Thursday, August 28, 2014



frank-lampard-volley
Siku kadhaa baada ya Frank Lampard kutangaza kustaafu soka la kimataifa – jana ilikuwa siku nyingine kwa wanasoka wawili wa kimataifa barani nao walitangaza uamuzi wa kuachana na soka la kimataifa.
140823111329_etoo512
Samuel Eto’o na Xabi Alonso kwa wakati tofauti jana walitumia mitandao ya kijamii kutangaza uamuzi wao wa kuachana na soka la kimataifa.
Alianza Xabi Alonso kupitia mtandao wa Twitter kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Spain.
Kiungo huyo wa Real Madrid ameshaitumikia Spain kwa muda wa miaka 11 na ameifungia nchi hiyo magoli 16 katika mechi 114.
Wakati huo huo mfungaji mabao mengi zaidi wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o ametangaza kustaafu soka la kimataifa.
Mshambuliaji huyo ambaye ameifungia Cameroon mabao 56 amejiunga na Everton ya Uingereza juzi .
Kufuatia kauli hiyo mshambuliaji huyo sasa hatakuwepo katika kipindi chote cha cha kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwezi Januari mwakani.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog