Wednesday, October 9, 2013



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa Kitaifa wa Uzazi wa Mpango na kuzindua rasmi Kampeni ya Nyota ya Kijani, wakati wa mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa Kitaifa wa Uzazi wa Mpango na kuzindua rasmi Kampeni ya Nyota ya Kijani, wakati wa mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza kitufye cha Laptop kuashiria kufungua rasmi Mkutano wa Kitaifa wa Uzazi wa Mpango na kuzindua rasmi Kampeni ya Nyota ya Kijani, wakati wa mkutano huo uliofanyika leo Oktoba 9, 2013 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jambii, Dkt. Hussein Mwinyi
ehemu ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akiwahutubia kwenye Mkutano huo
 Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Balozi wa Marie Stops Tanzania, Narietha Boniface, na Miss Tanzania 2013, wakati alipotembelea katika Mabanda la maonyesho la Marie Stops, alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye Mkutano wa Kitaifa wa Uzazi wa Mpango na Uzinduzi wa Kampeni ya Nyota ya Kijani, uliofanyika leo Okt. 9, 2013 kwenye Ukumbi wa Mliman City, Dar es Salaam
 ehemu ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akiwahutubia kwenye Mkutano huo
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Taaluma wa Shirika la Engender Health, Feddy Mwanga, wakati alipotembelea katika Banda hilo la maonyesho katika Mkutano wa Kitaifa wa Uzazi wa Mpango na Uzinduzi wa Kampeni ya Nyota ya Kijani, uliofanyika leo Okt. 9, 2013 kwenye Ukumbi wa Mliman City, Dar es Salaam.

 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais, kuhutubia kwenye mkutano huo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo wakati alipotembelea kwenye Banda la maonyesho la PSI, wakati alipotembelea katika Banda hilo la maonyesho katika Mkutano wa Kitaifa wa Uzazi wa Mpango na Uzinduzi wa Kampeni ya Nyota ya Kijani, uliofanyika leo Okt. 9, 2013 kwenye Ukumbi wa Mliman City, Dar es Salaam.

 Msanii Mrisho Mpoto, akitoa burudani yenye ujumbe wa Uzazi wa Mpango mbele ya mgeni rasmi wakati wa mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mliman City Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi nawaratibu wa Mkutano huo mara baada ya ufunguzi rasmi.
 
Rapper Nay Wa Mitego amesema amekuwa akisumbuliwa mno na maafisa usalama pamoja na vyombo mbalimbali vya habari wanaomdhania kuwa anajihusisha na biashara ya madaya ya kulevya kitu ambacho amekuwa akikanusha kwamba sio kweli.

Akiongea na Bongo leo kwa njia simu Nay amesema anasikitishwa kupokea taarifa zinazodai kuwa anajihusisha na biashara hiyo haramu, kitu ambacho hakifanyi kwakuwa anategemea shughuli zake za muziki zinazomlipa vizuri.

“Watu wamekuwa wakishangaa sifanyi show hata mwaka mzima lakini maisha yanaenda namiliki gari ndio maana wanaongea mengi huku media na maafisa usalama wananichunguza kila siku,” alisema Nay.
 
Msanii huyo wa Salam Zao amesema yupo kwenye maongezi na kampuni ya simu ili imfanye kama balozi wake.

“Nasubiria mambo yangu yaende poa, nimeingia mkataba wa kuwa balozi wa mtandao wa simu hapa nchini bado muda wake kuuweka wazi kwasababu tupo kwenye makubaliano zaidi na pia ikifika muda nataka kuanika vyanzo vyangu vyote



Unajua kama kitu hicho kingetokea hapa Africa,watu wengi wangesema kala 'majani' ni msemo unaotumika kwa mwanaume anayetawaliwa na mwanamke wake.

Seriously,mwanaume gani anayeweza kumruhusu girlfriend wake,mchumba au mke wake amdhalilishe hadharani namna hiyo?


Mwanamke mmoja wa kichina amekamatwa na polisi baada ya kumlazimisha boyfriend wake apige magoti huku akimpiga makofi usoni.

Udhalilishaji huu ulitokea ijumaa iliyopita kwenye mji wa Kowloon,Hong Kong baada ya Chui(boyfriend) kumchukua msichana mwingine na kumpeleka nyumbani kwake wakati  anamahusiano na Cheng(mpiga makofi).


Cheng alijua na akampigisha magoti boyfriend wake huyo mbele za watu wakipita.
Aliposisitiza kuwa hakumuita yule msichana kwake akisema 'sikiliza kwanza kabla hujanipiga',Cheng akaanza kumchapa makofi usoni huku anapiga kelele
 'You're slandering me!'




