Thursday, August 28, 2014


Ethiopia na Kenya zimetangaza niya ya kutaka kuwa wenyeji wa kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka wa 2017 baada ya Libya kujiondoa.

Libya ilitangaza kauli hiyo baada ya mapigano kuchacha baina ya makundi mawili hasimu yaliyowanyima waandalizi fursa ya kujenga viwanja vipya vya mashindano hayo.

Ethiopia, ambayo imewahi kuwa mwenyeji wa mashindano hayo katika miaka ya 1962, 1968 na 1976, imesema kuwa itawasilisha rasmi ombi lake mara moja

Rasi wa Shirikisho la soka la Ethiopia Junedin Basha ameiambia BBCMichezo kuwa tayari taifa hilo linaviwanja viwili vyenye hadhi ya kimataifa (Addis Ababa na Bahir Dar), na hivyo hoja kuu itakuwa kukamilisha viwanja viwili vipya ambavyo tayari vinaendelea kujengwa.

"Serikali inaari ya kuyaleta mashindano hayo hapa Ethiopia ."alisema

Kenya kwa upande wake imetangaza niya ya kuandaa mashindano hayo kwa pamoja na Tanzania Uganda au Rwanda.

Shirikisho la soka barani Afrika limetangaza tarehe 30 Septemba kuwa siku ya mwisho ya mataifa kuwasilisha maombi yao.

Tangazo rasmi ya nani atakayeandaa mashindano hayo itakuwa mwakani

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog