Wednesday, March 11, 2015


eto 
Ishu ya ubaguzi wa rangi kwa nchi za wenzetu bado imeendelea kuonekana kuchukua nafasi, hata katika soka matukio ya ubaguzi kwa baadhi ya wanasoka ambao ni weusi imeendelea kuchukua headlines.
Tukio la hivi karibuni la mashabiki wa Chelsea lilionyesha dhahiri kwamba bado hawana mapenzi na watu wa rangi nyeusi baada ya kumzuia shabiki mwenzao asipande ndani ya treni kutokana na kuwa mweusi.
etoo 
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Etoo ameweza kutunukiwa tuzo ya kupambana na ubaguzi wa rangi juzi jumatatu na Shirika lisilo la kiserikali la usuluhishi linalojulikana kama The European Council on Tolerance and Reconciliation (ECTR).
Mchezaji huyo raia wa Cameroon amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kupambana na mambo yanayohusu ubaguzi kwa kipindi chote ambacho amekuwa akicheza katika klabu mbalimbali za soka na hivi karibuni alilaani kitendo cha mashabiki wa chelsea kumbagua shabiki mwenzao kutokana na kuwa ni mtu mweusi wakati wakitoka uwanjani.
raci 
Etoo ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Sampdoria alipewa tuzo hiyo ya heshima na Shirika lisilo la kiserikali la The European Council on Tolerance and Reconciliation (ECT

Watu zaidi ya 30 wanasadikiwa kupoteza na maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya sana katika ajali mbaya iliyotokea mapema leo asubuhi,maeneo ya Changarawe,Mafinga Mkoani Iringa,iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea baada ya Lori hilo la Mizigo lililokuwa likitokea Jijini Dar kuelekea Mbeya kuligonga na kuliangukia basi hilo wakati lililokuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara wakati wakiwa kwenye mwendo walipokuwa wakipishana. 

Hali ya Uokoaji wa maiti na majeruhi walionasa kwenye ajali hiyo bado ni tete na hasa kutokana na ukosefu wa Gesi ya kukata basi hilo kukosekana eneo lote la Mafinga,Juhudi zinafanyika ili kuweza kuokoa majeruhi pamoja na maiti.

Tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hili ambalo ni la kusikitisha sana na ni msiba mkubwa kwa taifa,na tutaendelea kujuzana kupitia hapa hapa.

Mungu azipokee na kuzilaza mahala pema peponi roho za marehemu wote katika ajali hii na awajaalie kupona kwa haraka majeruhi wote.



samahani kwa picha



LEO JUMATANO Usiku Uwanjani Stamford Bridge Jijini London, Chelsea watakuwa Wenyeji wa Paris St Germain katika Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONS LIGI.
Kwenye Mechi ya kwanza huko Parc des Princes Jijini Paris Nchini France hapo Februari 17, Branislav Ivanovic aliifungia Chelsea Bao muhimu la Ugenini walipotoka Sare 1-1 na PSG.

Msimu uliopita, Chelsea iliitoa PSG kwenye Robo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI kwa faida ya Bao la Ugenini baada ya kupigwa 3-1 huko Parc des Princes katika Mechi ya Kwanza na kushinda 2-0 Uwanjani Stamford Bridge huku Bao lao la pili likipachikwa mwishoni na Demba Ba katika Dakika ya 87.
Eden Hazard 
Wakati Chelsea inatarajia kumrudisha Kikosini Kiungo wao Nemanja Matic ambae hajacheza tangu atumikie Kifungo cha Mechi mbli alichopewa baada ya kufungiwa kutokana na Rafu mbaya kwenye Mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Burnley Mwezi uliopita, David Luiz wa PSG anatarajiwa kurudi kwa mara ya kwanza Stamford Bridge tangu aihame Chelsea mwanzoni mwa Msimu.
David Luiz, Mchezaji wa Kimataifa wa Brazil, alipozongwa na Wanahabari kuelezea kuhusu Meneja wake wa zamani hasa kuhusu Lebo ya Meneja huyo wa Chelsea Jose Mourinho kupachikwa ni ‘Mtu Spesho’ alijibu: “Ni spesho kwenu si kwangu!”



 MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI

Mratibu wa KIBIKI CUP Haruna Saleh akiwa na mdau wa soka FRANK KIBIKI na wanahabari
 
NA MWANDISHI WETU, IRINGA
LIGI inayoshirikisha  watoto walio chini ya umri wa miaka 16, inaloitwa  Iringa Kibiki Childrens Cup 2015 yenye lengo la kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino) inatarajia kuanza kutimua vumbi jumamosi ikishirikisha timu nane za manispaa ya Iringa.
Mratibu wa ligi hiyo, Haruna Salehe alisema lengo la mpira huo ni kukuza vipaji vya watoto na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili na mauaji yanayofanywa kwa walemavu wa ngozi nchini.
Alisema ligi hiyo iliyobuniwa na kuendeshwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru, inatarajia kushirikisha timu nane za watoto katika manispaa ya Iringa.
“Lengo kubwa ni kukuza vipaji na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wenzetu walemavu wa ngozi ambao wamekuwa wakiuawa kila siku bila huruma jambo ambalo, hatutaki liendelee kwenye jamii yetu,”alisema.Alisema michuano hiyo itakuwa ikifanyika katika uwanja wa mwembetogwa ambao ni wa wazi ili watu wengi wapate nafasi ya kushiriki.
Kwa upande wake, mdau wa soka na mwanahabari wa gazeti hilo, Frank Kibiki alisema ameamua kubuni ligi hoyo ili kupanda mbegu ya kupenda michezo na kutambua vipaji vya soka tangu utotoni, ili iwe rahisi kuwapata wachezaji bora siku zijzo.
“Mpira ni ajira na huu hauna dini, kabira wala rangi, watu wote hata watoto wanaweza kushiriki kwenye mpira hivyo tumebuni jambo hili ili kuendelea kukuza vipaji huku tukibeba ujumbe wa kupinga ukatili kwa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi,”alisema.
Kibiki ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa soka kushiriki kwenye michuano hiyo ili kusaidia kuibua vipaji na kulifanya soka la Iringa kuwa endelevu.
Alisema tayari shirikisho la Soka, manispaa ya Iringa wametoa Baraka za kuanza kwa ligi hilo, ambalo watoto wameshaewa mafunzo ya kuwa waamuzi na washika vibendera hiyo wao wenyewe watajiongoza.
Kwa upande wao wadau wa soka, manispaa yaa Iringa waliitaka serika kutambua mchango na kuwekeza kwenye soka ili kusaidia kupandisha timu zilizopo na kuendelea kuibu vipaji ikiwemo michuano ya watoto.

waliotembelea blog