Watu wakajaa na kuanza kufilm tukio hilo la aina yake ambapo lilitumwa siku hiyohiyo YouTube.Watu wengine walipoanza kuingilia ugomvi huo wa kimapenzi Cheng akapayuka 'Haiwahusu!'
Watu wengi walioshuhudia walikuwa upande wa Chui,mwanamke mmoja akamwambia 'simama achana na mwanamke huyu mwenye sura mbaya,unastahili mzuri zaidi'
Mpita njia mmoja akawapigia simu polisi ambapo Cheng alikamatwa.
Mwanamke huyo mwenye miaka 20(Cheng)alikamatwa kwa kesi ya udhalilishaji wakati boyfriend wake mwenye miaka 23,Chui akipelekwa hospitali
Ephraim Kibonde akishuka kwenye gari baada ya ajali.
..Akilikagua gari lake.

Trafiki akiwa eneo la ajali.
Gari la Kibonde likiwa eneo la ‘round about’ ya kuelekea Mlimani City baada ya ajali.
Fundi akirekebisha gari hilo baada ya ajali.
Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde amepata ajali ya gari leo asubuhi  katika barabara ya Sam Nujoma kwenye ‘round about’ ya kuelekea Mlimani City. Gari alilokuwa anaendesha Kibonde aina ya Toyota Carina lenye nama za usajili T 733 BVE limeharibika kwa mbele katika ajali hiyo.
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Mama Land, kinachorushwa na Runinga ya Clouds ya jijini Dar, Benny Kinyaiya hivi karibuni alikombwa vitu kadhaa kwenye gari lake na vibaka mara baada ya kupaki gari nje ya nyumba yake. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kinyaiya alisema kuwa siku ya tukio saa nne usiku aliporejea nyumbani kwake maeneo ya Kinondoni Dar, aliegesha gari nje ya geti na kuingia ndani kuchukua kitu kisha aendelee na mishemishe zake.
 
Habari zinapasha kwamba, baada ya kuingia wezi hao walitumia fursa hiyo kuvunja vioo na kuiba redio na vitu vingine.
“Inauma sana kwani kilikuwa ni kitendo kama cha dakika chache tu, yaani kuingia ndani na kutoka tu tayari nimeshaibiwa, natamani hata nimkamate mmoja ili nimuoneshe mfano,” alisema Kinyaiya.

DIAMOND PLATNUM
Kuvujisha Nyimbo yangu hakuwezi kunipunguzia
wala Kunidhuru chochote... Sanasana utanizidishia
Umaarufu na kunipa Show zaidi... Kama nimeacha kurecord nyimbo
Studio kwako Uspanick, Relax.. tafta Msanii mwingine
Mkali zaidi yangu umrecordie Ngoma Ahit kushinda mimi...
.ila Kuvujisha Unajisumbua bure!

Hisia zangu za pelekea kuandika haya nikiwa na uzuni
ndani yake kwa kuwa muda nilioutmia na akili nliotumia
dhairi ni Mungu Pekee anajua ndio Maana aina budi
namwachia Mungu pia....Imani iliyo ndani yangu nikiamini
kuwa kutoa ya Moyoni uufanya Moyo kujengeka
Upya,Mwenyezi Mungu Atanijenga Upya na kuwaandalia kitu kipya hiv
karibun.Hii ni changamoto kwangu na Kuweza
kujua sheria na katiba za Muziki wangu na
kusimamia Haki zangu...... Nawapenda Sana Mashabiki Zangu..... #WCB #CocaBoy for Lif


MAKOMANDOO sita wa Jeshi la Marekani, wakiwamo wawili walioshiriki kumuua Kiongozi wa Al Qaeda, Osama bin Laden, wamefanikiwa kumuua kinara wa kundi la Al Shabaab anayedaiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi katika jengo la biashara la Westgate mjini Nairobi nchini Kenya mwezi uliopita na kusababisha vifo vya watu 68 na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, aliyeko ziarani nchini Indonesia, aliwaambia waandishi wa habari jana, kuwa gaidi huyo aliuawa wakati wa mapambano kati yake na makomandoo hao. Hata hivyo, hakumtaja jina.

John Kerry alisema “Jumamosi iliyopita, makamandoo hao wa Marekani, walishambulia nyumba ya kiongozi huyo mjini Barawe, Somalia. Mashambulizi yaliyofanywa na wanajeshi wa kikosi maalumu cha Marekani nchini Libya na Somalia, yanaonyesha dhamira ya Serikali ya Marekani kuwasaka magaidi.”

