kusaini tena Simba baada ya kukachwa na Yanga katika usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayotarajia kuanza mwezi ujao.
Yametimia, hatimaye Emmanuel Okwi amerejea katika kikosi chake cha zamani cha Simba.
Okwi rasmi anasaini leo kujiunga na Simba baada ya kuelewana na uongozi wa klabu hiyo.
Mganda huyo amechukua uamuzi wa kusaini kuichezea Simba baada ya Yanga kumtema.

Thursday, August 28, 2014

Screen Shot 2014-08-28 at 8.27.35 AM 
Toka nimeanza kuandika na kufatilia habari sijawahi kusikia jeshi la nchi limechukua hatamu kuendesha mashindano ya urembo tena mashindano yanayokutanisha warembo kutoka sehemu mbalimbali za taifa ili kumtafuta mshindi.
Stori hii ya kipekee inatokea Uganda ambapo jeshi la nchi hiyo limeamua hivyo baada ya kuona ubabaishaji unaofanywa na Waandaaji wa Miss Uganda shindano ambalo halikufanyika kwa miaka kadhaa kutokana na ubabaishaji.
Ripota wa TZA Kampala Bill the African, ameripoti kwamba mmoja kati ya wenye vyeo vyao jeshini ambae pia ni mdogo wake Rais Museven amesema jeshi limeamua kuchukua usimamizi wa mashindano haya kwa madai kwamba ni njia ya kuwavutia vijana wapende kilimo kitakachotangazwa kupitia haya mashindano ikiwa tayari pia jeshi hilo limechukua Wizara ya kilimo kwa ajili ya kuiongoza.
Screen Shot 2014-08-28 at 8.11.06 AM 
Bill alipozunguka mtaani kuwauliza watu maoni yao imekua 30 kwa 70 yani kuna ambao wanaona hakuna shida Wagumu hawa kuongoza mashindano hayo lakini wengine wengi wanapinga wakisema Jeshi hili linajulikana kabisa huwa halicheki na mtu wala halina urafiki na Raia sasa ndio wataweza kuendesha mashindano ya Urembo? ni vitu viwili tofauti kabisa.


frank-lampard-volley
Siku kadhaa baada ya Frank Lampard kutangaza kustaafu soka la kimataifa – jana ilikuwa siku nyingine kwa wanasoka wawili wa kimataifa barani nao walitangaza uamuzi wa kuachana na soka la kimataifa.
140823111329_etoo512
Samuel Eto’o na Xabi Alonso kwa wakati tofauti jana walitumia mitandao ya kijamii kutangaza uamuzi wao wa kuachana na soka la kimataifa.
Alianza Xabi Alonso kupitia mtandao wa Twitter kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Spain.
Kiungo huyo wa Real Madrid ameshaitumikia Spain kwa muda wa miaka 11 na ameifungia nchi hiyo magoli 16 katika mechi 114.
Wakati huo huo mfungaji mabao mengi zaidi wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o ametangaza kustaafu soka la kimataifa.
Mshambuliaji huyo ambaye ameifungia Cameroon mabao 56 amejiunga na Everton ya Uingereza juzi .
Kufuatia kauli hiyo mshambuliaji huyo sasa hatakuwepo katika kipindi chote cha cha kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwezi Januari mwakani.


IMG_6809.JPG

Wiki kadhaa baada ya kuteuliwa kuwa nahodha mpya wa Manchester United, mshambuliaji Wayne Rooney leo amepata uongozi mpya kwenye medani za soka.
Rooney ameteuliwa na kocha Roy Hodgson amemteua mshambuliaji huyo kuwa nahodha mpya wa timu hiyo ya taifa.
Rooney mwenye miaka 28 amechukua mikoba iliyoachwa na kiungo wa Liverpool, Steven Gerrard aliyestaafu.
Rooney aliwahi kuvaa kitambaa cha unahodha akiiongoza England kwenye mechi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya San Marino, Oktoba 2012.

Staa huyo amewapiku wachezaji wenzake kipa Joe Hart na beki Gary Cahill ambao nao walikuwa wakitajwa kuchukua uongozi huo.


