Tuesday, October 27, 2015


Ligi Kuu soka Tanzania bara inaendelea tena kwa michezo kadhaa kupigwa siku ya Jumatano ya October 28 na Alhamisi ya October 29. Ligi hiyo inaendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali ambapo uwanja wa Taifa Dar Es Salaam utapigwa mchezo ambao unatajwa kuwa na presha kwa kocha wa Simba Dylan Kerr ambaye kuna tetesi kuwa uongozi wa Simba umempa mechi mbili afanye vizuri ili kunusuru kibarua chake.

Hii ni ratiba ya mechi za October 28 na 29.


Ratiba za mechi za Ligi Kuu Tanzania bara October 28 na 29
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara October 27


Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon Rigobert Song ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Chad.
Song, mwenye umri wa miaka 39, aliteuliwa Jumatatu kumrithi Mfaransa Emmanuel Tregoat, ambaye mkataba wake ulimalizika Septemba 30.
"Haitakuwa rahisi kufuzu kwa Kombe la Taifa Bingwa Afrika 2017 lakini tuko tayari kujikaza kisabuni,” difenda huyo wa zamani wa Liverpool na West Ham amesema.
Kibarua cha kwanza kwa Song kitakuwa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Misri Novemba.
Les Sao watakuwa wenyeji wa Misri kwenye mechi ya kwanza mjini N'Djamena tarehe 14 mwezi huu. Kutakuwa na mechi ya marudiano baadaye Misri.
Tregoat alifahamishwa mapema Septemba, baada ya kuchapwa 5-1 na Misri kwamba mkataba wake hautaongezwa.
Modou Kouta alifanywa kocha wa muda kandaa timu hiyo kwa mechi ya kufuzu kwa CHAN dhidi ya Gabon, ambayo walishindwa 2-1 kwa jumla.
Chad sasa wameweka matumaini yao kwenye Song, licha yake kukosa uzoefu katika ukufunzi.
Wakati wa uchezaji wake, Song alichezea Indomitable Lions mechi zaidi ya 100, na aliibuka Mwafrika wa kwanza kucheza katika fainali nne za Kombe la Dunia.


Mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney ameruhusiwa kufanyiwa Mechi ya Kumuenzi na mapato yote ya Mechi hiyo kwenda kwenye Mifuko ya Hisani.
Mechi hii imepitishwa baada ya Mashabiki kuiomba Klabu kutambua mchango mkubwa uliotukuka wa Rooney kwa Klabu hiyo.
Sasa Mechi hii itachezwa Old Trafford hao Agosti 3, 2016 dhidi ya Wapinzani ambao watapangwa baadae.
Akiongelea uamuzi huu, Rooney alisema: “Usiku wa Mechi utakuwa spesho kwangu na Familia yangu na nategemea tunaweza pia tukaleta kitu kimoja au viwili vya kushtukiza!”
Nae Mtendaji Mkuu wa Man United, Ed Woodward amesema: "Kuanzia Mechi yake ya kwanza aliyopiga Hetitriki hadi sasa ana Goli 236, Wayne amekuwa ndio Mtu mkuu
Katika kipindi cha mafanikio makuu ya Klabu!”
Habari hizi zimekuja wakati Oktoba 24 Rooney alitimiza Umri wa Miaka 30 na katika kipindi ambacho ananyooshewa kidole kuhusu uchezaji wake akiwa amefunga Bao 2 tu za Ligi katika Mechi 9 Msimu huu.


Timu ya Taifa Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi Novemba 7, 2015 jijini Dar es salaam.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehmu ya kujipima kwa Twiga Stars inayonolewa na kocha Rogasian Kaijage, ambayo ilishiriki Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) mwezi Agosti – Septemba nchini Congo – Brazzavile.
Awali Twiga Stars ilikua icheze mchezo huo nchini Malawi Oktoba 24, kabla ya chama cha soka nchini humo (FAM) kuahirisha mchezo huo, na sasa mchezo huo utacheza nchini Tanzania Novemba 07, 2015.

Muigizaji Kingwendu ni miongoni mwa mastaa ambao wamechukua headline za kugombea Ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kama Afande Sele, Professor Jay, Muigizaji Frank na wengineo.
Stori iliyonifikia ni kwamba muigizaji huyo hakufanikiwa kupata Ubunge kupitia tiketi ya CUF katika  jimbo la Kisarawe mkoa wa Pwani.
Akiongea na ripota wa millardayo.com alisema…’Matokeo ya mwanzo yalikuwa yanaonesha kwamba mimi naongoza, lakini mwishoni katika hesabu ikaonekana amenishinda‘- KINGWENDU
‘Matokeo yanaonesha Suleimani Jako wa CCM ameshinda, nimejaribu na nimethubutu kwa mara ya kwanza..! najua nimekosea wapi na ntajipanga upya na ntaenda kusomea siasa zaidi’– KINGWENDU
‘Hakuna mtu aliyenishawishi kugombea ubunge, bali ni mimi mwenyewe niliamua baada ya kuona pia baadhi ya wasanii wenzangu wanagombania‘-KINGWENDU

waliotembelea blog