Wednesday, April 22, 2015


Sina mbavu mieee nipisheeee!!! Chicharito baada ya kuizima Atletico Madrid usiku huu!Chicharito akishangilia bao lake la pekee baada ya kuifungia na kuipa Ushindi Real usiku huu dhidi ya Atletico Madria kwenye marudiano ya Klabu Bingwa Ulaya. Bao hilo limewapeleka Real Madrid Nusu Fainali ya 31 na Droo ya Nusu Fainali itachezeshwa Ijumaa ya wiki hii.Javier Hernández aliwafungia bao Real Madrid dakika za majeruhi na kufanya 1-0 dhidi ya Atletico Madrid, Ni Baada ya kupewa pasi ndani ya boksi na Staa wa Real Cristiano Ronaldo na kufunga bao hilo la Ushindi. Real wamesonga hatua ya Nusu faonali kwa Ushindi wa bao la Chicharito. Mtanange huu pia Atletico Madrid walimaliza pungufu wachezaji 10 Uwanjani baada ya mwenzao Arda Turan kuoneshwa kadi njano ya pili na kuoneshwa kadi Nyekundu kwa kumchrzea rafu mbaya mchezaji wa Real Madrid Sergio Ramos.Cristiano Ronaldo akiendesha..mpira wakati wa kipindi cha kwanza
Chicharito hoi! akishangaa kuona mpaka kipindi cha kwanza kinakatika bado 0-0, Ngoma ngumu!Ronaldo akiachia shutiRonaldo tena..Arda Turan akioneshwa kadi ya njanoSergio Ramos kwenye patashika mpira wa kichwa!Arda Turan akimwangaisha Fabio wa RealRonaldo akijishika kichwa katika kipindi cha kwanzaSergio Ramos chini akijiuguza katika kipindi cha kwanza.Kikosi cha Real Madrid kilichoanza dhidi ya Atletico MadridKikosi cha Atletico MadridDiego Semeone na Carlo Ancelotti wakisaliniana kabla ya kipute kuanza BernabeuMashabiki wa Real madrid wakiwapungia Mastaa waoVIKOSI:
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Ramos, Coentrao, Pepe, Kroos, Isco, Rodriguez, Ronaldo, Hernandez.
Akiba: Navas, Arbeloa, Khedira, Lucas Silva, Illarmendi, Jese.
Atletico Madrid: Oblak, Juanfran, Miranda, Godin, Jesus Gamez, Tiago, Koke, Saul, Arda, Griezmann, Mandzukic.
Akiba: Moya, Siqueira, Gimenez, Raul Garcia, Gabi, Jimenez, Torres.
Refa: Felix Brych
Robo Fainali-Mechi za Marudiano
Mechi zote mbili kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku

Jumatano Aprili 22
Real Madrid vs Atletico Madrid [Santiago Bernabeu, Madrid, Spain] [0-0]
AS Monaco vs Juventus [Stade Louis II, Monaco, France] [0-1]

Wachezaji wa Atletico Madrid Joao Miranda, Antoine Griezmann na Mario Mandzukic wakipasha kwenye Uwanja wa Bernabeu usiku huu, Tayari kwa marudiano ya Robo Fainal, Mshindi kwenda Nusu Fainali

Wakwanza kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga akiwa ameshilia bango linaloonyesha huduma mpya ya Airtel Wi-Fi intaneti maalum kwa wanavyuo iliyozinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza Mwanza katika chuo cha St Augustine (SAUT) pamoja nae anaefuata ni raisi wa serikali ya wanafunzi Sogone Wambura, Mshauri wa wanafunzi chuoni hapo bw,Liberates Ndegeulaya na Afisa masoko wa Airtel Mwanza Bw, Emanuel Raphael
Afisa masoko wa Airtel bw, Prospa Mwanda akitoa maelekezo ya jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi inavyofanyaka kazi kwa kasi kwa Raisi wa wanafunzi chuo kikuu cha SAUT mwanza Bw, Sogone Wambura (wakwanza kulia) na Makamu wa Raisi wa chuo hicho Bi, Pearl Mecar (kati) mara baada ya Airtel kuzindua huduma hiyo chuoni hapo jana.
Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akionyesha kwa wanafunzi wa SAUT Mwanza (hawapo pichani) muonekano wa vocha za huduma mpya ya Airtel Wi-Fi intaneti iliyozinduliwa chuoni hapo jana maalumu kwaajili ya kuwapa wanafunzi intaneti nafuu na yenye kasi zaidi.