DSCN1093
  • Serengeti fiesta Moshi wapewa fursa ya kuonja radha
Mhehimiwa Temba ametangaza rasmi kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la “Wazee wa jiji” jumamosi hii. Serengeti fiesta Moshi wamepewa fursa ya kuonja radha ya wimbo huo siku ya Jumamosi katika uwanja Majengo Jijini humo.
Mheshimiwa Temba ambaye ni mzawa wa jiji hilo anatarajia kutumia fura ya Serengeti fiesta Moshi kuuzindua wimbo huo kwa mara ya kwanza.
“Ni matumaini yangu kuwa Wanamoshi wataniunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja wa Manjengo siku ya Jumamosi Agosti 30, kushuhudia shoo kali nitakayoifanya sanjari na nyota wengine wa muziki watakaotumbuiza katika tamasha hilo.
Baadhi ya wasanii watakaowasha moto katika jukwaa la Serengeti fiesta Moshi ni pamoja na Ali kiba, Ney waMitego, Dully Sykes, Jambo Squad, Stamina, Maua, Recho, Shaa and Mapacha, Chege na Temba na wengine wengi.
Chege ameishukuru kampuni ya Serebgeti kupitia kinyaji chake mashuhuri, Serengeti Premium Lager, kwa kutoa fursa kwa wasanii kukutana na mashabiki zao na kuwapa burudani. “Burudani la Serengeti fiesta ni moja ya mifano dhahiri inayoonyesha jinsi Watanzania tunavyopendana bila kujali utofauti wa makabila yetu na dini zetu.”
Temba ameyashauri makampuni mengine yanayopatikana ukanda wa Afrika Mashariki na kati kuiga mfano wa Serengeti Fiesta ili kudumisha udugu na ujamaa katika nchi wanazofanya kazi.
Pia ameishauri kampuni ya Serengeti fiesta kuangalia uwezekano wa kulisambaza burudani hili katika nchi nyingine Africa…ikianzia na Afrika ya Mashariki.
“Burudani inanguvu ya kipekee sana katika maisha ya manadamu. Kwa kuisambaza Serengeti fiesta katika nchi nyingine Afrika mashariki kutaifanya jumuia hii kuungana zaidi na kuwa kitu kimoja,” alisema Temba.
Baada ya Mohi, Burudani la Serengeti fiesta litaelekea mikoa mingine kama Musoma, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma, Moshi, Arusha, Mtwara na baadae jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi alipowasili eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi baada ya kuwasili eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi baada ya kuwasili eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Wengine ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe Issa Ntambuka.
Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi akisalimiana na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospeter Muhongo eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Wasanii wa ngoma ya utamaduni kutoka Burundi wakiburudisha kwenye sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi akisalimiana na baadhi ya Watanzania walikuwepo eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipokea nyimbo za Taifa za nchi zao eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Sehemu ya umati wa wananchi wa Tanzania na Burundi kwenye sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa Tanzania na Burundi katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu pamoja na Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Naibu Katibu Mkuu Wizara Uchukuzi Dkt Charles Tizeba eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika picha ya kumbukumbu na wataalamu wa Tanzania na Burundi eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakitembelea eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipata maelezo na kuangalia vifaa vya upimaji eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizindua kwa pamoja eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipongezana kwa furaha katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakichanganjya udongo na kujenga kwa pamoja alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi na wananchi wa nchi zao wakisimama wakati nyimbo za Taifa za Burundi na Tanzania zikipigwa katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakijipatia chakula cha mchana katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiagana katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa


Ethiopia na Kenya zimetangaza niya ya kutaka kuwa wenyeji wa kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka wa 2017 baada ya Libya kujiondoa.

Libya ilitangaza kauli hiyo baada ya mapigano kuchacha baina ya makundi mawili hasimu yaliyowanyima waandalizi fursa ya kujenga viwanja vipya vya mashindano hayo.

Ethiopia, ambayo imewahi kuwa mwenyeji wa mashindano hayo katika miaka ya 1962, 1968 na 1976, imesema kuwa itawasilisha rasmi ombi lake mara moja

Rasi wa Shirikisho la soka la Ethiopia Junedin Basha ameiambia BBCMichezo kuwa tayari taifa hilo linaviwanja viwili vyenye hadhi ya kimataifa (Addis Ababa na Bahir Dar), na hivyo hoja kuu itakuwa kukamilisha viwanja viwili vipya ambavyo tayari vinaendelea kujengwa.

"Serikali inaari ya kuyaleta mashindano hayo hapa Ethiopia ."alisema

Kenya kwa upande wake imetangaza niya ya kuandaa mashindano hayo kwa pamoja na Tanzania Uganda au Rwanda.

Shirikisho la soka barani Afrika limetangaza tarehe 30 Septemba kuwa siku ya mwisho ya mataifa kuwasilisha maombi yao.

Tangazo rasmi ya nani atakayeandaa mashindano hayo itakuwa mwakani

waliotembelea blog