- Serengeti fiesta Moshi wapewa fursa ya kuonja radha
Mhehimiwa Temba ametangaza rasmi kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la “Wazee
wa jiji” jumamosi hii. Serengeti fiesta Moshi wamepewa fursa ya kuonja
radha ya wimbo huo siku ya Jumamosi katika uwanja Majengo Jijini humo.
Mheshimiwa Temba ambaye ni mzawa wa jiji
hilo anatarajia kutumia fura ya Serengeti fiesta Moshi kuuzindua wimbo
huo kwa mara ya kwanza.
“Ni matumaini yangu kuwa Wanamoshi
wataniunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja wa Manjengo
siku ya Jumamosi Agosti 30, kushuhudia shoo kali nitakayoifanya sanjari
na nyota wengine wa muziki watakaotumbuiza katika tamasha hilo.
Baadhi ya wasanii watakaowasha moto
katika jukwaa la Serengeti fiesta Moshi ni pamoja na Ali kiba, Ney
waMitego, Dully Sykes, Jambo Squad, Stamina, Maua, Recho, Shaa and
Mapacha, Chege na Temba na wengine wengi.
Chege ameishukuru kampuni ya Serebgeti
kupitia kinyaji chake mashuhuri, Serengeti Premium Lager, kwa kutoa
fursa kwa wasanii kukutana na mashabiki zao na kuwapa burudani.
“Burudani la Serengeti fiesta ni moja ya mifano dhahiri inayoonyesha
jinsi Watanzania tunavyopendana bila kujali utofauti wa makabila yetu na
dini zetu.”
Temba ameyashauri makampuni mengine
yanayopatikana ukanda wa Afrika Mashariki na kati kuiga mfano wa
Serengeti Fiesta ili kudumisha udugu na ujamaa katika nchi wanazofanya
kazi.
Pia ameishauri kampuni ya Serengeti
fiesta kuangalia uwezekano wa kulisambaza burudani hili katika nchi
nyingine Africa…ikianzia na Afrika ya Mashariki.
“Burudani inanguvu ya kipekee sana katika
maisha ya manadamu. Kwa kuisambaza Serengeti fiesta katika nchi
nyingine Afrika mashariki kutaifanya jumuia hii kuungana zaidi na kuwa
kitu kimoja,” alisema Temba.
Baada ya Mohi, Burudani la Serengeti
fiesta litaelekea mikoa mingine kama Musoma, Shinyanga, Kigoma, Tabora,
Singida, Dodoma, Moshi, Arusha, Mtwara na baadae jijini Dar es salaam.
0 maoni:
Post a Comment