Dakika 90 zilimalizika kwa 0-0, Juventus wakasonga mbele hatua ya Nusu Fainali baada ya Ushndi wao wa kwanza wa bao 1-0 kuwabeba mpaka leo.Mchezo umemalizika dakika 90 bila kufungana na kuumaliza kwa sare ya nguvu sawa ya 0-0, Ushindi wa Kwanza wa Juventus wa bao 1-0 dhidi ya As Monaco ndio umekuwa nguzo kwao Juve baada ya leo kwenye marudiano kutoshana nguvu.
VIKOSI:
Monaco:
Subasic, Fabinho, Raggi, Abdennour, Kurzawa, Joao Moutinho, Toulalan, Kondogbia, Bernardo Silva, Martial, Carrasco.
Akiba: Stekelenburg, Dirar, Berbatov, Matheus Carvalho, Wallace Santos, Germain, Echiejile.
Juventus: Buffon, Lichtsteiner, Barzagli, Bonucci, Chiellini, Evra, Marchisio, Pirlo, Vidal, Tevez, Morata.
Akiba: Storari, Ogbonna, Llorente, Padoin, Sturaro, Matri, Pereyra.
Refa:
William Collum
Robo Fainali-Mechi za Marudiano
Mechi zote mbili kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku

Jumatano Aprili 22
Real Madrid vs Atletico Madrid [Santiago Bernabeu, Madrid, Spain] [0-0]
AS Monaco vs Juventus [Stade Louis II, Monaco, France] [0-1]


www.bukobasports.com
Robin van Persie Jana alicheza Mechi yake ya kwanza tangu apone Enka yake wakati Kikosi cha Vijana wa chini ya Miaka 21 wa Manchester United walipotoka Sare 1-1 na wenzao wa Leicester City katika Mechi ya Ligi ya Vijana ambayo Man United ndio Vinara.
Jumamosi Van Persie alikuwa Benchi wakati Man United inacheza huko Stamford Bridge Mechi ya Ligi Kuu England na kufungwa 1-0 na Chelsea lakini Jana alicheza Dakika 62.
Lakini kwenye Mechi na Leicester, Adnan Januzaj, Miaka 20, na Rafael da Silva, Miaka 24, waliumia na kutolewa.
Januzaj alitoka Dakika ya 54 baada kupata tatizo la Musuli na Rafael kubadilishwa mwishoni mw Kipindi cha Kwanza baada kuumia mbavu.

Habari nyingine njema kwa Man United ni kumaliza Kifungo cha Mechi 6 kwa Sentahafu Jony Evans ambae Jana alicheza Dakika zote 90.
Evans alifungiwa pamoja na Straika wa Newcastle Papiss Cisse baada ya kutemeana mate wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England Mwezi uliopita.
Van Persie, mwenye Miaka 31, ndie aliemtengenezea Sean Goss kuisawazishia Man United katika Dakika ya 32 baada ya Harry Panayiotou kuipa Leicester Bao katika Dakika ya 18.

Van Persie na Evans sasa watajumuika na Majeruhi waliopona, Daley Blind na Marcos Rojo, kurudi Kikosini kuikabili Everton Wikiendi hii huko Goodison Park kwenye Mechi ya Ligi Kuu England lakini hadi sasa hamna uhakika kama Michael Carrick atakuwa fiti kwa Mechi hiyo.

Kutoka kushoto ni Juma Herman(meneja wa Green Palm Hotel, Issaya Mwakilasa aka Wakuvwanga, Jhikolabwino Manyika, Kelvina John, Mwenyekiti Masoud Kipanya na Tonny Alphonce(Mtangazaji Metro fm 99.4

Siku ya Ijumaa ya tarehe 17/04/2015 ujumbe wa Imetosha Foundation ukiongozwa na Mwenyekiti Masoud Kipanya ulifanya mahojiano katika kituo cha redio cha Metro Fm 99.4 kwenye kipindi cha Pambazuko la Metro fm 99.4 ikiwa ni katika mfululizo wa kujitambulisha kanda ya ziwa kwa taasisi hiyo inayopinga mauaji kwa watu wenye ualbino kwa njia ya elimu. 

Msanii wa vichekesho (comedian) Wakuvwanga ambaye ni mjumbe wa taasisi hiyo alitoa kali alipoulizwa angependekeza adhabu gani kwa watakaopatikana na hatia ya kuua watu wenye ualbino? akajibu "Kwa kuwa hawa si watu bali ni wanyama kutokana na vitendo vyao viovu basi napendekeza serikali iwapeleke Mikumi national park iwafungie ndani ya senyenge ili watalii wawe wanaenda kuwaona kama wanavyoenda kuwaona Simba na wanyama wengine! Kipindi hicho maridhawa kiliendeshwa na watangazaji Tonny Alphonce na Katumba Madua
Mtangazaji wa kipindi cha Pambazuko la Metro Fm, Tonny Alphonce akimuuliza swali Masoud Kipanya.
Masoud Kipanya akijibu swali toka kwa mtangazaji wa Metro Fm 99.4zaji Tonny Alphonce.
Tonny akimpiga swali Wakuvwanga, anayesikiliza kwa umakini wa hali ya juu, soma uone jibu lake!
Kutoka kushoto ni Katumba Madua, Wakuvwanga na  msanii wa muziki wa Reggae Jhikoman

