MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI
Mratibu wa KIBIKI CUP Haruna Saleh akiwa na mdau wa soka FRANK KIBIKI na wanahabari
Mratibu wa KIBIKI CUP Haruna Saleh akiwa na mdau wa soka FRANK KIBIKI na wanahabari
NA
MWANDISHI WETU, IRINGA
LIGI
inayoshirikisha watoto walio chini ya
umri wa miaka 16, inaloitwa Iringa
Kibiki Childrens Cup 2015 yenye lengo la kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino)
inatarajia kuanza kutimua vumbi jumamosi ikishirikisha timu nane za manispaa ya
Iringa.
Mratibu
wa ligi hiyo, Haruna Salehe alisema lengo la mpira huo ni kukuza vipaji vya
watoto na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili na mauaji yanayofanywa kwa walemavu
wa ngozi nchini.
Alisema
ligi hiyo iliyobuniwa na kuendeshwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru,
inatarajia kushirikisha timu nane za watoto katika manispaa ya Iringa.
“Lengo
kubwa ni kukuza vipaji na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia hasa
kwa wenzetu walemavu wa ngozi ambao wamekuwa wakiuawa kila siku bila huruma
jambo ambalo, hatutaki liendelee kwenye jamii yetu,”alisema.Alisema
michuano hiyo itakuwa ikifanyika katika uwanja wa mwembetogwa ambao ni wa wazi
ili watu wengi wapate nafasi ya kushiriki.
Kwa
upande wake, mdau wa soka na mwanahabari wa gazeti hilo, Frank Kibiki alisema ameamua kubuni
ligi hoyo ili kupanda mbegu ya kupenda michezo na kutambua vipaji vya soka
tangu utotoni, ili iwe rahisi kuwapata wachezaji bora siku zijzo.
“Mpira
ni ajira na huu hauna dini, kabira wala rangi, watu wote hata watoto wanaweza
kushiriki kwenye mpira hivyo tumebuni jambo hili ili kuendelea kukuza vipaji
huku tukibeba ujumbe wa kupinga ukatili kwa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi,”alisema.
Kibiki
ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa soka kushiriki kwenye michuano hiyo ili
kusaidia kuibua vipaji na kulifanya soka la Iringa kuwa endelevu.
Alisema
tayari shirikisho la Soka, manispaa ya Iringa wametoa Baraka za kuanza kwa ligi
hilo, ambalo
watoto wameshaewa mafunzo ya kuwa waamuzi na washika vibendera hiyo wao wenyewe
watajiongoza.
Kwa
upande wao wadau wa soka, manispaa yaa Iringa waliitaka serika kutambua mchango
na kuwekeza kwenye soka ili kusaidia kupandisha timu zilizopo na kuendelea
kuibu vipaji ikiwemo michuano ya watoto.
0 maoni:
Post a Comment