Wednesday, September 17, 2014


ARSENE Wenger amewalaumu wachezaji wake kwa kushindwa kuonesha kiwango kizuri baada ya kufunbgwa 2-0 na Borrusia Dortmund katika mchezo wa ligi ya mabingwa jana usiku (Uefa), huku wakirudi nyumbani na balaa kufuatia mkali wao Jack Wilshere kupata majeruhi.
Wilshere alitegua kifundo chake cha mguu wa kulia katika dakika za majeruhi na Wenger amekiri kuwa ameumia sehemu ile ile ambayo ilimuweka nje ya uwanja kwa miezi 17.
"Ni vigumu sana  kusema jinsi ilivyo mbaya," alisema kocha wa Arsenal. "Kwa kawaida isingekuwa mbaya sana , lakini nina wasiwasi kidogo kutokana na historia yake".
Arsenal's Jack Wilshere went down injured late on to add to Arsene Wenger's mounting problems
Jack Wilshere akianguka chini dakika za mwisho na kupata majeruhi iliyomchanganya Wenger ambaye ana matatizo hayo katika kikosi chake 
Jack Wilshere has injured his right ankle, which has been problematic for him over the past two years
Jack Wilshere ameumia kifundo cha mguu wa kulia kilichomsumbia miaka miwili iliyopita

"Ulikuwa usiku mgumu sana," alisema Wenger. "Dortmund walikuwa timu bora. Tulikuwa na kiwango kibovu.Ni vigumu kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja kwasababu kama timu hatujawa katika kiwango sawa"
"Tatizo liko pale pale, tulipata nafasi za kufunga kipindi cha kwanza. Tulikamatwa katika mashambulizi mawili ya kushitukiza. Kwa mara ya kwanza tulipoteza mpira mita 80 kutoka kwenye goli letu. Kulikuwa na watu wengi wa kuzuia goli hilo. Bado tulikuwa watu watatu dhidi ya mmoja. Ni ngumu kuelewa jinsi gani tulifungwa"

waliotembelea blog