Alisema kwamba, taarifa za kiintelijensia, zinaonyesha kinara huyo ambaye alikuwa mshirika mkuu wa Kundi la Al-Shabaab, alihusika moja kwa moja katika shambulio la kigaidi katika jumba la maduka la Westgate.

Kerry alisema kwamba, baada ya kumaliza kazi hiyo, wanajeshi hao waliondoka mjini Barawe na kurudi Marekani.


Ni katika operesheni hii ambapo pia makomandoo wa Marekani walimkamata kiongozi wa Kundi la Al-Qaeda, Anas al Libi katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. Anas al-Liby, anahusishwa na matukio mengi makubwa yakiwamo ya kuwavizia watu wenye asili ya Marekani kuwakamata na kuwafanyia vitendo vya kinyama


Zitto Kabwe amekanusha uvumi ulioenea kuwa anampango  wa  kumuoa mtoto wa Rais Kikwete na ndio maana amepunguza makali yake Bungeni ya kuuliza maswali na kuchangia hoja ...

Zitto alitoa kauli hiyo  juzi wakati akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mpanda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Maridadi....

Alisema uko uvumi ambao umeenea hapa nchini kuwa makali yake yamekupungua bungeni kutokana na yeye kutoka  kimapenzi na  mtoto wa Rais Kikwete wakati sio kweli .

Alifafanua kuwa yeye Bungeni hayuko kwa ajiri ya kupigana ngumi bali yeye siku zote toka amekuwa mbunge amekuwa akipigania kutoa hoja zenye nguvu ndani ya Bunge kama hana hoja za msingi huwa hakulupuki ovyo ovyo

Alieleza ndio maana katika kikao kijacho cha Bunge ameisha wasilisha maombi ya mswada binafsi wa kupendekeza kufutwa kwa sheria ya mwaka 1976 sheria namba 3 ambayo amedai inavinyima haki na uhuru vyombo vya habari ..

Wako viongozi ambao  wamekuwa wakiitumia vibaya sheria hiyo na hasa pale wanapo kuwa wamekosolewa au kuandikwa vibaya na magazeti ...


Alisema kitendo cha kuyafungia magazeti ya Mtanzania na Mwananchi ni ukiukwaji wa katiba kwani kila mwananchi ana haki ya kupata habari na kitendo hicho kinapunguza ajira kwa vijana 
 
Alisema leo hii Serikali inapenda kufanya mambo yake kisiri na ndio maana hata mishahara yetu sisi wabunge ambao mmetuchagua nyinyi wananchi hamuijui wakati ni haki yenu .


Mshahara wa Mbunge kwa mwezi ni Tsh 11,200,000 wakati waziri mkuu anapata mshara wa shilingi milioni 26 kwa mwezi na kila kitu anapata bure .Kama ni kosa kutamka mshahara basi namie nichukuliwe hatua kama magazeti yalivyo fungiwa na kesho nikiwa Wilayani Sikonge ntataja na Rais anapata mshahara kiasi gani kwa mwezi 

Kuhusu katiba aliomba marekebisho ya katiba yazingatie zaidi kuwapa mamlaka ya maamuzi wananchi kuliko viongozi kama ilivyo sasa na alishauri mbunge awe mbunge tuu na asiwe waziri kwani mbunge anapo kuwa waziri matokeo yake ni wananchi waliomchagua kukosa uwakilishi bungeni  ..  

Alisema anao mfano hai kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda toka amechaguliwa kuingia Bungeni mwaka 2000 hajawahi kuuliza swali hata moja bungeni kama kuna mtu anaushahidi wa swali lolote ambalo Pinda aliwahi kuuliza yeye Zito yuko tayari kumpa shilingi laki mbili .



Alifafanua kuwa Pinda alichaguliwa kuwa Mbunge kwa mara ya kwanza na aliteuliwa kuwa naibu wa Tamisemi hivyo nafasi hiyo ya uwaziri imembana muda wote .

