Toka
nimeanza kuandika na kufatilia habari sijawahi kusikia jeshi la nchi
limechukua hatamu kuendesha mashindano ya urembo tena mashindano
yanayokutanisha warembo kutoka sehemu mbalimbali za taifa ili kumtafuta
mshindi.
Stori
hii ya kipekee inatokea Uganda ambapo jeshi la nchi hiyo limeamua hivyo
baada ya kuona ubabaishaji unaofanywa na Waandaaji wa Miss Uganda
shindano ambalo halikufanyika kwa miaka kadhaa kutokana na ubabaishaji.
Ripota wa TZA Kampala
Bill the African, ameripoti kwamba mmoja kati ya wenye vyeo vyao
jeshini ambae pia ni mdogo wake Rais Museven amesema jeshi limeamua
kuchukua usimamizi wa mashindano haya kwa madai kwamba ni njia ya
kuwavutia vijana wapende kilimo kitakachotangazwa kupitia haya
mashindano ikiwa tayari pia jeshi hilo limechukua Wizara ya kilimo kwa
ajili ya kuiongoza.
Bill
alipozunguka mtaani kuwauliza watu maoni yao imekua 30 kwa 70 yani kuna
ambao wanaona hakuna shida Wagumu hawa kuongoza mashindano hayo lakini
wengine wengi wanapinga wakisema Jeshi hili linajulikana kabisa huwa
halicheki na mtu wala halina urafiki na Raia sasa ndio wataweza
kuendesha mashindano ya Urembo? ni vitu viwili tofauti kabisa.
0 maoni:
Post a Comment