Moja ya studio za Metro Fm 99.4 ambazo wanazo tatu katika jengo hilo lililopo kati kati ya jiji la Mwanza
Picha ya Pamoja ndani ya Metro fm 99.4 toka kushoto ni Juma Herman, Mkala Fundikira, Kelvina John, George Binagi, Tonny Alphonce, Rosier, Sophia George, Wakuvwanga Masoud na Katumba Madua.
Jhikoman kushoto, Rosier(receiptionist) na Masoud.
Masoud akibadilishana mawazo na Sphia George wa Metro fm 99.4 ya Mwanza wiki iliyopita ujumbe wa Imetosha Foundation ulipotembelea studio za kituo hicho cha redio.


Nyema akipongezwa kwa kuifungia Barca bao mbili usiku huu dhidi ya PSG.Neymar dakika ya 34 aliifungia Barca bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya PSG kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira uliopigwa
Daniel Alves. Kipindi cha pili hakuna aliyeliona lango l mwenzake Timu zilishambuliana mara kwa mara. Ushindi huu Barca wanasonga hatua ya Nusu Fainali kwenda kukamilisha Timu Nne za Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.
Iniesta akiendesha!
Neymar dakika ya 14 aliifungia bao la kwanza Barcelona baada ya kutanguliziwa mpira mbele na Andrés Iniesta Luján na kukatiza kwa mabeki na kufunga bao hilo akimpiga chenga pia kipa wa PSG Sirigu.VIKOSI:
Barcelona:
Ter Stegen, Dani Alves, Pique, Mascherano, Jordi Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta, Messi, Suarez, Neymar.
Akiba: Bravo, Xavi, Pedro, Rafinha, Bartra, Sergi Roberto, Adriano.

PSG: Sirigu, van der Wiel, Marquinhos, Luiz, Maxwell, Verratti, Cabaye, Matuidi, Cavani, Ibrahimovic, Pastore.
Akiba: Douchez, Camara, Lucas Moura, Bahebeck, Digne, Lavezzi, Rabiot.
Refa: Svein Oddvar Moen

Barcelona vs Paris Saint-Germain


Robert Lewandowski dakika ya 40 tena alifunga bao jingine na kufanya 5-0 baada ya kupata pasi kutoka kwa Thomas Müller.  Hadi mapumziko Bayern walikuwa mbele ya bao 5-0 dhidi ya Timu ya FC Porto. Raha iliyokuwa ikisubiriwa na Mashabiki!! Thomas Müller akishangilia na mwenzake.Thiago Fc Porto Chalii!! Ushindi wa gemu ya kwanza wameivurunda!! hoi!Hii ndiyo raha ya kuwa Meneja!! unashangilia mpaka unajisahau!
Bao la FC Porto lilifungwa dakika ya 73 na Jackson Martínez akipewa pasi na H. Herrera na kufanya 5-1. Xabi Alonso Aliwafunga bao la sita na kufanya mtanange kumalizika kwa bao 6-1 na jumla ya mabao kuwa 7-4. Kwa matokeo hayo Bayern Munich wanakwenda hatua ya Nusu Fainali.
Kocha wa FC Porto hana hamu kipindi cha kwanza tuu kashapagwa kwa kipigo!!Jerome Boateng of Munich and his teammates celebrate scoring their team's second goal
Dakika ya 36 kipindi cha kwanza Thomas Müller aliipa bao la 4 Bayern Munich na kufanya bao jumla kuwa 5-3 baada ya kupata ushirikiano safi kutoka kwa Thiago Alcántara na kufunga bao hilo.
Robert Lewandowski alifunga bao la tatu dakika ya 27 kwa kichwa baada ya kupata krosi safi ya juu kutoka kwa Thomas Müller na kufanya bao kuwa 3-0 dhidi ya FC Porto.
Jerome Boateng dakika ya 22 aliwafungia bao la pili Bayern Munich na kufanya 2-0 dhidi ya FC Porto na Agg kuwa 3-3 baada ya kupata pasi kutoka kwa Holger Badstuber. 
Thiago Alcântara kipindi cha kwanza dakika ya 14 aliwapatia bao la kuongoza baada ya kupata mpira kutoka kwa Juan Bernat. UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Robo Fainali-Mechi za Marudiano

Jumanne Aprili 21
Bayern Munich vs FC Porto [Allianz Arena, Munich, Germany] (1-3)
Barcelona vs Paris Saint-Germain [Nou Camp, Barcelona, Spain] (3-1) 

waliotembelea blog