-Katavi yetu

HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameweka wazi mshahara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
SOMA ZAIDI....
Zitto ameutaja mshahara huo wa Pinda anayejitambulisha kama ‘mtoto wa mkulima’ juzi mjini Mpanda na jana wilayani Sikonge wakati akihutubia mikutano ya hadhara katika ziara ya Kanda ya Magharibi kwa ajili ya ujenzi wa chama.
Alisema Pinda anapokea jumla ya sh milioni 26, ambazo ni kiasi kikubwa kulinganisha na uchumi wa nchi.
Akichanganua alisema Pinda anapokea sh mil. 11.2 kama mbunge, sh mil. 8 kwa nafasi ya waziri na kiasi kinachosalia kufikia sh mil. 26 kwa nafasi yake ya uwaziri mkuu.
Alisema sababu hiyo ya mishahara mikubwa isiyokatwa kodi ndiyo huwafanya viongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wakali pale vyombo vya habari vinapotaka kuwafahamisha wananchi namna watumishi wao wanavyojilipa.
“Nimeanza na mshahara wa waziri mkuu pia siku zijazo nitataja na wa rais, kwa kuwa amesaini makubaliano na Serikali ya Marekani kuendesha nchi kwa uwazi, na moja ya uwazi ni kwa muajiri kujua kiasi anachomlipa mwajiriwa wake,” alisema Zitto.
Hatua ya Zitto imekuja baada ya kuwapo mvutano mkubwa kuhusiana na kile kinachodaiwa ‘usiri’ wa mishahara ya watumishi wa umma, wakati ni haki ya walipa kodi kujua kile wanachowalipa walioomba kuwaongoza.
Kodi ya laini za simu
Akizungumzia sakata la kodi katika laini za simu, Zitto alisema CCM ina ajenda ya kisiasa kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.
Alisema serikali baada ya kubaini watu wengi wanapeana taarifa kwa njia ya ujumbe mfupi, hususan katika masuala ya kisiasa, wakaona njia sahihi ya kudhibiti ni kuwatoza kodi ya laini ili kupunguza hatari ya mawasiliano hayo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.
“Sikuwepo bungeni wakati wabunge wa CCM wanapitisha kadhia hiyo ya kuwanyonya wananchi, wenzangu wakaniambai tukasema hapana, kwa maana tuliona hii leo kuna Watanzania wengi wasio na uwezo wa kuhudumia simu kwa kiasi cha sh 1,000 kwa mwezi,” alisema Zitto.
Akijibu maswali ya wananchi mjini Mpanda waliotaka kujua sababu ya kupunguza makali bungeni, Zitto alisema hakuna makali yaliyopungua bali ni mitazamo ya watu.
Alisema kwa kushirikiana na wabunge wenzake wa upinzani wamekuwa wakisimamia hoja zenye manufaa kwa wananachi huku wabunge wanaojipambanua kuwa majasiri kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwaunga mkono wazi wazi.
Akiwa  wilayani Sikonge, Zitto alisema Watanzania hawawezi kujivunia uhuru huku mama zao, watoto wao na wazee wao wakiwa hawana uhakika wa kupata huduma bora ya afya, elimu na maji safi.
Alisema kwa sasa Tanzania ni taifa moja lililogawanyika katika nchi mbili za wenye fedha na wasio na fedha.
Alisema nchi ya wenye fedha, familia zao husoma katika shule bora, zenye mazingira bora na walimu wazuri, hutibiwa katika hospitali zenye hadhi na huduma muhimu na ikibidi nje ya nchi, huku nchi ya wasio na fedha  familia zao wakiishi kwa shida, kusoma katika majengo ya shule na walimu wasiopata mishahara ya kuridhis

Watu wawili wanaotuhumiwa kuwa ni wezi a.k.a Wapigaji/Matapeli wamekamatwa usiku huu kwenye hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam.

Watu hao ambao wamekamatwa ni Bw. Takula Mayenga mkazi wa Mbezi Temboni na Bw. Juma Hamis ambaye ni mkazi wa Tabata wakiwa na nyaraka tofauti ikiwemo kitambulisho kinachotaja kuwa ni cha Idara ya Usalama wa Taifa, kadi za benki pamoja na simu zaidi ya kumi,wakiwa katika harakati za kumtapeli mwanadada mmoja aliejitambulisha kwa jina la Rebecca ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Biashara cha CBE,Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaa  .

Akisimulia tukio dada huyo ambaye alipatwa na tukio hilo la kutapeliwa Ijumaa ya wiki iliyopita alisema kuwa, ilikuwa ni Ijumaa iliyopita wakiwa wamekaa katika fukwe wakipunga upepo ndipo alipokuja tapeli huyo na kukaa nao na baadae aliwawekea madawa ya kulevya na kuondoka na dada huyo kwenda kumtupa baharini.
 Kava ya nje ya Kitambulisho hicho kinaonekana namna hii.
 Watuhumiwa hao wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi.
 Kitambulisho hicho kinavyoonekana kwa nyuma.
 Mtuhumiwa wa Uwizi aliejitambulisha kwa jina la Juma Hamis huku akiwa na Kitambulisho cha Kazi cha Idara ya Usalama wa Taifa chenye jina la Kenedy Magige.
 Mtuhumiwa mwenza wa Tukio hilo la Wizi,aliejitambulisha kwa jina la Takula Manyenga mwenye umri wa Miaka 28,akidhibitiwa kwa kufungwa kamba mara baada ya kukamatwa Usiku huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam.
 Watuhumiwa wote wawili wakipakiwa ndani ya Gari la Polisi kutoka katika Kituo cha Kawe,Jijini Dar es Salaam.
 Askari Polisi wakiwa eneo la tukuo kuhakikisha Usalama unapatikana eneo hilo.
 Askari Polisi wakiwa na Watuhumiwa hao wakati wakiendelea na Ukaguzi ndani ya Gari hilo aina ya Toyota Prado lenye nambari za Usajili T 445 BCY.
 Askari Polisi wakiendelea na Ukaguzi ndani ya Gari hilo,ambapo ndani ya Gari hilo kulikutwa na Simu zaidi ya kumi ambazo zilichukuliwa na Polisi hao.
 Gari walilokuwa wakilitumia Watuhumiwa hao.
 
