Wednesday, April 22, 2015


www.bukobasports.com
Robin van Persie Jana alicheza Mechi yake ya kwanza tangu apone Enka yake wakati Kikosi cha Vijana wa chini ya Miaka 21 wa Manchester United walipotoka Sare 1-1 na wenzao wa Leicester City katika Mechi ya Ligi ya Vijana ambayo Man United ndio Vinara.
Jumamosi Van Persie alikuwa Benchi wakati Man United inacheza huko Stamford Bridge Mechi ya Ligi Kuu England na kufungwa 1-0 na Chelsea lakini Jana alicheza Dakika 62.
Lakini kwenye Mechi na Leicester, Adnan Januzaj, Miaka 20, na Rafael da Silva, Miaka 24, waliumia na kutolewa.
Januzaj alitoka Dakika ya 54 baada kupata tatizo la Musuli na Rafael kubadilishwa mwishoni mw Kipindi cha Kwanza baada kuumia mbavu.

Habari nyingine njema kwa Man United ni kumaliza Kifungo cha Mechi 6 kwa Sentahafu Jony Evans ambae Jana alicheza Dakika zote 90.
Evans alifungiwa pamoja na Straika wa Newcastle Papiss Cisse baada ya kutemeana mate wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England Mwezi uliopita.
Van Persie, mwenye Miaka 31, ndie aliemtengenezea Sean Goss kuisawazishia Man United katika Dakika ya 32 baada ya Harry Panayiotou kuipa Leicester Bao katika Dakika ya 18.

Van Persie na Evans sasa watajumuika na Majeruhi waliopona, Daley Blind na Marcos Rojo, kurudi Kikosini kuikabili Everton Wikiendi hii huko Goodison Park kwenye Mechi ya Ligi Kuu England lakini hadi sasa hamna uhakika kama Michael Carrick atakuwa fiti kwa Mechi hiyo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog