Sunday, February 2, 2014



Meneja wa Manchester United David Moyes anahisi kuwa klabu yake isingekosa bahati hivyo kiasi cha kupata kichapo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya Stoke City.
Ni mechi yao ya nane kushindwa katika ligi kuu msimu huu.
Charlie Adam aliwawezesha wenyeji kupata ushindi kwa bao la kwanza na kisha kuingiza bao la pili baada ya Robin van Persie kupatia Man U bao la kufutia machozi.
"sijui tufanyeje tuweze kushinda,'' alisema Moyes baada ya mechi. Nadhani tu hatuna bahati hata kidogo.''
Tulicheza vyema, lakini kwa bao la kwanza la wenyeji lilitokana na Man U la pili pili lilikuwa la kubahatisha,'' aliongeza Moyes.
Mchezaji aliyesajiliwa hivi karibuni, Juan Mata, Van Persie na Rooney wote walicheza katika kikosi cha kwanza kilichoshambulia sana Stoke.
Van Persie alisaidia Man U kwa bao lake na kwa mchezo mzuri ingawa walishindwa tu kuingiza mabao.
Licha ya shinikizo kutoka kwa Man U, bahati haikuwa yao.
"tulikuwa na nafasi nzuri za kuingiza mabao lakini haikuwezekana,'' alisema Moyes
"ndio, Wayne alikaribia kuingiza bao , ingawa ilikuwa vigumu kwa mabao.Tungestahili kupata mabao kutokana na wachezaji walivyocheza, yaani tujilaumu sisi wenyewe tu,'' aliongeza Moyes.
United wangali katika nafasi ya saba kwenye jedwali la pointi, wakiwa nyuma kwa pointi kumi na tatu dhidi ya Man City wanaoongoza jedwali hilo ambao watacheza na Chelsea Jumatatu.
Pia wako nyuma ya Liverpool ambao ni wa nne kwa alama sita .



Libya mabingwa wa CHAN 2014
Libya imepata ushindi wake wa kwanza wa kombe la taifa bingwa Afrika kwa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Ghana mjini Cape Town Afrika Kusini.
Mechi ya fainali kati ya nchi hizo mbili ilikamilika kwa sare tasa kabla ya Joshua Tijani wa Ghana kukosa bao la penalti na kuipa Libya ushindi wake.
Abdul Mohamed wa Ghana alikuwa na fursa nzuri zaidi kuipa timu yake ushindi katika dakika za ziada za mechi hiyo baada ya dakika 90.
Walinda lango wa timu zote mbili waliokoa mabao mawili kila mmoja kabla ya Tijani kukosa bao lake.
Mechi sita katika kipindi cha siku 20 ikiwemo dakika za ziada kwa kila mechi ya nusu fainali iliyochezwa Jumatano, iliwachokesha wachezaji hao kwani walishindwa kabisa kuiongiza mabao wakati wa mechi kiasi cha kuenda penalti.
Timu zote mbili zilikuwa na nafasi nzuri kupata ushindi katika kipindi cha pili cha mchezo huo ingawa hakuna aliyefanikiwa.
Ikizingatiwa historia ya michuano kati ya nchi hizo mbili, kipindi cha ziada hakikuwa,jambo la ajabu.
Mechi zao mbili walizocheza mwaka huu na katika michuano ya mwaka 2009 iliisha kwa sare ya bao moja. Ghana ilishinda michuano ya mwaka 1982 baada ya timu kwenda sare ya bao moja hadi dakika ya tisini.
Nigeria iliicharaza Zimbabwe 1-0 kuchukua nafasi ya tatu

waliotembelea blog