 Ulinzi mkali kwa watuhumiwa hao.
Msafara wa kuelekea kituoni.

Mbunge wa jimbo la bukoba mjini ambae pia ni waziri wa maliasili na utalii balozi khamisi kagasheki amelazimika kusitisha ziara ya kiserikali huko nchini Kuwait na kurudi jimboni kwake kwa ajili ya kuwafariji wananchi walioathilika na mafuriko.   Mara baada ya kuwasili alikutana na viongozi mbalilmbali na alipewa taarifa ya kila kata ili aweze kupata hali halisi ya madhala yalijitokeza kwa kila kata,  baada ya kupata taarifa  alianza ziara ya kutembelea waanga wa mafuriko na kuona hali halisi,mh kagasheki alishuhudia majumba yakiwa yamebomoka na ualibifu mkubwa wa vifaa,lakini pia watu wengi walikuwa hawana mahala pa kuishi kutokana na nyumba zao kujaa maji, Balozi kagasheki ameweza kutoa msaada wa chakula kwa waanga wote,lakini pia kwa wale ambao nyumba zao zimebomoka kuta ameweza kutoa pesa ili waweze kurekebisha , mh kagasheki alisema wakati serikali ikifanya tathimini yeye kama mbunge swala hili limemgusa sana kwa hiyo ameona afanye awezalo kwa haraka wakati taratibu zingine zikifanywa.

VIONGOZI MBALIMBALI KUTOKA KWENYE KATA ZA MANISPAA YA BUKOBA
BALOZI KAGASHEKI AKIPOKEA TAARIFA YA MAAFA YA MAFURIKO JIMBONI KWAKE

KATIBU WA CCM BUKOBA MJINI JANATH MUSA KAYANDA AKIELEZA KWA UFUPI MAENEO YALIYOATHILIKA NA MAFURIKO



Rais wa Cameroon Paul Biya amemshawishi mwanasoka Samuel Eto'o kutafakari upya mipango yake ya kujizulu kutoka soka ya kimataifa

Mshambulizi huyo wa Chelsea alikutana na waakilishi wa Rais mjini Yaounde kujadili mustakabali wa mchezaji huyo kuhusu soka ya kimataifa.

Sasa atakwenda Ufaransa kujiunga na timu ya taifa inayojiandaa kucheza dhidi ya Tunisia katika michuano ya kufuzu kwa kombe la Dunia Brazil mwaka 2014. Baada ya kukutana na Eto'o, alikubali kuchezea Cameroon kwa mara nyingine.

Etoo mwenye umri wa miaka 32 aliwambia wenzake kuwa hatacheza tena soka ya nyumbani punde tu baada ya Cameroon kuicharaza Libya na kuingia katika awamu ya pili ya kufuzu kwa kombe la dunia.

Licha ya ripoti za yeye kuacha kucheza soka, kocha wa timu ya Cameroon Volker Finke alimteua Eto'o kuchezea timu ya taifa ya Cameroon dhidi ya Tunisia ingawa mwenyewe hakuwa ametoa taarifa rasmi.

Eto'o amekuwa na uhusiano tete na maafisa wa soka nchini Cameroon katika siku za nyuma ikiwemo hata kuongoza timu ya taifa kwenye mgomo uliosambaratisha mechi ya kirafiki dhidi ya Algeria.

Eto’o aliadhibiwa kwa kupigwa marufuku kucheza mechi 15 ingawa baada ya kukata rufaa alipunguziwa adhabu hadi mechi 8

Hata baada ya adhabu yake kumalizika alikataa kuichezea Cameroon kwa miezi kadhaa.

Pia sio mara ya kwanza kwa Rais Biya kuingilia kati na kumzuia mchezaji kujiuzulu kutoka katika majukumu ya kitaifa.

waliotembelea blog